Home » » RASIMU YA KATIBA MPYA HII HAPA

RASIMU YA KATIBA MPYA HII HAPA

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Tuesday, June 4, 2013 | 2:37 AM


Toleo la Rasimu ya Katiba limechapishwa kwenye Gazeti la Serikali kwa

mujibu wa kifungu cha 18(5) cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura ya

83, kwa madhumuni ya kuwepo kwa wananchi kusoma na kutoa maoni zaidi

kwa Tume kuhusu maudhui yaliyomo kwenye Rasimu ya Katiba.

Dar es Salaam, J

OSEPH S. WARIOBA,

3 Juni, 2013

Mwenyekiti wa Tume

ii


RASIMU YA KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA

TANZANIA YA MWAKA 2013


________

YALIYOMO

______

Ibara Kichwa cha Habari


UTANGULIZI

SURA YA KWANZA

J
AMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

SEHEMU YA KWANZA

M
IPAKA, ALAMA, LUGHA, UTAMADUNI NA TUNU ZA TAIFA

1. Jamhuri ya Muungano

2. Eneo la Jamhuri ya Muungano

3. Alama na Siku Kuu za Taifa

4. Lugha ya Taifa na lugha za alama

5. Tunu za Taifa

SEHEMU YA PILI

M
AMLAKA YA WANANCHI, UTII NA HIFADHI YA KATIBA

6. Mamlaka ya wananchi

7. Watu na Serikali

8. Mamlaka na utii wa Katiba

9. Hifadhi ya Katiba

SURA YA PILI

M
ALENGO MUHIMU, MISINGI YA MWELEKEO WA

S
HUGHULI ZA SERIKALI NA SERA ZA KITAIFA

10. Utekelezaji wa malengo ya Taifa

11. Malengo Makuu

12. Sera kuhusu Mambo ya Nje

SURA YA TATU

M
AADILI NA MIIKO YA UONGOZI WA UMMA

SEHEMU YA KWANZA

M
AADILI YA UONGOZI WA UMMA

13. Dhamana ya Uongozi wa Umma

iii


14. Kanuni za Uongozi wa Umma

15. Zawadi katika Utumishi wa Umma

16. Wajibu wa kutangaza mali na madeni

17. Mgongano wa kimaslahi

18. Matumizi ya mali ya umma

19. Matumizi ya masharti ya maadili kwa watumishi wa umma

SEHEMU YA PILI

M
IIKO YA UONGOZI WA UMMA

20. Utii wa Miiko ya Uongozi wa Umma

21. Marufuku kwa baadhi ya vitendo

SURA YA NNE

H
AKI ZA BINADAMU, WAJIBU WA RAIA NA MAMLAKA ZA NCHI

SEHEMU YA KWANZA

H
AKI ZA BINADAMU

22. Uhuru, utu na usawa wa binadamu

23. Haki ya kuwa hai

24. Marufuku kuhusu ubaguzi

25. Haki ya kutokuwa mtumwa

26. Uhuru wa mtu binafsi

27. Haki ya faragha na usalama wa mtu

28. Uhuru wa mtu kwenda anakotaka

29. Uhuru wa maoni

30. Uhuru wa habari na vyombo vya habari

31. Uhuru wa imani ya dini

32. Uhuru wa watu kujumuika na kushirikiana na wengine

33. Uhuru wa kushiriki shughuli za umma

34. Haki ya kufanya kazi

35. Haki za wafanyakazi na waajiri

36. Haki ya kumiliki mali

37. Haki ya uraia

38. Haki ya mtuhumiwa na mfungwa

39. Haki ya watu walio chini ya ulinzi

40. Uhuru na haki ya mazingira safi na salama

41. Haki ya elimu na kujifunza

42. Haki ya mtoto

43. Haki na wajibu wa vijana

44. Haki za watu wenye ulemavu

45. Haki za makundi madogo katika jamii

46. Haki za wanawake

47. Haki za wazee

iv


SEHEMU YA PILI

W
AJIBU WA RAIA NA MAMLAKA ZA NCHI

(a) Wajibu wa Raia kwa Taifa48. Wajibu wa kushiriki kazi

49. Ulinzi wa mali ya umma

50. Haki na wajibu muhimu

(b) Wajibu wa Mamlaka za Nchi51. Hifadhi ya haki za binadamu

52. Usimamizi wa haki za binadamu

53. Mipaka ya haki za binadamu

SURA YA TANO

U
RAIA KATIKA JAMHURI YA MUUNGANO

SURA YA SITA

M
UUNDO WA JAMHURI YA MUUNGANO

57. Muundo wa Muungano

58. Vyombo vya utendaji vya Jamhuri ya Muungano

59. Mamlaka ya Serikali ya Muungano

60. Mambo ya Muungano

61. Washirika wa Muungano

62. Mamlaka ya Washirika wa Muungano

63. Mahusiano kati ya Washirika wa Muungano

64. Mawaziri Wakaazi

65. Mamlaka ya wananchi

66. Wajibu wa kulinda Muungano

SURA YA SABA

S
ERIKALI YA JAMHURI YA MUUNGANO

SEHEMU YA KWANZA

S
ERIKALI, RAIS NA MAKAMU WA RAIS

(a) Serikali67. Serikali ya Jamhuri ya Muungano

54. Uraia wa Jamhuri ya Muungano

55. Uraia wa kuzaliwa

56. Uraia wa kuandikishwa

v


(b)
Rais


68. Rais wa Jamhuri ya Muungano

69. Madaraka na majukumu ya Rais

70. Utekelezaji wa madaraka ya Rais

71. Rais kuzingatia ushauri

72. Rais kushindwa kumudu majukumu yake

73. Utekelezaji wa majukumu ya Rais akiwa hayupo

(c) Uchaguzi wa Rais74. Uchaguzi wa Rais

75. Sifa za Rais

76. Haki ya kuchaguliwa tena

77. Utaratibu wa Uchaguzi wa Rais

78. Malalamiko kuhusu uhalali wa uchaguzi wa Urais

79. Kiapo cha Rais

(d) Masharti Mahsusi kuhusu Mamlaka ya Rais80. Madaraka ya kutangaza vita

81. Madaraka ya Rais kutangaza hali ya hatari

82. Mamlaka ya Rais kutoa msamaha

83. Kinga dhidi ya mashtaka ya Rais

84. Bunge kumshtaki Rais

85. Maslahi ya Rais

(e) Makamu wa Rais86. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano

87. Upatikanaji wa Makamu wa Rais

88. Sifa za Makamu wa Rais

89. Kiapo cha Makamu wa Rais

90. Wakati wa Makamu wa Rais kushika madaraka

91. Bunge kumuondoa Makamu wa Rais

SEHEMU YA PILI

B
ARAZA LA MAWAZIRI LA SERIKALI YA JAMHURI YA MUUNGANO

(a) Baraza la Mawaziri92. Kuundwa kwa Baraza la Mawaziri

93. Uteuzi wa Mawaziri na Naibu Mawaziri

94. Sifa za Mawaziri na Naibu Mawaziri

95. Kiapo, muda na masharti ya kazi ya Waziri na Naibu Waziri

96. Utekelezaji wa shughuli za Serikali Bungeni

vi


(b) Mwanasheria Mkuu wa Serikali97. Mwanasheria Mkuu wa Serikali

(c) Katibu Mkuu Kiongozi na Makatibu Wakuu98. Katibu Mkuu Kiongozi

99. Makatibu Wakuu

(d) Utendaji Kazi wa Baraza la Mawaziri100. Kamati Maalumu ya Makatibu Wakuu

101. Sekretarieti ya Baraza la Mawaziri

SURA YA NANE

U
RATIBU WA MAHUSIANO YA WASHIRIKA WA MUUNGANO

102. Tume ya Mahusiano ya Uratibu wa Serikali

103. Malengo ya Tume

104. Majukumu ya Tume

SURA YA TISA

B
UNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO

SEHEMU YA KWANZA

K
UUNDWA KWA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO

105. Bunge la Jamhuri ya Muungano

106. Muda wa Bunge

107. Madaraka ya Bunge

108. Mipaka ya Bunge katika kutumia madaraka yake

109. Madaraka ya Bunge kutunga sheria

110. Utaratibu wa kutunga sheria

111. Utaratibu wa kubadilisha Katiba hii na baadhi ya sheria

112. Utaratibu wa kubadilisha masharti mahususi

113. Utaratibu wa kutunga sheria kuhusu mambo ya fedha

114. Madaraka ya Mkuu wa Nchi kuhusu Muswada wa Sheria

115. Kupitishwa kwa hoja za Serikali

SEHEMU YA PILI

W
ABUNGE

(a) Uchaguzi wa Wabunge116. Uchaguzi wa Wabunge

117. Sifa za kuchaguliwa kuwa Mbunge

118. Watu wenye Madaraka Serikalini kukoma utumishi

119. Utaratibu wa uchaguzi wa Wabunge

120. Kiapo cha Wabunge

121. Masharti ya kazi ya Wabunge

vii


122. Muda wa Wabunge kushika madaraka

123. Uwajibikaji wa Wabunge

124. Haki ya wapiga kura kumwajibisha Mbunge.

125. Uamuzi wa suala kama mtu ni Mbunge

126. Tamko Rasmi la Wabunge kuhusu Maadili ya Viongozi

127. Wabunge kutoa taarifa ya mali

SEHEMU YA TATU

U
ONGOZI WA BUNGE

(a) Spika na Naibu Spika128. Spika na mamlaka yake

129. Ukomo wa mamlaka ya Bunge

130. Naibu Spika

131. Utaratibu wa kumchagua Spika na Naibu Spika

132. Sifa za mtu anayefaa kuchaguliwa kuwa Spika au Naibu Spika.

(b) Ofisi ya Bunge133. Katibu wa Bunge

134. Sekretarieti ya Bunge

SEHEMU YA NNE

U
TARATIBU WA SHUGHULI BUNGENI

135. Kanuni za Kudumu za Bunge

136. Rais kulihutubia Bunge

137. Mikutano ya Bunge

138. Uongozi na vikao vya Bunge

139. Akidi ya vikao vya Bunge.

140. Kamati za Bunge

SEHEMU YA TANO

M
ADARAKA NA HAKI ZA BUNGE

141. Uhuru wa majadiliano Bungeni

142. Mipaka ya majadiliano Bungeni

SURA YA KUMI

M
AHAKAMA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

SEHEMU YA KWANZA

M
ISINGI YA UTOAJI HAKI NA UHURU WA MAHAKAMA

143. Kuanzishwa kwa Mahakama ya Tanzania

144. Misingi ya utoaji haki

145. Uhuru wa Mahakama

viii


SEHEMU YA PILI

M
UUNDO WA MAHAKAMA

(a) Mahakama za Jamhuri ya Muungano146. Muundo wa Mahakama

(b) Mahakama ya Juu ya Jamhuri ya Muungano147. Mahakama ya Juu

148. Akidi ya vikao vya Mahakama ya Juu

149. Madaraka ya Mahakama ya Juu

150. Madaraka ya Majaji wa Mahakama ya Juu

(c) Uteuzi wa Majaji wa Mahakama ya Juu151. Uteuzi wa Jaji Mkuu

152. Uteuzi wa Naibu Jaji Mkuu

153. Uteuzi wa Majaji wa Mahakama ya Juu

154. Kiapo cha Majaji wa Mahakama ya Juu

155. Muda wa kuwa madarakani kwa Jaji Mkuu, Naibu Jaji Mkuu na Majaji wengine

156. Utaratibu wa kukaimu katika Mahakama ya Juu

157. Utaratibu wa kushughulikia nidhamu ya Majaji wa Mahakama ya Juu

(d)Mahakama ya Rufani ya Jamhuri ya Muungano158. Mahakama ya Rufani

159. Akidi ya vikao vya Mahakama ya Rufani

160. Mamlaka ya Mahakama ya Rufani

161. Mamlaka ya Majaji wa Mahakama ya Rufani

(e)Uteuzi wa Majaji wa Mahakama ya Rufani162. Uteuzi wa Mwenyekiti wa Mahakama ya Rufani

163. Uteuzi wa Majaji wa Mahakama ya Rufani

164. Kiapo cha Majaji wa Mahakama ya Rufani

165. Muda wa kuwa madarakani kwa Mwenyekiti na Majaji wengine wa Mahakama

ya Rufani

166. Utaratibu wa kukaimu katika Mahakama ya Rufani

167. Utaratibu wa kushughulikia nidhamu ya Majaji wa Mahakama ya Rufani

(f)Usimamizi wa Shughuli za Mahakama168. Msajili wa Mahakama

169. Majukumu ya Msajili wa Mahakama

170. Mtendaji Mkuu wa Mahakama

171. Majukumu ya Mtendaji Mkuu wa Mahakama

ix


SEHEMU YA TATU

T
UME YA UTUMISHI WA MAHAKAMA NA MFUKO WA MAHAKAMA

(a) Tume ya Utumishi wa Mahakama172. Tume ya Utumishi wa Mahakama

173. Majukumu ya Tume ya Utumishi wa Mahakama

174. Uanachama katika vyama vya siasa

(b) Mfuko wa Mahakama175. Mfuko wa Mahakama

SURA YA KUMI NA MOJA

U
TUMISHI KATIKA JAMHURI YA MUUNGANO

176. Misingi mikuu ya Utumishi wa Umma

177. Masharti kuhusu utumishi katika Jamhuri ya Muungano

178. Tume ya Utumishi wa Umma

179. Mamlaka na majukumu ya Tume

SURA YA KUMI NA MBILI

U
CHAGUZI KATIKA VYOMBO VYA UWAKILISHI

NA

VYAMA VYA SIASA

SEHEMU YA KWANZA

U
WAKILISHI WA WANANCHI

180. Ushiriki katika vyombo vya uwakilishi

SEHEMU YA PILI

T
UME HURU YA UCHAGUZI

(a) Muundo wa Tume Huru yaUchaguzi181. Kuundwa kwa Tume Huru ya Uchaguzi

182. Kamati ya Uteuzi

183. Ukomo wa kushika madaraka ya Ujumbe wa Tume Huru ya Uchaguzi

184. Wajibu wa Tume Huru ya Uchaguzi

185. Malalamiko kuhusu uchaguzi

(b) Vyama vya Siasa186. Vyama vya siasa

(c) Mkurugenzi wa Uchaguzi na Msajili wa Vyama vya Siasa187. Utekelezaji wa majukumu ya Tume Huru ya Uchaguzi

x


SURA YA KUMI NA TATU

T
AASISI ZA UWAJIBIKAJI

SEHEMU YA KWANZA

T
UME YA MAADILI YA UONGOZI NA UWAJIBIKAJI

188. Tume ya Maadili ya Uongozi na Uwajibikaji

189. Majukumu ya jumla ya Tume

190. Muda wa kukaa madarakani wa Wajumbe wa Tume

191. Kuondolewa madarani kwa Wajumbe wa Tume

192. Uhuru wa Tume

193. Uwezeshaji wa nyenzo na rasilimali

SEHEMU YA PILI

T
UME YA HAKI ZA BINADAMU

194. Tume ya Haki za Binadamu

195. Kazi na majukumu ya Tume

196. Muda wa kukaa madarakani wa Wajumbe wa Tume

197. Kuondolewa madarani kwa Wajumbe wa Tume

198. Uhuru wa Tume

199. Uwezeshaji wa nyenzo na rasilimali

SEHEMU YA TATU

M
DHIBITI NA MKAGUZI MKUU WA HESABU ZA SERIKALI

200. Uteuzi wa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali

201. Sifa za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali

202. Kazi na majukumu yake

203. Muda wa kukaa madarakani

204. Kuondolewa madarakani

205. Uwezeshaji wa nyezo na rasilimali

SURA YAKUMI NA NNE

M
ASHARTI KUHUSU FEDHA ZA JAMHURI YA MUUNGANO

(a) Mfuko Mkuu wa Hazina na Fedha za

Jamhuri ya Muungano206. Mfuko Mkuu wa Hazina ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano

207. Masharti ya kutoa fedha za matumizi katika Mfuko Mkuu wa Hazina ya Serikali

208. Utaratibu wa kuidhinisha matumizi ya fedha zilizomo katika Mfuko Mkuu wa

Hazina ya Serikali

209. Utaratibu wa kuidhinisha matumizi ya fedha kabla ya Sheria ya Matumizi ya

Fedha za Serikali kuanza kutumika

210. Mfuko wa matumizi ya dharura

211. Mishahara ya baadhi ya watumishi kudhaminiwa na Mfuko Mkuu

xi


(b) Deni la Taifa na Mikopo ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano212. Deni la Taifa

213. Mamlaka ya kukopa ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano

214. Mamlaka ya Kukopa fedha kwa Serikali za Washirika wa Muungano

(c) Vyanzo vya Mapato ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano215. Vyanzo vya mapato vya Serikali ya Jamhuri ya Muungano

216. Manunuzi ya umma

(d) Benki Kuu217. Benki Kuu ya Jamhuri ya Muungano

218. Benki za Serikali za Washirika

SURA YA KUMI NA TANO

U
LINZI NA USALAMA KATIKA JAMHURI YA MUUNGANO

(a) Ulinzi na Usalama wa Taifa219. Usalama wa Taifa

220. Taasisi za ulinzi na usalama wa Taifa

221. Kuanzishwa kwa Baraza la Ulinzi na Usalama la Taifa

222. Majukumu ya Baraza la Ulinzi na Usalama la Taifa

(b)Jeshi la Wananchi wa Tanzania223. Kuanzishwa kwa Jeshi la Wananchi wa Tanzania

224. Uteuzi wa Mkuu wa Majeshi

225. Madaraka ya Amiri Jeshi Mkuu

226. Tume ya Utumishi ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania

(b) Polisi wa Jamhuri ya Muungano227. Jeshi la Polisi wa Tanzania

228. Misingi ya utendaji wa Jeshi la Polisi

229. Uteuzi wa Mkuu wa Jeshi la Polisi

230. Majukumu na uhuru wa Mkuu wa Jeshi la Polisi

231. Tume ya Utumishi wa Jeshi la Polisi

232. Polisi wa Washirika wa Muungano

(e) Idara ya Usalama ya Jamhuri ya Muungano233. Kuanzishwa kwa Idara ya Usalama ya Taifa

234. Uteuzi wa Mkurugenzi wa Idara ya Usalama wa Taifa

235. Usalama wa Washirika wa Muungano

xii


______

NYONGEZA

_______

SURA YA KUMI NA SITA

M
ENGINEYO

236. Masharti kuhusu utaratibu wa kukabidhi madaraka

237. Masharti kuhusu madaraka ya kazi

238. Ufafanuzi

239. Jina la Katiba na kuanza kutumika

240. Kufutwa kwa Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya Mwaka 1977

1


UTANGULIZI

K
WA KUWA, Sisi,
Wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tumeamua

rasmi na kwa dhati kujenga katika nchi yetu jamii inayoheshimu na kuzingatia misingi ya

utu, uhuru, haki, usawa, udugu, amani, umoja na mshikamano katika nyanja zote za

maisha yetu;

N
A KWA KUWA,
tunaamini kuwa misingi hiyo inaweza tu kutekelezwa katika

jamii yenye mfumo wa demokrasia na utawala bora ambayo Serikali yake inasimamiwa

na Bunge lenye Wabunge waliochaguliwa na wanaowawakilisha wananchi na Mahakama

huru zinazotekeleza wajibu wa kutoa haki bila woga wala upendeleo wowote, na

kuhakikisha kuwa haki za binadamu zinalindwa na kudumishwa na kwamba wajibu wa

kila mtu unatekelezwa kwa uaminifu;

N
A KWA KUWA,
umuhimu wa kutunza mali ya Mamlaka za Nchi na ya pamoja,

kupiga vita aina zote za uharibifu, ubadhilifu, na kuhimiza matumizi bora na endelevu ya

rasilimali na maliasili zetu pamoja na kulinda na kuhifadhi mazingira yetu kwa

mustakabali wa maisha ya kizazi cha sasa na vizazi vijavyo;

N
A KWA KUWA,
umuhimu na faida za kujenga, kukuza na kuendeleza, amani,

umoja, urafiki na ushirikiano miongoni mwa Watanzania, Mataifa mbalimbali ya Afrika

na Dunia kwa ujumla;

K
WA KUWA,
azma ya kujenga Umoja wa Bara la Afrika katika misingi ya

Umajimui wa Afrika ambao inadhihirishwa na Muungano wa iliyokuwa Jamhuri ya

Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar;

N
A KWA KUENDELEZA
, dhamira yetu hiyo ni muhimu:

(a) kulinda, kuimarisha na kuudumisha Muungano wa nchi za Jamhuri ya

Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar;

(b) kujenga Taifa huru na linalojitegemea;

(c) kuimarisha na kuendeleza utawala wa sheria;

(d) kukuza na kuendeleza maadili, uwajibikaji na uwazi;

(e) kujenga umoja na mshikamano utakaowezesha kutimiza malengo ya kisiasa,

kiuchumi, kijamii, kimazingira na kulinda urithi kwa ujumla;

(f) kujenga na kuendeleza ukuu wa mamlaka ya watu;

(g) kujenga na kuendeleza utii wa mamlaka ya Katiba; na

(h) kuimarisha na kudumisha uzalendo kwa Taifa miongoni mwa Watanzania;

N
A KWA KUZINGATIA,
urithi tulioachiwa na Waasisi wa Taifa letu wa kujenga

nchi yenye Umoja wa Watu wake ambao hawabaguani kwa misingi ya ukabila, udini,

rangi, jinsi au ubaguzi wa aina nyingine yoyote;

N
A KWA KUZINGATIA,
uzoefu wa zaidi ya Miaka Hamsini ya Uhuru na Miaka

Hamsini ya Muungano wa Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar na

umuhimu wa ushiriki mpana na bayana wa wananchi katika utungaji wa Katiba ya

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania;

2


HIVYO BASI, KATIBA HII YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

ILIYOPENDEKEZWA NA BUNGE MAALUM LA KATIBA

imetungwa na SISI

WANANCHI WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

kupitia KURA

YA MAONI

kwa madhumuni ya kujenga jamii kama hiyo, na kuhakikisha kuwa Jamhuri

ya Muungano wa Tanzania inaongozwa na Serikali yenye kufuata misingi ya demokrasia

na utawala wa sheria, kujitegemea na isiyokuwa na dini.


3

SURA YA KWANZA

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

SEHEMU YA KWANZA

M
IPAKA, ALAMA, LUGHA, UTAMADUNI NA TUNU ZA TAIFA

Jamhuri ya

Muungano


1.-(

1) Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni Shirikisho lenye

mamlaka kamili ambayo imetokana na Muungano wa nchi mbili za

Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar ambazo kabla

ya Hati za Makubaliano ya Muungano ya mwaka 1964 zilikuwa nchi

huru.

(2) Jamhuri ya Muungano ni Shirikisho la kidemokrasia

linalofuata mfumo wa vyama vingi vya siasa, usawa wa binadamu
,

kujitegemea, utawala wa sheria na kuheshimu haki za binadamu.

(3) Hati ya Makubaliano ya Muungano iliyorejewa katika Ibara

ndogo ya (1), ndio msingi mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

na Katiba hii, kwa kadri itakavyorekebishwa, itakuwa ni mwendelezo wa

Makubaliano hayo.

Eneo la

Jamhuri ya

Muungano


2.

Eneo la Jamhuri ya Muungano ni eneo lote la Tanzania Bara

ikijumuisha sehemu yake ya bahari na eneo lote la Zanzibar ikijumuisha

sehemu yake ya bahari.

Alama na Siku

Kuu za Taifa


3.

-(1) Alama za Taifa ni:

(a) Bendera ya Taifa;

(b) Wimbo wa Taifa; na

(c) Nembo ya Taifa,

kama zitakavyoainishwa katika sheria itakayotungwa na Bunge.

(2) Siku Kuu za Kitaifa zitakuwa ni:

(a)Siku ya Uhuru wa Tanganyika, itakayoadhimishwa tarehe 9

Disemba;

(b)Siku ya Mapinduzi ya Zanzibar, itakayoadhimishwa tarehe 12

Januari;

(c)Siku ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar,

itakayoadhimishwa tarehe 26 Aprili; na

(d)Siku Kuu nyingine zitakazoainishwa na sheria za nchi.

(3) Kila Siku Kuu ya Kitaifa itakuwa ni siku ya mapumziko.

Lugha ya Taifa

na lugha za

alama


4.

-(1) Lugha ya Taifa ya Jamhuri ya Muungano ni Kiswahili na

itatumika katika mawasiliano rasmi ya kitaifa na kiserikali.

(2) Bila ya kuathiri masharti ya Ibara ndogo ya (1), lugha ya

Kiingereza inaweza kutumika kuwa lugha rasmi ya mawasiliano ya

kiserikali pale itakapohitajika.

(3) Serikali itaweka mazingira yatakayowezesha kuwepo kwa

mawasiliano ya lugha mbadala zikiwemo lugha za alama na nukta nundu

kwenye sehemu muhimu za umma na katika vyombo vya habari

vinavyotangaza habari zake kitaifa kwa ajili ya watu wenye mahitaji

maalum.


4

Tunu za Taifa

5. Jamhuri ya Muungano itaenzi na kuzingatia Tunu za Taifa

zifuatazo:

(a)utu;

(b) uzalendo;

(c)uadilifu;

(d)umoja;

(e)uwazi;

(f)uwajibikaji; na

(g)lugha ya Taifa.

SEHEMU YA PILI

M
AMLAKA YA WANANCHI, UTII NA HIFADHI YA KATIBA

Mamlaka ya

wananchi


6.

Jamhuri ya Muungano ni nchi inayofuata misingi ya

demokrasia inayozingatia haki ya kijamii, na kwa hiyo:

(a) wananchi ndio msingi wa mamlaka za nchi, na Serikali

itapata madaraka na mamlaka yake kutoka kwa wananchi

ambao kwa umoja na ujumla wao wanaimiliki na kuipatia

Katiba hii uhalali;

(b) lengo kuu la Serikali litakuwa ni maendeleo na ustawi wa

wananchi;

(c) Serikali itawajibika kwa wananchi; na

(d) wananchi watashiriki katika shughuli za Serikali kwa

mujibu wa masharti ya Katiba hii.

Watu na

Serikali


7

.-(1) Muundo wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano na vyombo

vyake, katika uendeshaji na utekelezaji wa shughuli zake utazingatia

azma ya kukuza umoja wa kitaifa na kudumisha heshima ya Taifa.

(2) Kwa madhumuni ya masharti ya Ibara ndogo (1), mamlaka

ya nchi na vyombo vyake vinawajibika kuelekeza sera na shughuli zake

zote kwa lengo la kuhakikisha kwamba:

(a)utu na haki nyingine zote za binadamu zinaheshimiwa na

kuthaminiwa;

(b)sheria za nchi zinasimamiwa na kutekelezwa;

(c)Serikali itahakikisha kuwa shughuli zinazofanywa

zinatekelezwa kwa njia ambazo zitahakikisha kwamba

utajiri wa Taifa unaendelezwa, unahifadhiwa na

unatumiwa kwa manufaa ya wananchi wote kwa jumla na

pia kuzuia mtu kumnyonya mtu mwingine;

(d)ardhi ikiwa rasilimali kuu na msingi wa Taifa, inalindwa,

inatunzwa na kutumiwa na wananchi wa Tanzania kwa

manufaa, maslahi na ustawi wa kizazi cha sasa na vizazi

vijavyo;

(e)maendeleo ya uchumi wa Taifa yanapangwa na kukuzwa

kwa ulinganifu na kwa pamoja na kwa namna ambayo

inawanufaisha wananchi wote;

(f)kila mtu mwenye uwezo wa kufanya kazi anafanya kazi,

na kazi maana yake ni shughuli yoyote ya halali

inayompatia mtu kipato chake;


5

(g)utu, heshima na haki nyingine zote za binadamu

zinahifadhiwa na kudumishwa kwa kuzingatia mila na

desturi za kitanzania na kwa kufuata mikataba mbalimbali

iliyoridhiwa na Jamhuri ya Muungano;

(h)mamlaka za nchi zinatoa fursa na haki zilizo sawa kwa

wananchi wote, wanawake na waume, bila ya kujali rangi,

kabila, nasaba, dini au hali ya mtu;

(i)aina zote za dhulma, vitisho, ubaguzi, unyanyasaji,

rushwa, uonevu au upendeleozinaondolewa nchini;

(j)utajiri wa rasilimali na maliasili za Taifa unaelekezwa

katika kuleta maendeleo, kuondoa umaskini, ujinga na

maradhi; na

(k)nchi inatawaliwa kwa kufuata misingi ya demokrasia na

kujitegemea.

Mamlaka na

utii wa Katiba


8.

-(1) Bila ya kuathiri masharti ya Katiba za Washirika wa

Muungano kwa mambo yasiyo ya Muungano, Katiba hii itakuwa sheria

kuu katika Jamhuri ya Muungano.

(2) Mtu yeyote, chombo, taasisi, jumuiya na wakala wowote wa

mamlaka ya nchi na mamlaka binafsi zinao wajibu wa kuzingatia

masharti ya Katiba hii na kuyatii.

(3) Sheria yoyote, mila, desturi au uamuzi wowote wa chombo

cha dola, ofisa wa Serikali au mtu binafsi ni sharti ufuate na kuendana na

masharti yaliyomo kwenye Katiba hii na kwamba, sheria, mila, desturi

au uamuzi wowote ambao hautawiana au kwenda sambamba na masharti

ya Katiba hii utakuwa batili.

Hifadhi ya

Katiba


9

.-(1) Mtu au kikundi cha watu hakitachukua au kushikilia

mamlaka ya nchi isipokuwa kwa mujibu wa Katiba hii.

(2) Kitendo chochote kinachokiuka masharti ya Ibara ndogo ya

(1) ni batili na ni kitendo cha uhaini kama itakavyoelezwa katika sheria

za nchi.

(3) Kwa madhumuni ya kuhifadhi masharti ya Ibara ndogo ya (1)

na (2), Serikali itaweka utaratibu wa kuisambaza Katiba hii kwa

wananchi na kuiweka katika mitaala ya elimu ili kuwezesha wananchi

kuifahamu, kuilinda na kuitii.

SURA YA PILI

M
ALENGO MUHIMU, MISINGI YA MWELEKEO WA

S
HUGHULI ZA SERIKALI NA SERA ZA KITAIFA

Utekelezaji wa

malengo ya

Taifa


10.

-(1) Malengo ya Taifa yaliyoainishwa ndani ya Katiba hii

yatakuwa ni mwongozo kwa Serikali, Bunge, Mahakama, vyama vya

siasa, taasisi, asasi na mamlaka nyingine na kwa kila mwananchi

katika matumizi au kutafsiri masharti ya Katiba hii au sheria nyingine

yoyote na katika utekelezaji wa uamuzi wa kisera kwa madhumuni ya

kujenga jamii huru, makini na iliyo bora.

(2) Serikali itatoa taarifa Bungeni si chini ya mara moja katika


6

kila mwaka, kuhusu hatua zilizochukuliwa na mamlaka ya nchi ili

kuhakikisha utekelezaji wa malengo ya Taifa yaliyoainishwa katika

Katiba hii.

Malengo

Makuu


11.

-(1) Lengo Kuu la Katiba hii ni kulinda, kuimarisha na

kudumisha udugu, amani, umoja na utengamanowa wananchi wa

Jamhuri ya Muungano kwa kuzingatia ustawi wa wananchi na kujenga

Taifa huru lenye demokrasia, utawala bora na kujitegemea.

(2) Bila ya kuathiri masharti ya Ibara ndogo ya (1), lengo hilo

kuu litaendelezwa na kuimarishwa katika nyanja zote kuu,

ikijumuisha nyanja za kisiasa, kiuchumi, kijamii, kiutamaduni na

kimazingira.

(3) Katika kutekeleza malengo ya Taifa ya:

(a) kisiasa, Serikali itachukua hatua zinazofaa ili –

(i) kuhakikisha kuwa inazuia, inapinga na kuondoa

dhulma, vitisho, ubaguzi, unyanyasaji, rushwa,

uonevu na upendeleo miongoni mwa wananchi

kwa misingi ya asili ya mtu, sehemu anayotoka,

nasaba,kabila, jinsi, dini au imani yake;

(ii) kuhakikisha uwepo wa amani na kujenga

utamaduni wa kuenzi, kuheshimu na kudumisha

amani, umoja na utengamano, ushirikiano na

uvumilivu wa kisiasa kwa madhumuni ya kukuza

maendeleo ya kijamii na kiuchumi;

(iii) kuhakikisha uwepo wa ulinzi, usalama na ustawi

wa watu na mali zao, na kuepuka kufanya jambo

lolote litakalohatarisha au kwenda kinyume na

lengo hilo;

(b) kijamii, Serikali inachukua hatua zinazofaa ili:

(i) kuhakikisha kwamba heshima ya binadamu

inahifadhiwa na kudumishwa kwa kufuata mila,

desturi na Kanuni za Tangazo la Dunia kuhusu

Haki za Binadamu na mikataba mingine ya

kimataifa iliyoridhiwa na Tanzania;

(ii) kuhakikisha kwamba Serikali na vyombo vyake

vyote vya umma vinatoa nafasi na fursa zilizo

sawa kwa raia wote, bila ya kujali rangi, kabila,

dini, nasaba, hali ya mtu au mahali alipo;

(iii) kujenga utamaduni wa kuwepo ushirikiano,

maelewano na maridhiano, uvumilivu na

kuheshimu mila, desturi na imani ya dini ya kila

mtu;

(iv) kuhakikisha kuwa msaada na hifadhi ya jamii

inatolewa kwa watu wasiojiweza, wazee,


7

wagonjwa, watoto na watu wenye ulemavu;

(c) kiuchumi, Serikali inachukua hatua zinazofaa ili:

(i) kuwaletea wananchi maisha bora kwa kuondoa

umaskini;

(ii) kuhakikisha kwamba shughuli za Serikali

zinatekelezwa kwa njia ambazo zitahakikisha

kuwa utajiri wa Taifa unaendelezwa,

unahifadhiwa na unatumiwa kwa manufaa ya

wananchi wote kwa jumla na pia kuzuia mtu

kumnyonya mtu mwingine;

(iii) kuweka mazingira bora kwa ajili ya kuanzisha na

kuendeleza vyombo vya uwakilishi wa wakulima,

wafugaji na wavuvi;

(iv) kuweka mazingira bora ya kufanya biashara na

kukuza fursa za uwekezaji;

(v) kuweka mazingira bora kwa ajili ya kukuza

kilimo, ufugaji na uvuvi kwa kuhakikisha kuwa

wakulima, wafugaji na wavuvi wanakuwa na

ardhi na nyenzo kwa ajili ya kuendeleza shughuli

zao;

(vi) kuweka mazingira bora ya uzalishaji wa mazao

kwa wakulima, wafugaji na wavuvi, utafutaji na

uendelezaji wa masoko ya mazao yao;

(vii) kuweka utaratibu mzuri wa upangaji na

usimamiaji wa mizania ya bei za mazao na

pembejeo;

(viii) kuimarisha na kuendeleza uwekezaji wa ndani,

upatikanaji wa pembejeo za kilimo, maeneo ya

ufugaji na vifaa vya uvuvi;

(ix) kuhakikisha kunakuwa na upatikanaji wa fursa na

nafasi za wazi kwa watu wote na kuanzisha

shughuli za kiuchumi na kukuza mazingira yaliyo

bora kwa ajili ya kuhamasisha sekta binafsi

katika uchumi;

(x) kuhakikisha kuwa kila mtu mwenye uwezo wa

kufanya kazi anapata fursa ya kufanya kazi, kwa

maana ya kufanya shughuli yoyote halali

inayompatia kipato;

(xi) kuweka utaratibu unaofaa kwa ajili ya

kufanikisha utekelezaji wa haki ya mtu kujipatia

elimu na kuwa huru kupata fursa sawa ya

kutafuta elimu katika fani anayoipenda hadi

kufikia upeo wowote kulingana na stahili na

uwezo wake;

(d) kiutamaduni, Serikali itachukua hatua zinazofaa ili:

(i) kulinda na kuhifadhi urithi wa asili, malikale na

sehemu zenye umuhimu wa kihistoria au kidini ili

kuepuka uharibifu, udhalilishaji na wizi au

utoroshwaji nje ya nchi;


8

(ii) kulinda, kuhifadhi na kuendeleza tamaduni za

watu wa jamii mbalimbali ambazo zinaendeleza

na kukuza utu na hadhi yao kwa namna ambayo

haikinzani na Misingi ya Kitaifa, na Malengo

Muhimu na Sera za Taifa;

(iii) kutambua, kulinda na kuendeleza lugha ya

Kiswahili; na

(e) kimazingira, Serikali itachukua hatua zinazofaa ili

kuhakikisha kuwa ni haki na jukumu la kila kizazi kulinda

na kudumisha mazingira kwa faida ya kizazi cha sasa na

vizazi vijavyo.

Sera kuhusu

Mambo

ya Nje


12.

Sera ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Muungano inalenga

nainazingatia maslahi ya Taifa na mamlaka kamili ya nchi na kwamba

sera hiyo inatekelezwa kwa uwazi ili:

(a) kukuza ushirikiano wa kikanda na ushirikiano wa

kimataifa;

(b) kukuza ushirikiano wa kiuchumi wenye tija kwa Taifa;

(c) kuleta maendeleo ya kiuchumi kwa mataifa ya Afrika

kwa kushiriki katika hatua mbalimbali za mtangamano

wa kiuchumi wa kikanda;

(d) kuheshimu sheria za kimataifa;

(e) kuzingatia mikataba ya kimataifa, mikataba ya kikanda

yenye maslahi kwa Jamhuri ya Muungano na kutatua

migogoro ya kimataifa kwa njia ya majadiliano,

usuluhishi, maridhiano na mahakama;

(f) kukuza uzingatiaji wa haki za binadamu na uhuru wa

watu;

(g) kupambana na makosa ya kimataifa ya kijinai; na

(h) kuheshimu uhuru wa mataifa mengine.

SURA YA TATU

MAADILI NA MIIKO YA UONGOZI NA UTUMISHI WA UMMA

SEHEMU YA KWANZA

M
AADILI YA VIONGOZI WA UMMA

Dhamana ya

Uongozi wa

Umma


13.

-(1) Madaraka anayopewa kiongozi wa umma:

(a) ni dhamana na atatumia madaraka hayo na kutekeleza

wajibu wake kwa:

(i) kuzingatia masharti ya Katiba hii;

(ii) kuheshimu wananchi;

(iii) namna inayokuza hadhi ya taifa na kulinda

heshima ya ofisi anayoitumikia; na

(iv) kukuza imani na heshima ya ofisi kwa

wananchi;

(b) yanatoa wajibu kwa kiongozi kuwatumikia wananchi.

(2) Dhamana ya uongozi na heshima kwa kiongozi wa umma

itazingatia mambo yafuatayo:


9

(a) uteuzi kwa misingi ya mwenendo wa mtu, uwezo, sifa

au uchaguzi uliyo huru na haki;

(b) uwezo pasipo upendeleo katika kufanya uamuzi na

kuhakikisha kwamba uamuzi haufuati udugu, ukabila,

udini, upendeleo, rushwa au vigezo vingine visivyo

sahihi;

(c) utoaji wa huduma pasipo upendeleo na kwa kufuata

maslahi ya umma kwa kuonyesha-

(i) uaminifu katika utekelezaji wa kazi za umma;

(ii) wajibu wa kutangaza maslahi binafsi ili kuepuka

mgongano wa maslahi;

(d) uwajibikaji kwa umma katika kufanya uamuzi na

vitendo; na

(e) nidhamu na kujituma katika kutoa huduma kwa umma.

Kanuni za

Uongozi wa

Umma


14.

-(1) Kiongozi wa umma, akiwa ama katika kazi za ofisi au

kazi binafsi au wakati amejumuika na watu wengine, atahakikisha

kwamba mwenendo wake:

(a) hauruhusu kutokea mgongano wa maslahi kati ya

maslahi binafsi na maslahi ya utumishi wa umma;

(b) hauhatarishi maslahi ya umma kwa ajili ya maslahi

binafsi; au

(c) haushushi hadhi ya ofisi anayofanyia kazi.

(2) Kwa madhumuni ya Ibara ndogo ya (1), mamlaka ya nchi

itaweka utaratibu wa sheria utakaowezesha Tume ya Maadili ya

Uongozi na Uwajibikaji kusimamia utekelezaji wa masharti

yanayohusu kanuni za uongozi wa umma.

(3) Wadhifa “Kiongozi wa Umma” kama ulivyotumika katika

Sehemu hii utajumuisha viongozi wa kuchaguliwa na kuteuliwa kama

watakavyoainishwa kwenye sheria itakayotungwa na Bunge.

Zawadi katika

Utumishi wa

Umma


15.

-(1) Zawadi au kitu chochote kitakachotolewa kwa

mtumishi wa umma katika shughuli za kiserikali ni zawadi kwa

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na itawasilishwa kwa Katibu

Mkuu Kiongozi kupitia kwa Katibu Mkuu wa Wizara au taasisi ya

Serikali inayohusika, akiainisha:

(a) aina ya zawadi;

(b) thamani ya zawadi;

(c) sababu ya kupewa zawadi; na

(d) mtu au mamlaka iliyotoa zawadi hiyo.

(2) Mtumishi wa Umma -

(a) hatafungua au kuendesha akaunti ya benki nje ya

Jamhuri ya Muungano isipokuwa tu kwa namna

ambayo sheria za nchi zinaruhusu; na

(b) hataomba au kupokea mkopo au faida yoyote kwa

namna au mazingira ambayo yanashusha hadhi au

heshima ya mtumishi wa umma.


10

(3) Bunge litatunga sheria itakayosimamia, pamoja na mambo

mengine, thamani, kiwango, aina na uhifadhi wa zawadi inayohusika

na masharti ya Sehemu hii na masharti mengine yanayohusu

utekelezaji wa masharti ya Ibara hii.

Wajibu wa

kutangaza mali

na madeni


16.

-(1) Kiongozi wa Umma atalazimika kutangaza, ndani ya

siku thelathini baada ya kupata uongozi na baada ya kuacha uongozi,

mali na thamani zake na madeni yake katika Tume ya Maadili na

Uwajibikaji.

(2) Bila ya kuathiri masharti ya Ibara ndogo ya (1), Kiongozi

wa Umma atalazimika kutangaza mali zake na madeni:

(a) yake binafsi;

(b) ya mwenza wake wa ndoa; na

(c) watoto wake walio chini ya umri wa miaka kumi na nane,

mara moja kila mwaka, au kadri itakavyoamuliwa na sheria.

Mgongano wa

kimaslahi


17.

-(1) Kiongozi wa Umma hatashiriki katika jambo au

shughuli yoyote ambayo ana maslahi nayo yeye binafsi, mwenza

wake, mtoto wake, jamaa yake, rafiki au mtu yeyote wake wa karibu.

(2) Kiongozi wa umma hatozungumzia kitu chochote katika

Baraza la Mawaziri, Bunge, kamati au chombo kingine chochote

rasmi ambacho ana maslahi nacho ya moja kwa moja au vinginevyo,

isipokuwa tu kama atatoa taarifa ya mgongano huo wa maslahi katika

vyombo hivyo.

(3) Itakuwa ni marufuku kwa Kiongozi yeyote wa Umma,

kushiriki kuongeza au kwa namna yoyote ile, kuboresha maslahi

yanayohusu wadhifa alionao, na endapo atashiriki, basi masharti hayo

mapya yataanza kutumika kwa Kiongozi atakayekuja baada ya yeye

kuondoka au kumaliza muda wa kukaa madarakani.

(4) Bunge litatunga sheria itakayosimamia, pamoja na mambo

mengine, masuala ya:

(a) ngazi au orodha ya Viongozi wa Umma, wanaopaswa

kutangaza mali zao;

(b) utaratibu wa utwaaji wa mali za Viongozi wa Umma

zilizopatikana kwa njia za ukiukaji wa sheria;

(c) utaratibu wa kumwajibisha Kiongozi wa Umma aliyeenda

kinyume na maadili na Miiko ya Uongozi;

(d) uanzishaji wa mitaala inayohusu maadili na uraia,

mashuleni na vyuoni; na

(e) uanzishaji wa mitaala inayohusu Katiba mashuleni na

vyuoni.

(5) Kiongozi wa Umma hataruhusiwa kushika nyadhifa mbili

au zaidi au kutumikia Mihimili ya Dola zaidi ya mmoja kwa wakati

mmoja.

Matumizi ya

mali ya umma


18.

Haitaruhusiwa kwa Kiongozi yeyote wa Umma kutumia au

kuruhusu kutumika kwa mali yoyote ya umma, zikiwemo

zilizokodishwa kwa Serikali, kwa madhumuni ya kumpatia yeye

binafsi au mtu mwingine yeyote manufaa ya kiuchumi.


11

Matumizi ya

masharti ya

maadili kwa

Watumishi wa

Umma


19.

Masharti yaliyoainishwa katika Ibara za 13 mpaka 18

yatatumika pia kwa watumishi wa umma baada ya kufanyiwa

marekebisho stahiki.

SEHEMU YA PILI

M
IIKO YA UONGOZI WA UMMA

Utii wa Miiko

ya Uongozi wa

Umma


20

.-(1) Bila ya kuathiri masharti yoyote ya Katiba hii, kiongozi

yeyote wa Umma atapaswa kuheshimu na kutii maadili ya viongozi

wa umma, ikiwemo Miiko ya Uongozi.

(2) Miiko ya Uongozi inayorejewa katika Ibara ndogo (1),

itakuwa kama ifuatavyo:

(a) Kiongozi wa umma hatopaswa:

(i) kuvunja au kukiuka masharti ya Katiba ya

Jamhuri ya Muungano;

(ii) kutoa au kupokea rushwa;

(iii) kujilimbikizia mali kinyume cha sheria;

(iv) kusema uongo au kutoa taarifa zisizo za ukweli;

(v) kutoa siri za Serikali kinyume na sheria;

(vi) kutumia wadhifa, nafasi au cheo chake kwa

manufaa yake binafsi, familia yake, ndugu, jamaa

au marafiki zake au mtu yeyote aliye na uhusiano

naye wa karibu;

(vii) kufanya vitendo vya uzembe, uvivu, ubaguzi,

kiburi, dharau au unyanyasaji wa kijinsia.

(b)Kiongozi wa umma atapaswa:

(i) kuheshimu na kuendeleza dhana ya uwajibikaji

wa pamoja, kwa viongozi wanaohusika; na

(ii) kuheshimu na kuendeleza maadili ya viongozi wa

umma, ikijumuisha:

(aa) kuwa na tabia na mienendo inayokubalika

katika jamii;

(bb) kuheshimu, kutunza na kulinda mali za

umma; na

(cc) kutambua, kuheshimu na kuzingatia

Kanuni za Maadili na Mienendo ya

Watumishi wa Umma, Kanuni za Kudumu

za Watumishi wa Umma, nyaraka za

umma na miongozo mbalimbali ya Serikali

kuhusu viongozi na watumishi wa umma.

(iii) kutenganisha shughuli za biashara na masuala

yanayohusiana na uongozi.

(3) Kiongozi yeyote wa umma ambaye anatuhumiwa na

kuthibitika kwa makosa ya:

(a) kimaadili;

(b) udhalilishaji wa mtu au wa kijinsia; na

(c) wizi au ubadhirifu wa mali za umma,


12

atasimamishwa kazi mpaka suala lake litakapoamuliwa kwa mujibu

wa sheria au taratibu nyingine zinazowahusu viongozi wa umma.

Marufuku

baadhi ya

vitendo


21

.-(1) Mtumishi wa umma aliye katika ajira ya kudumu

hataruhusiwa kuingia katika ajira nyingine yoyote yenye malipo ya

mshahara.

(2) Mtumishi wa umma haruhusiwi kuchaguliwa au kuteuliwa

kushika madaraka katika chama cha siasa.

(3) Mtumishi wa umma aliyestaafu na anayepokea malipo ya

pensheni kutokana na fedha za umma haruhusiwi kuwa mwenyekiti,

mkurugenzi au mtumishi zaidi ya vipindi viwili katika:

(a) shirika au kampuni inayomilikiwa au kuendeshwa kwa

fedha za umma; au

(b) chombo chochote cha umma.

SURA YA NNE

HAKI ZA BINADAMU, WAJIBU WA RAIA NA MAMLAKA ZA NCHI

SEHEMU YA KWANZA

H
AKI ZA BINADAMU

Uhuru, utu na

usawa wa

binadamu


22.

-(1) Binadamu wote huzaliwa huru na wote ni sawa.

(2) Kila mtu anayo haki ya kuheshimiwa, kutambuliwa na

kuthaminiwa utu wake.

Haki ya

kuishi


23.

Kila mtu anayo haki ya kuishi na kupata hifadhi ya maisha

yake kutoka katika Serikali na jamii kwa mujibu wa sheria.

Marufuku

kuhusu

ubaguzi


24.

-(1) Watu wote ni sawa mbele ya sheria na wanayo haki ya

kulindwa na kupata haki sawa mbele ya sheria.

(2) Ni marufuku kwa mtu yeyote kubaguliwa na mtu, mamlaka ya

nchi au mamlaka yoyote inayotekeleza madaraka yake chini ya sheria

yoyote au katika kutekeleza kazi au shughuli yoyote ya mamlaka ya nchi.

(3) Ni marufuku kwa sheria yoyote iliyotungwa na mamlaka

yoyote katika Jamhuri ya Muungano kuweka sharti lolote ambalo ni la

ubaguzi ama wa dhahiri au kwa taathira yake.

(4) Haki ya raia, wajibu na maslahi ya kila mtu na jumuiya ya

watu yatalindwa na kuamuliwa na mahakama na vyombo vinginevyo vya

mamlaka ya nchi vilivyowekwa kwa mujibu wa sheria.

(5) Kwa madhumuni ya masharti ya Ibara hii na kwa kuzingatia

masharti ya Ibara ndogo ya (4), neno “kubagua” maana yake ni kutimiza

utashi, haki au mahitaji mengineyo kwa watu mbalimbali kwa kuzingatia

utaifa wao, kabila, mahala walipotokea, maoni yao ya kisiasa, rangi, dini,

jinsi au hali yao ya maisha kwa namna ambayo watu wa aina fulani

wanafanywa au kuhesabiwa kuwa dhaifu au duni na kuwekewa vikwazo

au masharti ya vipingamizi ambapo watu wa aina nyingine wanatendewa

tofauti au wanapewa fursa au faida iliyoko nje ya masharti au sifa za

lazima.


13

(6) Neno “kubagua” lilivyotumiwa katika Ibara ndogo ya (2),

halitafafanuliwa kwa namna ambayo itaizuia mamlaka ya nchi kuchukua

hatua za makusudi zenye lengo la kurekebisha matatizo mahsusi katika

jamii.

(7) Kwa madhumuni ya kuhakikisha usawa mbele ya sheria,

mamlaka ya nchi itaweka utaratibu unaofaa na unaozingatia misingi

kwamba -

(a) wakati haki na wajibu kwa mtu yeyote vinapohitajika

kufanyiwa uamuzi na mahakama au mamlaka nyingine

inayohusika, basi mtu huyo atakuwa na haki ya kupewa

fursa ya kusikilizwa kwa ukamilifu, na pia atakuwa na haki

ya kukata rufani au kupata nafuu nyingine ya kisheria

kutokana na uamuzi wa mahakama au mamlaka nyingine

inayohusika;

(b) ni marufuku kwa mtu aliyeshtakiwa kwa kosa la jinai

kutendewa kama mtu aliyehukumiwa kwa kutenda kosa

hilo hadi itakapothibitika mahakamani kuwa anayo hatia

ya kutenda kosa hilo;

(c) ni marufuku kwa mtu kuadhibiwa kwa sababu ya kitendo

chochote ambacho wakati alipotenda kitendo hicho

hakikuwa ni kosa chini ya sheria;

(d) ni marufuku kwa mtu kupewa adhabu ambayo ni kubwa

kuliko adhabu iliyokuwapo wakati kosa linalohusika

lilipotendeka;

(e) kwa ajili ya kuhifadhi haki ya usawa wa binadamu,

heshima ya mtu na faragha itahifadhiwa katika shughuli

zote zinazohusu upelelezi wa tuhuma na uendeshaji wa

masharti ya jinai na katika shughuli nyingine ambazo mtu

anakuwa katika kizuizi cha mamlaka ya nchi au katika

kuhakikisha utekelezaji wa adhabu; na

(f) ni marufuku kwa mtu kuteswa, kuadhibiwa kinyama au

kupewa adhabu zinazotweza au kudhalilisha.

Haki ya

kutokuwa

mtumwa


25.

-(1) Kila mtu ana haki ya kutotendewa au kutotumikishwa kama

mtumwa, kutofanyishwa kazi za kulazimishwa au kutweza, na kwa msingi

huo, ni marufuku kwa mtu:

(a)kufanywa au kutendewa kama mtumwa;

(b)kulazimishwa kufanya kazi bila hiyari yake; au

(c)kusafirishwa kwa nia ya kufanyiwa biashara au faida ya mtu

mwingine.

(2) Biashara ya kusafirisha binadamu ni marufuku katika Jamhuri

ya Muungano.

Uhuru wa mtu

binafsi


26

.-(1) Kila mtu anayo haki ya kuwa huru na kuishi akiwa mtu

huru.

(2) Kwa madhumuni ya kuhifadhi haki ya mtu kuwa huru na

kuishi kwa uhuru, itakuwa ni marufuku kwa mtu yeyote kukamatwa,

kufungwa, kufungiwa, kuwekwa kizuizini, kuhamishwa kwa nguvu au

kunyang’anywa uhuru wake vinginevyo, isipokuwa tu katika

14


(a)hali na kwa kufuata utaratibu uliowekwa na sheria; au

(b)kutekeleza hukumu, amri au adhabu iliyotolewa na

mahakama kutokana na shauri au kutiwa hatiani kwa kosa la

jinai.

Haki ya

faragha na

usalama wa

mtu


27.

-(1) Kila mtu anastahili kuheshimiwa na kupata hifadhi kwa

nafsi yake, maisha yake binafsi na familia yake na nyumbani kwake,

kutoteswa au kudhalilishwa, na pia heshima na hifadhi ya maskani yake na

mawasiliano yake ya binafsi.

(2) Kwa madhumuni ya kuhifadhi haki ya mtu, mamlaka ya nchi

itaweka utaratibu wa sheria kuhusu hali, namna na kiasi ambacho haki ya

mtu ya faragha na ya usalama wa nafsi yake, mali na maskani yake,

yanaweza kuingiliwa bila ya kuathiri masharti ya Ibara hii.

Uhuru wa mtu

kwenda

anakotaka


28.

-(1) Kila raia anayo haki ya kwenda kokote katika Jamhuri ya

Muungano wa Tanzania na kuishi katika sehemu yoyote, kutoka nje ya

nchi na kuingia, na pia haki ya kutoshurutishwa, kuhama au kufukuzwa

kutoka katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

(2) Kitendo chochote halali au sheria yoyote yenye madhumuni

ya -

(a) kupunguza uhuru wa mtu kwenda anakotaka na kumweka

chini ya ulinzi au kifungoni; au

(b) kuweka mipaka kwa matumizi ya uhuru wa mtu kwenda

anakotaka ili-

(i) kutekeleza hukumu au amri ya mahakama;

(ii) kumlazimisha kutimiza kwanza wajibu wowote

anaotakiwa na sheria nyingine kuutimiza; au

(iii) kulinda manufaa ya umma kwa jumla au

kuhifadhi maslahi fulani mahsusi au maslahi ya

sehemu fulani ya umma,

hakitahesabiwa au sheria hiyo haitahesabiwa kuwa ni kinyume cha

masharti ya Ibara hii.

Uhuru wa

maoni


29.

-(1) Kila mtu:

(a) anao uhuru wa-

(i) kuwa na maoni na kueleza fikra zake;

(ii) kufanya mawasiliano na vile vile anayo haki ya

kutoingiliwa katika mawasiliano yake;

(iii) ubunifu na sanaa;

(iv) kitaaluma na tafiti za kisayansi; na

(b) anayo haki ya kupewa taarifa wakati wowote kuhusu:

(i) matukio mbalimbali muhimu kwa maisha na

shughuli za wananchi; na

(ii) utekelezaji wa mamlaka ya nchi kuhusu sera za

kitaifa na shughuli ya maendeleo ya jamii; na

(iii) masuala mengine muhimu kwa jamii.

(2) Utekelezaji wa haki zilizoainishwa katika Ibara ndogo ya (1),

utajumuisha wajibu muhimu kwa mwananchi na wajibu huo unaweza

kupunguza haki hizo kutokana na:


15

(a) vita au machafuko ya kisiasa; au

(b) propaganda kuhusu vita, ushawishi wa chuki kwa misingi

ya rangi, ukabila, ubaguzi wa kijinsia, dini au masuala

yoyote yanayoweza kuleta madhara kwa Taifa.

Uhuru wa

habari na

vyombo vya

habari


30

.-(1) Kila mtu anao uhuru wa-

(a) kutafuta, kupata na kutumia habari na taarifa na

kusambaza taarifa hizo; na

(b) kuanzisha vyombo vya habari na njia nyingine za

upashanaji wa habari bila kujali mipaka ya nchi.

(2) Vyombo vya habari vitakuwa huru na vile vile vitakuwa na:

(a)haki ya kupata, kutumia na kusambaza habari na taarifa

wanazopata;

(b)wajibu wa:

(i) kusambaza habari na taarifa kwa wananchi; na

(ii) kuheshimu na kulinda utu, heshima, uhuru na staha

ya wananchi dhidi ya habari na taarifa

wanazozitumia, wanazozitayarisha na kuzisambaza.

(3) Serikali na taasisi zake, asasi za kiraia na watu binafsi

watakuwa na wajibu wa kutoa habari kwa umma juu ya shughuli na

utekelezaji wa shughuli zao.

(4) Masharti ya Ibara hii yatalazimika kuzingatia masharti ya

sheria ya nchi itakayotungwa kwa ajili hiyo na kwa madhumuni ya

kulinda usalama wa Taifa, amani, maadili ya umma, haki, staha na uhuru

wa watu wengine.

Uhuru wa

imani ya dini


31.

-(1) Kila mtu anao uhuru wa mawazo, imani na uchaguzi

katika mambo ya imani ya dini na anao uhuru pia wa kubadilisha dini,

imani yake au kutokuwa na imani na dini.

(2) Kazi ya kutangaza dini, kufanya ibada na kueneza dini itakuwa

ni huru na jambo la hiari kwa mtu binafsi ili mradi asivunje sheria za nchi.

(3) Shughuli ya uendeshaji wa jumuiya za dini itakuwa nje ya

shughuli za mamlaka ya Serikali.

(4) Hifadhi ya haki zilizotajwa katika Ibara hii itakuwa chini ya

taratibu zilizowekwa na sheria ambazo ni muhimu katika jamii ya

kidemokrasia kwa ajili ya usalama, amani, maadili na umoja wa jamii na

wa kitaifa na vitasimamiwa kwa utaratibu ulioainishwa kwenye sheria za

nchi.

(5) Ni marufuku kwa mtu, kikundi au taasisi ya dini kutumia uhuru

wa kutangaza dini kwa kukashifu imani na dini nyingine, kujenga chuki au

kuchochea vurugu na ghasia kwa madai ya kutetea imani au dini.

(6) Dini na imani ya dini haitatumika kwa namna yoyote

itakayowagawa wananchi, kuleta uhasama au kuharibu amani miongoni

mwa wananchi.

(7) Neno “dini” kama lilivyotumika katika Ibara hii litatafsiriwa

kwamba maana yake ni pamoja na madhehebu ya dini, na maneno

mengine yanayofanana au kuambatana na neno hilo nayo yatatafsiriwa

kwa maana hiyo.


16

Uhuru wa mtu

kujumuika na

kushirikiana

na

wengine


32.

Kila mtu anastahili kuwa huru, bila ya kuathiri sheria za nchi,

kukutana na watu wengine kwa hiari yake na kwa amani, kujumuika na

kushirikiana na watu wengine, kutoa mawazo hadharani, na hasa zaidi

kuanzisha au kujiunga na vyama au mashirika yaliyoanzishwa kwa

madhumuni ya kuhifadhi au kuendeleza imani au maslahi yake au maslahi

mengineyo.

Uhuru wa

kushiriki

shughuli

za umma


33.-

(1) Kila raia wa Jamhuri ya Muungano ana haki ya kushiriki

katika shughuli za utawala wa nchi, ama moja kwa moja au kwa kupitia

wawakilishi waliochaguliwa na wananchi kwa hiari yao, kwa kuzingatia

utaratibu uliowekwa kwa mujibu wa sheria.

(2) Kila raia ana haki na uhuru wa kushiriki kwa ukamilifu katika

kufikia uamuzi juu ya mambo yanayomhusu yeye, maisha yake au

yanayolihusu Taifa.

Haki ya

kufanya kazi


34.

-(1) Kila mtu ana haki ya kufanya kazi ya kuajiriwa au kujiajiri

mwenyewe.

(2) Kila mtu ana haki na fursa sawa kushika nafasi yoyote ya

kazi, uongozi au shughuli yoyote iliyo chini ya mamlaka ya nchi.

Haki za

wafanyakazi

na waajiri


35.

-(1) Kila mfanyakazi ana haki zifuatazo:

(a) kufanya kazi bila ubaguzi wa aina yoyote;

(b) kupata ujira na malipo halali kulingana na kiasi na sifa za kazi

anayofanya;

(c) kuunda au kujiunga na chama cha wafanyakazi mahala pa

kazi; na

(d) kushiriki katika shughuli za chama cha wafanyakazi;

(2) Kila chama cha waajiri na wafanyakazikitakuwa na haki ya:

(a)kuamua kuhusu uongozi, programu na shughuli zake; na

(b)kuanzisha, kujiunga na kusimamia shirikisho lao.

(3) Kila chama cha wafanyakazikitakuwa na haki ya kufanya

majadiliano ya pamoja na mwajiri na kuingia mikataba ya hali bora ya kazi.

(4) Bunge litatunga sheria itakayoweka masharti kuhusu haki za

wafanyakazi na utaratibu utakaowezesha wafanyakazi kutumia haki zao.

Haki ya

kumiliki mali


36.

-(1) Kila mtu anayo haki ya kumiliki mali na hifadhi ya mali

yake aliyonayo kwa mujibu wa sheria.

(2) Bila ya kuathiri masharti ya Ibara ndogo ya (1), itakuwa ni

marufuku kwa mtu yeyote kunyang’anywa mali yake kwa madhumuni ya

kuitaifisha au madhumuni mengine bila malipo yanayolingana na thamani

halisi ya mali hiyo na yatakayotolewa mapema.

(3) Kwa madhumuni ya masharti ya Ibara hii, haki ya umiliki na

hifadhi ya mali haitahusu mali iliyothibitishwa kwamba haikupatikana

kwa njia halali.

Haki ya uraia

37. Kila raia ana haki ya kutambuliwa uraia wake na kwa

madhumuni haya, mamlaka ya nchi itaweka utaratibu wa sheria

utakaowezesha wananchi kupata hati ya kuzaliwa, kitambulisho cha uraia


17

wake bila ya upendeleo na ubaguzi wa aina yoyote, na pale inapohitajika,

nyaraka za kumwezesha kusafiri.

Haki ya

mtuhumiwa

na mfungwa


38.

-(1) Mtu aliyekamatwa au aliyewekwa kizuizini anayo haki ya:

(a) kuelezwa kwa lugha anayoifahamu -

(i) sababu ya kukamatwa;

(ii) haki ya kutokutoa maelezo yoyote; na

(iii) matokeo ya kutoa maelezo;

(b) kutoa maelezo;

(c)kuwasiliana na wakili na mtu mwingine ambaye msaada wake

ni muhimu kwa mtuhumiwa;

(d)kutolazimishwa kutoa maelezo ya kukiri kosa ambayo

yatatumika kama ushahidi dhidi yake; na

(e) kupelekwa mahakamani mapema iwezekanavyo.

(2) Mamlaka za nchi zitaweka utaratibu wa sheria utakaowezesha:

(a) mtuhumiwa kupata nakala ya mashtaka yanayomkabili na

kumbukumbu ya mwenendo wa mashtaka;

(b) mtuhumiwa au mfungwa kupata nakala ya mwenendo wa

mashtaka baada ya shauri kukamilika mahakamani;

(c) mtuhumiwa au mfungwa kufikishwa mahakamani ili

kuthibitisha uwepo wake.

Haki ya

watu waliyo

chini ya

ulinzi


39

.-(1) Mtu aliye katika kizuizi au ulinzi ataendelea kuwa na haki

zote za msingi zilizoainishwa katika Katiba hii kwa kiwango anachostahiki

katika mazingira ya kuwekwa kizuizini au katika ulinzi.

(2) Mtu aliye katika kizuizi au ulinzi ana haki ya kuiomba

mahakama ili mamlaka ya nchi inayomuhifadhi kueleza sababu za yeye

kuwekwa au kuendelea kuwa katika kizuizi au ulinzi.

(3) Raia wa Jamhuri ya Muungano hatapelekwa katikanchi ya nje

yoyote kujibu mashtaka au kufanyiwa mahojiano ya aina yoyote kinyume

cha ridhaa yake.

Uhuru na haki

ya mazingira

safi na salama


40.

-(1) Kila mtu anayeishi katika Jamhuri ya Muungano ana haki

ya kuishi katika mazingira safi, salama na ya kiafya.

(2) Haki ya kuishi katika mazingira safi, salama na ya kiafya

inahusisha haki kwa kila raia kutumia maeneo ya umma au sehemu

mbalimbali za mazingira yaliyotengwa kwa madhumuni ya burudani,

elimu, afya, ibada, utamaduni na shughuli za kiuchumi.

(3) Mtu yeyote anayeishi Tanzania anao wajibu wa kutunza na

kuendeleza mazingira na kutoa taarifa kwa mamlaka za nchi kuhusu

shughuli au jambo lolote ambalo ni hatarishi au linauwezekano mkubwa

wa kuharibu au kuathiri mazingira.

Haki ya elimu

na kujifunza


41.-

(1) Kila mtu ana haki ya:

(a) kupata fursa ya kupata elimu bila ya vikwazo;


18

(b)kupata elimu bora ya msingibila ya malipo na inayomtayarisha

kikamilifu mwanafunzi ama kuendelea na elimu ya ngazi

inayofuatia au kuweka msingi wa kuanza kujitegemea;

(c)kwa elimu inayotolewa nje ya utaratibu wa umma, kupata

elimu kwa gharama nafuu; na

(d)kupata fursa sawa ya kupata elimu ya juu ili mradi ana sifa

stahiki kupata elimu hiyo,

bila ya ubaguzi wa aina yoyote.

(2) Kwa madhumuni ya Ibara ndogo ya (1), kila mtu ana haki ya

kuchagua taaluma na ajira anayoitaka kwa mujibu wa elimu yake na ujuzi

aliyonao.

Haki ya

mtoto


42.-

(1) Kila mtoto ana haki ya-

(a) kupewa jina na uraia;

(b) kutoa mawazo, kusikilizwa na kulindwa dhidi ya uonevu,

ukatili na udhalilishaji;

(c) kucheza na kupata elimu;

(d) kuhifadhiwa katika mazingira mazuri, kwa walio katika

ukinzani na sheria;

(e) kupata lishe bora, makazi na huduma ya afya; na

(f) kushiriki katika shughuli zinazolingana na umri alionao; na

(g) kupata malezi na ulinzi wa wazazi, walezi au mamlaka ya

nchi,

bila ya ubaguzi wa rangi, utaifa, lugha, mtazamo wa kisiasa, jamii

anayotokea, mali, uzazi, kabila, dini, jinsi au aina nyingine za hadhi.

(2) Mamlaka ya nchi itaweka utaratibu wa sheria utakaowezesha

utekelezaji na usimamizi wa haki za mtoto kwa kufuata msingi wa kutoa

kipaumbele kwa maslahi na manufaa ya mtoto.

Haki na

wajibu wa

vijana


43.

Kila kijana ana haki na wajibu wa kushiriki kikamilifu katika

shughuli za maendeleo ya Jamhuri ya Muungano pamoja na jamii kwa

ujumla, na kwa mantiki hiyo, Serikali ya Jamhuri ya Muungano, Serikali

za Washirika wa Muungano na jamii zitahakikisha kuwa vijana

wanawekewa mazingira mazuri ya kuwa raia wema na kupatiwa fursa za

kushiriki kikamilifu katika nyanja za kisiasa, kiuchumi,kijamii na

kiutamaduni.

Haki za

watu wenye

ulemavu


44

.-(1) Mtu mwenye ulemavu anastahiki:

(a) kuheshimiwa, kutambuliwa na kutendewa kwa namna

ambayo haishushi utu wake;

(b) kupata elimu kwa kutumia vifaa maalum na kushiriki

katika shughuli za kijamii;

(c) kuwekewa miundombinu na mazingira yatakayowezesha

kwenda anapotaka, kutumia vyombo vya usafiri na kupata

habari;

(d) kutumia lugha za alama, maandishi ya nukta nundu au njia

nyingine zinazofaa;


19

(e) haki ya kusoma na kuchanganyika na watu wengine; na

(f) haki ya kupata ajira na kugombea nafasi za uongozi katika

nyadhifa mbalimbali kwa usawa.

(2) Mamlaka ya nchi itaweka utaratibu wa sheria utakaowezesha

watu wenye ulemavu kushiriki katika nafasi za uwakilishi.

Haki za

makundi

madogo

katika jamii


45

.-(1) Mamlaka ya nchi itaweka utaratibu wa sheria

utakaowezesha makundi madogo katika jamii:

(a) kushiriki katika uongozi wa mamlaka za nchi;

(b) yanapewa fursa maalum za elimu na fursa za kujiendeleza

kiuchumi na fursa za ajira;na

(c) kutengewa maeneo ya ardhi ambayo kwa desturi makundi

hayo kuitumuia kama eneo la kuishi na kupata riziki ya

chakula.

(2) Serikali na mamlaka za nchi zitachukua hatua za makusudi za

kukuza na kuendeleza shughuli za kiuchumi na kuweka miundombinu ya

makazi, elimu na afya kwa ajili ya kizazi cha sasa na vijavyo vya jamii ya

watu walio katika makundi madogo.

Haki za

wanawake


46

.-(1) Kila mwanamke ana haki ya:

(a) kuheshimiwa utu wake;

(b)kuwa salama dhidi ya unyonyaji na ukatili;

(c)kushiriki bila ya ubaguzi katika chaguzi na ngazi zote za

maamuzi;

(d)kupata ujira sawa na mwanaume katika kazi;

(e)kulindwa dhidi ya ubaguzi, uonevu na mila zenye madhara;

(f) kulindwa kwa ajira yake wakati wa ujauzito na pale

anapojifungua; na

(g)kupata huduma ya juu ya afya inayopatikana.

(2) Mamlaka husika za nchi zitaweka utaratibu wa kisheria

utakaosimamia masuala yanayohusu utekelezaji wa masharti ya Ibara hii

ikiwa ni pamoja na kukuza utu, usalama na fursa za wanawake wakiwemo

wajane.

Haki za

wazee


47

. Mamlaka ya nchi itaweka utaratibu utakaowezesha wazee

kupata fursa ya:

(a) kushiriki katika shughuli za kijamii;

(b) kuendeleza maisha yao;

(c) kutambuliwa utu wao na kuheshimiwa pasipo

kudharauliwa;

(d) kulelewa na kupata misaada kutoka katika familia zao,

jamii na mamlaka ya nchi; na

(e) kupewa fursa ya kuendelea kutumia utaalamu na ujuzi wao

kwa faida na manufaa ya jamii.


20

SEHEMU YA PILI

W
AJIBU WA RAIA NA MAMLAKA ZA NCHI

(a) Wajibu wa Raia kwa TaifaWajibu wa

kushiriki kazi


48.

-(1) Kila mtu ana wajibu wa -

(a) kushiriki kwa kujituma na kwa uaminifu katika kazi halali

ya uzalishaji mali; na

(b) kuwa na nidhamu ya kazi na kujitahidi kufikia malengo ya

uzalishaji mali yake binafsi na yale malengo ya pamoja

yanayotakiwa au yaliyowekwa na sheria.

(2) Bila ya kujali masharti ya Ibara ndogo ya (1), kazi yoyote ya

shuruti ni marufuku katika Jamhuri ya Muungano.

(3) Kwa madhumuni ya Katiba hii, kazi yoyote haitahesabiwa

kuwa ni kazi ya shuruti au kazi ya kikatili au ya kutweza endapo kazi

hiyo, kwa mujibu wa sheria ni -

(a) kazi ambayo haina budi ifanywe kutokana na

hukumu au amri ya mahakama;

(b) kazi ambayo haina budi kufanywa na askari wa jeshi

lolote katika kutekeleza majukumu yao;

(c) kazi ambayo haina budi kufanywa kutokana na kuwapo hali

ya hatari au baa lolote linalotishia uhai na ustawi wa

jamii; na

(d) kazi au huduma yoyote ambayo ni sehemu ya -

(i) majukumu ya kawaida ya kuhakikisha ustawi wa

jamii;

(ii) ujenzi wa Taifa wa lazima kwa mujibu wa sheria;

(iii) jitihada za Taifa za kutumia uwezo wa kila mtu

kufanya kazi kwa ajili ya kuimarisha ustawi wa

jamii na uchumi wa Taifa na kuhakikisha

maendeleo na tija ya kitaifa.

Ulinzi wa

mali ya

umma


49

.-(1) Kila raia anao wajibu wa kulinda maliasili ya Taifa, mali

ya mamlaka ya nchi na mali yoyote inayomilikiwa kwa pamoja na

wananchi, na pia kuiheshimu mali ya mtu mwingine.

(2) Kila mtu ana wajibu wa kulinda, kuhifadhi na kudumisha

rasilimali za nchi na maliasili za Taifa.

(3) Kila mtu anao wajibu wa kutunza vizuri mali ya mamlaka ya

nchi na mali inayomilikiwa kwa pamoja, kupiga vita aina zote za

uharibifu na ubadhirifu, na kuendesha uchumi wa Taifa kwa makini

kwa kuzingatia mipango endelevu na haki ya vizazi vijavyo.

Haki na

wajibu

muhimu


50.

-(1) Kila raia wa Jamhuri ya Muungano anayo haki ya

kufaidi haki za msingi za binadamu, na matokeo ya kila mtu kutekeleza

wajibu wake kwa jamii, kama zilivyofafanuliwa katika Katiba hii.

(2) Kila raia katika Jamhuri ya Muungano anayo haki ya

kupata hifadhi sawa chini ya sheria za Jamhuri ya Muungano.

(3) Mtu yeyote katika Jamhuri ya Muungano hatakuwa na haki,

hadhi au cheo maalum kwa misingi ya nasaba, jadi au urithi wake.

(4) Ni marufuku kwa sheria yoyote kutoa haki, hadhi au cheo


21

maalum kwa mtu yeyote wa Jamhuri ya Muungano kwa misingi ya

nasaba, jadi au urithi.

(5) Ili watu wote wafaidi haki na uhuru uliotajwa katika Katiba

hii, kila mtu anao wajibu wa kutenda na kuendesha shughuli zake kwa

namna ambayo haitaingilia haki na uhuru wa watu wengine au maslahi

ya umma.

(b) Wajibu wa Mamlaka za NchiHifadhi ya

haki za

binadamu


51

.-(1) Serikali na mamlaka zote za nchi zinao wajibu wa

kuzingatia na kuhifadhi haki za binadamu ikiwa ni msingi wa uhuru kama

ilivyoainishwa katika Katiba hii.

(2) Haki na uhuru wa kila mtu kama zilivyoainishwa katika Katiba

hii zitaheshimiwa, kuhifadhiwa na kudumishwa na mamlaka za nchi,

mamlaka binafsi na kila mwananchi.

(3) Haki na uhuru ambao umeainishwa katika mikataba ya

kimataifa kuhusu haki za binadamu ambazo Jamhuri ya Muungano

imeridhia, isipokuwa masharti ambayo Jamhuri ya Muungano imeeleza

wazi kutojifunga nayo, zitakuwa Sehemu ya Haki za Binadamu

zilizoainishwa katika Sura hii.

Usimamizi

wa haki za

binadamu


52.-

(1) Katika kutafsiri masharti ya Sura hii ya Haki za

Binadamu, Mahakama, Baraza au chombo kingine chochote cha

kufanya uamuzi kitazingatia mambo yafuatayo:

(a) haki ya usawa, utu na uhuru wa mtu binafsi;

(b) sheria za kimataifa na haki za binadamu; na

(c) haki za jamii na maslahi ya jamii kwa ujumla.

(2) Mtu anayeamini kuwa masharti yaliyomo katika Sura hii

yamekiukwa au yanaelekea kukiukwa na mamlaka, chombo cha

uamuzi, au sheria au sera yoyote, dhidi yake, anaweza kuwasilisha au

kufungua shauri katika Mahakama Kuu kwa hati maalumu ya maombi

kwa mujibu wa sheria za nchi ili kupata nafuu inayohitajika.

(3) Mahakama inaweza, kwa mujibu wa Ibara ndogo ya (1)

kutoa maelekezo itakayoona yanafaa, kuweka zuio, katazo au kuamuru

jambo lifanyike ambalo lilikuwa limenyimwa.

(4) Shauri katika Mahakama ya kudai haki za kikatiba kwa

mujibu wa masharti ya Ibara hii yanaweza kufunguliwa na:

(a) Mtu anayejiwakilisha mwenyewe au taasisi

inayowawakilisha wanachama wake;

(b) mtu anayemwakilisha mtu ambaye hawezi kujiwakilisha

mwenyewe kwa mujibu wa sheria; au

(c) mtu anayewakilisha kundi la watu wenye malengo

yanayofanana au jamii ya watu fulani wenye kuvunjiwa

haki husika.

Mipaka ya

haki za

binadamu


53.

-(1) Haki zote zilizoainishwa katika Sura hii ya Katiba

endapo zitahitajika kuwekewa mipaka ni lazima mipaka hiyo kutumika

kwa uwazi na kidemokrasia kwa kuzingatia utu, usawa, uhuru na

vigezo muhimu, ikijumuisha:


22

(a) aina ya haki;

(b) umuhimu na sababu za kuweka mipaka;

(c) asili na ukubwa wa mpaka husika;

(d) uhusiano baina ya mpaka husika na sababu yake;

(e) njia nyepesi ya kufikia madhumuni ya matumizi ya mpaka

husika; na

(f) umuhimu wa kulinda usalama wa nchi.

(2) Bunge litatunga sheria, ambayo pamoja na mambo mengine,

itasimamia matumizi na utekelezaji wa masharti ya Ibara hii.

SURA YA TANO

U
RAIA KATIKA JAMHURI YA MUUNGANO

Uraia wa

Jamhuri ya

Muungano


54

.-(1) Mtu ambaye,kablaya Katiba hii kuanza kutumika, ni raia wa Jamhuri

ya Muungano ataendelea kuwa raia wa Tanzania.

(2) Uraia wa Jamhuri ya Muungano ni wa aina mbili na utapatikana kwa njia

ya kuzaliwa au kujiandikisha.

Uraia wa

kuzaliwa


55

.-(1) Kila mtu anayezaliwa Tanzania Bara au Zanzibar atakuwa raia wa

Jamhuri ya Muungano iwapo, wakati wa tarehe ya kuzaliwa, mama au baba yake ni

au alikuwa raia wa Jamhuri ya Muungano.

(2) Kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii, mtu aliyezaliwa nje ya Tanzania

atakuwa ni raia wa Jamhuri ya Muungano kwa kuzaliwa kuanzia tarehe ya kuzaliwa

kwake ikiwa wazazi wake au mmoja kati ya wazazi wake ni raia wa Jamhuri ya

Muungano.

(3) Endapo mmoja kati ya wazazi alifariki kabla ya mtu huyo kuzaliwa,

uraia wa mzazi huyo wakati wa kifo chake unatumika, kwa madhumuni ya

kutambua uraia wa mtu huyo aliyezaliwa baada ya mzazi aliyefariki kama kwamba

mzazi huyo alikuwa anaishi hadi kuzaliwa kwa mtu huyo.

(4) Mtoto mwenye umri chini ya miaka saba akikutwa ndani ya mipaka ya

Jamhuri ya Muunganokatika mazingira ambayo wazazi wake hawajulikani,

atahesabika kuwa ni raia wa Jamhuri ya Muungano wa kuzaliwa.

(5) Mtoto aliye na umri wa chini ya miaka kumi na nane ambaye wazazi

wake sio raia wa Tanzania, akiasiliwa na raia wa Jamhuri ya Muungano, kwa

kuasiliwa kwake huko, kutawezesha mtoto huyo kuwa raia wa Jamhuri ya

Muungano wa kujiandikisha.

Uraia wa

kuandikishwa


56

.-(1) Mara baada ya kuanza kutumika kwa Katiba hii, mtu ambaye

amekuwa mkazi wa Tanzania Bara au Zanzibar kwa muda uliowekwa na sheria

inayotumika Tanzania Bara au Zanzibar, na ambaye ametimiza masharti yote ya

sheria ya Bunge la Tanzania Bara au Baraza la Wawakilishi la Zanzibar, anaweza

kuomba kuandikishwa kuwa raia wa Jamhuri ya Muungano.

(2) Mtu aliyefunga ndoa na raia wa Jamhuri ya Muunganoanaweza kutuma

maombi ya kuandikishwa kuwa raia wa Jamhuri ya Muungano.

(3)Endapo ndoa iliyorejewa katika Ibara ndogo ya (2) itavunjika, kama mtu

huyo hakuukana uraia wake, ataendelea kuwa raia wa Jamhuri ya Muungano.

(4) Mtoto aliyezaliwa katika ndoa iliyorejewa katika Ibara ndogo ya (2),

ataendelea kuwa raia wa Jamhuri ya Muungano isipokuwa kama ataukana uraia huo

au ataomba na kupata uraia wa nchi nyingine.


23

SURA YA SITA

M
UUNDO WA JAMHURI YA MUUNGANO

Muundo wa

Muungano


57

.-(1) Jamhuri ya Muungano itakuwa na muundo wa shirikisho lenye

serikali tatu ambazo ni:

(a) Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania;

(b) Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar; na

(c) Serikali ya Tanzania Bara.

(2) Shughuli za Jamhuri ya Muungano zitatekelezwa na kusimamiwa

na:

(a) Serikali ya Jamhuri ya Muungano;

(b) Bunge la Jamhuri ya Muungano; na

(c) Mahakama ya Jamhuri ya Muungano.

(3) Muundo, madaraka na mambo mengine ya kiutendaji yahusuyo

Serikali yaTanzania Bara na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar yataainishwa

katika Katiba za Washirika wa Muungano.

Vyombo

vya utendaji

vya Jamhuri

ya

Muungano


58.-

(1) Serikali ya Jamhuri ya Muungano itakuwa ndiyo chombo

chenye mamlaka ya utendaji, Bunge litakuwa na mamlaka ya kutunga sheria

kwa mambo ya Muungano na kusimamia utekelezaji wa shughuli za Serikali

ya Jamhuri ya Muungano na Mahakama itakuwa ni chombo cha utoaji haki.

(2) Kila chombo kilichotajwa katika ibara hii kitaundwa na kutekeleza

majukumu yake kwa kufuata masharti ya Katiba hii.

Mamlaka

ya Serikali

ya

Muungano


59

.-(1) Serikali ya Jamhuri ya Muungano itakuwa na mamlaka ya

utekelezaji kwa mambo yote yaliyoorodheshwa kuwa Mambo ya Muungano, na

wakati inapotekeleza majukumu yake, itazingatia mamlaka yake iliyopewa chini

ya Katiba hii.

(2)Utekelezaji wa majukumu ya Serikali utafanywa kwa namna na kwa

misingi iliyowekwa na Katiba hii au sheria iliyotungwa na Bunge.

(3) Bila ya kuathiri aukukiuka masharti ya Ibara hii, Serikali ya Jamhuri

ya Muungano, kwa makubaliano na masharti maalum baina yake na Serikali ya

Zanzibar au Serikali ya Tanzania Bara, inaweza kutekeleza jambo lolote lililo

chini ya mamlaka ya Serikali ya Zanzibar au Serikali ya Tanzania Bara kwa

mujibu wa masharti ya makubaliano hayo.


Mambo ya

Muungano


60

. Kwa ajili ya utekelezaji bora wa shughuli za Serikali ya Jamhuri ya

Muungano, na kwa ajili ya mgawanyo wa madaraka juu ya shughuli hizo

baina ya vyombo vilivyotajwa katika Ibara ya 58, Serikali ya Muungano

itakuwa na mamlaka juu ya mambo ya Muungano yalivyoorodheshwa katika

Nyongeza ya Katiba hii.

Washirika

wa

Muungano


61

.-(1) Kwa mujibu wa Katiba hii, Washirika wa Muungano ni

Tanzania Bara na Zanzibar.

(2) Serikali ya Tanzania Bara itakuwa na mamlaka juu ya mambo yote

(5) Bunge litatunga sheria, pamoja na mambo mengine, kusimamia masuala

yanayohusu uraia wa Jamhuri ya Muungano.


24

yasiyo ya Muungano yahusuyo Tanzania Bara.

(3) Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itakuwa na mamlaka juu ya

mambo yote yasiyo ya Muungano yahusuyo Zanzibar.

(4) Washirika wa Muungano watatekeleza majukumu yao kwa

kuzingatia masharti ya Katiba hii na Katiba zao.

(5)

Washirika wa Muungano watakuwa na hadhi na haki sawa ndani

ya Jamhuri ya Muungano na watatekeleza majukumu yao kwa masuala yote

yasiyo ya Muungano katika mamlaka ya Washirika wa Muungano kwa

mujibu wa masharti yatakayowekwa na Katiba za Washirika wa Muungano.

Mamlaka

ya

Washirika

wa

Muungano


62

.-(1) Kila Mshirika wa Muungano atakuwa na mamlaka na haki zote

juu ya mambo yote yasiyo ya Muungano, na katika utekelezaji wa mamlaka

hayo, kila Mshirika wa Muungano atazingatia misingi ya ushirikiano na

mshirika mwingine kwa kuzingatia haki na usawakwa ajili ya ustawi ulio bora

kwa wananchi wa pande zote mbili za Jamhuri ya Muungano.

(2) Bila ya kuathiri mipaka iliyowekwa na Katiba hii, kila Mshirika wa

Muungano atakuwa na uwezo na uhuru wa kuanzisha mahusiano au

ushirikiano na jumuiya au taasisi yoyote ya kikanda au kimataifa kwa mambo

yaliyo chini ya mamlaka yake kwa mujibu wa Katiba ya Mshirika wa

Muungano.

(3
) Mshirika wa Muungano anaweza, wakati wa kutekeleza majukumu

yake chini ya Ibara ndogo ya (2), kuomba mashirikiano kutoka Serikali ya

Jamhuri ya Muungano kwa ajili ya kufanikisha mahusiano na jumuiya au

taasisi ya kimataifa au kikanda, na Serikali ya Jamhuri Muungano inaweza

kutoa ushirikiano kwa mshirika huyo kwa namna itakavyohitajika.

Mahusiano

kati ya

Washirika

wa

Muungano


63

.-(1) Kila Mshirika wa Muungano anaweza, katika kutekeleza

majukumu yake katika maeneo mbalimbali, kutekeleza majukumu hayo

kwa misingi ya kushirikiana na kushauriana na Mshirika wa Muungano

mwingine au baina ya Mshirika wa Muungano na Serikali ya Jamhuri ya

Muungano kwa lengo la kukuza na kulinda maslahi ya Taifa na maendeleo

ya wananchi.

(2) Washirika wa Muungano na Serikali ya Jamhuri ya Muungano

wanaweza kushauriana na kushirikiana katika mambo ya uongozi, utawala,

vyombo vya uwakilishi na kimahakama.

(3) Utendaji wa Serikali za Washirika wa Muungano au wa chombo

chochote kati ya vyombo vya serikali hizo na uendeshaji wa shughuli,

utatekelezwa kwa kuzingatia umoja wa Jamhuri ya Muungano na nia na

umuhimu wa haja ya kukuza umoja wa kitaifa na kudumisha heshima ya

Taifa.

Mawaziri

Wakaazi


64.-

(1) Kila Mshirika wa Muungano atateua Waziri Mkaazi

atakayeratibu na kusimamia mahusiano baina ya Serikali za Washirika na

kati ya Serikali ya Mshirika na Serikali ya Jamhuri ya Muungano.

(2)Mawaziri Wakaazi watakuwa na ofisi zao na watafanya kazi

wakiwa Makao Makuu ya Serikali ya Muungano.

(3) Pamoja na majukumu mengine watakayopangiwa na Serikali

za Washirika wa Muungano, Mawaziri Wakaazi watakuwa na majukumu

yafuatayo:


25

Wajibu wa

kulinda

Muungano


66.-

(1) Bila ya kuathiri wajibu wa kila raia kwa mujibu wa Katiba

hii, viongozi wakuu wenye mamlaka ya utendaji katika Jamhuri ya

Muungano waliotajwa katika Ibara ndogo ya (3) watawajibika, kila mmoja

wao katika kutekeleza madaraka waliyopewa kwa mujibu wa Katiba hii au

Katiba za Washirika wa Muungano kuhakikisha kuwa analinda, kuimarisha

na kudumisha Muungano.

(2) Kwa madhumuni ya masharti ya Ibara ndogo ya (1), kila

mmojawapo wa viongozi wakuu waliotajwa katika Ibara ndogo ya (3),

kabla ya kushika madaraka yake ataapa kuutetea na kuudumisha

Muungano kwa mujibu wa Katiba hii.

(3) Viongozi Wakuu wanaohusika na masharti ya Ibara hii ni:

(a) Rais wa Jamhuri ya Muungano;

(b) Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano;

(c) Rais wa Tanzania Bara; na

(d) Rais wa Zanzibar.

SURA YA SABA

SERIKALI YA JAMHURI YA MUUNGANO

SEHEMU YA KWANZA

S
ERIKALI, RAIS NA MAKAMU WA RAIS

(a) SerikaliSerikali ya

Jamhuri ya

Muungano


67.-

(1) Kutakuwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa

Tanzania ambayo itaundwa na Rais, Makamu wa Rais na Mawaziri wa

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

(2) Serikali ya Jamhuri ya Muungano itakuwa na mamlaka juu

ya mambo yote ya Muungano katika Jamhuri ya Muungano.

(3) Mamlaka ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano yatahusu

utekelezaji na hifadhi ya Katiba hii na pia mambo mengine ambayo

(a) kushughulikia mambo yasiyo ya Muungano yanayohusu

ushirikiano au mahusiano ya kimataifa; na

(b) kuwa kiungo baina ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano na

Serikali za Washirika wa Muungano na baina ya Serikali za

Washirika wa Muungano.

Mamlaka ya

wananchi


65

.-(1) Serikali ya Jamhuri ya Muungano itapata mamlaka yake

kutoka kwa wananchi kupitia uchaguzi wa kidemokrasia utakaoendeshwa

na kusimamiwa na chombo kitakachopewa mamlaka na Katiba hii, na

vilevile, Serikali ya Tanzania Bara na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar

zitapata mamlaka kupitia uchaguzi wa kidemokrasia utakaoendeshwa na

kusimamiwa na vyombo vitakavyopewa mamlaka chini ya Katiba zao.

(2) Serikali za Washirika wa Muungano, katika kutekeleza

mamlaka zao, zitawajibika kustawisha mamlaka ya wananchi kwa kugatua

madaraka kwa serikali za mitaa zitakazoanzishwa kwa mujibu wa Katiba

ya Tanzania Bara au Katiba ya Zanzibar, kama itakavyokuwa.


26

yameainishwa katika sheria za nchi.

(4) Madaraka ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano

yatatekelezwa na Rais mwenyewe, au kwa kukasimu madaraka hayo

kwa Makamu wa Rais au watu wengine wenye madaraka katika

utumishi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano.

(5) Ifahamike kwamba masharti yaliyomo katika Ibara hii

hayatahesabiwa kwamba:

(a) yanahamishia kwa Rais madaraka yoyote ya kisheria

yaliyowekwa na sheria mikononi mwa mtu au mamlaka

yoyote ambayo si Rais; au

(b) yanalizuia Bunge kukabidhi madaraka yoyote ya kisheria

mikononi mwa mtu au watu au mamlaka nyingine yoyote

ambayo si Rais.

(b)
Rais


Rais wa

Jamhuri

ya

Muungano


68.-

(1) Kutakuwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano.

(2) Rais wa Jamhuri ya Muungano atakuwa Mkuu wa Nchi,

Kiongozi wa Serikali na Amiri Jeshi Mkuu na:

(a) atakuwa alama na taswira ya Jamhuri ya Muungano wa

Tanzania na watu wake;

(b) atakuwa alama ya umoja na uhuru wa nchi na mamlaka

yake;na

(c) atakuwa na dhamana ya kukuza na kuhifadhi umoja wa

kitaifa.

Madaraka

na

majukumu

ya Rais


69.-

(1)Rais akiwa Mkuu wa Nchi, atakuwa na madaraka na

majukumu yafuatayo:

(a) kuisimamia na kuilinda Katiba;

(b) kulinda utaifa wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania;

(c) kuhutubia na kufungua rasmi Bunge Jipya na kulivunja

Bunge baada ya kumaliza muda wake;

(d) kuhutubia na kufungua rasmi Kalenda ya Mwaka ya

Mahakama;

(e) kuidhinisha uwasilishaji Bungeni makisio ya mapato na

matumizi ya Serikali, Bunge na Mahakama katika mwaka

wa fedha;

(f) kuweka saini katika Muswada wa Sheria uliyopitishwa na

Bunge;

(g) kutunuku nishani za heshima kwa niaba ya Watu wa

Jamhuri ya Muungano kwa ujumla;

(h) kuteua Mabalozi,Watu watakaoiwakilisha Tanzania nje ya

nchi na wawakilishi wa nchi katika taasisi mbalimbali za

kimataifa;

(i) kupokea hati za utambulisho za Mabalozi wa nchi za nje

nchini;

(j) kutoa msamaha kwa mtu yeyote anayetumikia adhabu


27

iliyotolewa na Mahakama kwa mujibu wa sheria za nchi; na

(k) kuidhinisha utekelezaji wa adhabu ya kifo iliyotolewa kwa

mujibu wa sheria za nchi.

(2) Rais akiwa Amiri Jeshi Mkuu, atakuwa na madaraka na

majukumu yafuatayo:

(a) kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Ulinzi na Usalama wa

Taifa;

(b) kuamuru Majeshi ya Ulinzi kwenda vitani au kusitisha vita;

(c) kutia saini makubaliano ya amani au kusitisha vita;

(d) kutangaza hali ya hatari au hali ya kuzingirwa eneo fulani;

(e) kuteua Wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama; na

(f) kuwapandisha vyeo maofisa wa vyombo vya ulinzi na

usalama katika ngazi mbalimbali na kutoa kamisheni kwa

maofisa wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania.

(3) Akiwa Kiongozi wa Serikali, Rais wa Jamhuri ya Muungano

atakuwa na madaraka na majukumu yafuatayo:

(a) kuongoza vikao vya Baraza la Mawaziri la Jamhuri ya

Muungano;

(b) kupanga, kuelekeza, kusimamia na kuratibu majukumu ya

wizara na taasisi za serikali;

(c) kuwateua Mawaziri na Naibu Mawaziri wa Serikali ya Jamhuri

ya Muungano;

(d) kumteua Katibu Mkuu Kiongozi na Makatibu Wakuu;

(e) kumteua Mwanasheria Mkuu na Naibu Mwanasheria Mkuu wa

Serikali; na

(f) kuwateua makamishna wa Tume mbalimbali zilizoanzishwa

kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii.

(4) Katika kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa Ibara hii,

Rais ataepuka kujinasibisha, kwa namna yoyote ile, na chama chochote cha

siasa au kundi lolote kwa namna ambayo inaathiri umoja wa wananchi.

Utekelezaji

wa

madaraka

ya Rais


70.

-(1) Katika utekelezaji wa madaraka ya Rais kwa mujibu wa

Sura hii na kwa kuzingatia masharti ya Ibara ndogo ya (3), Rais ana

mamlaka ya kuanzisha au kufuta nafasi za madaraka katika utumishi wa

Serikali ya Jamhuri ya Muungano.

(2)Rais atakuwa na madaraka ya kuteua watu wa kushika nafasi za

madaraka ya viongozi wanaowajibika kuweka sera za idara na taasisi za

Serikali, na watendaji wakuu wanaowajibika kusimamia utekelezaji wa

sera za idara na taasisi hizo katika utumishi wa Serikali ya Jamhuri ya

Muungano.

(3) Katika utekelezaji wa madaraka kama ilivyoainishwa katika

Ibara ndogo ya (1) na (2), Rais atazingatia masharti kuhusu uthibitisho wa

Bunge katika nafasi za madaraka na vile vile ushauri wa mamlaka za

Serikali, Bunge au Mahakama zilizopewa madaraka ya kumshauri katika

kufanya uteuzi, kuanzisha au kufuta nafasi za madaraka katika utumishi wa

Serikali.

(4) Mamlaka ya kuwateua watu wengine wote wasiokuwa

viongozi wala watendaji wakuu, kushika nafasi za madaraka katika


28

utumishi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano, na mamlaka ya

kuwapandisha vyeo watu hao, kuwaondoa katika madaraka, kuwafukuza

kazi, kuwasimamisha kazi na mamlaka ya kudhibiti nidhamu ya watu

waliokabidhiwa madaraka, yatakuwa mikononi mwa Tume za Utumishi na

mamlaka za nchi zilizotajwa na kupewa madaraka hayo na sheria za nchi.

(5) Masharti ya Ibara ndogo ya (2) na ya (3) hayazuii Rais

kuchukua hatua za kudhibiti nidhamu ya watumishi na utumishi katika

Serikali ya Jamhuri ya Muungano.

Rais

kuzingatia

ushauri


71.

-(1) Mbali na kuzingatia masharti yaliyomo katika Katiba hii,

na sheria za nchi, Rais atakuwa na wajibu wa kufuata na kuzingatia

ushauri atakaopewa na mamlaka za nchi, na endapo hakubaliani na

ushauri aliopewa sharti atoe sababu katika Baraza la Mawaziri kuhusu

sababu ya kutokubaliana na ushauri aliopewa.

(2) Kwa madhumuni ya Ibara ndogo ya (1), Rais hatalazimika

kuufuata ushauri aliopewa ambao unakwenda kinyume au kukiuka

masharti ya Katiba au haukuzi wala kuhifadhi maslahi ya taifa na wananchi

walio wengi.

Rais

kushindwa

kumudu

majukumu

yake


72.-

(1) Endapo Baraza la Mawaziri litaona kuwa Rais hawezi

kumudu kazi zake kwa sababu ya maradhi ya mwili au akili, linaweza

kuwasilisha kwa Jaji Mkuu azimio la kumwomba Jaji Mkuu athibitishe

kwamba Rais, kwa sababu ya maradhi ya mwili au ya akili, hawezi

kumudu kazi zake.

(2) Baada ya kupokea azimio lililowasilishwa kwa mujibu wa Ibara

ndogo ya (1), Jaji Mkuu atateua bodi ya utabibu ambayo itachunguza suala

hilo na kumshauri Jaji Mkuu ipasavyo.

(3) Jaji Mkuu anaweza, baada ya kutafakari ushauri na ushahidi wa

kitabibu, kuwasilisha kwa Spika hati ya kuthibitisha kwamba kutokana na

maradhi ya mwili au akili, Rais ameshindwa kumudu kazi zake, na iwapo

Jaji Mkuu hatabatilisha hati hiyo ndani ya siku saba kutokana na Rais

kupata nafuu na kurejea kazini, basi itahesabiwa kwamba kiti cha Rais ki

wazi, na masharti yaliyomo katika Ibara ndogo ya (5) na (6) yatatumika.

(4) Bodi ya utabibu itakayoteuliwa kwa mujibu wa Ibara ndogo ya

(3) itajumuisha watu wasiopungua watatu watakaoteuliwa kutoka

miongoni mwa madaktari bingwa wanaotambuliwa na sheria inayohusu

madaktari ya Tanzania.

(5) Endapo kiti cha Rais kitakuwa wazi kutokana na Rais kufariki

dunia, kujiuzulu, kupoteza sifa za uchaguzi, kutomudu kazi zake kutokana

na maradhi ya mwili au akili au kushindwa kutekeleza kazi na shughuli za

Rais, basi Makamu wa Rais ataapishwa na kushika madaraka ya Rais kwa

muda uliobaki katika kipindi cha miaka mitano na kwa masharti

yaliyoelezwa katika Ibara ya 76.

(6) Mara tu baada ya kuapishwa, au kwa vyovyote vile ndani ya

kipindi kisichozidi siku kumi na nne tangu alipoapishwa, Rais:

(a) baada ya kushauriana na chama cha siasa anachotoka;au

(b) baada ya kushauriana na Baraza la Ulinzi naUsalama wa Taifa,

kwa Rais aliyetokana kwa utaratibu wa mgombea huru,

atapendekeza jina la mtu atakayekuwa Makamu wa Rais na uteuzi huo


29

utathibitishwa na Bunge kwa kura zaidi ya asilimia hamsini ya Wabunge

wote.

Utekelezaji

wa

majukumu

ya Rais

akiwa

hayupo


73.-

(1) Ikitokea kwamba kiti cha Rais kiko wazi kutokana na

masharti yaliyomo katika Ibara ya 72 au endapo kiti cha Rais kiko wazi

kutokana na sababu nyingine yoyote, na endapo Rais atakuwa hayupo

katika Jamhuri ya Muungano, kazi na shughuli za Rais zitatekelezwa na

mmoja wapo wa wafuatao, kwa kufuata orodha kama ilivyopangwa, yaani–

(a) Makamu wa Rais au kama nafasi yake iko wazi au kama naye

hayupo au ni mgonjwa, basi;

(b) Waziri Mwandamizi; au

(c) kamaWaziri Mwandamizi nafasi yake iko wazi au kama naye

hayupo au ni mgonjwa, basi Waziri mwingine yeyote

atakayeteuliwa na Baraza la Mawaziri.

(2) Endapo yeyote kati ya watu waliotajwa katika aya ya (a), (b) na

(c) za Ibara ndogo ya (1) atatekeleza kazi na shughuli za Rais kutokana na

sababu kwamba mtu mwingine anayemtangulia katika orodha hiyo hayupo,

basi mtu huyo ataacha kutekeleza kazi na shughuli hizo mara tu mtu huyo

mwingine anayemtangulia atakaporejea na akashika na kuanza kutekeleza

kazi na shughuli za Rais.

(3) Mtu yoyote atakayekaimu nafasi ya madaraka ya Rais, kwa

namna yoyote ile, hatakuwa na madaraka katika mambo yafuatayo:

(a) kuteua aukumuondoa madarakani kiongozi yoyote yule

aliyeteuliwa na Rais kwa mujibu wa Katiba hii; au

(b) jambo jingine lolote kama litakavyoainishwa na Rais katika hati

ya kukasimu madaraka yake.

(4) Kwa madhumuni ya Ibara ndogo ya (2) na (3), Rais atakasimu

madaraka yake kwa hati maalumu aliyotia saini yake.

(c) Uchaguzi wa RaisUchaguzi

wa Rais


74.

-(1) Rais atachaguliwa na wananchi kwa mujibu wa masharti ya

Katiba hii na kwa mujibu wa sheria za nchi.

(2) Nafasi ya madaraka ya Rais itakuwa wazi na uchaguzi wa Rais

utafanyika baada ya Rais kumaliza muda wake wa kuwa madarakani kwa

mujibu wa Katiba hii.

(3) Endapo kutatokea jambo lolote kati ya mambo yafuatayo,

hakutakuwa na Uchaguzi wa Rais na badala yake nafasi hiyo itajazwa na

Makamu wa Rais kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii, yaani:

(a) Rais kujiuzulu;

(b) Rais kupoteza sifa za kuchaguliwa katika nafasi ya

madaraka ya Rais;

(c) Rais kushtakiwa Bungeni na kuondolewa katika madaraka kwa

mujibu wa Katiba hii;

(d) ikithibitika kwamba Rais hawezi kumudu nafasi ya madaraka

ya Rais; au

(e) Rais kufariki dunia.

Sifa za

Rais


75

. Mtu atakuwa na sifa ya kuchaguliwa kushika nafasi ya


30

madaraka ya Rais wa Jamhuri ya Muungano ikiwa:

(a) ni raia wa kuzaliwa wa Jamhuri ya Muungano kwa mujibu wa

Katiba hii na sheria za nchi;

(b) ni mwenye akili timamu;

(c) angalau mmoja kati ya wazazi wake ni raia wa kuzaliwa wa

Jamhuri ya Muungano;

(d) wakati wa kugombea, ana umri usiopungua miaka arobaini;

(e) anazo sifa za kumwezesha kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri

ya Muungano kwa mujibu wa Katiba hii;

(f) anayo angalau shahada ya kwanza ya chuo kikuu

kinachotambuliwa kwa mujibu wa sheria za nchi;

(g) ni mwanachama na mgombea aliyependekezwa na chama cha

siasa au mgombea huru;

(h) sera zake au sera za chama chake si za mrengo wa kuligawa

Taifa kwa misingi ya ukabila, udini, rangi au jinsia;

(i) ni mwadilifu na anafuata maadili ya Taifa;

(j) mwenendo wake binafsi hautiliwi shaka na jamii;

(k) hajatiwa hatiani kwa kosa lolote la jinailinalohusu kukosa

uaminifu; na

(l) katika kipindi cha miaka mitano kabla ya tarehe ya Uchaguzi

Mkuu hajawahi kutiwa hatiani katika Mahakama yoyote kwa

kosa lolote la kukwepa kulipa kodi yoyote ya Serikali.

Haki ya

kuchaguli

wa tena


76

.-(1) Mtu ambaye ni Rais anaweza kuchaguliwa tena kushika kiti

hicho kwa kipindi kingine cha miaka mitano.

(2) Mtu hatakuwa na sifa ya kugombea na kuchaguliwa zaidi ya

vipindi viwili katika nafasi ya madaraka ya Rais.

(3) Mtu aliyewahi kuwa Rais wa Tanzania Bara au Zanzibar

hatapoteza sifa za kugombea na kuchaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya

Muungano kwa sababu aliwahi kushika nafasi ya madaraka ya Rais wa

Tanzania Bara au Rais wa Zanzibar.

(4) Endapo mtu aliyekuwa anashika nafasi ya madaraka ya

Makamu wa Rais, atashika nafasi ya madaraka ya Rais kwa mujibu wa

masharti ya Ibara ya 72 kwa kipindi kisichozidi miezi thelathini na sita, mtu

huyo anayo haki ya kugombea nafasi ya madaraka ya Rais katika uchaguzi

wa Rais utakaofuata.

(5) Mtu aliyechaguliwa kushika nafasi ya madaraka ya Rais kwa

mujibu wa masharti ya Ibara ndogo ya (4), atahesabiwa kuwa ameshika

nafasi ya madaraka ya Rais katika vipindi viwili na hataruhusiwa kugombea

nafasi ya madaraka ya Rais katika kipindi kingine.

Utaratibu

wa

Uchaguzi

wa Rais


77.

-(1) Katika Uchaguzi wa Rais, kila chama cha siasa

kinachopenda kushiriki katika uchaguzi wa Rais kitawasilisha kwa

Tume Huru ya Uchaguzi ya Jamhuri ya Muungano, kwa mujibu wa sheria za

nchi, jina la mwanachama mmoja anayependekezwa kwa nafasi ya

madaraka ya Rais.

(2) Endapo ni Mgombea huru, kwa kuzingatia sifa zilizoainishwa

katika Katiba hii, atawasilisha jina lakekwenye Tume Huru ya Uchaguzi.

(3) Mapendekezo ya majina ya wagombea katika uchaguzi wa Rais


31

yatawasilishwa kwa Tume Huru ya Uchaguzi katika siku na kwa utaratibu

uliyoainishwa katika sheria za nchi.

(4) Endapo itafika saa na siku iliyotajwa kwa ajili ya

kuwasilisha mapendekezo ya majina ya wagombea, ni mgombea mmoja tu

ambaye anapendekezwa kuwa halali, Tume Huru ya Uchaguzi itawasilisha

jina lake kwa wananchi, nao watapiga kura ya kumkubali au

kumkataa kwa mujibu wa masharti yaliyoainishwa katika sheria za

nchi.

(5) Uchaguzi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano utafanyika siku

itakayoteuliwa na Tume Huru ya Uchaguzi kwa mujibu wa sheria za nchi.

(6) Mgombea wa nafasi ya madaraka ya Rais atatangazwa kuwa

amechaguliwa kuwa Rais iwapo atapata kura zinazozidi asilimia

hamsini ya kura zote zilizopigwa kwa nafasi ya madaraka ya Rais.

(7) Endapo katika Uchaguzi wa Rais hakuna mgombea

aliyekidhi masharti ya Ibara ndogo ya (6), basi uchaguzi utarudiwa

ndani ya siku sitini kwa wagombea walioshika nafasi ya kwanza na ya

pili.

Malalamiko

kuhusu

uhalali wa

uchaguzi

wa Urais


78.-

(1) Kwa kuzingatia masharti ya Ibara ndogo ya (2), endapo

mtu yeyote aliyeshiriki kama mgombea nafasi ya madaraka ya Rais

katika Uchaguzi wa Rais hakuridhika na matokeo ya uchaguzi huo,

anaweza kuwasilisha malalamiko katika Mahakama ya Juu kupinga

matokeo wa Rais yaliyotangazwa na Tume Huru ya Uchaguzi.

(2) Malalamiko ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa Rais

yatawasilishwa Mahakama ya Juu ndani ya muda wa siku saba baada ya

siku ya kutangazwa kwa matokeo ya Uchaguzi wa Rais.

(3) Mahakama ya Juu itasikiliza na kutoa uamuzi wa shauri la

kupinga matokeo ya uchaguzi wa Rais katika kipindi cha siku kumi na

nne tangu kupokea malalamiko yaliyowasilishwa kwa mujibu wa Ibara

ndogo ya (2) na uamuzi huo utakuwa wa mwisho.

(4) Kwa madhumuni ya Ibara ndogo ya (3), Mahakama ya Juu

inaweza kutoa uamuzi bila kutoa sababu za uamuzi na sababu hizo

zikatolewa ndani ya kipindi kisichozidi siku thelathini tangu siku ya

kutoa uamuzi.

(5) Iwapo Mahakama ya Juu itaamua kuwa matokeo ya Uchaguzi

wa Rais si halali, Uchaguzi wa Rais utarudiwa ndani ya siku sitini baada

ya uamuzi kutolewa.

Kiapo cha

Rais


79.

-(1) Rais Mteule ataapishwa na Jaji Mkuu na atashika nafasi

ya madaraka ya Rais mapema iwezekanavyo baada ya kutangazwa

kwamba amechaguliwa kuwa Rais, lakini kwa hali yoyote, hatashika

madaraka kabla ya kupita siku thelathini kutoka siku matokeo ya Uchaguzi

wa Rais yalipotangazwa na Tume Huru ya Uchaguzi au siku ya kuthibitishwa

na Mahakama ya Juu.

(2) Isipokuwa kama atajiuzulu au atafariki mapema zaidi, Rais

Mteule atashika nafasi ya madaraka ya Rais kwa muda wa miaka mitano

tangu siku alipochaguliwa kuwa Rais.

(3) Rais atashika nafasi ya madaraka ya Rais hadi-

(a) siku ambapo Rais mteule ataapa kushika nafasi ya madaraka


32

ya Rais;

(b) siku ambapo atafariki dunia;

(c) siku atakapojiuzulu; au

(d) atakapoacha kushika nafasi ya madaraka ya Rais kwa mujibu

wa masharti ya Katiba hii.

(d) Masharti Mahsusi kuhusu RaisMadaraka

ya

kutangaza

vita


80

.-(1) Kwa kuzingatia masharti ya Ibara hii, Rais atakuwa na

mamlaka ya kutangaza kuwepo kwa vita kati ya Jamhuri ya Muungano na

nchi nyingine au kundi lolote lile baada ya kupata idhini ya Bunge.

(2)Bila kujali masharti ya Ibara ndogo ya (1), endapo Jamhuri ya

Muungano itakuwa imevamiwa au kundi lolote limeanzisha vita ndani ya

Jamhuri ya Muungano basi, Rais anaweza, baada ya kushauriana na Baraza

la Ulinzi na Usalama la Taifa, kutangaza kuwepo kwa vita katika Jamhuri ya

Muungano.

(3) Baada ya kutoa tangazo kwa mujibu wa Ibara ndogo ya

(2), Rais atalitaarifu Bunge kwa kupeleka nakala ya tangazo hilo kwa

Spika wa Bunge ambaye, ndani ya siku kumi na nne kuanzia tarehe

ya tangazo, ataitisha Mkutano wa Bunge ili kulijulisha Bunge kuhusu

tangazo lililotolewa na Rais.

Madaraka

ya Rais

kutangaza

hali ya

hatari


81.-

(1) Bila ya kuathiri masharti ya Katiba hii, au sheria

iliyotungwa na Bunge kwa ajili hiyo, Rais anaweza, baada ya kushauriana

na Baraza la Ulinzi na Usalama wa Taifa, kutangaza hali ya hatari au hali

ya kuzingirwa kwa eneo fulani la Jamhuri ya Muungano au katika sehemu

yake yoyote.

(2) Rais anaweza tu kutangaza kuwa kuna hali ya hatari iwapo-

(a) Jamhuri ya Muungano iko katika vita;

(b) kuna hatari hasa kwamba Jamhuri ya Muungano inakaribia

kuvamiwa na kuingia katika hali ya vita;

(c) kuna hali halisi ya kuvurugika kwa amani katika jamii au

kutoweka kwa usalama wa jamii katika Jamhuri ya Muungano

au sehemu yake yoyote kiasi kwamba ni lazima kuchukua hatua

za pekee ili kurejesha amani na usalama;

(d) kuna hatari dhahiri na kubwa, kiasi kwamba amani katika jamii

itavurugika na usalama wa raia kutoweka katika Jamhuri ya

Muungano au sehemu yake yoyote ambayo haiwezi kuepukika

isipokuwa kwa kutumia mamlaka ya pekee;

(e) karibu kutatokea tukio la hatari au tukio la balaa au la baa ya

kimazingira ambalo linatishia jamii au sehemu ya jamii katika

Jamhuri ya Muungano; au

(f) kuna aina nyingineyo ya hatari ambayo kwa dhahiri ni tishio

kwa usalama wa nchi.

(3) Endapo inatangazwa kwamba kuna hali ya hatari katika Jamhuri

ya Muungano au eneo lolote la Jamhuri ya Muungano, Rais atawasilisha

nakala ya tangazo hilo kwa Spika wa Bunge ambaye, ndani ya siku

zisizozidi kumi na nne tangu kutolewa kwa tangazo hilo, ataitisha mkutano


33

wa Bunge ili kulijulisha Bunge juu ya taarifa ya hali ya hatari

iliyotangazwa na Rais.

(4) Bunge linaweza kutunga sheria itakayoweka masharti kuhusu

nyakati na taratibu ambazo zitawawezesha baadhi ya watu wenye

kusimamia utekelezaji wa mamlaka ya Serikali katika sehemu mahsusi za

Jamhuri ya Muungano kumuomba Rais kutumia madaraka aliyopewa na

Ibara hii kuhusiana na yoyote kati ya sehemu hizo endapo katika sehemu

hizo, kunatokea lolote kati ya hali zilizotajwa katika aya ya (c), (d) na (e)

za Ibara ndogo ya (2) na hali hiyo haivuki mipaka ya sehemu hizo, na pia,

kwa ajili ya kufafanua utekelezaji wa mamlaka ya Serikali wakati wa hali

ya hatari.

(5) Tangazo la hali ya hatari lililotolewa na Rais kwa mujibu wa

Ibara hii litakoma kutumika iwapo litafutwa na Rais.

(6) Kwa madhumuni ya kuondoa mashaka juu ya ufafanuzi au

utekelezaji wa masharti ya Ibara hii, masharti ya sheria iliyotungwa na

Bunge na ya sheria nyingine yoyote inayohusu utangazaji wa hali ya hatari

kama ilivyotajwa katika Ibara hii, yatatumika tu katika sehemu ya Jamhuri

ya Muungano ambapo hali hiyo ya hatari imetangazwa.

Mamlaka

ya Rais

kutoa

msamaha


82

.-(1) Rais kwa mamlaka ya Mkuu wa Nchi, anayo mamlaka ya:

(a) kutoa msamaha kwa mtu yeyote aliyepatikana na hatia kwa

kosa lolote mbele ya Mahakama dhidi ya Jamhuri ya

Muunganokwa masharti maalum kama yatakavyoainishwa

katika sheria iliyotungwa na Bunge; au

(b) kubatilisha adhabu ya kifo kuwa adhabu ya kifungo cha

maisha.

(2) Masharti ya Ibara hii yatatumika kwa mtu aliyehukumiwana

kuadhibiwa akiwa Zanzibar na kwa adhabu zilizotolewa Zanzibar kwa

mujibu wa sheria iliyotungwa na Bunge inayotumika Zanzibar, hali

kadhalika, masharti hayo yatatumika kwa mtu aliyehukumiwa na

kuadhibiwa Tanzania Bara kwa mujibu wa sheria iliyotungwa na Bunge

inayotumika Tanzania Bara.

(3) Kwa madhumuni ya Ibara hii, kutakuwa na Kamati ya Taifa ya

Ushauri ambayo itakuwa na wajibu wa kumshauri Rais kuhusu kutoa

msamaha kwa mtu yeyote aliyepatikana na hatia mahakamani na anatumikia

adhabu.

(4) Utaratibu wa namna ya utekelezaji wa madaraka kwa mujibu

wa Ibara hii, muundo, majukumu na utendaji kazi wa Kamati ya Taifa ya

Ushauri vitaainishwa na sheria itakayotungwa na Bunge.

Kinga

dhidi ya

mashtaka

ya Rais


83

.-(1) Wakati Rais akiwa madarakani, hatashitakiwa wala mtu

yeyote hataendesha mashtaka ya aina yoyote dhidi yake mahakamani kwa

ajili ya kosa lolote la jinai.

(2) Wakati Rais ameshika madaraka kwa mujibu wa Katiba hii,

haitaruhusiwa kufungua mahakamani shauri la madai kuhusu jambo lolote

alilolitenda au alilokosa kulitenda yeye binafsi kama raia ama kabla au

baada ya kushika madaraka ya Rais, ila tu kama angalau siku thelathini

kabla ya shauri kufunguliwa mahakamani, Rais atapewa au ametumiwa

taarifa ya madai kwa maandishi kwa kufuata utaratibu uliowekwa kwa


34

mujibu wa sheria iliyotungwa na Bunge, na taarifa hiyo ikiwa inatoa maelezo

kuhusu chanzo cha shauri hilo, kiini cha madai yenyewe, jina lake na anwani

ya mahali anapoishi huyo mdai na jambo hasa analodai.

(3) Isipokuwa kama ataacha kushika madaraka ya Rais kutokana

na kura ya kutokuwa na imani na Rais, haitakuwa halali kwa mtu

kumshtaki au kufungua mahakamani shauri lolote la jinai au la madai

dhidi ya mtu aliyekuwa anashika madaraka ya Rais baada ya kuacha

madaraka hayo kutokana na jambo alilofanya wakati alipokuwa bado

anashika madaraka ya Rais.

Bunge

kumshtaki

Rais


84

.-(1) Bunge linaweza kupitisha azimio la kumuondoa Rais

madarakani endapo itatolewa hoja ya kumshtaki Rais na ikapitishwa kwa

mujibu wa masharti ya Ibara hii.

(2) Bila ya kuathiri masharti mengineyo ya Ibara hii, hoja

yoyote ya kumshtaki Rais haitatolewa isipokuwa tu kama itadaiwa

kwamba Rais ametenda mojawapo ya makosa yafuatayo:

(a) ukiukwaji mkubwa wa masharti ya Katiba hii;

(b) makosa makubwa ya jinai;

(c) kuzuia kwa namna yoyote ile yeyekuchunguzwa kwa mujibu

wa Ibara hii;

(d) uhaini;

(e) rushwa;

(f) amekuwa na mwenendo unaodhalilisha nafasi ya madaraka ya

Rais wa Jamhuri ya Muungano;

(g) kupuuza au kukataa kutekeleza uamuzi au amri halali za

Mahakama; au

(h) ametenda vitendo ambavyo vinakiuka kanuni zamaadili au miiko

ya uongozi;

(3) Bunge halitapitisha hoja ya kumshtaki Rais isipokuwa tu kama-

(a) haitatolewa hoja ya namna hiyo ndani ya miezi kumi na miwili

tangu hoja kama hiyo ilipotolewa na ikakataliwa na Bunge; na

(b) taarifa ya maandishi, iliyotiwa saini na kuungwa mkono na

Wabunge wasiopungua asilimia ishirini na tano ya Wabunge

wote itawasilishwa kwa Spika siku kumi na nne kabla ya

kikao ambapo hoja hiyo inakusudiwa kutolewa Bungeni.

(4) Taarifa itakayowasilishwa kwa mujibu wa Ibara ndogo ya

(3)(b) itafafanua makosa aliyoyatenda Rais, na itapendekeza kuwa Tume

ya Uchunguzi iundwe ili ichunguze tuhuma zilizotolewa dhidi ya Rais.

(5) Wakati wowote baada ya kupokea taarifa iliyotiwa saini na

Wabunge na kujiridhisha kuwa masharti ya Katiba kwa ajili ya

kuwasilisha hoja yametimizwa, Spika atamruhusu mtoa hoja

kuiwasilisha mbele ya Bunge na kisha Spika atalitaka Bunge, bila ya

kufanya majadiliano, lipige kura juu ya hoja ya kuunda Kamati ya

Uchunguzi.

(6) Endapo hoja ya kuunda Kamati ya Uchunguzi itaungwa

mkono na Wabunge wasiopungua asilimia sabini na tano ya Wabunge

wote, Spika atatangaza majina ya wajumbe wa Kamati ya Uchunguzi.


35

(7) Kamati ya Uchunguzi, kwa madhumuni ya Ibara hii, itakuwa na

wajumbe wafuatao:

(a) Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano, ambaye atakuwa

Mwenyekiti wa Kamati;

(b) Jaji Mkuu wa Tanzania Bara;

(c) Jaji Mkuu wa Zanzibar; na

(d) wajumbe wengine sita watakaoteuliwa na Spika.

(8) Endapo Bunge litapitisha hoja ya kuunda Kamatiya Uchunguzi,

Rais atahesabiwa kuwa hayupo kazini na nafasi ya madaraka ya Rais

yatatekelezwa na Makamu wa Rais hadi Spika atakapomfahamisha Rais juu

ya Azimio la Bunge kuhusiana na mashtaka yaliyotolewa dhidi yake.

(9) Ndani ya siku saba baada ya Kamati ya Uchunguzi kuundwa,

itachunguza na kuchambua mashtaka dhidi ya Rais, pamoja na kumpatia

Rais fursa ya kujieleza, kwa kufuata utaratibu uliowekwa na Kanuni za

Kudumu za Bunge.

(10) Mapema iwezekanavyo, na kwa vyovyote vile katika muda

usiozidi siku tisini, Kamati ya Uchunguzi itatoa taarifa yake kwa Spika.

(11) Baada ya Spika kupokea taarifa ya Kamati ya Uchunguzi,

taarifa hiyo itawasilishwa Bungeni kwa kufuata utaratibu uliowekwa na

Kanuni za Kudumu za Bunge.

(12) Baada ya taarifa ya Kamati ya Uchunguzi kuwasilishwa,

Bunge litaijadili taarifa hiyo na kutoa fursa kwa Rais kujieleza, na kisha,

kwa kura za Wabunge wasiopungua asilimia sabini na tano ya Wabunge

wote, Bunge litapitisha azimio kuwa mashtaka dhidi ya Rais ama

yamethibitika au hayakuthibitika.

(13) Endapo Bunge litapitisha azimio kuwa mashtaka dhidi ya Rais

yamethibitika na kwamba hastahili kuendelea kushika nafasi ya madaraka

ya Rais, Spika atamfahamisha Rais na juu ya Azimio la Bunge na Rais

atakuwa ameondolewa madarakani na Makamu wa Rais ataapishwa mara

moja kushika madaraka ya Rais.

(14) Endapo Rais ataacha kushika nafasi ya madaraka ya Rais

kutokana na mashtaka dhidi yake kuthibitika, hatakuwa na haki ya kupata

malipo yoyote ya uzeeni, posho wala kupata haki au nafuu nyingine

anazopewa Rais au mtu aliyekuwa Rais kwa mujibu wa Katiba au sheria za

nchi.

Maslahi

ya Rais


85

.-(1) Rais atalipwa mshahara na malipo mengineyo kama

yatakavyoainishwa na Tume ya Utumishi wa Umma na atakapostaafu

atapokea malipo ya uzeeni na stahili nyingine kutoka Mfuko Mkuu wa

Hazina ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano.

(2) Mshahara na malipo mengineyo yote ya Rais

hayatapunguzwa wakati Rais atakapokuwa bado ameshika madaraka

yake kwa mujibu wa Katiba hii.


36

(e) Makamu wa RaisMakamu

wa Rais wa

Jamhuri ya

Muungano


8
6.-(1) Kutakuwa na Makamu wa Rais ambaye atakuwa ndiye

Msaidizi Mkuu wa Rais kuhusu mambo yote ya Jamhuri ya Muungano kwa

jumla na:

(a) atafanya kazi zote atakazoagizwa na Rais;

(b) atakuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mahusiano ya Serikali; na

(c) atafanya kazi zote za Rais kama Rais hayuko kazini au yuko nje

ya nchi.

(2) Katika utekelezaji wa madaraka yake, Makamu wa Rais

atatekeleza au kusababisha utekelezaji wa jambo lolote au mambo yoyote

ambayo Rais ataagiza kwamba yatekelezwe.

(3) Bila kuathiri masharti ya Katiba hii, Makamu wa Rais

atawajibika kwa Rais kuhusu utekelezaji wa majukumu yake.

87.-

(1) Bila ya kuathiri masharti ya Ibara ya 72,Makamu wa Rais

atapatikana kwa kuchaguliwa katika uchaguzi pamoja na Rais, baada ya

kupendekezwa na chama chake au mgombea huru wakati ule ule

anapopendekezwa mgombea nafasi ya madaraka yaRais na watapigiwa kura

kwa pamoja.

(2) Endapo mgombea wa nafasi ya madaraka ya Rais atachaguliwa

basi na Makamu wa Rais atakuwa amechaguliwa.

(3) Mtu atateuliwa kugombea nafasi ya madaraka ya Makamu wa

Rais kwa kufuata kanuni kwamba endapo mgombea nafasi ya madaraka ya

Rais wa Jamhuri ya Muungano atatoka sehemu moja ya Washirika wa

Muungano, basi Makamu wa Rais atakuwa ni mtu anayetoka sehemu ya pili

ya Washirika Muungano.

Sifa za

Makamu

wa Rais


88.-

(1) Mtu hatateuliwa kugombea au kushika nafasi ya madaraka ya

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano isipokuwa tu kama anazo sifa

za kuchaguliwa kama Rais.

(2) Chama chochote au mtu yoyote anayekusudia kugombea kiti cha

Urais kama mgombea huru hatazuiwa kumpendekeza mtu yeyote kuwa

mgombea nafasi ya madaraka ya Makamu wa Rais kwa sababu tu kwamba

mtu huyo kwa wakati huo ameshika kiti cha Rais wa Zanzibar au Rais wa

Tanzania Bara.

(3) Makamu wa Rais hatakuwa na wadhifa mwingine wowote wa

kiserikali uliotajwa katika Katiba hii au sheria iliyotungwa na Bunge.

(4) Endapo mtu ambaye ni Rais wa Tanzania Bara au Rais wa

Zanzibar anateuliwa au kuchaguliwa kuwa Makamu wa Rais ataacha kiti cha

Rais wa Tanzania Bara au cha Rais wa Zanzibar, kadri itakavyokuwa.

Kiapo cha

Makamu

wa

Rais


89

. Makamu wa Rais, kabla ya kushika madaraka yake ataapishwa

na Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano, kiapo cha uaminifu na pia kiapo

kingine chochote kinachohusika na utendaji wa kazi yake kitakachowekwa

kwa mujibu wa Sheria iliyotungwa na Bunge.


37

Wakati

wa

Makamu

wa

Rais

kushika

madaraka


90

.-(1) Makamu wa Rais atashika nafasi yamadaraka ya Makamu wa

Rais siku hiyo hiyo Rais anaposhika madaraka.

(2) Makamu wa Rais aliyeteuliwa kwa mujibu wa Ibara ya 72 ataapa

na kushika madaraka yake baada ya uteuzi wake kuthibitishwa na Bunge.

(3) Isipokuwa kama atajiuzulu au atafariki mapema zaidi, mtu

aliyechaguliwa, au kuteuliwa kwa mujibu wa Ibara ya 72 kuwa Makamu wa

Rais, bila ya kuathiri masharti mengine ya Ibara hii, atashika kiti cha

Makamu wa Rais kwa muda wa miaka mitano tangu alipochaguliwa kuwa

Makamu wa Rais.

(4) Makamu wa Rais atashika kiti hicho hadi-

(a) muda wake utakapokwisha;

(b) akifariki dunia akiwa katika madaraka;

(c) atakapojiuzulu;

(d) atakapoapishwa kuwa Rais baada ya nafasi ya madaraka ya Rais

kuwa wazi;

(e) atakapotiwa hatiani kwa kosa lolote la jinai linaloonyesha utovu

wake wa uaminifu;

(f) atakapoapishwa Rais mwingine kushika nafasi ya madaraka ya

Rais pamoja na Makamu wake;

(g) atakapoondolewa madarakani baada ya kushtakiwa Bungeni kwa

mujibu wa masharti ya Katiba hii;

(h) atakapoacha kushika nafasi ya madaraka ya Makamu wa Rais

vinginevyo kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii.

Bunge

kumuondoa

Makamu

wa Rais


91.-

(1) Bunge litakuwa na madaraka ya kumshtaki Makamu wa Rais

kwa utaratibu unaotumika kumshtaki Rais kwa mujibu wa Katiba hii,

isipokuwa kwamba, hoja yoyote ya kumshtaki Makamu wa Rais itatolewa tu

iwapo:

(a) Rais amewasilisha hati kwa Spika inayoeleza kwamba Makamu

wa Rais ameacha au ameshindwa kutekeleza kazi za madaraka

ya Makamu wa Rais;

(b) amekuwa na mwenendo unaodhalilisha nafasi ya madaraka ya

Rais wa Jamhuri ya Muungano au kiti cha Makamu wa Rais; au

(c) anadaiwa kutenda kosa lolote kati ya makosa yanayoweza

kusababisha Rais kushtakiwa na Bunge kwa mujibu wa Katiba

hii,

isipokuwa kwamba, haitatolewa hoja ya namna hiyo ndani ya miezi kumi na

miwili tangu hoja hiyo ilipotolewa na ikakataliwa na Bunge.

(2) Masharti mengine kuhusu utaratibu wa kumshtaki Rais

yatatumika wakati wa kumuondoa madarakani Makamu wa Rais.

(3) Ikitokea kwamba kiti cha Makamu wa Rais ki wazi kutokana na

masharti yaliyomo katika Ibara ndogo ya (1), kifo au kujiuzulu basi mapema

iwezekanavyo na kwa vyovyote ndani ya siku zisizozidi kumi na nne baada

ya kushika madaraka yake, Rais atamteua mtu atakayekuwa Makamu wa

Rais na uteuzi huo utathibitishwa na Bunge kwa kura za Wabunge walio

wengi.


38

(4) Masharti mengine yote ya Ibara ya 84 yatatumika pia kuhusiana

na Makamu wa Rais isipokuwa tu kwamba Makamu wa Rais aliyeondolewa

tena madarakani chini ya Ibara ndogo ya (3), hatakuwa na sifa tena za

kushika nafasi ya Rais, Makamu wa Rais, Rais wa Tanzania Bara wala Rais

wa Zanzibar.

(5) Endapo Makamu wa Rais ataacha kushika nafasi ya madaraka

ya Makamu waRais kutokana na mashtaka dhidi yake kuthibitika,

hatakuwa na haki ya kupata malipo yoyote ya uzeeni, posho wala kupata

haki au nafuu nyinginezo anazopewa Makamu wa Rais au mtu aliyekuwa

Makamu wa Rais kwa mujibu wa Katiba au sheria za nchi.

SEHEMU YA PILI

B
ARAZA LA MAWAZIRI LA SERIKALI YA JAMHURI YA MUUNGANO

(a) Baraza la MawaziriKuundwa

kwa

Baraza la

Mawaziri


92.

-(1) Kutakuwa na Baraza la Mawaziri la Jamhuri ya Muungano

litakalokuwa na wajumbe wafuatao:

(a) Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano; na

(b) Mawaziri wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano.

(2) Mwanasheria Mkuu wa Serikali atahudhuria vikao vya Baraza la

Mawaziri lakini hatakuwa na haki ya kupiga kura.

(3) Baraza la Mawaziri ndicho chombo kikuu cha kumshauri Rais

kuhusu mambo yanayohusu utekelezaji wa madaraka na matumizi ya

mamlaka ya Rais.

(4) Bunge naMahakama hazitakuwa na uwezo wa kisheria

kuchunguza kama ushauri wowote au ushauri wa aina gani ulitolewa na

Baraza la Mawaziri kwa Rais.

Uteuzi wa

Mawaziri

na Naibu

Mawaziri


93.

-(1) Kutakuwa na Mawaziri na Naibu Mawaziri wa Serikali ya

Jamhuri ya Muungano watakaoteuliwa na Rais kwa kushauriana na Makamu

wa Rais na baadaye kuthibitishwa na Bunge.

(2) Kwa madhumuni ya Ibara ndogo ya (1), idadi ya Mawaziri wa

Serikali ya Jamhuri ya Muungano haitozidi kumi na tano.

(3) Serikali ya Jamhuri ya Muungano itakuwa na Wizara kwa

kuzingatia mamlaka ya Serikali kwa mujibu wa Katiba hii.

(4) Uteuzi wa Mawaziri na Naibu Waziri wa Serikali ya Jamhuri ya

Muungano utazingatia uwakilishi na uwiano wa Washirika wa Muungano.

(5) Majukumu ya Waziri na Naibu Waziri yatakuwa kama

yatakavyoainishwa na Rais kwenye Hati ya Uteuzi.

Sifa za

Mawaziri

na Naibu

Mawaziri


94.-

(1) Mtu atateuliwa kuwa Waziri au Naibu Waziri wa Serikali ya

Jamhuri ya Muungano ikiwa:

(a) ni raia wa kuzaliwa wa Jamhuri ya Muungano kwa mujibu wa

Sheria za nchi;na

(b) angalau ana shahada ya kwanza ya Chuo Kikuu

kinachotambulika kwa mujibu wa Sheria za nchi.


39

(2) Watu wafuatao hawatakuwa na sifa ya kuteuliwa kuwa

Mawaziri au Naibu Mawaziri katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano:

(a) Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, Wabunge wa

Bunge la Tanzania Bara, wajumbe wa Baraza la Wawakilishi la

Zanzibar au madiwani kutoka Washirika waMuungano;

(b) mtu aliyewahi kutiwa hatiani kwa makosa ya ubadhirifu wa

mali za umma, ama katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano,

Serikali ya Tanzania Bara au Serikali ya Mapinduzi ya

Zanzibar.

Kiapo,

muda na

masharti

ya kazi ya

Waziri na

Naibu

Waziri


95.

-(1) Waziri au Naibu Waziri hatashika nafasi ya madaraka mpaka

awe ameapa mbele ya Rais kiapo cha uaminifu na pia kiapo kingine

chochote kinachohusika na utendaji wa kazi yake kitakachowekwa na

sheria za nchi.

(2) Muda wa kushika nafasi ya madaraka ya Waziri au Naibu Waziri

utaanza tarehe ambayo Waziri au Naibu Waziri anayehusika ataapishwa.

(3) Kila Waziri anawajibika binafsi na kwa pamoja kwa Rais

katika utekelezaji wa majukumu na katika kutumia nafasi ya madaraka ya

Waziri.

(4) Waziri au Naibu Waziri atashika nafasi ya madaraka kwamuda

wote isipokuwa kama:

(a) atajiuzulu au kufariki;

(b) Rais atatengua uteuzi au kumwachisha kazi; au

(c) saa ishirini na nne zimetimia kabla ya Rais mteule kushika

madaraka ya Rais.

Utekelezaji

wa

shughuli

za

Serikali

Bungeni


96.

-(1) Mawaziri na Naibu Mawaziri hawatakuwa na haki ya

kuhudhuria vikao vya Bunge isipokuwa tu:

(a) endapo kutakuwa na hoja mahsusi ambayo Bunge linahitaji

ufafanuzi kwa Waziri husika; au

(b) endapo Serikali au Waziri ataomba na kuruhusiwa kuwasilisha

au kuitolea ufafanuzi hoja yoyote Bungeni.

(2) Kwa madhumuni ya Ibara ndogo ya (2), Waziri

atakayeruhusiwa kuhudhuria kikao cha Bunge anaweza kulihutubia Bunge.

(3) Serikali ya Jamhuri ya Muungano, chini ya mamlaka ya Rais,

ndiyo itakuwa na uwezo wa kufanya maamuzi juu ya sera za Serikali kwa

jumla, na Mawaziri, watawajibika kwa pamoja Bungeni kuhusu utekelezaji

wa sera nashughuli za Serikali ya Jamhuri ya Muungano.

(4) Kila Waziri atahudhuria vikao vya Kamati za Bunge kila

atakapohitajika na kutoa maelezo au ufafanuzi wa suala lolote linalohusu

utendaji katika nafasi ya madaraka yake.

(5) Kwa kuzingatia masharti mengine ya jumla ya Katiba hii,

Mawaziri watatoa maelezo au taarifa ambazo zinahitajika kutolewa

Bungeni kwa mujibu wa sheria za nchi.


40

(b) Mwanasheria Mkuu wa SerikaliMwanasheria

Mkuu wa

Serikali


97.

-(1) Kutakuwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye katika Katiba hii atatajwa tu

kwa kifupi kama "Mwanasheria Mkuu" ambaye atateuliwa na Rais na

kuthibitishwa na Bunge.

(2) Mtu anayestahili kuwa Mwanasheria Mkuu sharti awe na sifa

zifuatazo:

(a) awe ni raia wa kuzaliwa wa Jamhuri ya Muungano;

(b) awe na shahada ya Sheria ya Chuo Kikuu

kinachotambuliwa kwa mujibu wa sheria za nchi;

(c) awe ni mweledi na mwenye sifa ya kuteuliwa kuwa

wakili wa Mahakama;

(d) awe ni mtumishi mwandamizi katika utumishi wa umma

au taasisi zake;

(e) awe ni mtu ambaye amedumu na sifa hizo kwa muda

usiopungua miaka kumi na tano; na

(f) ana tabia njema na mwenendo usiotiliwa shaka na jamii.

(3) Mwanasheria Mkuu atakuwa ndiye mshauri mkuu wa Serikali ya

Jamhuri ya Muungano kuhusu mambo ya sheria na, kwa ajili hiyo,

atawajibika kutoa ushauri kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano kuhusu

mambo yote ya kisheria, na kutekeleza shughuli nyinginezo zozote

zenye asili au kuhusiana na sheria zitakazopelekwa kwake au

atakazoagizwa na Rais kuzitekeleza.

(4) Mwanasheria Mkuu atatekeleza kazi au shughuli nyingine

zilizokabidhiwa kwake na Katiba hii au sheria za nchi.

(5) Katika kutekeleza kazi zake, Mwanasheria Mkuu atakuwa na

haki ya kuhudhuria na kusikilizwa na Mahakama katika Jamhuri ya

Muungano na Mahakama Kuu za Washirika wa Muungano.

(c) Katibu Mkuu Kiongozi na Makatibu WakuuKatibu

Mkuu

Kiongozi


98

.-(1) Kutakuwa na Katibu Mkuu Kiongozi atakayeteuliwa na

Rais kutoka miongoni mwa watumishi waandamizi na kuthibitishwa na

Bunge.

(2) Katibu Mkuu Kiongozi atakuwa Katibu wa Baraza la Mawaziri,

Mwenyekiti wa Vikao vya Kamati Maalum ya Makatibu Wakuu na Mkuu

wa Utumishi wa Umma.

(3) Akiwa Mkuu wa Utumishi wa Umma, Katibu Mkuu Kiongozi

atakuwa na mamlaka ya kutoa maelekezo ya mara kwa mara kuhusiana na

masuala ya utumishi wa umma.

(4) Katika wadhifa wake wa Katibu wa Baraza la Mawaziri, Katibu

Mkuu Kiongozi atakuwa Mtendaji Mkuu katika Ofisi ya Baraza la

Mawaziri, na atatekeleza shughuli zifuatazo kwa kufuata maagizo ya jumla

au maalum atakayopewa na Rais, yaani:

(a) kuandaa ratiba ya mikutano na kutayarisha orodha ya shughuli

za Baraza la Mawaziri;

(b) kuandika na kuweka kumbukumbu za mikutano;


41

(c) kutoa taarifa na maelezo ya uamuzi wa Baraza la Mawaziri

kwa kila mtu au chombo cha umma kinachohusika na

uamuzi uliotolewa; na

(d) kutekeleza kazi na shughuli nyingine zozote ambazo Rais

ameagiza.

Makatibu

Wakuu


99.

-(1) Kutakuwa na Makatibu Wakuu watakaoteuliwa na Rais

kutoka miongoni mwa Watumishi Waandamizi katika utumishi wa umma

kama watakavyopendekezwa na Tume ya Utumishi wa Umma.

(2) Kila Katibu Mkuu atakuwa kiongozi na Mtendaji Mkuu wa

Wizara ya Serikali aliyopangiwa na Rais na atashika nafasi ya madaraka

ya Katibu Mkuu na kutekeleza majukumu yake kama itakavyoainishwa

katika sheria za nchi.

(3) Rais anaweza, kwa mapendekezo ya Tume ya Utumishi wa

Umma, kumteua mtumishi mwandamizi katika Utumishi wa Umma

kuwa Naibu Katibu Mkuu.

(4) Kila Katibu Mkuu atakuwa mshauri wa mwisho kwa Waziri

kwa masuala yote ya utendaji na atatoa ushauri kwa Baraza la

Mawaziri katika vikao na Kamati zitakazoitishwa na Katibu wa Baraza

la Mawaziri.

(5) Katibu Mkuu Kiongozi, Katibu Mkuu na Naibu Katibu

Mkuu hatashika madaraka yake mpaka kwanza aape mbele ya Rais

kiapo cha utii na uaminifu au kiapo kingine chochote kinachohusu

utendaji wa kazi zake.

(d) Utendaji Kazi wa Baraza la MawaziriKamati

Maalumu

ya

Makatibu

Wakuu


100.

Kutakuwa na Kamati Maalum ya Makatibu Wakuu

itakayoongozwa na Katibu Mkuu Kiongozi ambayo itakuwa na

majukumu ya kuchambua na kulishauri Baraza la Mawaziri juu ya

masuala mbalimbali kabla ya kuwasilishwa na kufanyiwa uamuzi na

Baraza hilo na itatekeleza majukumu mengine kama itakavyopangiwa

na Baraza la Mawaziri.

Sekretarieti

ya

Baraza la

Mawaziri


101.-

(1) Kutakuwa na Sekretarieti ya Baraza la Mawaziri

ambayo itakuwa na jukumu la kuhudumia Baraza la Mawaziri, Kamati

Maalum ya Makatibu Wakuu na kutekeleza majukumu mengine kama

itakavyopangiwa na Baraza la Mawaziri.

(2) Bunge linaweza kutunga sheria kuhusu utaratibu na

utekelezaji wa shughuli za Serikali.

SURA YA NANE

U
RATIBU WA MAHUSIANO YA WASHIRIKA WA MUUNGANO

Tume ya

Mahusiano

ya

Uratibu

wa

Serikali


102

.(1)Kutakuwa na Tume ya kusimamia na kuratibu

mahusiano baina ya Serikali ya Muungano na Serikali za Washirika wa

Muungano na kusimamia na kuratibu mahusiano baina ya Serikali za

Washirika wa Muungano, ambayo itajulikana kwa kifupi kama “Tume

ya Mahusiano na Uratibu wa Serikali”.


42

(2) Tume ya Mahusiano na Uratibu wa Serikali itaundwa na

wajumbe wafuatao:

(a) Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano ambaye

atakuwa Mwenyekiti;

(b) Rais wa Tanzania Bara;

(c) Rais wa Zanzibar;

(d) Mawaziri Wakaazi;

(e) Waziri mwenye dhamana ya mambo ya nje wa Serikali ya

Jamhuri ya Muungano.

Malengo

ya Tume


103.

Tume ya Mahusiano na Uratibu wa Serikali itakuwa na

malengo yafuatayo:

(a) kuweka utaratibu borana endelevu wa mashauriano na

mashirikiano baina ya Serikali ya Muungano na Serikali za

Washirika wa Muungano;

(b) kukuza na kuwezesha uratibu na mashirikiano miongoni

mwa Washirika wa Muungano kuhusu masuala yasiyo ya

Muungano kwa lengo la kuwezesha kufanana kwa kiwango

cha utoaji huduma kwa wananchi wote;

(c) kuweka mazingira mazuri kwa ajili ya Serikali ya

Muungano na Serikali za Washirika wa Muungano kujadili

juu ya utekelezaji wa mambo ya Muungano na yasiyo ya

Muungano kwa manufaa na ustawi wa wananchi wote; na

(d) kuweka mazingira mazuri ya utatuzi wa migogoro baina ya

Serikali ya Muungano na Washirika wa Muungano.

Majukum

u ya

Tume


104.-

(1) Tume ya Mahusiano na Uratibu ya Serikali itakuwa na

jukumu maalumu la kuwezesha uratibu na ushirikiano katika

kutekeleza masharti ya Katiba hii, sera, sheria, mipango na mikakati

baina ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Serikali za Washirika

wa Muungano na baina ya Serikali za Washirika na pia itakuwa

chombo maalumu kwa ajili ya:

(a) mashauriano na mashirikiano baina ya:

(i) Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Serikali za

Washirika wa Muungano; na

(ii) Serikali za Washirika wa Muungano zenyewe

katikamasuala yasiyo ya Muungano;

(b) kusimamia, kuratibu na kuhakikisha kwamba kuna kuwiana

kwa sera na sheria za Washirika wa Muungano katika masuala

yasiyo ya Muungano;

(c) mashauriano na ushirikiano baina ya Jamhuri ya Muungano na

taasisi za kimataifa kwa niaba ya nchi;

(d) usimamizi na ukuzaji wa masuala yenye maslahi kwa Taifa;

(e) usuluhishi na utatuzi wa migogoro baina ya:

(i) Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Serikali za

Washirika wa Muungano; na

(ii) Serikali za Washirika wa Muungano katika masuala

yasiyo ya Muungano;

(2) Kwa madhumuni ya Ibara ndogo ya (1)(e), endapo upande


43

wowote katika mgogoro hautaridhika na uamuzi wa Tume ya

Mahusiano na Uratibu wa Serikali, unaweza kukata rufani katika

Mahakama ya Juu na uamuzi wa Mahakama hio utakuwa ni wa

mwisho.

(3) Bunge linaweza kutunga sheria kwa ajili ya:

(a) kusimamia mahusiano na uratibu baina ya Serikali za

Washirika wa Muungano na kati yaSerikali ya Jamhuri ya

Muungano na Serikali za Washirika wa Muungano; na

(b) kuweka utaratibu wa utatuzi wa migogoro kwa mujibu wa

Ibara hii.

SURA YA TISA

BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO

SEHEMU YA KWANZA

K
UUNDWA KWA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO

Bunge la

Jamhuri ya

Muungano


105.

-(1) Kutakuwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano.

(2) Wajumbe wa Bunge watakuwa wa aina zifuatazo:

(a) Wabunge waliochaguliwa kuwakilisha majimbo ya

uchaguzi;

(b) Wabunge watano watakaoteuliwa na Rais kutoka miongoni

mwa watu wenye sifa za kuchaguliwa kuwa wabunge

kuwakilisha watu wenye ulemavu kwa kuzingatia uwiano wa

Washirika wa Muungano.

(3) Kwa madhumuni ya Ibara ya ndogo (2)(a), kila mkoa kwa

upande wa Tanzania Bara na wilaya kwa upande wa Zanzibar, itakuwa ni

jimbo la uchaguzi.

(4) Katika kila Jimbo la Uchaguzi kutakuwa na nafasi mbili za

ubunge, moja kwa ajili ya mwanamke na moja kwa ajili ya mwanamme.

(5) Wabunge wote katika kila Jimbo la Uchaguzi watapatikana kwa

kupigiwa kura na wananchi kwa mujibu wa masharti ya Katiba hiina sheria

inayoweka utaratibu kuhusu mambo ya uchaguzi.

Muda wa

Bunge


106

.-(1) Bila ya kuathiri masharti mengineyo ya Katiba hii, maisha

ya kila Bunge yatakuwa ni muda wa miaka mitano.

(2) Kwa madhumuni ya Ibara ndogo ya (1), maneno "maisha ya

Bunge" maana yake ni muda wote unaoanzia tarehe ambapo Bunge Jipya

litaitishwa kukutana kwa mara ya kwanza baada ya uchaguzi wa wabunge

na kuishia tarehe ya kuvunjwa kwa Bunge kwa ajili ya kuwezesha

uchaguzi mwingine kufanyika.

Madaraka

ya Bunge


107.

-(1) Bunge ndicho chombo kikuu cha Jamhuri ya Muungano

chenye madaraka, kwa niaba ya wananchi, kuisimamia Serikali ya Jamhuri

ya Muungano na vyombo vyake vyote katika utekelezaji wa majukumu

yake kwa mujibu wa Katiba hii.

(2)Katika kutekeleza majukumu yake, Bunge litakuwa na madaraka

yafuatayo:

(a) kujadili na kutoa ushauri katika mambo yote yenye maslahi


44

kwa taifa na umma wa Watanzania;

(b) kumuuliza Waziri yeyote suala lolote kuhusu mambo ya umma

katika Jamhuri ya Muungano ambayo yako katika wajibu wake;

(c) kujadili mgawanyo na kuidhinisha matumizi ya fedha kwa

Wizara, taasisi na mashirika ya Serikali;

(d) kujadili utekelezaji wa kila Wizara wakati wa Mkutano wa

Bunge wa kila mwaka wa bajeti;

(e) kujadili na kuidhinisha mpango wowote wa muda

mrefu au wa muda mfupi unaokusudiwa kutekelezwa na

Serikali katika Jamhuri ya Muungano;

(f) kutunga sheria ya kusimamia utekelezaji wa mpango

wowote wa muda mrefu au muda mfupi;

(g) kujadili na kuridhia mikataba ya kimataifa inayohusu

Jamhuriya Muungano na ambayo kwa masharti yake

inahitajikuridhiwa; na

(h) kujadili na kuridhia mikataba yote inayohusisha rasilimali na

maliasili zinazosimamiwa na Serikali ya Jamhuri ya

Muungano.

(3) Bunge litaisimamia Serikali kwa kuangalia mwenendo wa

utendaji wa Rais, Makamu wa Rais, Mawaziri na watendaji wakuu katika

utumishi wa umma.

Mipaka

ya Bunge

katika

kutumia

madaraka

yake


108.

-(1) Katika kutekeleza madaraka ya kuisimamia Serikali kwa

mujibu wa Katiba hii, wajibu wa Bunge itakuwa nikuishauri Serikali na

endapo Bunge halitaridhishwa na hatua zilizochukuliwa na Serikali katika

utekelezaji wa suala lililotolewa ushauri, basi Bunge litakuwa na haki ya

kuiwajibisha Serikali kwa mujibu wa madaraka iliyopewa katika Katiba

hii.

(2) Kwa madhumuni ya Ibara ndogo ya (1), Bunge halitachukua

hatua yoyote ya kiutendaji ambayo, kwa desturi ni shughuli za Serikali, na

halitatoa maagizo yoyote ya kiutendaji kwa Serikali na Watumishi wa

Umma, isipokuwa Bunge litashauri kuhusu suala lolote lililo katika

dhamana ya Waziri anayehusika.

Madaraka

ya

Bunge

kutunga

sheria


109.

-(1) Mamlaka ya kutunga sheria juu ya mambo yote

yanayohusu Jamhuri ya Muungano yatakuwa chini yaBunge.

(2) Mamlaka ya kutunga sheria katika Tanzania Bara na

Zanzibar juu ya mambo yote yasiyo ya Muungano yatakuwa chini ya

Bunge la Tanzania Bara na Baraza la Wawakilishi la Zanzibar.

(3) Endapo sheria iliyotungwa na Bunge inahusu jambo lolote

ambalo liko chini ya mamlaka ya Bunge la Tanzania Bara au Baraza la

Wawakilishi la Zanzibar, sheria hiyo itakuwa batili na itatenguka.

(4) Endapo sheria iliyotungwa na Bunge la Tanzania Bara au

Baraza la Wawakilishi la Zanzibar inahusu jambo lolote ambalo liko

chini ya mamlaka ya Bunge la Jamhuri ya Muungano, sheria hiyo

itakuwa batili na itatenguka.

(5)Bila ya kuathiri kutumika kwa Katiba ya Tanzania Bara na


45

Katiba ya Zanzibar, Katiba hii itakuwa na nguvu ya sheria katika

Jamhuri ya Muungano kwa mambo yanayohusu Muungano na endapo

sheria nyingine yoyote itakiuka masharti yaliyomo katika Katiba hii, basi

sheria hiyo nyingine, kwa kiasi kinachokiuka Katiba hii, itakuwa batili.

Utaratibu

wa

kutunga

sheria


110.-

(1) Bunge litatumia madaraka yake ya kutunga sheria kwa

kujadili na kupitisha Muswada wa Sheria ambao utawekwa saini na Rais.

(2) Bila kuathiri masharti ya Ibara ndogo ya (3), Muswada wa

Sheria unaweza kuandikwa na Serikali, Kamati ya Bunge au kikundi cha

Wabunge.

(3) Wakati wa kuandaa muswada wa sheria kuhusu jambo lolote la

Muungano, Serikali ya Jamhuri ya Muungano itahakikisha kwamba

inawashirikisha wananchi kwa ajili ya kupata maoni na mapendekezo juu

ya muswada huo.

(4) Bunge litatunga Kanuni za Kudumu zitakazoweka utaratibu

wa:

(a) kuwasilisha, kujadili na kupitisha Muswada wa Sheria; na

(b) utekelezaji bora wa masharti ya Ibara ndogo ya (3).

Utaratibu

wa

Kubadilisha

Katiba hii

na

baadhi ya

sheria


111

.-(1) Kwa kuzingatia masharti ya Ibara ya 110,Bunge linaweza

kutunga Sheria kwa ajili ya kubadilisha masharti yoyote ya Katiba hii kwa

kufuata Kanuni kwamba, Muswada wa Sheria kwa ajili ya kubadilisha

masharti yoyote ya Katiba hii utaungwa mkono kwa kura zisizopungua

theluthi mbiliya kura za Wabunge wote kutoka kila upande wa Muungano.

(2) Kwa madhumuni ya ufafanuzi wa masharti ya Ibara ndogo ya

(1) kubadilisha masharti ya Katiba hii au masharti ya sheria,maana yake ni

pamoja na kurekebisha au kusahihisha masharti haya au kufuta na kuweka

masharti mengine badala yake au kusisitiza au kubadilisha matumizi ya

masharti hayo.

Utaratibu

wa

kubadilisha

masharti

mahusus


112.

Bunge halitaweza kufanya mabadiliko ya Katiba kwa lengo la:

(a) kuongeza au kupunguza jambo lolote la Muungano; na

(b) uwepo wa Jamhuri ya Muungano,

mpaka kwanza mabadiliko hayo yaungwe mkono na wananchi wa

Washirika wa Muungano kwa Kura ya Maoni itakayoendeshwa na

kusimamiwa na Tume Huru ya Uchaguzi ya Jamhuri ya Muungano wa

Tanzania kwa mujibu wa sheria itakayotungwa na Bunge.

Utaratibu

wa

kutunga

sheria

kuhusu

mambo

ya fedha


113

.-(1) Bunge halitashughulikia jambo lolote kati ya mambo

yanayohusika na Ibara hii isipokuwa kama Rais amependekeza kwamba

jambo hilo lishughulikiwe na Bunge na pendekezo hilo la Rais liwe

limewasilishwa kwenye Bunge na Waziri.

(2) Mambo yanayohusika na Ibara hii ni yafuatayo:

(a) Muswada wa Sheria kwa ajili ya jambo lolote kati ya mambo

yafuatayo:


46

(i) kutoza kodi au kubadilisha kodi kwa namna

nyingine yoyote isipokuwa kupunguza;

(ii) kuagiza kwamba malipo au matumizi ya fedha

yafanywe kutokana na Mfuko Mkuu wa Hazina ya

Serikali au mfuko mwingine wowote wa Serikali au

kubadilisha kiwango hicho na namna nyingine

yoyote isipokuwa kupunguza;

(b) kuagiza kwamba malipo au matumizi ya fedha yafanywe

kutokana na Mfuko Mkuu wa Hazina ya Serikali au mfuko

mwingine wowote wa Serikali wakati ikifahamika kwamba

fedha iliyomo katika mifuko hiyo haikupangiwa itolewe kwa

ajili ya malipo au matumizi hayo, au kuagiza kwamba malipo

au matumizi yanayofanywa kutokana na mifuko hiyo

yaongezwe;

(c) kufuta au kusamehe deni lolote linalotakiwa lilipwe kwa

Serikali ya Jamhuri ya Muungano; au

(d) hoja au mabadiliko yoyote ya hoja kwa ajili ya lolote kati ya

mambo yaliyoelezwa katika aya ya (a) ya Ibara hii ndogo.

Madaraka

ya Mkuu

wa Nchi

kuhusu

Muswada

wa Sheria


114

.-(1) Muswadawa Sheria uliopitishwa na Bunge sharti kupata

saini ya Rais, ili kuthibitisha kukubaliwa kwake na Rais.

(2) Muswada wa Sheria uliyowasilishwa kwa Rais kwa ajili ya

kupata kibali utawekewa saini na Rais ndani ya siku zisizozidi thelathini

kutoka siku ambayo Muswada huo uliwasilishwa na kupokelewa na

Katibu wa Baraza la Mawaziri.

(3) Baada ya Muswada wa Sheria kuwasilishwa kwa Rais kwa

ajili ya kupata kibali chake, Rais anaweza kuukubali au kukataa kukubali

Muswada huo, na iwapo Rais atakataa kukubali Muswada huo basi

ataurudisha Bungeni pamoja na maelezo ya sababu za kukataa kukubali

Muswada huo.

(4) Baada ya Muswada wa Sheria kurudishwa Bungeni na Rais

kwa mujibu wa masharti ya Ibara hii, hauwezi kupelekwa tena kwa Rais

kwa ajili ya kupata kibali chake kabla kumalizika muda wa siku sitini tangu

uliporudishwa;

(5) Endapo katika kujadiliwa tena Bungeni kabla haujapelekwa

tena kwa Rais, Muswada uliorudishwa Bungeni na Rais umeungwa mkono

na Wabunge ambao idadi yao haipungui theluthi mbiliya Wabunge wote

basi, Muswada huo unaweza kuwasilishwa mapema zaidi kwa Rais.

(6) Iwapo Muswada uliorudishwa Bungeni na Rais na katika

kujadili ukaungwa mkono na Wabunge ambao idadi yao haipungui theluthi

mbiliya Wabunge wote na kupelekwa tena kwa Rais kwa ajili ya kupata

kibali chake, basi Rais atatakiwa kuweka saini kukubali Muswada wa

sheria husika kabla ya kumalizika muda wa siku sitini na endapo siku

sitini zitapita tangu Muswada huo ulipowasilishwa tena kwa Rais pasipo

Rais kuweka saini, itahesabika kwamba Muswada huo umepata kibali cha

Rais na utakuwa sheria ya nchi.

Kupitishwa

kwa hoja

za Serikali


115.-

(1) Endapo Bunge halitaridhishwa na mchanganuo au

mgawanyo wa hoja ya Bajeti iliyowasilishwa na serikali, Bunge linaweza


47

kurudisha hoja kuhusu Bajeti ya Serikali pamoja na mapendekezomahsusi

kuhusiana na upungufuuliobainika.

(2) Serikali itawajibika kuyafanyia kazi mapendekezo ya Bunge kwa

kadri itakavyowezekana na kisha kuwasilisha tena Bungeni hoja husika

pamoja na maelezo ya utekelezaji wa maelekezo ya Bunge na endapo Bunge

litakataa kwa mara ya pili hoja kuhusu Bajeti ya Serikali, basi hoja hiyo

itahesabika kuwa imepitishwa na Bunge.

SEHEMU YA PILI

WABUNGE


(a) Uchaguzi wa WabungeUchaguzi

wa

Wabunge


116

.-(1) Kila baada ya Bunge kumaliza muda wake wa kipindi cha

miaka mitano, kutakuwa na uchaguzi wa Wabunge katika Majimbo ya

uchaguzi kama itakavyotangazwa na Tume Huru ya Uchaguzi

utakaofanyika kwa mujibu wa sheria itakayotungwa na Bunge.

(2) Kutakuwa na uchaguzi wa Mbunge katika jimbo la uchaguzi

ikiwa:

kiti cha Mbunge aliyechaguliwa kuwakilisha jimbo la uchaguzi kwa

utaratibu wa mgombea huru, kitakuwa wazi kwa sababu nyingine yoyote

isiyohusika na Bunge kumaliza muda wake.

(3) Endapo tarehe ya Bunge kumaliza muda wake imetangazwa au

inafahamika, hakutakuwa na uchaguzi mdogo wa mbunge ndani ya kipindi

cha miezi kumi na minane kabla ya tarehe hiyo.

(4) Endapo Mbunge anayetokana na chama cha siasa atapoteza sifa

za kuwa mbunge kwa sababu yoyote isiyokuwa ya Bunge kumaliza muda

wake, Tume Huru ya Uchaguzi ya Jamhuri, kwa mujibu wa masharti

yatakayowekwa na sheria itakayotungwa na Bunge kwa ajili hiyo, itamteua

na kumtangaza kuwa mbunge mtumwingine kutoka kwenye orodha ya

majina ya wagombea iliyowasilishwa na chama hicho kwa mujibu wa Ibara

ndogo ya (5).

(5) Orodha ya majina ya wagombea kutoka kila chama cha siasa

iliyowasilishwa kwa Tume Huru ya Uchaguzi ya Jamhuri ya Muungano

katika Uchaguzi Mkuu ndiyo itakayotumiwa na Tume Huru ya Uchaguzi ya

Jamhuri ya Muungano baada ya kushauriana na chama cha siasa

kinachohusika, kwa madhumuni ya kujaza nafasi ya Mbunge inapotokea

kuwa wazi, wakati wowote wa Maisha ya Bunge.

Sifa za

kuchaguliwa

kuwa

Mbunge


117.

-(1) Bila ya kuathiri masharti yaliyomo katika Ibara hii, mtu

yeyote atakuwa na sifa za kuchaguliwa au kuteuliwa kuwa Mbunge

endapo:

(a) ni raia wa Jamhuri ya Muungano aliyetimiza umri wa miaka

ishirini na tano wakati wa kugombea;

(b) anajua kusoma na kuandika lugha ya Kiswahili au Kiingereza

na ana elimu isiyopungua kidato cha nne;

(c) ni mwanachama aliyependekezwa na chama cha siasa au

mgombea huru;

(d)ni mwadilifu na anayeheshimu haki za binadamu na

asiyedharau wala kubagua watu kwa misingi ya kabila, dini,


48

jinsi, maumbile au hali zao katika jamii; na

(e)katika kipindi cha miaka mitano kabla ya tarehe ya uchaguzi

hakuwahi kutiwa hatiani katika mahakama kwa kosa la

kukwepa kulipa kodi yoyote ya Serikali.

(2) Mtu hatakuwa na sifa za kugombea kuchaguliwa kuwa

Mbunge-

(a) ikiwa mtu huyo aliwahi kuwa Mbunge kwa vipindi vitatu

vya miaka mitano; au

(b) ikiwa imethibitishwa rasmi kwamba mtu huyo ana ugonjwa

wa akili;

(c) ikiwa mtu huyo amehukumiwa na Mahakama yoyote katika

Jamhuri ya Muungano na kupewa adhabu ya kifo au ya

kufungwa gerezani kwa muda unaozidi miezi sita kwa

kukutwa na hatia ya kosa lolote, vyovyote linavyoitwa,

linaloambatana na kukosa uaminifu; au

(d) ikiwa katika kipindi cha miaka mitano kabla ya tarehe ya

uchaguzi amepata kuhukumiwa na kupewa adhabu ya

kifungo kwa kosa linaloambatana na kukosa uaminifu au

kwa kuvunja sheria inayohusiana na Maadili ya Viongozi

wa Umma;

(e) ikiwa mtu huyo ana maslahi yoyote katika mkataba wa

Serikali wa aina yoyote aliyowekewa miiko maalum kwa

mujibu wa sheria iliyotungwa na Bunge, na iwapo amekiuka

miiko hiyo;

(f) ikiwa mtu huyo anashika madaraka ya ofisa mwandamizi

katika utumishi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano au

Washirika wa Muungano; au

(g) ikiwa kwa mujibu wa sheria iliyotungwa na Bunge

inayoshughulikia makosa yanayohusika na uchaguzi wa

aina yoyote, mtu huyo amezuiliwa kujiandikisha kama

mpiga kura au kupiga kura katika uchaguzi wa Wabunge.

(3) Bunge linaweza kutunga sheria kwa ajili ya kuweka masharti

yatakayomzuia mtu asichaguliwe kuwa Mbunge wa kuwakilisha Jimbo la

Uchaguzi ikiwa mtu huyo ni mwenye madaraka yanayohusika na shughuli

za kuongoza au kusimamia uchaguzi wa Wabunge au shughuli za

uandikishaji wa wapiga kura kwa ajili ya uchaguzi wa Wabunge.

(4) Katika aya ya (e) ya Ibara ndogo ya (2) ya Ibara hii "mkataba

wa Serikali" maana yake ni mapatano yoyote ya mkataba ambayo

mmojawapo wa walioshiriki ni Serikali ya Jamhuri ya Muungano au

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar au Serikali ya Tanzania Bara, Idara au

Taasisi yoyote ya Serikali yoyote kati ya hizo au mtumishi yeyote wa

Serikali aliyeshiriki katika majadiliano ya mkataba husika kwa niaba ya

Serikali yoyote miongoni mwa hizo.

(5) Watu wenye nyadhifa zifuatazo katika Utumishi wa Umma

hawatakuwa na sifa ya kuwa Wabunge:

(a) Rais na Makamu wa Rais;

(b) Rais wa Tanzania Bara na Rais wa Zanzibar na Makamu

wao;

(c) Spika na Naibu Spika wa Bunge;


49

(d) Waziri na Naibu Waziri;

(e) Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Naibu Mwanasheria

Mkuu wa Serikali;

(f)Katibu wa Baraza la Mawaziri na Makatibu Wakuu;

(g)viongozi na watumishi wa vyombo vya ulinzi na usalama;

(h) mtu ambaye ameajiriwa katika vyombo vya dola kama

askari;

(i) Katibu Mkuu na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Serikali;

(j)Jaji Mkuu, Jaji au Hakimu wa Mahakama, Wakili wa

Serikali na Ofisa Sheria Katika Serikali ya Jamhuri ya

Muungano au Serikali za Washirika;

(k)Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali;

(l) Mjumbe wa Tume Huru ya Uchaguzi; na

(m) mtu yeyote aliyeajiriwa, kuteuliwa au kuchaguliwa katika

utumishi wa umma.

(6) Kwa madhumuni ya kutoa fursa ya kukata rufani kwa mtu

yeyote:

(a) aliyethibitishwa rasmi kisheria kuwa ana ugonjwa wa akili;

(b) aliyehukumiwa na kupewa adhabu ya kifo au kufungwa

gerezani au chuo cha mafunzo; au

(c) aliyepatikana na hatia ya kosa lolote lililotajwa katika sheria

kwa mujibu wa Ibara ndogo ya (2),

mamlaka ya nchi itaweka utaratibu wa sheria kwa ajili ya kuweka masharti

kwamba hukumu inayopingwa haitakuwa na nguvu kwa ajili ya utekelezaji

wa masharti ya Ibara ndogo ya (2) hadi upite muda uliotajwa katika sheria

hiyo.

Watu

wenye

madaraka

Serikalini

kukoma

utumishi


118.

Iwapo mtu mwenye madaraka katika utumishi wa umma ya

aina iliyotajwa katika sheria itakayotungwa na Bungeataamua-

(a) kugombea nafasi ya kisiasa ya aina yoyote chini ya Katiba hii; au

(b) kugombea uongozi wa ngazi yoyote katika chama cha siasa,

mtu huyo atahesabiwa kuwa utumishi wake umekoma tangu siku ya

kuteuliwa kuwa mgombea wa nafasi ya kisiasa au kugombea uongozi

katika chama cha siasa.

Utaratibu

wa

uchaguzi

wa

Wabunge


119.-

(1) Wabunge wanaowakilisha majimbo ya uchaguzi

watachaguliwa na wananchi kwa kufuata masharti ya Katiba hii na vile vile

masharti ya sheria iliyotungwa na Bunge kwa mujibu wa Katiba hii,

inayoweka masharti kuhusu uchaguzi wa Wabunge.

(2) Wagombea uchaguzi katika majimbo ya Uchaguzi watatakiwa

kuwasilisha majina yao kwa Tume Huru ya Uchaguzi ya Jamhuri ya

Muungano wa Tanzania kwa mujibu wa utaratibu uliowekwa na sheria

iliyotungwa na Bunge.

Kiapo cha

Wabunge


120

. Kila Mbunge atatakiwa kuapishwa katika Bunge kiapo cha

uaminifu kabla hajaanza kushiriki katika shughuli za Bunge, lakini

Mbunge anaweza kushiriki katika uchaguzi wa Spika hata kabla

hajaapishwa.


50

Masharti

ya kazi ya

Wabunge


121

. Wabunge watashika madaraka yao kwa mujibu wa Katiba hii,

na watalipwa mshahara, posho na malipo mengine kama yatakavyopangwa

na Tume ya Utumishi wa Umma kwa mujibu wa sheria za nchi.

Muda wa

Wabunge

kushika

madaraka


122.

-(1) Mbunge atakoma kuwa Mbunge ikiwa litatokea lolote kati

ya mambo yafuatayo:

(a) tukio lolote ambalo, kama asingekuwa Mbunge lingemfanya

asiwe au apoteze sifa za kuchaguliwa au kuteuliwa kwa mujibu

wa masharti ya Katiba hii;

(b)atakosa kuhudhuria vikao vya Mikutano ya Bunge mitatu

mfululizo bila ya ruhusa ya Spika;

(c)itathibitishwa kwamba amevunja masharti ya Sheria ya

Maadili ya Viongozi wa Umma;

(d)atashindwa kufanya kazi za Mbunge kwa muda wa miezi sita

mfululizo kutokana na ugonjwa wa akili au afya ya mwili au

kizuizi ndani ya gereza;

(e)ikiwa atashindwa kutoa tamko rasmi kuhusu sifa za kuwa

Mbunge au taarifa rasmi kuhusu mali kwa mujibu wa

masharti ya Katiba hii katika muda uliowekwa mahsusi na

sheria za nchi;

(f) ikiwa atajiuzulu ubunge; au

(g) ikiwa ataondolewa madarakani kwa mujibu wa masharti ya

Katiba hii.

(2) Mbunge anaweza kukata rufani, kwa mujibu wa sheria za nchi

kupinga hukumu ya kuthibitishwa kwake kuwa ni mtu mwenye ugonjwa

wa akili au kupinga adhabu ya kufungwa gerezani, au kupinga kupatikana

kwake na hatia kwa kosa la aina iliyotajwa katika Ibara ndogo ya (1).

Uwajibikaji

wa

Wabunge


123

.-(1) Mbunge atashika madaraka yake kwa mujibu wa Katiba

hii, na wakati wote atawajibika moja kwa moja kwa wapiga kura wake na

chama chake cha siasa ikiwa mbunge huyo ametokana na chama cha siasa.

(2) Mbunge aliyependekezwa na chama cha siasa, hatapoteza

Ubunge wake ikiwa Mbunge huyo atafukuzwa au kuvuliwa uanachama wa

chama chake.

(3) Endapo mbunge, kwa ridhaa yake atajiondoa au kujivua

uanachama kutoka chama chake cha siasa, Mbunge huyo atapoteza sifa za

kuwa Mbunge na atasita kuwa Mbunge.

Haki ya

wapiga

kura

kumwajibisha

Mbunge.


124

.-(1) Bila ya kuathiri masharti ya Ibara ya123 ya Katiba hii,

wananchi watakuwa na haki ya kumuondoa Mbunge wao madarakani,

endapo Mbunge atafanya mojawapo au zaidi ya mambo yafuatayo:

(a) kuunga mkono sera ambazo zinaenda kinyume na maslahi ya

wapiga kura au kinyume na maslahi ya Taifa;

(b)kushindwa kuwasilisha au kutetea kwa dhati hoja zinazotokana na

kero za wapiga kura wake;

(c) kuacha kuishi au kuhamisha makaazi yake kutoka eneo la Jimbo la


51

Uchaguzi kwa zaidi ya miezi sita bila sababu za msingi;

(d)kutohudhuria vikao vya Bunge vitatu mfululizo bila ya ruhusa ya

Spika;

(e) kuajiriwa au kufanya kazi nyingine na kuacha kuzingatia kazi yake

ya kuonana na wapiga kura wake;

(f) kufanya biashara, kumiliki makampuni au kuwa na hisa katika

makampuni ambayo yana mikataba au mahusiano ya kibiashara na

taasisi za umma kwa namna ambayo inaleta mgongano wa

kimaslahi;

(g)kutiwa hatiani kwa kosa linalohusiana na rushwa au kosa jingine la

jinai;

(h)kutenda kitendo ambacho ni kinyume na maadili au kukosa

uaminifu; au

(i) mambo mengine yatakayoainishwa kwenye sheria ya Bunge.

(2) Bunge litatunga sheria kuweka masharti ya namna ya kuendesha

uchunguzi kwa Mbunge atakayeshindwa kutekeleza majukumu yake kwa

wapiga kura wake na utaratibu wa kumuondoa mbunge.

Uamuzi

wa

suala

kama

mtu ni

Mbunge


125.-(

1) Kila shauri kwa ajili ya kupata uamuzi juu ya suala-

(a) kama uchaguzi wa Mbunge ulikuwa halali au sivyo; au

(b) kama Mbunge amekoma kuwa Mbunge na nafasi ya madaraka

katika Bunge iko wazi au hapana,

litafunguliwa na kusikilizwa kwanza katika Mahakama Kuu.

(2) Bunge laweza kutunga sheria kwa ajili ya kuweka masharti

kuhusu mambo yafuatayo-

(a) watu wanaoweza kufungua shauri katika Mahakama Kuu kwa ajili

ya kupata uamuzi juu ya suala lolote kwa mujibu wa masharti ya

Ibara hii;

(b)sababu na nyakati za kufungua shauri la namna hiyo, utaratibu wa

kufungua shauri na masharti yanayotakiwa yatimizwe kwa kila

shauri kama hilo; na

(c)kutaja mamlaka ya Mahakama Kuu juu ya shauri kama hilo na

kueleza utaratibu wa kusikiliza shauri lenyewe.

Tamko

rasmi la

Wabunge

kuhusu

maadili

ya

Viongozi


126.

-(1) Kila Mbunge kabla ya kumalizika siku thelathini tangu

aapishwe kushika nafasi yamadaraka ya Mbunge sharti awasilishe kwa

Tume ya Maadili ya Uongozi na Uwajibikaji nakala mbili za tamko

rasmi kwamba hajapoteza sifa za kuwa mbunge kwa mujibu wa masharti

ya Katiba hii.

(2) Tamko rasmi lililotajwa katika Ibara ndogo ya (1),

litatolewa katika fomu maalum itakayowekwa kwa mujibu wa sheria

za nchi.

Wabunge

kutoa

taarifa ya

mali


127.

-(1) Kila Mbunge atawasilisha kwa Katibu wa Bunge nakala

mbili za taarifa rasmi katika fomu maalum maelezo ya mali yake na kadri

itakavyokuwa, mali ya mke au mume wake.


52

(2) Katibu wa Bunge atawasilisha kwa Tume ya Maadili ya

Uongozi na Uwajibikaji nakala moja ya kila taarifa rasmi iliyowasilishwa

kwake kwa mujibu wa masharti ya Ibara hii.

SEHEMU YA TATU

U
ONGOZI WA BUNGE

(a) Spika na Naibu SpikaSpika na

mamlaka

yake


128

.-(1) Kutakuwa na Spika wa Bunge ambaye atachaguliwa na

Wabunge na ambaye atakuwa ndiye Kiongozi wa Bunge na atawakilisha

Bunge katika vyombo na vikao vingine vyote nje ya Bunge.

(2) Waziri, Naibu Waziri, Mbunge au mtu mwenye madaraka ya

aina nyingine yoyote yatakayotajwa na Sheria iliyotungwa na Bunge kwa

madhumuni ya Ibara hii, hataweza kuchaguliwa kuwa Spika.

(3) Mtu yeyote atakayechaguliwa kuwa Spika atatakiwa, kabla ya

kumaliza siku thelathini tangu kuchaguliwa kwake, kuwasilisha kwa Tume

ya Maadili ya Viongozi na Uwajibikaji tamko rasmi kwamba hajapoteza

sifa za uchaguzi kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii, tamko hilo

litatolewa katika fomu maalum itakayowekwa kwa mujibu wa sheria

iliyotungwa na Bunge.

(4) Spika atatakiwa kuwasilisha kwa Rais nakala mbili za taarifa

rasmi ya maelezo ya mali yake, kadri itakavyokuwa, mali ya mke au mume

wake.

Ukomo

wa

mamlaka

ya Bunge


129.-

(1) Spika atakoma kuwa Spika na ataacha nafasi ya madaraka

ya Spika litokeapo lolote kati ya mambo yafuatayo-

(a) atachaguliwa kuwa Mbunge;

(b) kutatokea jambo lolote ambalo, kama asingekuwa Spika,

lingemfanya mtu huyo asiwe na sifa za uchaguzi au apoteze

sifa za uchaguzi wa Spika;

(c) ataondolewa kwenye madaraka ya Spika kwa Azimio la

Bunge lililoungwa mkono na Wabunge ambao idadi yao

haipungui theluthi mbili ya Wabunge wote; au

(d) atashindwa kuwasilisha kwa Rais tamko rasmi kwa mujibu

wa masharti ya Katiba hii; au

(e) atapatikana na hatia kwa kosa la kutoa habari za uongo, kwa

kiapo kinyume cha sheria kuhusu tamko rasmi lolote

lililotolewa kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii; au

(f) atashindwa kuwasilisha taarifa ya mali kwa mujibu wa

masharti ya Katiba hii kabla ya kumalizika muda uliowekwa

kwa ajili hiyo;au

(g) itathibitika kuwa amevunja masharti ya Sheria inayohusu

Maadili ya Viongozi wa Umma.

(2) Isipokuwa shughuli ya kumchagua Spika, hakuna shughuli

yoyote itakayotekelezwa katika Bunge wakati wowote ambao nafasi ya

madarakaya Spika itakuwa wazi.


53

Naibu

Spika


130

.-(1) Kutakuwa na Naibu Spika wa Bunge ambaye atachaguliwa

na Wabunge.

(2) Waziri, Naibu Waziri, Mbunge au mtu mwenye madaraka ya

aina nyingine yoyote yatakayotajwa na Sheria iliyotungwa na Bunge kwa

madhumuni ya Ibara hii, hataweza kuchaguliwa kuwa Naibu Spika.

(3) Wabunge watamchagua Naibu Spika nyakati zifuatazo-

(a) Bunge litakapokutana kwa mara ya kwanza baada ya Uchaguzi

Mkuu au mapema iwezekanavyo baada ya wakati huo; na

(b) katika kikao cha kwanza cha Bunge baada ya nafasi ya

madaraka yaNaibu Spika, kuwa wazi kwa sababu yoyote

isiyohusika na Bunge kuvunjwa au mapema iwezekanavyo

baada ya kikao hicho.

(4) Naibu Spika, atakoma kuwa Naibu Spika na ataacha nafasi ya

madaraka ya Naibu Spika litokeapo lolote kati ya mambo yafuatayo-

(a)atachaguliwa kuwa Mbunge;

(b) kutatokea jambo lolote ambalo kama asingekuwa Naibu Spika,

lingemfanya mtu huyo asiwe na sifa za uchaguzi au apoteze sifa

za uchaguzi wa Naibu Spika; au

(c) ataondolewa kwenye madaraka ya Naibu Spika kwa Azimio la

Bunge.

Utaratibu

wa

kumchagua

Spika na

Naibu

Spika


131

.-(1) Kutakuwa na uchaguzi wa Spika katika kikao cha kwanza

cha Mkutano wa Kwanza wa Bunge Jipya, na katika kikao cha kwanza

chochote mara baada ya kutokea nafasi ya madaraka ya Spika kuwa wazi.

(2) Kutakuwa na uchaguzi wa Naibu Spika wakati wowote katika

Mkutano wa Kwanza wa Bunge Jipya na vile vile katika kikao cha kwanza

cha Bunge kitakachofuata mara baada ya kutokea nafasi ya madaraka ya

Naibu Spika kuwa wazi.

(3) Uchaguzi wa Spika na Naibu Spika, utafanywa kwa kura ya siri,

na utaendeshwa kwa kufuata utaratibu uliowekwa na Kanuni za Bunge.

(4) Spika na Naibu Spika watachaguliwa kwa masharti kwamba,

endapo Spika atatoka upande mmoja wa Washirika wa Muungano, Naibu

Spika atatoka upande wa pili wa Washirika wa Muungano.

(5) Isipokuwa kama ataacha madaraka yake, Spika na Naibu Spika

watakaa madarakani kwa vipindi visivyozidi viwili vya miaka mitano.

(6) Mtu yeyote atakayechaguliwa kuwa Spika au Naibu Spika

atatakiwa, kabla ya kuanza kutekeleza madaraka yake, kuapishwa katika

Bunge kiapo cha uaminifu.

Sifa za

mtu

anayefaa

kuchaguliwa

kuwa

Spika au

Naibu

Spika.


132

. Mtu atastahili kuchaguliwa kuwa Spika au Naibu Spika

endapo atakuwa na sifa zifuatazo-

(a) angalau awe na elimu ya Chuo Kikuu kinachotambulika kwa

mujibu wa sheria za nchi;

(b) awe na sifa za kumuwezesha kuchaguliwa kuwa Mbunge;

(c) wakati wa kugombea, awe mwenye umri usiopungua miaka

arobaini; na


54

(d) asiwe kiongozi au amewahi kuwa kiongozi wa juu wa chama

cha siasa katika kipindi cha miaka mitano kabla ya tarehe ya

kuomba kuchaguliwa kushika nafasi ya madaraka ya Spika

au Naibu Spika.

(b) Ofisi ya BungeKatibu wa

Bunge


133

.-(1) Kutakuwa na Katibu wa Bunge ambaye atateuliwa na

Tume ya Utumishi ya Bunge kutoka miongoni mwa watu wenye madaraka

ya juu katika utumishi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano.

(2) Katibu wa Bunge atakuwa ndiye Mtendaji Mkuu wa Ofisi ya

Bunge na atawajibika kwa utendaji bora wa shughuli za Bunge kwa

kuzingatia masharti ya Katiba hii na sheria za nchi.

Sekretarieti

ya Bunge


134

.(1) Kutakuwa na Sekretarieti ya Bunge itakayokuwa na

watumishi kutoka sehemu zote Washirika wa Muungano kwa kuzingatia

ngazi za utumishi kwa mujibu wa mahitaji ya shughuli za Bunge kama

itakavyoamuliwa na Tume ya Utumishi ya Bunge.

(2) Sekretarieti ya Bunge chini ya uongozi wa Katibu wa Bunge,

itatekeleza kazi na shughuli zote zilizowekwa au zitakazokuwa ni muhimu

kwa ajili ya kuhakikisha utekelezaji bora wa shughuli za Bunge, Wabunge

na madaraka ya Bunge.

SEHEMU YA NNE

U
TARATIBU WA SHUGHULI BUNGENI

Kanuni za

Kudumu

za

Bunge


135

.-(1) Bila ya kuathiri masharti ya Katiba hii, Bunge linaweza

kutunga Kanuni za Kudumu kwa ajili ya kuweka utaratibu wa kutekeleza

shughuli zake.

(2) Kanuni za Kudumu zilizotungwa kwa mujibu wa Ibara hii,

zinaweza kuweka utaratibu wa Mawaziri kuiwakilisha Serikali ndani ya

Bunge, kusimamia utekelezaji wa shughuli za Sekretarieti ya Bunge,

utekelezaji wa Shughuli za Bunge ndani ya Bunge, Kamati na Kamati

Ndogo za Bunge.

Rais

kulihutubia

Bunge


136

.-(1) Rais atalihutubia Bunge Jipya katika Mkutano wa Kwanza

na kulifungua rasmi.

(2) Bila ya kuathiri masharti ya Ibara ndogo ya (1), Rais anaweza

wakati wowote kulihutubia Bunge au kupeleka kwenye Bunge taarifa

ambayo itasomwa na Kiongozi wa Shughuli za Serikali Bungeni.

(3) Rais anaweza kulihutubia Bunge katika kila kikao cha mwisho

wa mwaka kuelezea utekelezaji wa majukumu mbalimbali kwa mujibu wa

Katiba hii.

Mikutano

ya

Bunge


137

.-(1) Bunge litafanya mikutano yake mahali ambapo ni desturi

kufanya Mikutano hiyo au mahali pengine popote katika Jamhuri ya

Muungano patakapotajwa na Spika kwa ajili hiyo.

(2) Mkutano wa Kwanza wa Bunge Jipya katika Maisha ya Bunge


55

utaitishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano na utaanza siku ile ambayo

Bunge limegizwa kukutana, na kila Mkutano unaofuata utaanza siku

yoyote itakayopangwa na Bunge au siku yoyote itakayopangwa kwa

mujibu wa Kanuni za Bunge.

(3) Rais anaweza kuitisha Mkutano wa Bunge wakati wowote kwa

mujibu wa masharti ya Katiba hii.

Uongozi

na

vikao vya

Bunge


138.

Kila kikao cha Bunge kitaongozwa na mmoja wapo wa watu

wafuatao-

(a) Spika; au

(b) ikiwa Spika hayupo, Naibu Spika; au

(c) ikiwa Spika na Naibu Spika wote hawapo, Mbunge yeyote

aliyechaguliwa na Bunge kwa ajili hiyo.

Akidi ya

vikao vya

Bunge.


139

.-(1) Akidi ya kila kikao cha Bunge ni nusu ya Wabunge wote,

isipokuwa kama imeelezwa vinginevyo katika Katiba hii.

(2) Kila suala litakalowasilishwa kwa ajili ya kupata uamuzi wa

Bunge litaamuliwa kwa kufuata wingi wa kura za Wabunge waliohudhuria

na kupiga kura.

(3) Spika, Naibu Spika au mtu mwingine atakayeongoza kikao cha

Bunge, hatakuwa na kura ya kawaida bali atakuwa na kura ya uamuzi

kukitokea usawa wa kura.

Kamati za

Bunge


140

.-(1) Bunge linaweza kuunda Kamati za Bunge za namna

mbalimbali kadri litakavyoona inafaa kwa ajili ya utekelezaji bora wa

madaraka yake.

(2) Kanuni za Bunge zinaweza kufafanua muundo na shughuli za

Kamati za Bunge zitakazoundwa kwa mujibu wa masharti ya Ibara hii.

SEHEMU YA TANO

M
ADARAKA NA HAKI ZA BUNGE

Uhuru wa

majadilia

no

Bungeni


141

.-(1) Wabunge wakiwa Bungeni, watakuwa na uhuru wa kutoa

mawazo, maoni na majadiliano na uhuru huo hautavunjwa wala kuhojiwa

na chombo chochote katika Jamhuri ya Muungano, au katika Mahakama au

mahali pengine nje ya Bunge.

(2) Bila ya kuathiri masharti ya Katiba hii au sheria nyingine

yoyote, Bunge litakuwa na uhuru wa maoni na Mbunge yeyote akiwa

Bungeni kwa vyovyote itakavyokuwa, hatatakiwa kutoa kauli za uongo,

kuudhi au kumuumiza Mbunge au mtu mwingine yeyote katika jamii.

(3)Bila ya kuathiri masharti ya Ibara ndogo ya (2), Mbunge yeyote

hatashtakiwa kwa kosa la jinai au kufunguliwa shauri la madai

mahakamani kutokana na jambo lolote alilolisema ndani ya Bunge.

(4) Bunge linaweza kutunga sheria kwa ajili ya kuweka masharti ya

kuwezesha mahakama na sheria kuhifadhi na kutilia nguvu uhuru wa

mawazo, majadiliano na utaratibu wa shughuli katika Bunge.


56

Mipaka

ya

majadiliano

Bungeni


142.

-(1) Bila ya kuathiri masharti ya Katiba hii yanayolinda na

kuhifadhi uhuru wa mawazo na majadiliano katika Bunge, ni marufuku

kusema uongo Bungeni na kwa sababu hiyo, Mbunge anapokuwa

akizungumza ndani ya Bunge ana wajibu wa kuhakikisha kwamba

anatoa kauli au maelezo kuhusu jambo au suala ambalo yeye mwenyewe

anaamini kuwa ni la kweli na siyo jambo la kubuni au la kubahatisha tu.

(2) Mbunge anapokuwa akizungumza Bungeni hatahesabika wala

kutafsiriwa kuwa anasema uongo iwapo anafanya rejea ya habari kuhusu

jambo lililotangazwa au lililoandikwa na vyombo vya habari au nyaraka

nyingine yoyote ambayo chanzo chake kinafahamika au kitaelezwa na

Mbunge huyo.

SURA YA KUMI

MAHAKAMA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

SEHEMU YA KWANZA

M
ISINGI YA UTOAJI HAKI NA UHURU WA MAHAKAMA

Kuanzishwa

kwa

Mahakama

ya

Tanzania


143

.-(1) Kutakuwa na Mahakama ya Jamhuri ya Muungano

wa Tanzania.

(2) Mahakama ya Jamhuri ya Muunganokupitia Katiba hii,

itakuwa na mamlaka kutoka kwa wananchi na itatekeleza mamlaka

yake kupitia Mahakama ya Juu na Mahakama yaRufani.

(3) Mahakama ya Jamhuri ya Muunganoitakuwa ni chombo

chenye mamlaka ya mwisho ya utoaji haki katika Jamhuri ya

Muungano.

Misingi

ya utoaji

haki


144.

Katika kutoa uamuzi wa mashauri ya madai na jinai kwa

kuzingatia sheria, Mahakama ya Jamhuri ya Muunganoitafuata kanuni

zifuatazo, yaani:

(a) kutenda haki kwa wote bila kujali hali ya mtu kijamii,

kisiasa, kiutamaduni au kiuchumi;

(b) kutochelewesha haki bila sababu ya kimsingi;

(c) kutoa fidia ipasayo kwa watu wanaoathirika kutokana na

makosa ya watu wengine, na kwa mujibu wa sheria za

nchi zilizotungwa mahususi kwa ajili hiyo;

(d) kukuza na kuendeleza usuluhishi baina ya wanaohusika

katika migogoro; na

(e) kutenda haki bila kufungwa na masharti ya kiufundi

yanayoweza kuchelewesha au kukwamisha haki

kutendeka.

Uhuru wa

Mahakama


145.-

(1) Katika kutekeleza mamlaka ya utoaji haki, Mahakama

ya Jamhuri ya Muunganoitaongozwa na masharti ya Katiba hii na

haitaingiliwa ama kwa kudhibitiwa, kushinikizwa au kupewa maelekezo

na mtu au chombo chochote.

(2) Nafasi ya madaraka ya Jaji wa Mahakama ya Juu au

Mahakama ya Rufani haitafutwa wakati wowote ule ikiwa kuna mtu

ambaye kwa wakati huo anashikilia nafasi hiyo.


57

(3) Mishahara na malipo mengine ya Majaji wa Mahakama ya

Juu na Mahakama ya Rufani yatalipwa kutoka katika Mfuko Mkuu wa

Hazina ya Serikali.

(4) Mshahara na malipo mengine yanayolipwa kwa Jaji wa

Mahakama ya Juu au wa Mahakama ya Rufani hayatabadilishwa kwa

maana ya kumuondolea faida Jaji husika.

(5) Malipo ya mafao ya kustaafu ya Jaji wa Mahakama ya Juu au

Jaji wa Mahakama ya Rufani hayatabadilishwa kwa maana ya

kumuondolea faida Jaji husika wakati wote wa uhai wake.

(6) Mtumishi yeyote wa Mahakama hatoshtakiwa kwa jambo

lolote alilolifanya au kutolifanya kwa nia njema katika utekelezaji wa

shughuli ya utoaji haki kwa mujibu wa Sheria.

SEHEMU YA PILI

M
UUNDO WA MAHAKAMA

(a) Mahakama za Jamhuri ya MuunganoMuundo

wa

Mahakama


146.

-(1) Bila ya kuathiri masharti yoyote yaliyotangulia katika

Sehemu hii, kutakuwa na Muundo wa Mahakama katika Jamhuri ya

Muungano utakaokuwa kama ifuatavyo:

(a) Mahakama ya Juu; na

(b) Mahakama ya Rufani.

(2)Mahakama Kuu ya Tanzania Bara na Mahakama Kuu ya

Zanzibar zitakuwa na mamlaka sawa ya kusikiliza katika ngazi ya awali,

mashauri ya madai na jinai kuhusu Mambo ya Muungano katika maeneo

ya utawala ya Washirika wa Muungano.

(b) Mahakama ya Juu ya Jamhuri ya MuunganoMahakama

ya Juu


147.-

(1)Kutakuwa na Mahakama ya Juu ya Jamhuri ya

Muungano au kwa kifupi itaitwa “Mahakama ya Juu” ambayo itakuwa

na:

(a) Jaji Mkuu ambaye atakuwa Rais wa Mahakama ya Juu;

(b) Naibu Jaji Mkuu ambaye atakuwa Makamu wa Rais wa

Mahakama ya Juu; na

(c) Majaji wengine wa Mahakama ya Juu wasiopungua saba.

(2)Uteuzi wa Majaji wa Mahakama ya Juu utazingatia sifa

zitakazoainishwa katika Katiba hii na uwakilishi wa sehemu mbili za

Washirika waMuungano.

Akidi ya

vikao vya

Mahakama

ya Juu


148.-

(1)Akidi ya kikao cha Mahakama ya Juu itakuwa ni Majaji

wa Mahakama ya Juu watano.

(2) Akidi ya Majaji katika vikao vya Mahakama ya Juu kwa

madhumuni ya kusikiliza shauri linalohusu masuala yaliyoainishwa

katika Ibara ya 149(1) (a), (b), (c) na (e) itazingatia uwakilishi wa

sehemu mbili za Muungano.

(3) Kila shauri na rufani inayohitaji uamuzi wa Mahakama ya

Juu itaamuliwa kwa kufuata kauli ya walio wengi kati ya Majaji wa


58

Mahakama ya Juu waliosikiliza shauri au rufani hiyo.

Madaraka

ya

Mahakama

ya Juu


149.-

(1) Mahakama ya Juu itakuwa ni ngazi ya mwisho ya rufani

katika Jamhuri ya Muungano na itakuwa na madaraka ya:

(a) pekee na ya awali ya kusikiliza na kuamua mashauri

yanayohusu matokeo ya uchaguzi wa Rais wa Jamhuri ya

Muungano;

(b) kusikiliza na kuamua mashauri yanayoletwa na Serikali ya

Muungano au Serikali za Washirika kuhusu tafsiri ya Katiba

hii;

(c) kusikiliza na kuamua migogoro baina ya Washirika wa

Muungano au baina wa Mshirika wa Muungano na Serikali

ya Muungano;

(d) kusikiliza na kuamua rufani kutoka Mahakama ya Rufani;

(e) kutoa maoni ya kiushauri kwa Serikali ya Muungano au

Serikali za Washirika; na

(f) kusikiliza na kuamua shauri lolote litakalowasilishwa mbele

yake kwa mujibu wa Katiba hii au sheria nyingine yoyote

itakayoipa Mahakama hiyo mamlaka.

(2) Mahakama ya Jamhuri ya Muungano pamoja na mahakama

za Washirika wa Muungano, isipokuwa Mahakama ya Juu zitabanwa na

maamuzi ya Mahakama ya Juu.

(3) Mahakama ya Juu itaandaa Kanuni kwa ajili ya utekelezaji

wa mamlaka yake.

(4) Bunge linaweza kutunga sheria itakayoweka masharti zaidi

kuhusu uendeshaji wa Mahakama ya Juu.

Madaraka

ya Majaji

wa

Mahakama

ya Juu


150.-

(1) Jaji yeyote wa Mahakama ya Juu hatakuwa na mamlaka

ya kusikiliza na kuamua shauri lolote katika Mahakama ya Rufani au

katika Mahakama ya ngazi yoyoteiliyo chini ya mamlaka ya Washirika

wa Muungano.

(2) Bila kujali masharti ya Ibara ndogo ya (1) iwapo Jaji wa

Mahakama ya Juu, kabla ya kuteuliwa kwake alikuwa Jaji wa

Mahakama ya Rufani au Mahakama ya Washirika wa Muungano

aunyingine yoyote, Jaji huyo anaweza kuendelea kufanya kazi zake

katika Mahakama aliyotoka mpaka amalize kutayarisha na kutoa

hukumu au mpaka akamilishe shughuli nyingine yoyote inayohusika na

mashauri ambayo alikwishaanza kuyasikiliza kabla hajateuliwa kuwa

Jaji wa Mahakama ya Juu.

(3) Kwa kuzingatia masharti ya Ibara ndogo ya (2), itakuwa ni

halali kwa Jaji wa Mahakama ya Juu kutoa hukumu au uamuzi

mwingine wowote unaohusika kwa kutumia na kutaja nafasi ya

madaraka aliyokuwa akishika kabla ya kuteuliwa kuwa Jaji wa

Mahakama ya Juu na endapo hukumu hiyo au uamuzi huo utapingwa

kwa njia ya rufani itakayofikishwa mbele ya Mahakama ya Juu, Jaji

huyo hatakuwa na mamlaka ya kusikiliza rufani hiyo.


59

(c)Uteuzi wa Majaji wa Mahakama ya JuuUteuzi wa

Jaji Mkuu


151.

-(1) Jaji Mkuu atateuliwa na Rais kutoka miongoni mwa

majina ya watu watatu yaliyopendekezwa na Tume ya Utumishi wa

Mahakama na kabla ya kuapishwa jina lake litawasilishwa Bungeni kwa

ajili ya kuthibitishwa na Bunge.

(2) Jaji Mkuu ndiye atakuwa Mkuu wa Mhimili wa Mahakama

katika Jamhuri ya Muungano.

(3) Mtu ataweza kuteuliwa kuwa Jaji Mkuu endapo atakuwa

amefikisha umri wa miaka arobaini na tano au zaidi na mwenye sifa ya

uadilifu, tabia njema, uaminifu na:

(a) awe na shahada ya sheria kutoka katika chuo

kinachotambuliwa na mamlaka inayoshughulikia elimu ya juu

katika Jamhuri ya Muungano;

(b) awe amefanya kazi ya uhakimu, ujaji, utumishi wa umma au

uanataaluma akiwa na sifa ya kufanya kazi ya uwakili au ni

wakili wa kujitegemea;

(c) awe na sifa ya kusajiliwa kuwa wakili,

na amekuwa na sifa hizo mfululizo kwa muda usiopungua miaka kumi na

mitano.

Uteuzi wa

Naibu Jaji

Mkuu


152.-

(1) Naibu Jaji Mkuu atateuliwa na Rais kutoka miongoni

mwa majina ya watu watatu yatakayopendekezwa na Tume ya Utumishi

wa Mahakama na kabla ya kuapishwa jina lake litawasilishwa Bungeni

kwa ajili ya kuthibitishwa na Bunge.

(2) Mtu atateuliwa kuwa Naibu Jaji Mkuu endapo atakuwa na sifa

zilizoainishwa katika Ibara ya 151 na kwa kufuata kanuni kwamba endapo

Jaji Mkuu atatoka sehemu moja ya Muungano, basi Naibu Jaji Mkuu

atatoka sehemu ya pili ya Muungano.

(3) Naibu Jaji Mkuu atakuwa ndiye Msaidizi Mkuu wa Jaji Mkuu

katika utekelezaji wa majukumu yake kama Mkuu wa Mhimili wa

Mahakama.

Uteuzi wa

Majaji wa

Mahakama

ya Juu


153.-

(1) Majaji wa Mahakama ya Juu watateuliwa na Rais kutoka

miongoni mwa majina yatakayopendekezwa na Tume ya Utumishi wa

Mahakama na wataapishwa na Rais.

(2) Mtu ataweza kuteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama ya Juu endapo

atakuwa na sifa ya uadilifu, tabia njema na uaminifu na:

(a) awe na shahada ya sheria kutoka katika chuo

kinachotambuliwa kwa mujibu wa sheria za nchi;

(b) awe amefanya kazi ya uhakimu, ujaji, utumishi wa umma au

uanataaluma akiwa na sifa ya kufanya kazi ya uwakili au ni

wakili wa kujitegemea; na

(c) awe na sifa ya kusajiliwa kuwa wakili,

na amekuwa na sifa hizo mfululizo kwa muda usiopungua miaka kumi.

(3) Kwa kuzingatia masharti ya Ibara ndogo ya (2), iwapo Rais

ataridhika kwamba japokuwa:

(a) mtu mwenye sifa mojawapo ya hizo sifa zilizoainishwa

katika Ibara ndogo ya (2) hakuwa nayo sifa hiyo kwa muda


60

unaopungua miaka kumi; na

(b) mtu huyo ana uwezo, ujuzi na kwa kila hali anafaa

kukabidhiwa madaraka ya Jaji wa Mahakama ya Juu;

(c) kuna sababu za kumfanya mtu huyo kustahili kukabidhiwa

nafasi ya madaraka hayo,

basi Rais anaweza kutengua sharti la kuwa na sifa kwa muda usiopungua

miaka kumi, na baada ya kushauriana na Tume ya Utumishi wa

Mahakama, kumteua mtu huyo kuwa Jaji wa Mahakama ya Juu.

Kiapo cha

Majaji wa

Mahakama

ya Juu


154.

Jaji Mkuu, Naibu Jaji Mkuu au Jaji wa Mahakama ya Juu

atashika madaraka yake mara tu atakapokuwa ameapishwa na Rais kiapo

cha uaminifu na kiapo kingine chochote kinachohusika na utendaji wa

kazi kitakachowekwa kwa mujibu wa sheria iliyotungwa na Bunge.

Muda wa

kuwa

madarakani

kwa

Jaji Mkuu,

Naibu Jaji

Mkuu na

Majaji

wengine


155.-

(1) Jaji Mkuu na Naibu Jaji Mkuu watashika madaraka yao

mpaka watakapofikisha umri wa miaka sabini, isipokuwa tu kama:

(a) watajiuzulu;

(b) nafasi ya madaraka ya Jaji Mkuu itakuwa wazi kutokana na

maradhi au kifo; au

(c) atavuliwa wadhifa wa Jaji Mkuu kwa mujibu wa Katiba hii.

(2) Masharti ya Ibara ndogo ya (1) yatatumika pia kwa Naibu Jaji

Mkuu na Jaji wa Mahakama ya Juu.

(3) Bila ya kuathiri masharti ya Ibara ndogo ya (1) na (2), Jaji

Mkuu, Naibu Jaji Mkuu na Jaji wa Mahakama ya Juualiyetimiza umri wa

kustaafu atalazimika kuendelea kufanya kazi baada ya kutimiza umri huo

mpaka amalize kutayarisha na kutoa hukumu au mpaka akamilishe

shughuli nyingine yoyote inayohusika na mashauri ambayo alikwishaanza

kuyasikiliza kabla hajatimiza umri wa kustaafu.

Utaratibu

wa

kukaimu

katika

Mahakama

ya Juu


156.-(

1) Iwapo itatokea kwamba:-

(a) nafasi ya madaraka ya Jaji Mkuu itakuwa wazi;

(b) Jaji Mkuu hayupo katika Jamhuri ya Muungano; au

(c) Jaji Mkuu atashindwa kumudu kutekeleza kazi zake kwa

sababu yoyote,

Naibu Jaji Mkuu atatekeleza kazi za Jaji Mkuu mpaka atakapoteuliwa Jaji

Mkuu mwingine au mpaka Jaji Mkuu ambaye alikuwa hayupo au alikuwa

hamudu kazi zake atakaporejea kazini.

(2) Ikitokea kwamba nafasi ya madaraka ya Jaji wa Mahakama ya

Juuitakuwa wazi au endapo Jaji wa Mahakama ya Juu yeyote ameteuliwa

kutekeleza kazi za Naibu Jaji Mkuu au kama Jaji waMahakama ya Juu

atashindwa kutekeleza kazi zake kwa sababu yoyote, au Jaji Mkuu

atamshauri Rais kuwa kazi za Mahakama ya Juu zilivyo kwa wakati huo

zinahitaji ateuliwe Kaimu Jaji wa Mahakama ya Juu, basi Rais anaweza

kumteua Kaimu Jaji wa Mahakama ya Juu kutoka miongoni mwa watu

wanaoweza kuteuliwa kuwa Majaji wa Mahakama ya Juu kama


61

watakaopendekezwa na Tume ya Utumishi wa Mahakama.

(3) Mtu atakayeteuliwa kuwa Kaimu Jaji wa Mahakama ya Juu

atafanya kazi kama Kaimu Jaji wa Mahakama ya Juu kwa muda wote

utakaotajwa kwenye hati ya kuteuliwa kwake.

(4) Bila kujali masharti ya Ibara ndogo ya (2), mtu aliyeteuliwa

kuwa Kaimu Jaji wa Mahakama ya Juu ataendelea kufanya kazi kama

Kaimu Jaji wa Mahakama ya Juu mpaka amalize kutayarisha na kutoa

hukumu au mpaka amalize shughuli nyingine yoyote inayohusika na

rufani au mashauri mengine ambayo alikwishaanza kuyasikiliza kabla ya

muda wake wa uteuzi haujamalizika au uteuzi wake haujafutwa.

(5) Kwa madhumuni ya kuondoa mashaka, Kaimu Jaji

waMahakama ya Juu atakuwa na mamlaka kamili ya Jaji wa Mahakama

ya Juu na atatekeleza kazi zote za Jaji wa Mahakama ya Juu na kwamba

idadi ya Majaji wa Mahakama ya Juuiliyotajwa katika Ibara ya

147haitaathirika kwa sababu tu mmoja au zaidi ya Majaji wa Mahakama

ya Juu katika kikao chochote ni Kaimu Jaji wa Mahakama ya Juu.

Utaratibu

wa

kushughulikia

nidhamu

ya Majaji

wa

Mahakama

ya Juu


157

.-(1) Utaratibu wa kushughulikia nidhamu ya Majaji wa

Mahakama ya Juu, mbali na sababu zilizoainishwa katika Ibara ndogo ya

(2), utakuwa kama utakavyoelezwa na sheria itakayotungwa na Bunge.

(2) Jaji wa Mahakama ya Juu anaweza kuondolewa madarakani

kwa sababu ya kushindwa kutekeleza madaraka yake ama kutokana na

maradhi au sababu nyingine yoyote au kwa sababu ya tabia mbaya

inayoathiri maadili ya kazi ya Jaji au Sheria ya Maadili ya Viongozi wa

Umma; na hataweza kuondolewa kazini ila kwa mujibu wa masharti ya

Ibara ndogo ya (4).

(3) Endapo Rais anaona kuwa suala la kumuondoa Jaji kazini

linahitaji kuchunguzwa, basi katika hali hiyo utaratibu utakuwa kama

ufuatavyo:

(a) Rais anaweza, baada ya kushauriana na Jaji Mkuu,

kumsimamisha kazi Jaji huyo;

(b) Rais atateua Tume ambayo itakuwa na Mwenyekiti na

Wajumbe wengine wasiopungua wawili; na angalau nusu ya

wajumbe hao wawe ni Majaji wa Mahakama ya Juu au

Mahakama ya Rufani kutoka nchi yoyote iliyomo kwenye

Jumuiya ya Madola; na

(c) Tume hiyo itachunguza shauri lote kisha itatoa taarifa kwa

Rais kuhusu maelezo ya shauri hilo na itamshauri Rais kama

Jaji huyo anayehusika aondolewe kazini kwa mujibu wa

masharti ya Ibara hii kwa sababu ya kushindwa kufanyakazi

kutokana na maradhi au sababu nyingine yoyote au kwa

sababu ya tabia mbaya.

(4) EndapoTume iliyoteuliwa kwa mujibu wa masharti ya Ibara

ndogo ya (3) itamshauri Rais kwamba Jaji ambaye mwenendo wake

umechunguzwa na Tume hiyo aondolewe kazini kwa sababu ya

kushindwa kufanyakazi kutokana na maradhi au sababu nyingine yoyote

au kwa sababu ya tabia mbaya, Rais atamuondoa kazini Jaji huyo na

utumishi wake utakuwa umekoma.


62

(5) Ikiwa suala la kumuondoa Jaji kazini limepelekwa kwenye

Tume kwa ajili ya uchunguzi kwa mujibu wa masharti ya Ibara ndogo ya

(3), Rais anaweza kumsimamisha kazi Jaji huyo anayehusika, na Rais

anaweza wakati wowote kufuta uamuzi huo wa kumsimamisha kazi Jaji

huyo, na kwa hali yoyote uamuzi huo utabatilika ikiwa Tume itamshauri

Rais kwamba Jaji huyo asiondolewe kazini.

(6) Masharti ya Ibara hii hayatawahusu watu walioteuliwa

kukaimu nafasi ya Ujaji.

(d)Mahakama ya Rufani ya Jamhuri ya MuunganoMahakama

ya Rufani


158.-

(1) Kutakuwa na Mahakama ya Rufani ya Jamhuri ya

Muungano,itakayojulikana kwa kifupi kama “Mahakama ya Rufani” na

ambayo itakuwa na:

(a) Mwenyekiti wa Mahakama ya Rufani; na

(b) Majaji wengine wasiopungua kumi na saba.

(2) Majaji wa Mahakama ya Rufani watateuliwa kwa kuzingatia

sifa zitakazoainishwa katika Katiba hii na uwiano wa uwakilishi wa

sehemu mbili za Washirika waMuungano.

(3) Sheria zitakazotungwa kwa mujibu wa Katiba za Washirika wa

Muungano zitaweka masharti kuhusu utaratibu wa kuwasilisha rufani

mbele ya Mahakama ya Rufani, nyakati na sababu za kukata rufani.

Akidi ya

vikao vya

Mahakama

ya Rufani


159.-(

1) Akidi ya kila kikao cha Mahakama ya Rufani itakuwa ni

Majaji wa Mahakama ya Rufani wasiopungua watatu.

(2) Kila shauri na rufani inayohitaji uamuzi wa Mahakama ya

Rufani itaamuliwa kwa kufuata kauli ya walio wengi kati ya Majaji wa

Mahakama ya Rufani waliosikiliza shauri au rufani husika.

Mamlaka

ya

Mahakama

ya

Rufani


160.

-(1) Mahakama ya Rufani itakuwa na:

(a) mamlaka ya kusikiliza na kuamua juu ya kila rufani

inayowasilishwa mbele ya mahakama ya Rufani kutokana na

hukumu au uamuzi wowote wa Mahakama Kuu au mahakama

yoyote ya chini iliyopewa mamlaka maalum ya kuwa

Mahakama Kuu hizo;

(b) mamlaka ya kufanya mapitio ya maamuzi ya Mahakama Kuu;

na

(c) mamlaka nyinginekama itakavyoainishwa kwenye sheria

itakayotungwa na Bunge.

(2)Mahakama ya Rufani itaandaa Kanuni kwa ajili ya utekelezaji

wa mamlaka yake.

(3)Bunge linaweza kutunga sheria itakayoweka masharti zaidi

kuhusu uendeshaji wa Mahakama ya Rufani.


63

Mamlaka

ya Majaji

wa

Mahakama

ya Rufani


161.-(

1) Jaji yeyote wa Mahakama ya Rufani hatakuwa na

mamlaka ya kusikiliza na kuamua shauri lolote katika Mahakama ya ngazi

yoyote isipokuwa Mahakama ya Rufani.

(2) Bila yakujali masharti ya Ibara ndogo ya (1), iwapo Jaji wa

Mahakama ya Rufani kabla ya kuteuliwa kwake alikuwa Jaji wa

Mahakama ya Kuu za Washirika wa Muungano au hakimu wa mahakama

nyingine yoyote ya Washirika wa Muungano, Jaji huyo anaweza

kuendelea kufanya kazi katikamahakama aliyotoka mpaka amalize

kutayarisha na kutoa hukumu au mpaka akamilishe shughuli nyingine

yoyote inayohusika na mashauri ambayo alikwishaanza kuyasikiliza kabla

hajateuliwa kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani.

(3) Kwa kuzingatia masharti ya Ibara ndogo ya (2), itakuwa ni

halali kwa Jaji wa Mahakama ya Rufani kutoa hukumu au uamuzi

mwingine wowote unaohusika kwa kutumia na kutaja nafasi ya madaraka

aliyokuwa akishika kabla ya kuteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani

na endapo hukumu hiyo au uamuzi huo utapingwa kwa njia ya rufani

itakayowasilishwa mbele ya Mahakama ya Rufani, Jaji huyo hatakuwa na

mamlaka ya kusikiliza rufani hiyo.

(e)Uteuzi wa Majaji wa Mahakama ya RufaniUteuzi wa

Mwenyekiti

wa

Mahakama

ya Rufani


162.-

(1) Mwenyekiti wa Mahakama ya Rufani atateuliwa na Rais

kutoka miongoni mwa majina ya watu watatu yatakayopendekezwa na

Tume ya Utumishi wa Mahakama.

(2) Mwenyekiti wa Mahakama ya Rufani atakuwa ndiye Mkuu wa

Mahakama ya Rufani na msaidizi wa Jaji Mkuu katika utendaji wa kazi

katika Mahakama ya Rufani, na katika madaraka hayo, Mwenyekiti wa

Mahakama ya Rufani atatekeleza kazi na shughuli atakazopangiwa mara

kwa mara na Jaji Mkuu.

(3) Mtu anaweza kuteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Mahakama ya

Rufani endapo atakuwa amefikisha umri wa miaka arobaini na tano au

zaidi na mwenye sifa ya uadilifu, tabia njema na uaminifu na:

(a) awe na Shahada ya Sheria kutoka katika Chuo Kikuu

kinachotambuliwa na mamlaka inayoshughulikia elimu ya juu

katika Jamhuri ya Muungano;

(b) awe amefanya kazi ya uhakimu, ujaji, utumishi wa umma au

uanataaluma akiwa na sifa ya kufanya kazi ya uwakili au ni

Wakili wa Kujitegemea; na

(c) awe na sifa ya kusajiliwa kuwa wakili,

na amekuwa na sifa hizo mfululizo kwa muda usiopungua miaka kumi.

(4) Kwa kuzingatia masharti ya Ibara ndogo ya (2), iwapo Rais

ataridhika kwamba japokuwa:

(a) mtu mwenye sifa mojawapo ya hizo sifa zilizoainishwa

katika Ibara ndogo ya (2) hakuwa nayo sifa hiyo kwa muda

usiopungua miaka kumi;

(b) mtu huyo ana uwezo, ujuzi na kwa kila hali anafaa

kukabidhiwa madaraka ya Jaji wa Mahakama ya Rufani;


64

(c) kuna sababu za kumfanya mtu huyo astahili kukabidhiwa

madaraka hayo,

basi Rais anaweza kutengua sharti la kuwa na sifa kwa muda usiopungua

miaka kumi, na baada ya kushauriana na Tume ya Utumishi wa

Mahakama, Rais anaweza kumteua mtu huyo kuwa Jaji wa Mahakama ya

Rufani.

Uteuzi wa

Majaji wa

Mahakama

ya Rufani


163.-

(1) Majaji wa Mahakama ya Rufani watateuliwa na Rais

kutoka miongoni mwa majina yatakayopendekezwa na Tume ya Utumishi

wa Mahakama.

(2) Mtu anaweza kuteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani

endapo atakuwa na sifa ya uadilifu, tabia njema na uaminifu na:

(a) awe na shahada ya sheria kutoka katika chuo kinachotambuliwa na

mamlaka inayoshughulikia elimu ya juu katika Jamhuri ya

Muungano;

(b) awe amefanya kazi ya uhakimu, ujaji, utumishi wa umma au

uanataaluma akiwa na sifa ya kufanya kazi ya uwakili au ni wakili

wa kujitegemea; na

(c) awe na sifa ya kusajiliwa kuwa wakili,

na amekuwa na sifa hizo mfululizo kwa muda usiopungua miaka kumi.

Kiapo cha

Majaji wa

Mahakama

ya Rufani


164.

-Mwenyekiti wa Mahakama ya Rufani, au Jaji wa Mahakama

ya Rufani atashika madaraka yake mara tu atakapoapishwa na Rais kiapo

cha uaminifu na kiapo kingine chochote kinachohusika na utendaji wa

kazi kitakachowekwa kwa mujibu wa sheria iliyotungwa na Bunge.

Muda wa

kuwa

madarakani

kwa

Mwenyekiti

na Majaji

wengine wa

Mahakama

ya Rufani


165.

-(1) Mwenyekiti wa Mahakama ya Rufani atashika nafasi

yamadaraka ya Ofisi ya Mwenyekiti wa Mahakama ya Rufani mpaka

atakapofikisha umri wa miaka sabini, isipokuwa kama:

(a) atajiuzulu;

(b) kiti chake kitakuwa wazi kutokana na maradhi au kifo; au

(c) atavuliwa wadhifa wa Mwenyekiti wa Mahakama ya Rufani

kwa mujibu wa Katiba hii.

(2) Naibu Mwenyekiti wa Mahakama ya Rufani au Jaji wa

Mahakama ya Rufani atashika madaraka mpaka atakapotimiza umri wa

miaka sabini, isipokuwa kama:

(a) atajiuzulu;

(b) nafasi ya madaraka ya Mwenyekiti wa mahakama ya

Rufaniitakuwa wazi kutokana na maradhi au kifo; au

(c) atavuliwa wadhifa wake kwa mujibu wa Katiba hii.

(3) Bila ya kujali masharti ya Ibara ya ndogo ya (1)na (2), Jaji

aliyetimiza umri wa kustaafu atalazimika kuendelea kufanya kazi baada ya

kutimiza umri huo mpaka amalize kutayarisha na kutoa hukumu au mpaka

akamilishe shughuli nyingine yoyote inayohusika na mashauri ambayo

alikwishaanza kuyasikiliza kabla hajatimiza umri wa kustaafu.


65

Utaratibu

wa

kukaimu

katika

Mahakama

ya Rufani


166.-

(1) Iwapo itatokea kwamba:-

(a) nafasi ya madaraka ya Mwenyekiti wa Mahakama ya Rufani

ipo wazi;

(b) Mwenyekiti wa Mahakama ya Rufani hayupo katika Jamhuri

ya Muungano;

(c) Mwenyekiti wa Mahakama ya Rufani atashindwa kutekeleza

kazi yake kwa sababu yoyote,

Jaji Mkuu anaweza kumteua Jaji wa Mahakama ya Rufani yoyote

kutekeleza kazi za Mwenyekiti wa Mahakama ya Rufani mpaka

atakapoteuliwa Mwenyekiti wa Mahakama ya Rufani mwingine au mpaka

Mwenyekiti wa Mahakama ya Rufani ambaye alikuwa hayupo Tanzania

au alikuwa hawezi kumudu kazi zake kutokana na maradhi atakaporejea

kazini.

(2) Ikitokea kwamba kiti cha Jaji wa Mahakama ya Rufani

kitakuwa wazi au endapo Jaji wa Rufani yeyote ameteuliwa kutekeleza

kazi za Mwenyekiti wa Mahakama ya Rufani au Jaji wa Mahakama ya

Rufani atashindwa kutekeleza kazi zake kwa sababu yoyote, Jaji Mkuu

atamshauri Rais kuwa ufanisi wa kazi za Mahakama ya Rufani unahitaji

ateuliwe Kaimu Jaji wa Mahakama ya Rufani.

(3) Endapo Rais akiridhika na ushauri wa Jaji Mkuu, atamteua

Kaimu Jaji wa Mahakama ya Rufani kutoka miongoni mwa watu

wanaoweza kuteuliwa kuwa Majaji wa Mahakama ya Rufani.

(4) Mtu atakayeteuliwa kuwa Kaimu Jaji wa Rufani atafanya kazi

kama Kaimu Jaji wa Rufani kwa muda wote utakaotajwa wakati wa

kuteuliwa kwake, au kama muda haukutajwa, basi mpaka uteuzi

utakapofutwa na Rais.

(5) Bila kujali masharti ya Ibara ndogo ya (4), mtu aliyeteuliwa

kuwa Kaimu Jaji wa Rufani ataendelea kufanya kazi kama Kaimu Jaji wa

Mahakama ya Rufani mpaka amalize kutayarisha na kutoa hukumu au

mpaka amalize shughuli nyingine yoyote inayohusika na rufani au

mashauri mengine ambayo alikwishaanza kuyasikiliza kabla ya muda

wake wa kazi haujamalizika au uteuzi wake haujafutwa.

(6) Kwa madhumuni ya kuondoa shaka, Kaimu Jaji wa Mahakama

ya Rufani atakuwa na mamlaka kamili ya Jaji wa Mahakama ya Rufani na

atatekeleza kazi zote za Jaji wa Mahakama ya Rufani na kwamba idadi ya

Majaji iliyotajwa katika Ibara ya 158 haitaathirika kwa sababu tu akidi ya

Majaji wa Mahakama ya Rufani katika kikao chochote ni pamoja

naKaimu Jaji wa Mahakama ya Rufani.

Utaratibu

wa

kushughulikia

nidhamu

ya Majaji

wa

Mahakama

ya Rufani


167.-

(1) Utaratibu wa kushughulikia nidhamu ya Majaji wa

Mahakama ya Rufani, kwa sababu ambazo ni tofauti na zilizoainishwa

katika nafasi ya Ibara ndogo ya (2), utakuwa kama utakavyoelezwa katika

Sheria itakayotungwa na Bunge.

(2) Jaji wa Mahakama ya Rufani anaweza kuondolewa katika

nafasi ya madaraka yaJaji kwa sababu ya kushindwa kutekeleza kazi yake

kutokana na:


66

(a) maradhi ya akili au mwili;

(b) kukiuka Kanuni za Maadili ya Majaji wa Mahakama ya Rufani

zilizotungwa kwa mujibu wa sheria;

(c) kutokuwa na uwezo wa kumudu kazi za nafasi ya Jaji; au

(d) tabia mbaya au mwenendo usiofaa unaoathiri Sheria ya Maadili

ya Viongozi wa Umma.

(3) Mwenyekiti wa Mahakama ya Rufani, Naibu Mwenyekiti wa

Mahakama ya Rufani na Jaji wa Rufani wataweza kuondolewa katika

nafasi ya madaraka ya Jaji kwa kufuata utaratibu unaofanana na ule

uliowekwa kwa ajili ya kumuondoa kazini Jaji Mkuu, Naibu Jaji Mkuu na

Jaji wa Mahakama ya Juu kama ilivyoelezwa.

(f)Usimamizi wa Shughuli za MahakamaMsajili wa

Mahakama


168

.-(1)Kutakuwa na Msajili wa Mahakama atakayeteuliwa na

Rais kufuatia mapendekezo ya Tume ya Utumishi wa Mahakama na baada

kuidhinishwa na Bunge.

(2) Mtu hatateuliwa kushika nafasi ya Msajili wa Mahakama

isipokuwa tu kama:

(a) ana shahada ya sheria kutoka katika chuo kinachotambuliwa kwa

mujibu wa Sheria za nchi;

(b) awe amefanya kazi ya uhakimu, utumishi wa umma au

mwanataaluma akiwa na sifa ya kufanya kazi ya uwakili wa

Serikali au ni wakili wa kujitegemea;

(c) awe na sifa ya kusajiliwa kuwa wakili; na

(d) ni mwadilifu na mwenye tabia na mwenendo mwema,

na amekuwa na sifa hizo mfululizo kwa muda usiopungua miaka kumi.

Majukumu

ya Msajili

wa

Mahakama


169.-

(1) Msajili wa Mahakama atakuwa na majukumu yafuatayo:

(a) kusimamia utekelezaji wa shughuli za kimahakama;

(b) kuratibu masuala ya kimahakama; na

(c) majukumu mengine atakayopangiwa na Jaji Mkuu.

(2) Katika kutekeleza majukumu yake, Msajili wa Mahakama

atawajibika kwa Tume ya Utumishi wa Mahakama.

Mtendaji

Mkuu wa

Mahakama


170.

-(1) Kutakuwa na Mtendaji Mkuu wa Mahakama

atakayeteuliwa na Rais kutoka miongoni mwa Watumishi wa Umma

kufuatia mapendekezo ya Tume ya Utumishi wa Mahakama na

kuidhinishwa na Bunge.

(2) Mtu hatateuliwa kushika nafasi ya Mtendaji Mkuu wa

Mahakama isipokuwa tu kama ni:

(a) mtumishi wa umma mwandamizi;

(b) ana weledi na uzoefu katika masuala ya utawala na mambo ya

fedha; na

(c) mwadilifu na mwenye tabia na mwenendo mwema.


67

Majukumu

ya

Mtendaji

Mkuu wa

Mahakama


171.-

(1) Mtendaji Mkuu wa Mahakama atakuwa na majukumu

yafuatayo:

(a) Katibu wa Tume ya Utumishi wa Mahakama;

(b) Afisa Masuuli wa Mahakama;

(c) msimamizi mkuu wa Mfuko wa Mahakama;

(d) msimamizi wa masuala ya utawala ya Mahakama; na

(e) atatekeleza majukumu mengine atakayopangiwa na Jaji Mkuu.

(2) Katika kutekeleza majukumu yake, Mtendaji Mkuu wa

Mahakama atawajibika kwa Tume ya Utumishi wa Mahakama.

SEHEMU YA TATU

T
UME YA UTUMISHI WA MAHAKAMA NA MFUKO WA MAHAKAMA

(a) Tume ya Utumishi wa MahakamaTume ya

Utumishi

wa

Mahakama


172.-

(1) Kutakuwa na Tume ya Utumishi wa Mahakama ambayo

itaundwa na wajumbe tisa watakaoteuliwa na Rais kama ifutavyo:

(a) Jaji Mkuu ambaye atakuwa ni Mwenyekiti;

(b) Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano;

(c) Jaji mmoja wa Mahakama ya Juu;

(d) Jaji mmoja wa Mahakama ya Rufani;

(e) Mwakilishi wa Chama cha Wanasheria wa Tanzania Bara;

(f) Mwakilishi wa Chama cha Wanasheria wa Zanzibar;

(g) Wakuu Wawili wa vitivo vya sheria kutoka vyuo vikuu, mmoja

kutoka Tanzania Bara na moja kutoka Zanzibar

watakaopendekezwa na Jaji Mkuu; na

(h) Mtendaji Mkuu wa Mahakama ambaye atakuwa Katibu wa

Tume ya Utumishi wa Mahakama.

(2) Tume inaweza kumualika mtu mwingine yoyote mwenye

utaalamu mahususi kushiriki kikao chochote cha Tume, isipokuwa mtu

huyo hatakuwa nahaki ya kupiga kura.

(3) Tume itaweka utaratibu wa kuendesha vikao vyake.

Majukumu

ya Tume

ya

Utumishi

wa

Mahakama


173.-

(1) Tume ya Utumishi wa Mahakama itakuwa na wajibu wa

kuendeleza na kuwezesha uhuru na uwajibikaji wa Mahakama na utoaji

haki wenye ufanisi, mafanikio na uwazi.

(2) Tume ya Utumishi wa Mahakama itakuwa na wajibu wa:

(a) kupendekeza kwa Rais majina ya watu wanaofaa kuteuliwa

kuwa Majaji wa Mahakama ya Juu na Mahakama ya Rufani;

(b) kupitia na kupendekeza masharti ya utumishi wa Majaji na

watumishi wengine wa mahakama ikiwemo masuala

yanayohusu nidhamu na maslahi yao;

(c) kuteua wasajili na kuajiri watumishi wengine wa Mahakama,

kupokea malalamiko dhidi yao na kuwachukulia hatua za

kinidhamu ikiwemo kuwafukuza kazi kwa mujibu wa Sheria

itakayotungwa na Bunge;

(d) kuandaa na kutekeleza mipango ya kujiendeleza kielimu kwa

Majaji na watumishi wengine wa Mahakama;


68

(e) kupendekeza Serikalini maboresho ya Mahakama ili kuongeza

ufanisi katika utoaji haki;

(f) kutoa fursa ya majadiliano kuhusu utekelezaji wa majukumu

ya Mahakama ya Jamhuri ya Muunganona hivyo kumsaidia

Jaji Mkuu katika kutekeleza majukumu yake kwa malengo ya

kuleta ufanisi na mafanikio katika utoaji haki; na

(g) kutekeleza majukumu yoyote itakayopewa kwa mujibu wa

Katiba hii au sheria zingine.

(3) Katika kutekeleza majukumu yake, Tume itazingatia:

(a) uwazi katika mchakato wa uteuzi wa Majaji na ajira ya

watumishi wengine wa Mahakama ya Jamhuri ya

Muungano;

(b) uwakilishi wa sehemu mbili za Washirika wa Muungano; na

(c) uwakilishi wa kijinsia.

(4) Katika kutekeleza majukumu yake, Tume inaweza kukasimu

madaraka yake kwa kamati mbalimbali zitakazoundwa kwa mujibu wa

sheria itakayotungwa na Bunge.

(5) Bunge litatunga sheria itakayoweka masharti ya utekelezaji wa

majukumu ya Tume.

Uanachama

katika

vyama vya

siasa


174.

Itakuwa ni marufuku kwa Jaji wa Mahakama ya Juu, Jaji wa

Mahakama ya Rufani au Msajili wa Mahakama ya ngazi yoyote kuwa

mwanachama wa chama chochote cha siasa, isipokuwa atakuwa na haki

ya kupiga kura ya kuchagua viongozi katika vyombo vya uwakilishi.

(b) Mfuko wa MahakamaMfuko wa

Mahakama


175

.-(1) Kutakuwa na mfuko utakaojulikana kama Mfuko wa

Mahakama ya Jamhuri ya Muungano ambao utakuwa chini ya usimamizi

wa Mtendaji Mkuu wa Mahakama.

(2) Mfuko wa Mahakama ya Jamhuri ya Muungano utatumika kwa

ajili ya kugharamia shughuli za utawala na uendeshaji wa Mahakama ya

Jamhuri ya Muungano na shughuli zingine muhimu katika utekelezaji wa

majukumu ya Mahakama.

(3) Serikali itahakikisha kwamba katika kila bajeti ya mwaka wa

fedha wa Serikali, inatenga kwa kiwango kinachotosha fedha ambazo

zitaingizwa katika Mfuko wa Mahakama ya Jamhuri ya Muungano.

(4) Bunge litatunga sheria itakayoweka masharti kuhusu

uendeshaji wa Mfuko wa MahakamayaJamhuri ya Muungano.

SURA YA KUMI NA MOJA

U
TUMISHI WA JAMHURI YA MUUNGANO

Misingi

mikuu ya

Utumishi

wa Umma


176.-

(1) Utumishi wa umma katika Jamhuri ya Muungano

utazingatia misingi na kanuni zifuatazo:

(a) utumishi wa umma ni dhamana kutoka kwa wananchi na hivyo

mtumishi anatakiwa kutumikia wananchi kwa uadilifu,


69

uaminifu na unyenyekevu;

(b) kudumisha na kukuza viwango vya juu vya maadili ya

kitaaluma;

(c) kuhamasisha matumizi bora na yenye tija ya raslimali;

(d) kutoa huduma kwa umma kwa njia ya haki, usawa na bila

upendeleo;

(e) kuhamasisha wananchi kushiriki kwenye maandalizi ya sera

mbalimbali za nchi;

(f) kuitikia matakwa na mahitaji ya watu kwa haraka na kwa

wakati unaofaa;

(g) kujitolea katika utekelezaji wa sera na mipango ya kitaifa;

(h) uwajibikaji wa viongozi kwa makosa yanayofanyika chini yao;

(i) kuhamasisha sera ya uwazi katika kutoa habari za kweli kwa

umma na kwa wakati ufaao; na

(j) kuhakikisha kwamba watu watateuliwa katika nafasi

mbalimbali kwa kuzingatia uwezo wa kitaaluma, weledi,

maarifa, ujuzi na uzoefu wao katika eneo husika.

(2) Misingi na Kanuni za Utumishi wa Umma zilizoainishwa katika

Ibara hii zitazingatiwa na kutumika katika uteuzi wa kushika nafasi za

madaraka ya uongozi katika:

(a) mamlaka katika mihimili yote ya Dola;

(b) taasisi na idara zote za Serikali; na

(c) mashirika yote ya Serikali.

(3) Bunge litatunga sheria kuweka masharti ya utekelezaji wa

misingi ya utumishi iliyoainishwa katika Ibara ndogo ya (1).

Masharti

kuhusu

utumishi

katika

Jamhuri ya

Muungano


177.

Bila ya kuathiri masharti ya Katiba hii, utumishi wa umma na

uongozi katika Jamhuri ya Muungano utazingatia misingi kwamba utoaji wa

ajira na uteuzi wa viongozi utakuwa kwa uwiano baina ya Washirika wa

Muungano, kwa kuzingatia weledi na taaluma katika eneo au nyanja husika.

Tume ya

Utumishi

wa Umma


178

.-(1) Kutakuwa na Tume ya Utumishi wa Umma itakayokuwa

na Mwenyekiti na wajumbe wengine sita watakaoteuliwa na Rais na

kuidhinishwa na Bunge.

(2) Katika kuteua wajumbe wa Tume ya Utumishi wa Umma, Rais

atazingatia Kanuni za Utumishi wa Umma zilizoainishwa katika Katiba

hii.

(3) Kutakuwa na Katibu wa Tume ya Utumishi wa Umma ambaye

atakuwa ndiye Mtendaji Mkuu na mtekelezaji wa majukumu ya kila siku

ya Tume.

(4) Katibu wa Tume ya Utumishi wa Umma atateuliwa na Rais

baada ya kuidhinishwa na Bunge kutoka miongoni mwa watumishi

waandamizi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano.

Mamlaka

na

Majukumu

ya Tume


179

.-(1) Tume ya Utumishi wa Umma itakuwa ni chombo cha juu

katika Utumishi wa Umma chenye mamlaka ya kusimamia na kuratibu

mambo yote kuhusu Utumishi wa Umma.

(2) Bila ya kuathiri masharti ya Ibara ndogo ya (1), majukumu ya


70

Tume ya Utumishi wa Umma yatakuwa ni:

(a) kumshauri Rais juu ya uteuzi wa viongozi katika nafasi

mbalimbali kwa mujibu wa Katiba hii;

(b) kutoa miongozo mbalimbali na kusimamia mchakato wa ajira

katika utumishi wa umma kwa kuzingatia vigezo stahiki;

(c) bila kuathiri masharti ya Katiba hii, kuteua watu kuhudumu au

kushikilia ofisi kwa muda katika idara ya utumishi wa umma,

kuidhinisha uteuzi na kudhibiti nidhamu na kuwaondoa

watumishi wanaohudumu au kushikilia ofisi hizo;

(d) kusimamia na kuhamasisha utekelezaji wa misingi na kanuni za

utumishi katika sekta zote za utumishi wa umma;

(e) kushughulikia rufani zinazowasilishwa na watumishi wa umma

dhidi ya uamuzi wa mamlaka mbalimbali za nidhamu katika

utumishi wa umma;

(f) kutekeleza majukumu mengine yoyote kama

yatakavyoainishwa katika sheria itakayotungwa na Bunge juu

masuala ya utumishi wa umma na sheria nyingine za nchi;

(g) kuunda na kudurusu mishahara na marupurupu ya watumishi

wa umma, ikiwemo viongozi wa juu wa nchi, viongozi wa

kisiasa, watumishi waliopo chini ya utumishi wa Mahakama,

Bunge na Serikali; na

(h) kusawazisha mishahara na marupurupu ya maafisa wote wa

Serikali, Bunge, Mahakama na maofisa wa umma pamoja na

maofisa wa majeshi ya ulinzi na usalama.

SURA YA KUMI NA MBILI

UCHAGUZI KATIKA VYOMBO VYA UWAKILISHI

NA VYAMA VYA SIASA

SEHEMU YA KWANZA

U
WAKILISHI WA WANANCHI

Ushiriki

katika

vyombo vya

uwakilishi


180.

-(1) Kila raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

mwenye umri wa miaka kumi na nane au zaidi mwenye akili timamu

ana haki ya kupiga kura na haki ya kuandikishwa kwa ajili ya kupiga

kura katika uchaguzi au kura ya maoni.

(2) Kwa madhumuni ya Ibara ndogo ya (1), mamlaka ya

uchaguzi itazingatia misingi ifuatayo:

(a) wananchi wanatumia haki ya kisiasa kwa mujibu wa

Katiba hii;

(b) watu wenye ulemavu wanapewa fursa za uwakilishi;

(c) haki ya kila mtu kupiga kura moja kufuatana na utashi

wa uwakilishi na kura sawa; na

(d) uchaguzi ulio huru na ambao -

(i) ni wa kura ya siri;

(ii) hauna matumizi ya nguvu, vitisho, vishawishi

wala rushwa;

(iii) haukuwa na matamshi au vitendo vinavyoashiria

ukabila, ukanda, udini, dharau na kashfa kwa


71

jinsia au unyanyapaa kwa walemavu au makundi

madogo katika jamii;

(iv) unaendeshwa na kusimamiwa na chombo huru;

na

(v) unaendeshwa bila upendeleo au kuegemea

upande wowote, uliyo makini na inayoonyesha

uwajibikaji wa watendaji.

(3) Ili kutekeleza masharti ya Ibara ndogo ya (1) na (2),

mamlaka ya nchi itaweka utaratibu wa sheria utakaowezesha:

(a) mamlaka zinazosimamia uchaguzi kutangaza majimbo

kwa madhumuni ya uchaguzi wa wabunge;

(b) uteuzi wa wagombea;

(c) uandikishaji endelevu wa wapiga kura;

(d) kuendesha na kusimamia uchaguzi na kura ya maoni;

(e) kuweka utaratibu wa kuandikisha raia wa Jamhuri ya

Muungano wa Tanzania wanaoishi nje ili kuweza

kupiga kura katika uchaguzi au kura ya maoni; na

(f) utaratibu wa kufanya uchaguzi kuwa mwepesi, wazi na

unaozingatia mahitaji ya watu wenye mahitaji maalum.

(4) Kwa madhumuni ya Ibara ndogo ya (2), kwa lengo la

kukuza demokrasia, kulinda Katiba na kuhakikisha panakuwepo

uchaguzi huru, kila mpiga kura ana haki ya kufungua shauri

Mahakamani kupinga matokeo ya uchaguzi isipokuwa matokeo ya

uchaguzi wa Rais,anayoamini yamevunja au kukiuka masharti ya

Katiba hii.

SEHEMU YA PILI

T
UME HURU YA UCHAGUZI

(a)

Muundo wa Tume Huru ya Uchaguzi na Vyama vya

SiasaKuundwa

kwa Tume

Huru ya

Uchaguzi


181.

-(1) Kutakuwa na Tume Huru ya Uchaguzi ya Jamhuri ya

Muungano kwa ajili ya kusimamia na kuratibu shughuli za uchaguzi na

masuala yanayohusu vyama vya siasa na ambayo pia itaitwa “Tume

Huru ya Uchaguzi”.

(2) Tume Huru ya Uchaguzi itaundwa na Mwenyekiti, Makamu

Mwenyekiti na wajumbe wengine saba watakaoteuliwa na Rais baada ya

kupendekezwa na Kamati ya Uteuzi.

(3) Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na wajumbe wa Tume

Huru ya Uchaguzi watashika madaraka mara baada ya kuthibitishwa na

Bunge.

(4) Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi

watakuwa na sifa zifuatazo:

(a) awe ni raia wa kuzaliwa na angalau mmoja kati ya wazazi

wake ni raia wa kuzaliwa wa Tanzania;

(b) awe ni mtu aliyewahi kushika wadhifa wa Jaji wa Makakama

ya Juu, Mahakama ya Rufani au Mahakama Kuu na ameshika


72

wadhifa huo kwa kipindi kisichopungua miaka mitano;

(c) awe ni mtu mwaminifu, mwadilifu, na mwenye mwenendo

usiotiliwa shaka na jamii;

(d) awe ni mtu ambaye siyo kiongozi, hajawahi kushika wadhifa

wowote wa kisiasa katika chama chochote cha kisiasa; na

(e) awe ni mtu ambaye hajawahi kutiwa hatiani kwa kosa lolote

la jinai linalohusiana na uaminifu.

(5) Mjumbe wa Tume Huru ya Uchaguzi atakuwa na sifa

zifuatazo:

(a) awe ni raia wa kuzaliwa na angalau mmoja kati ya wazazi

wake ni raia wa kuzaliwa wa Tanzania;

(b) awe ni mtu mwaminifu, mwadilifu, na mwenye mwenendo

usiotiliwa shaka na jamii;

(c) awe ni mtu ambaye siyo kiongozi na hajawahi kushika

wadhifa wowote wa kisiasa katika chama chochote cha

kisiasa;

(d) awe na elimu ya shahada ya chuo kikuu kinachotambuliwa

kwa mujibu wa sheria za nchi; na

(e) awe ni mtu ambaye hajawahi kutiwa hatiani kwa kosa lolote

la jinai linalohusu kukosa uaminifu.

(6) Kwa madhumuni ya Ibarahii, watu wafuatao hawatakuwa na

sifa ya kuwa Wajumbe wa Tume Huru ya Uchaguzi:

(a) Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, Mbunge wa

Bunge la Tanzania Bara, Mwakilishi wa Baraza la

Wawakilishi, Diwani au Sheha katika Serikali ya Tanzania

Bara au Zanzibar mtawalia;

(b) mtu ambaye ni mtumishi wa umma; au

(c) mtu ambaye anashika nafasi ya madaraka katika asasi zisizo

za kiserikali au aliyewahi kushika nafasi ya madaraka katika

asasi zisizo za kiserikali ndani ya muda usiozidi miaka mitano

kabla ya uteuzi kufanyika.

(7) Uteuzi wa Wajumbe wa Tume Huru ya Uchaguzi utazingatia

uwakilishi na uwiano wa Washirika wa Muungano.

Kamati ya

Uteuzi


182

.-(1) Kutakuwa na Kamati ya Uteuzi wa Mwenyekiti,

Makamu Mwenyekiti na Wajumbe wa Tume Huru ya Uchaguzi

itakayokuwa na muundo ufuatao:

(a) Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano ambaye atakuwa ni

Mwenyekiti;

(b) Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano ambaye

atakuwa Makamu Mwenyekiti;

(c) Spika wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar;

(d) Spika wa Bunge la Tanzania Bara;

(e) Jaji Mkuu wa Tanzania Bara;

(f) Jaji Mkuu wa Zanzibar; na

(g) Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu.

(2) Mkurugenzi wa Tume Huru ya Uchaguzi atakuwa Katibu wa


73

Kamati ya Uteuzi.

(3) Kamati ya Uteuzi itakuwa na jukumu la kupokea na

kuchambua majina ya watu walioomba kuwa wajumbe wa Tume Huru

ya Uchaguzi kwa mujibu wa utaratibu utakaoainishwa na sheria

iliyotungwa na Bunge.

(4) Kwa kuzingatia masharti ya Ibara ndogo ya (3), Kamati ya

Uteuzi mara baada ya kuchambua majina ya watu walioomba kuwa

wajumbe wa Tume Huru ya Uchaguzi, itapendekeza kwa Rais majina ya

watu wanaofaa kuteuliwa kuwa wajumbe wa Tume Huru ya Uchaguzi.

(5) Rais atateua Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na Wajumbe

wa Tume Huru ya Uchaguzi kutoka miongoni mwa majina

yaliyowasilishwa na Kamati ya Uteuzi na atawasilisha majina hayo

Bungeni kwa ajili ya kuthibitishwa na Bunge.

(6) Bunge litatunga Sheria ambayo pamoja na mambo na

mengine itaweka masharti kuhusu kiapo cha Mwenyekiti, Makamu

Mwenyekiti na Wajumbe wengine wa Tume Huru ya Uchaguzi.

Ukomo wa

kushika

madaraka ya

Tume Huru

ya Uchaguzi


183.-

(1) Mjumbe wa Tume atashika madaraka kwa kipindi cha

miaka mitano na anaweza kuteuliwa tena kwa kipindi kingine kimoja cha

miaka mitano.

(2) Mtu atakoma kuwa mjumbe wa Tume endapo litatokea tukio

lolote kati ya matukio yafuatayo:

(a) kifo;

(b) kujiuzulu;

(c) kutokuwa na uwezo wa kutekeleza majukumu yake kwa

sababu za kiafya;

(d) kuondolewa kwa makosa ya kukiuka Kanuni za Maadili ya

Uongozi wa Umma;

(e) kutiwa hatiani kwa kosa ambalo adhabu yake ni kifungo

gerezani kwa muda unaozidi siku saba; au

(f) kupoteza sifa ya kuteuliwa kuwa mjumbe.

(2) Kwa madhumuni ya utekelezaji bora wa majukumu ya Tume,

kutakuwa na kanuni za maadili kama zitakazoainishwa na Sheria

itakayotungwa na Bunge.

(3) Mjumbe wa Tume Huru ya Uchaguzi ambaye atakiuka

masharti ya Kanuni za Maadili ya Tume atapoteza sifa za kuendelea

kuwa mjumbe.

(4) Endapo suala la kumuondoa Mjumbe wa Tume Huru ya

Uchaguzi kwa kukiuka Kanuni za Maadili ya Uongozi wa Umma

litajitokeza, Rais atateua Kamati itakayoundwa na:

(a) Jaji wa Mahakama ya Rufani ambaye atakuwa Mwenyekiti;

(b) Kamishna wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora;

(c) Mjumbe wa Tume ya Maadili na Uwajibikaji; na

(d) Mawakili, mmoja kutoka Tanzania Bara na mmoja kutoka

Zanzibar watakaopendekezwa na Chama cha Wanasheria

Tanganyika na Chama cha Wanasheria Zanzibar,

na Kamati hiyo itafanya uchunguzi wa suala hilo na kisha kutoa


74

mapendekezo kwa Rais.

(5) Endapo, baada ya uchunguzi,Kamati itapendekeza kuwa

mjumbe huyo asiondolewe, suala la kumuondoa mjumbe huyo litasita.

(6) Kamati itaweka utaratibu wa kufanya uchunguzi.

Wajibu wa

Tume Huru

ya Uchaguzi


184

.-(1) Tume Huru ya Uchaguzi itakuwa na wajibu wa:

(a) kusimamia na kuendesha shughuli zote za uchaguzi wa

Wabunge na Rais katika Jamhuri ya Muungano wa

Tanzania;

(b) kusimamia na kuendesha kura ya maoni;

(c) kusimamia na kuratibu uandikishaji wa wapiga kura katika

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania;

(d) kusimamia na kuratibu uandikishaji na shughuli za vyama

vya siasa kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii na sheria za

nchi;

(e) kutayarisha na kuchapisha ripoti za kila mwaka kuhusu ripoti

za ukaguzi wa fedha wa kila chama cha kisiasa; na

(f) kusimamia fedha za ruzuku za Vyama vya Kisiasa.

(2) Tume Huru ya Uchaguzi ya Jamhuri ya Muungano itakuwa

pia na wajibu wa kutoa elimu kwa wapiga kura katika uchaguzi au kura

ya maoni na kuratibu na kusimamia wananchi, asasi za kiraia, taasisi,

jumuiya au makundi ya watu yatakaotoa elimu hiyo.

(3) Tume Huru ya Uchaguzi pia ina wajibu wa kuhakikisha

kuwepo kwa:

(a) uhuru wa wananchi katika kutumia haki ya uchaguzi na

kuchaguliwa kupitia vyama vya siasa au mgombea huru;

(b) uwakilishi unaozingatia jinsia;

(c) uwakilishi wa watu wenye ulemavu au mahitaji maalumu

katika jamii;

(d) uzingatiaji wa misingi ya upigaji kura wa mtu mmoja kura

moja kwa kuzingatia uwakilishi wenye usawa; na

(e) uhuru wa uchaguzi wa haki.

(4) Tume Huru ya Uchaguzi inaweza kutekeleza shughuli zake

bila kujali kwamba kuna nafasi ya madaraka ya mjumbe iliyo wazi

miongoni mwa wajumbe au kwamba Mjumbe mmojawapo hayupo,

lakini kila uamuzi wa Tume Huru ya Uchaguzi ni lazima uungwe mkono

na wajumbe walio wengi kati ya Wajumbe wote wa Tume Huru ya

Uchaguzi.

(5) Katika kutekeleza madaraka yake kwa mujibu wa masharti ya

Katiba hii, Tume ya Uchaguzi haitalazimika kufuata amri au maagizo ya

mtu yeyote au idara yoyote ya Serikali, au maoni ya chama chochote cha

siasa.

(6) Katika utekelezaji wa madaraka yake kwa mujibu wa Katiba

hii, Tume Huru ya Uchaguzi itashauriana mara kwa mara na Tume ya

Uchaguzi ya Tanzania Bara na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar.

(7) Itakuwa ni marufuku kwa watu wanaohusika na uchaguzi

kujiunga na chama chochote cha siasa, isipokuwa tu kwamba kila mmoja

wao atakuwa na haki ya kupiga kura kuchagua wajumbe katika vyombo


75

vya uwakilishi.

(8) Kwa madhumuni ya Ibara ndogo ya (8), watu wanaohusika na

uchaguzi ni-

(a) Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi;

(b) Makamu Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi;

(c) Wajumbe wote wa Tume Huru ya Uchaguzi;

(d) Mkurugenzi wa Uchaguzi pamoja na watumishi wote wa

Tume Huru ya Uchaguzi;

(e) Msajili wa Vyama vya Siasa; na

(f) Wasimamizi wote wa Uchaguzi.

Malalamiko

kuhusu

uchaguzi


185.

-(1) Tume Huru ya Uchaguzi itasimamia na kutatua mapema

iwezekanavyo malalamiko yanayohusu kuteuliwa kwa mgombea katika

uchaguzi.

(2) Kesi za malalamiko kuhusu uchaguzi wa Wabunge

zitafunguliwa Mahakama ya Rufaa mapema iwezekanavyo baada ya

Tume Huru ya Uchaguzi kutangaza matokeo na kwa vyovyote vile si

zaidi ya muda ulioainishwa katika sheria za nchi.

(3) Kwa madhumuni ya Ibara ndogo ya (2) shauri la malalamiko

kuhusu uchaguzi wa Mbunge itasikilizwa na Jaji mmoja wa Mahakama

ya Rufani.

(b) Vyama vya SiasaVyama vya

siasa


186.

-(1) Jamhuri ya Muungano ni nchi ya kidemokrasia yenye

kufuata mfumo wa demokrasia ya vyama vingi vya siasa.

(2) Bila ya kujali masharti ya Ibara ndogo ya (1), haitakuwa halali

kwa chombo chochote cha siasa kuandikishwa ambacho kutokana na

Katiba au sera yake-

(a) kinakusudia kukuza au kupigania maslahi ya-

(i) imani au kundi lolote la dini;

(ii) kundi lolote la kikabila, pahala watu watokeapo, rangi au

jinsia;

(iii)eneo fulani tu katika sehemu yoyote ya Jamhuri ya

Muungano;

(b) kinapigania kuvunjwa kwa Jamhuri ya Muungano:

(c) kinakubali au kupigania matumizi ya nguvu au mapambano

kama njia za kufikia malengo yake ya kisiasa;

(d) kinapigania au kinakusudia kuendesha shughuli zake za

kisiasa katika sehemu moja tu ya Jamhuri ya Muungano; au

(e) hakiruhusu uongozi wake kuchaguliwa kwa vipindi na kwa

njia za kidemokrasia.

(3) Bila ya kuathiri sheria za nchi zinazohusika ni marufuku kwa

mtu yeyote kulazimishwa kujiunga na chama chochote au kwa chama

cha siasa kukataliwa kusajiliwa kwa sababu tu ya itikadi au falsafa.

(4) Bunge linaweza kutunga sheria inayoweka masharti

yatakayohakikisha kuwa vyama vya siasa vinazingatia mipaka na vigezo

vilivyowekwa na masharti ya Ibara ndogo ya (2) kuhusu uhuru na haki

ya watu kushirikiana na kujumuika.

(5) Mambo yote yanayohusu uandikishaji na uendeshaji wa


76

vyama vya siasa nchini yatasimamiwa kwa mujibu wa masharti ya

Katiba hii na sheria iliyotungwa na Bunge kwa ajili hiyo.

(c) Mkurugenzi wa Uchaguzi na Msajili wa Vyama vya SiasaUtekelezaji

wa

majukumu

ya Tume

Huru ya

Uchaguzi


187.-

(1) Kwa madhumuni ya utekekelezaji wa majukumu yake,

Tume Huru ya Uchaguzi itagawanywa katika sehemu kuu mbili, sehemu

ya uchaguzi na sehemu ya usajili wa vyama vya siasa.

(2) Kwa madhumuni ya Ibara ndogo ya (1), kutakuwa na:

(a) Mkurugenzi wa Uchaguzi ambaye atakuwa ndiye msimamizi

na mtekelezaji mkuu wa majukumu ya kila siku ya Tume

Huru ya Uchaguzi kuhusiana na masuala ya uchaguzi,

uandikishaji wa wapiga kura na uendeshaji wa kura ya maoni;

na

(b) Msajili wa Vyama vya Siasa ambaye atakuwa ndiye

msimamizi na mtekelezaji mkuu wa majukumu ya Tume

kuhusiana na usajili na usimamizi wa shughuli za vyama vya

siasa.

(3) Mkurugenzi wa Uchaguzi na Msajili wa Vyama vya Siasa

watatekeleza majukumu yao kwa kufuata utaratibu ulioainishwa na

sheria za nchi kuhusu masuala ya uchaguzi na vyama vya siasa.

(4) Mkurugenzi wa Uchaguzi na Msajili wa Vyama vya Siasa

watatekeleza majukumu yao kwa kusaidiwa na watendaji ambao ni

watumishi wa umma kwa kadri ya idadi inayohitajika.

(5) Uteuzi wa Mkurugenzi wa Uchaguzi na Msajili wa Vyama

vya Siasa utafanywa na Rais baada ya kuthibitishwa na Bunge.

(6) Katika kutekeleza majukumu yao, Mkurugenzi wa Uchaguzi

na Msajili wa Vyama vya Siasa watawajibika kwa Tume Huru ya

Uchaguzi.

SURA YA KUMI NA TATU

TAASISI ZA UWAJIBIKAJI

SEHEMU YA KWANZA

T
UME YA MAADILI YA UONGOZI NA UWAJIBIKAJI

Tume ya

Maadili ya

Uongozi na

Uwajibikaji


188

.-(1) Kutakuwa na Tume ambayo itaitwa Tume ya Maadili ya

Uongozi na Uwajibikaji itayoundwa na Mwenyekiti na Makamu

Mwenyekiti na wajumbe wengine wasiozidi saba.

(2) Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Maadili ya

Uongozi na Uwajibikaji watateuliwa na Rais baada ya kupendekezwa na

Tume ya Utumishi wa Umma.

(3) Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti watashika madaraka

yao baada ya kuthibitishwa na Bunge.

(4) Sifa za Mwenyekiti wa Tume zitakuwa kama ifuatavyo:

(a) awe raia;

(b) mtu mwenye shahada ya chuo kikuu kinachotambulika kwa

mujibu wa sheria za nchi;


77

(c) mtu mwenye uzoefu katika utumishi wa umma kwa kipindi

kisichopungua miaka kumi; na

(d) mtu mwenye heshima, weledi uaminifu, uadilifu na asiye na

tabia au mienendo yenye kutiliwa shaka.

(5) Sifa za Makamu Mwenyekiti zitakuwa kama inavyoainishwa

katika Ibara ndogo ya (4).

Majukumu

ya jumla ya

Tume


189

.-(1) Majukumu ya jumla ya Tume ya Maadili ya Uongozi na

Uwajibikaji yatakuwa ni kufuatilia na kuchunguza tabia na mwenendo

wa viongozi na watumishi wa umma kwa madhumuni ya kusimamia na

kuhakikisha kuwa Maadili ya Uongozi wa Umma na Miiko ya Uongozi

wa Umma inazingatiwa, inalindwa na kuheshimiwa katika utumishi wa

Serikali, Bunge, Mahakama, taasisi na idara nyingine zote za umma.

(2) Bila ya kuathiri masharti ya jumla ya Ibara ndogo ya (1),

majukumu mahsusi ya Tume yatakuwa ni:

(a)kusimamia maadili na uwajibikaji katika utumishi wa umma;

(b)kufanya upekuzi na kufuatilia kumbukumbu za wanaoomba

nafasi za uongozi wa umma;

(c)kuchunguza tabia na mwenendo wa mtumishi au kiongozi wa

umma na kuchukua hatua pale inapostahili, ikiwa ni pamoja

na kuwafikisha watumishi watakaobainika, kuvunja maadili

na miiko ya kazi katika vyombo vya sheria;

(d)kusimamia sheria itakayotungwa na Bunge kuhusu maadili na

uwajibikaji wa viongozi na watumishi wa umma;

(e)kushughulikia masuala ya ubadhirifu wa fedha na mali za

umma;

(f)kufanya uchambuzi yakinifu kwa viongozi wa umma

wanaopewa dhamana kabla ya kuingia madarakani;

(g)kutoa elimu ya maadili kwa umma kuhusu miiko na maadili

ya viongozi wa umma;

(h)kufanya uchunguzi kwa maamuzi yake yenyewe, au baada ya

kupokea malalamiko kutoka kwa mtu yeyote, kutokana na

kutenda au kutokutenda kwa Kiongozi au mtumishi yeyote

wa umma, au wakala wa Serikali, ikiwa kitendo

kilichotendwa au kutokutendwa ni kinyume cha maadili ya

umma;

(i) kumuelekeza, baada ya kupata malalamiko au itapoona

inafaa, kiongozi au mtumishi wa umma au wakala wa Serikali

au chombo chochote cha umma kufanya tendo lolote au

jambo lolote linalotakiwa na sheria, au kuacha, kuzuia au

kusahihisha utendaji mbaya au usiosahihi wa majukumu

yake;

(j) kutoa maelekezo kuhusu kuchukuliwa hatua kiongozi au

mtumishi yeyote wa umma;

(k)kumuelekeza kiongozi au mtumishi wa umma, kwa mujibu

wa sheria, kutoa nyaraka zinazohusiana na matumizi ya ofisi,

matumizi ya fedha au mali za umma, au kutoa taarifa ya

matumizi mabaya kwa Tume, kwa hatua stahiki.

(l) kuomba msaada au taarifa muhimu kutoka kwa mamlaka


78

yoyote ya Serikali au binafsi katika kutekeleza wajibu wake,

na kukagua, kama ni lazima, kumbukumbu muhimu na

nyaraka husika;

(m) kwa kuzingatia sheria, kutangaza kwa umma, mambo yote

yanayohusiana na uchunguzi iliyoufanya, iwapo mazingira

yanaruhusu;

(n) kuchunguza jambo au mazingira yoyote yanayokiuka au

kusababisha ukiukaji wa maadili; na

(o) kuandaa kanuni za taratibu na matumizi ya mamlaka au

utekelezaji wa kazi na majukumu ya Tume kama

itakavyoelekezwa na sheria.

Muda wa

kukaa

madarakani

kwa

Wajumbe

wa Tume


190

.Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na Wajumbe wa Tume

watakaa madarakani kwa vipindi viwili tu vya miaka mitatu kila kimoja,

ikizingatiwa kwamba uteuzi wa wajumbe wa Tume utafanywa kwa

namna ambayo Wajumbe wa Tume hawataanza au kumaliza muda wao

kwa wakati mmoja.

Kuondolewa

madarakani

kwa

Wajumbe

wa Tume


191

.-(1) Mwenyekiti wa Tume au mjumbe yeyote wa Tume

anaweza kuondolewa madarakani kwa:

(a)kutokuwa na uwezo wa kutekeleza majukumu yake kwa

sababu za kiafya kutokana na matatizo ya akili au kimwili;

(b)kukiuka Kanuni za Maadili ya Viongozi wa Umma;

(c)kukiuka Miiko ya Uongozi;

(d)kukosa weledi; au

(e)utovu wa nidhamu.

(2) Mwenyekiti au mjumbe wa Tume anaweza kuondolewa

madarakani kutokana na mapendekezo ya Tume ya Utumishi wa Umma

au kwa maombi ya mtu yeyote kwa Tume ya Utumishi wa Umma, kwa

masharti kwamba:

(a)maombi hayo yawe ya maandishi; na

(b)yaainishe masuala yanayolalamikiwa.

(3) Baada ya kupokea maombi hayo au endapo malalamiko

yametolewa na Tume yenyewe, Tume itaunda Kamati Maalum

itakayofanya uchunguzi kuhusu malalamiko hayo.

(4) Masuala ya Kamati Maalum yanayohusu:

(a)idadi ya wajumbe;

(b)sifa za wajumbe; na

(c)muda wa kufanya kazi,

yatakuwa kama itakavyoamuliwa na Tume.

(5) Baada ya kupokea taarifa yenye mapendekezo ya Kamati

Maalum, Tume itapeleka mapendekezo ya Kamati Maalum kwa Rais

kwa uamuzi.

Uhuru wa

Tume


192

.-(1) Tume itakuwa huru na kwa mantiki hiyo haitaingiliwa na

mtu au mamlaka yoyote katika utekelezaji wa majukumu yake.

(2) Bunge litatunga sheria itakayoweka masharti kuhusu:


79

(a) utaratibu wa utekelezaji wa majukumu ya Tume;

(b) utayarishaji na utoaji wa taarifa za Tume;

(c) utaratibu wa utoaji wa mapendekezo na maamuzi ya Tume;

(d) watumishi wa Tume; na

(e) masuala mengine muhimu yanayoihusu Tume.

Uwezeshaji

wa nyenzo

na rasilimali


193

. Serikali itahakikisha kuwa Tume ya Maadili ya Uongozi na

Uwajibikaji inapatiwa fedha, nyenzo na rasilimali watu ya kutosha kadri

hali itakavyoruhusu ili kutekeleza kazi na wajibu wake kwa ufanisi.

SEHEMU YA PILI

T
UME YA HAKI ZA BINADAMU

Tume ya

Haki za

Binadamu


194.-

(1) Kutakuwa na tume itakayoitwa Tume ya Haki za

Binadamu itakayoundwa na Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na

Wajumbewasiozidi saba.

(2) Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Haki za

Binadamu watateuliwa na Rais baada ya kupendekezwa na Tume ya

Utumishi wa Umma.

(3) Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti watashika madaraka yao

baada ya kuthibitishwa na Bunge.

(4) Sifa za Mwenyekiti wa Tume zitakuwa kama ifuatavyo:

(a)awe raia;

(b)mtu mwenye shahada ya sheria;

(c)mtu mwenye uzoefu wa utumishi wa umma kwa kipindi

kisichopungua miaka kumi; na

(d)mtu mwenye heshima,weledi uaminifu, uadilifu na asiye na

tabia au mwenendo wenye kutiliwa shaka na jamii.

(5) Sifa za Makamu Mwenyekiti zitakuwa kama zilivyoainishwa

katika Ibara ndogo ya (4).

Kazi na

majukumu

ya Tume


195

. Kazi na majukumu ya Tume ya Haki za Binadamu

yatakuwa kama ifuatavyo:

(a) kuhamasisha hifadhi ya haki za binadamu na wajibu kwa

jamii kwa mujibu wa katiba na sheria za nchi;

(b) kupokea malalamiko juu ya uvunjaji wa haki za binadamu

kwa ujumla;

(c) kuchunguza uvunjaji wa haki za binadamu na ukiukwaji wa

misingi ya utawala bora;

(d) kufanya utafiti na kutoa elimu kwa umma kuhusu haki za

binadamu na utawala bora;

(e) kufungua mashauri Mahakamani ili kuzuia vitendo vya

uvunjaji wa haki za binadamu au kurekebisha haki

inayotokana na uvunjwaji huo wa haki za binadamu au

ukiukwaji wa misingi ya utawala bora;

(f) kuchunguza mwenendo wa mtu yeyote anayehusika au

taasisi yeyote inayohusika na masharti ya Ibara hii katika

utekelezaji wa kawaida wa madaraka ya kazi au majukumu


80

yake au utekelezaji unaokiuka madaraka hayo;

(g) kutoa ushauri kwa Serikali na vyombo vingine vya umma na

vya sekta binafsi kuhusu haki za binadamu na utawala bora;

na

(h) kuchukua hatua zinazostahiki kwa ajili ya kukuza na

kuendeleza usuluhishi na suluhu miongoni mwa watu na

taasisi mbalimbali wanaofika au kufikishwa mbele ya Tume.

Muda wa

kukaa

madarakani

kwa

Wajumbe

wa Tume


196

. Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na Wajumbe wa Tume

watakaa madarakani kwa vipindi viwili tu vya miaka mitatu kila kimoja,

ikizingatiwa kwamba uteuzi wa wajumbe wa Tume utafanywa kwa

namna ambayo Wajumbe wa Tume hawataanza au kumaliza muda wao

kwa wakati mmoja.

Kuondolewa

madarakani

kwa

Wajumbe wa

Tume


197

.-(1) Mwenyekiti na Makamu wa Mwenyekiti wa Tume au

mjumbe yeyote wa Tume anaweza kuondolewa madarakani kwa:

(a) kutokuwa na uwezo wa kutekeleza majukumu yake kutokana

na matatizo ya akili au kimwili;

(b) kukiuka kanuni za maadili ya Viongozi wa Umma;

(c) kukiuka Miiko ya Uongozi;

(d) kukosa weledi; na

(e) utovu wa nidhamu.

(2) Mwenyekiti, Makamu wa Mwenyekiti au mjumbe wa Tume

anaweza kundolewa madarakani kutokana na mapendekezo ya Tume ya

Utumishi wa Umma au kwa maombi ya mtu yeyote kwa Tume ya

Utumishi wa Umma, ambapo:

(a) maombi hayo yawe ya maandishi; na

(b) yaainishe masuala yanayolalamikiwa.

(3) Baada ya kupokea maombi hayo au endapo malalamiko

yametolewa na Tume yenyewe, Tume itaunda Kamati Maalum

itakayofanya uchunguzi kuhusu malalamiko hayo.

(4) Masuala yanayohusu:

(a) idadi ya wajumbe;

(b) sifa za wajumbe; na

(c) muda wa kufanya kazi za Kamati Maalum,

yatakuwa kama itakavyoamuliwa na Tume.

(5) Baada ya kupokea ripoti ya Kamati Maalum, Tume itapeleka

mapendekezo ya Kamati Maalum kwa Rais kwa uamuzi.

Uhuru wa

Tume


198

.-(1) Tume itakuwa huru; na kwa mantiki hiyo, haitaingiliwa

na mtu au mamlaka yoyote katika utekelezaji wa majukumu yake.

(2) Bunge litatunga sheria itakayoweka masharti kuhusu:

(a) utaratibu wa utekelezaji wa majukumu ya Tume;

(b) utayarishaji na utoaji wa taarifa za Tume;

(c) utaratibu wa utoaji wa mapendekezo na maamuzi ya Tume;


81

(d) watumishi wa Tume; na

(e) masuala mengine muhimu yanayoihusu Tume.

Uwezeshaji

wa nyenzo

na rasilimali


199

. Serikali itahakikisha kuwa Tume ya Haki za Binadamu

inapatiwa fedha, nyenzo na rasilimali watu ya kutosha kadri hali

itakavyoruhusu ili kutekeleza kazi na wajibu wake kwa ufanisi.

SEHEMU YA TATU

M
DHIBITI NA MKAGUZI MKUU WA HESABU ZA SERIKALI

Uteuzi wa

Mdhibiti na

Mkaguzi

Mkuu wa

Hesabu za

Serikali


200.

-(1) Kutakuwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za

Serikali ambaye atateuliwa na Rais baada ya kupendekezwa na Tume ya

Utumishi wa Umma.

(2) Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ya Serikali

atashika wadhifa huo mara tu baada ya kuthibitishwa na Bunge la

Jamhuri ya Muungano.

Sifa za

Mdhibiti na

Mkaguzi

Mkuu wa

Hesabu za

Serikali


201.

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali

atateuliwa kutoka miongoni mwa watumishi wa umma wenye sifa

zifuatazo:

(a) aweamefuzu mafunzo ya juu ya uhasibu na kusajiliwa na

mamlaka husika;

(b) ana uzoefu usiyopungua miaka kumi na tano katika utumishi

wa umma;

(c)ana uzoefu usiyopungua miaka kumi na tano katika masuala

yanayohusu ukaguzi wa hesabu za Serikali; na

(d)ni mtu mwenye heshima, weledi, uaminifu, uadilifu na asiye

na upendeleo unaotiliwa shaka na jamii.

Kazi na

majukumu

yake


202.

-(1) Kazi na majukumu ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa

Hesabu za Serikali yatakuwa ni:

(a)kuhakikisha kwamba fedha zozote zinazokusudiwa kutolewa

kutoka Mfuko Mkuu wa Hazina ya Serikali matumizi yake

yameidhinishwa na kwamba zitatolewa kwa mujibu wa

masharti ya Katiba hii, na iwapo atatosheka kwamba masharti

hayo yatatekelezwa ipasavyo, basi ataidhinisha fedha hizo

zitolewe;

(b) kuhakikisha kwamba fedha zote ambazo matumizi yake

yameidhinishwa yatokane na fedha zilizomo katika Mfuko

Mkuu wa Hazina ya Serikali au fedha ambazo matumizi yake

yameidhinishwa na sheria iliyotungwa na Bunge, na

kwambazimetumika kwa ajili ya shughuli zilizohusika na

matumizi ya fedha hizo na matumizi hayo yamefanywa kwa

kufuata idhini iliyotolewa kuhusu matumizi hayo;

(c)angalau, mara moja kila mwaka, kufanya ukaguzi na kutoa

taarifa juu ya ukaguzi wa hesabu za Serikali ya Jamhuri ya

Muungano, hesabu zinazosimamiwa na watumishi wote wa

Serikali ya Jamhuri ya Muungano na hesabu za Mahakama

zote za Jamhuri ya Muungano na zinazosimamiwa na Katibu


82

wa Bunge; na

(d)kutayarisha ripoti ya mwaka na kuiwasilisha Bungeni kwa

ajili ya kujadiliwa na kutolewa mapendekezo.

(2) Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali atakuwa

huru katika utekelezaji wa kazi na majukumu yake, na kwa mantiki hiyo,

hataingiliwa na mtu au mamlaka yoyote katika utekelezaji wa kazi zake.

(3) Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali na kila

mtumishi wa Serikali aliyeruhusiwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu

wa Hesabu za Serikali atakuwa na haki ya kuchunguza vitabu,

kumbukumbu, hati nyinginezo zote zinazohusika na hesabu za aina

yoyote iliyotajwa katika ibara ndogo ya (2) ya Ibara hii.

(4) Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali

atawasilisha kwa Rais kila taarifa atakayotoa kwa mujibu wa masharti

ya Katiba hii.

(5) Baada ya kupokea taarifa hiyo, Rais atawaagiza watu

wanaohusika wawasilishe taarifa hiyo kwenye kikao cha kwanza cha

Bunge kitakachofanyika baada ya Rais kupokea taarifa hiyo na itabidi

iwasilishwe katika kikao hicho kabla ya kupita siku saba tangu siku ile

ulipoanza Mkutano huo, na iwapo Rais hatachukua hatua za kuwasilisha

taarifa hiyo kwa Spika wa Bunge, basi Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu

za Serikali atawasilisha taarifa hiyo kwa Spika wa Bunge au kwa Naibu

Spika iwapo nafasi ya madaraka ya Spika iko wazi,ambaye atawasilisha

taarifa hiyo kwa Bunge.

(6) Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali atakuwa

pia na jukumu la kutekeleza kazi na shughuli nyingine, na atakuwa na

madaraka mengine ya namna mbalimbali, kama itakavyoelezwa na sheria

kuhusu hesabu za Serikali ya Jamhuri ya Muungano au hesabu za

vyombo vya umma au hesabu za mashirika.

(7) Katika kutekeleza madaraka yake kwa mujibu wa masharti

ya ibara ndogo ya (1), (3), (4) na (5) ya Ibara hii, Mdhibiti na Mkaguzi

Mkuu wa Hesabu za Serikali hatalazimika kufuata amri au maagizo ya

mtu mwingine yeyote au idara yoyote ya Serikali,lakini maelezo hayo

ya ibara hii ndogo hayataizuia Mahakama nayo kutumia madaraka yake

kwa ajili ya kuchunguza kama Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu

za Serikali ametekeleza madaraka yake kwa mujibu wa masharti ya

Katiba hii au sivyo.

(8) Bunge linaweza kutunga sheria itakayosimamia, pamoja na

mambo mengine, matumizi ya mamlaka ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu

wa Hesabu za Serikali.

Muda wa

kukaa

madarakani


203.

-(1) Muda wa kukaa madarakani kwa Mdhibiti na Mkaguzi

Mkuu wa Hesabu za Serikali itakuwa ni kipindi kimoja cha miaka saba

mfululizo.

(2) Bila ya kujali masharti ya ibara ndogo ya (1), Mdhibiti na

Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali anaweza kujiuzulu wadhifa wake

kwa kutoa taarifa ya siku thelathini kwa Rais.

Kuondolewa

madarakani


204.

-(1) Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali

anaweza kuondolewa madarakani kwa:


83

(a)kutokuwa na uwezo wa kutekeleza majukumu yake kutokana

na matatizo ya afya ya akili au kimwili;

(b)kukiuka kanuni za Maadili ya Uongozi wa Umma;

(c)kukiuka Miiko ya Uongozi wa Umma;

(d)kukosa weledi; na

(e)utovu wa nidhamu.

(2) Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali anaweza

kuondolewa madarakani kutokana na mapendekezo ya Tume ya

Utumishi wa Umma au kwa maombi ya mtu yeyote kwa Tume ya

Utumishi wa Umma, ambapo:

(a)maombi hayo yawe ya maandishi; na

(b)yaainishe masuala yanayolalamikiwa.

(3) Baada ya kupokea maombi hayo au endapo malalamiko

yametolewa na Tume yenyewe, Tume itaunda Kamati Maalum

itakayofanya uchunguzi kuhusu malalamiko hayo.

(4) Masuala yanayohusu:

(a)idadi ya wajumbe;

(b)sifa za wajumbe; na

(c)muda wa kufanya kazi za Kamati,

yatakuwa kama itakavyoamuliwa na Tume.

(5) Baada ya kupokea ripoti ya Kamati Maalum, Tume itapeleka

mapendekezo ya Kamati Maalum kwa Rais kwa uamuzi.

Uwezeshaji

wa nyenzo

na rasilimali


205

. Serikali itahakikisha kuwa Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi

Mkuu wa Hesabu za Serikali inapatiwa fedha, nyenzo na rasilimali watu

ya kutosha ili kulinda uhuru wake katika kutekeleza kazi na majukumu

yake kwa ufanisi.

SURA YA KUMI NA NNE

M
ASHARTI KUHUSU FEDHA ZA JAMHURI YA MUUNGANO

(a) Mfuko Mkuu wa Hazina na Fedha za

Jamhuri ya MuunganoMfuko

Mkuu wa

Hazina ya

Serikali ya

Jamhuri ya

Muungano


206.

Kutakuwa na Mfuko Mkuu wa Hazina wa Serikali ya Jamhuri

ya Muungano utakaoitwa “Mfuko Mkuu wa Hazina” ambamo fedha zote

zitakazopatikana kwa njia mbalimbali zitawekwa, isipokuwa:

(a) fedha ambazo zimetajwa katika Sheria kuwa zitumike kwa

shughuli maalum au ziwekwe katika mfuko mwingine kwa ajili ya

matumizi maalum; au

(b) fedha ambazo kwa mujibu wa sheria, taasisi za Serikali

zimeruhusiwa kukusanya na kubaki nazo kwa ajili ya kugharamia

uendeshaji wa taasisi hizo.

Masharti ya

kutoa fedha

za matumizi

katika

Mfuko

Mkuu wa

Hazina ya


207.-

(1) Fedha zinaweza kutolewa kutoka Mfuko Mkuu wa Hazina

ya Serikali kwa ajili ya matumizi kwa kuzingatia masharti yafuatayo:

(a) fedha hizo ziwe kwa ajili ya matumizi ambayo

yameidhinishwa kuwa yatokane na fedha zilizomo katika

Mfuko Mkuu wa Hazina ya Serikali na idhini hiyo iwe


84

Serikali.

imetolewa na Katiba hii au sheria nyingine yoyote; na

(b) fedha hizo ziwe kwa ajili ya matumizi ambayo

yameidhinishwa ama na Sheria ya Matumizi ya Serikali

iliyotungwa mahsusi na Bunge au sheria nyingine yoyote

iliyotungwa na Bunge.

(2) Kwa kuzingatia masharti ya Ibara ndogo ya (1), fedha zilizomo

katika Mfuko Mkuu wa Hazina ya Serikali zitatolewa kutoka Mfuko huo

kwa ajili ya matumizi kwa kuzingatia masharti kuwa matumizi hayo yawe

yameidhinishwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.

(3) Fedha zilizomo katika mfuko Maalum wowote wa Serikali,

isipokuwa Mfuko Mkuu wa Hazina ya Serikali, hazitatolewa kutoka mfuko

huo kwa ajili ya matumizi isipokuwa kwa mujibu wa Sheria inayoidhinisha

matumizi hayo.

Utaratibu wa

kuidhinisha

matumizi ya

fedha

zilizomo

katika

Mfuko

Mkuu wa

Hazina ya

Serikali.


208.-

(1) Rais atatoa maagizo kwa watu wanaohusika kutayarishana

kuwasilisha kwenye Bunge katika kila mwaka wa fedha wa Serikali

makadirio ya mapato na matumizi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano

kwa ajili ya kipindi cha mwaka wa fedha unaofuata.

(2) Baada ya Bunge kuyakubali Makadirio ya Matumizi

yaliyoainishwa katika Ibarandogo ya (1) kutawasilishwa kwenye Bunge

Muswada wa Sheria ya Matumizi ya Fedha za Serikali, kwa ajili ya

kuidhinisha matumizi ya fedha kutoka Mfuko Mkuu wa Hazina ya Serikali

zitakazogharamia shughuli mbalimbali za Serikali zinazohusu makadirio

hayo.

(3) ikiwa katika mwaka wa fedha wowote inaonekana kwamba:

(a) fedha za matumizi zilizoidhinishwa na Sheria ya Matumizi ya

Fedha za Serikali kwa ajili ya kugharamia shughuli fulani

hazitoshi;

(b) imekuwa lazima kulipa gharama za shughuli ambayo

haikupangiwa fedha za matumizi kwa mujibu wa Sheria;

(c) kuna fedha ambazo zimetumiwa kwa ajili ya shughuli fulani

kwa kiasi kinachozidi kiwango cha matumizi yaliyoidhinishwa

na Sheria ya Matumizi ya Fedha za Serikali kuhusu shughuli

hiyo;

(d) fedha zimetumiwa kulipia gharama za shughuli ambayo

haikupangiwa fedha za matumizi kwa mujibu wa Sheria,

kutawasilishwa kwenye Bunge makadirio ya matumizi ya nyongeza au,

kadri itakavyokuwa, maelezo ya matumizi ya ziada, na baada ya Bunge

kuyakubali hayo makadirio ya matumizi ya nyongeza au maelezo ya

matumizi ya ziada, kutawasilishwa kwenye Bunge Muswada wa Sheria ya

Matumizi ya Fedha za Serikali kwa ajili ya kuidhinisha matumizi ya fedha

kutoka Mfuko Mkuu wa Hazina ya Serikali, na fedha hizo zitagharamia

shughuli zinazohusika na hayo makadirio au maelezo.

Utaratibu wa

kuidhinisha

matumizi ya

fedha kabla


209.-

(1) Iwapo mwaka wa fedha wa Serikali umeanza na Sheria ya

Matumizi ya Fedha za Serikali inayohusika na mwaka huo haijaanza

kutumika, Rais anaweza kuidhinisha fedha itolewe kutoka Mfuko Mkuu


85

ya Sheria ya

Matumizi ya

Fedha za

Serikali

kuanza

kutumika


wa Hazina ya Serikali kwa ajili ya kugharamia shughuli za lazima za

Serikali, na fedha hizo zitatumiwa mpaka ipite miezi minne tangu mwanzo

wa mwaka wa fedha mpaka Sheria ya Matumizi ya Fedha za

Serikaliitakapoanza kutumika, kutegemea na lipi kati ya mambo hayo

litatokea mapema zaidi.

(2) Bunge linaweza kutunga sheria kwa ajili ya kuweka masharti ya

kuidhinisha matumizi ya fedha kutoka Mfuko Mkuu wa Hazina ya Serikali

kwa kufuata utaratibu ulioelezwa katika Ibara ndogo ya (1).

Mfuko wa

Matumizi ya

Dharura.


210.-

(1) Kutakuwa na Mfuko wa Matumizi ya Dharura ambao

matumizi yake yatawekewa masharti na Sheria itakayotungwa na Bunge.

(2) Sheria iliyotajwa katika Ibara ndogo ya (1) itaruhusu Rais au

Waziri mwenye dhamana ya masuala ya fedha, pale anaporidhika kuwa

kuna:

(a) jambo la haraka na la dharura na ambalo halikutazamiwa

kutokea na ambalo halikupangiwa fedha, kuazima fedha

kutoka Mfuko wa Matumizi ya Dharura kwa ajili ya

kugharamia jambo hilo; au

(b) jambo la haraka na la dharura kama ilivyoelezwa katika aya

ya (a) ya Ibara ndogo ya (2), kutumia fedha zilizotengwa

mahsusi kwa ajili ya kugharamia shughuli fulani kulipia

gharama za jambo hilo.

(3) Iwapo fedha zimeazimwa kutoka Mfuko wa Matumizi ya

Dharura au fedha zilizotengwa mahsusi kwa ajili ya shughuli fulani

zimetumiwa kugharamia jambo la haraka na la dharura, basi

kutawasilishwa kwenye Bunge makadirio ya matumizi ya nyongeza, na

baada ya Bunge kuyakubali makadirio hayo Muswada wa Sheria ya

Matumizi ya Fedha za Serikali utakaowasilishwa kwenye Bunge kwa ajili

ya kuidhinisha matumizi hayo utahakikisha kwamba fedha zozote

zilizoazimwa kwenye Mfuko wa Matumizi ya Dharura zitarudishwa

kwenye Mfuko huo kutoka katika fedha za matumizi yatakayoidhinishwa

na Muswada huo.

Mishahara ya

baadhi ya

watumishi

kudhaminiwa

na Mfuko

Mkuu


211.-

(1) Watumishi wa Serikali wanaohusika na masharti ya Ibara

hii watalipwa mishahara na posho kama itakavyoelezwa na sheria

itakayotungwa na Bunge.

(2) Fedha za malipo ya mishahara na posho za watumishi wa

Serikali wanaohusika na masharti ya Ibara hii pamoja na fedha za malipo

ya uzeeni na kiinua mgongo kwa wale wanaostahili malipo hayo miongoni

mwa watumishi hao zitatolewa kutoka Mfuko Mkuu wa Hazina ya

Serikali.

(3) Mshahara anaolipwa mtumishi wa Serikali anayehusika na

masharti ya Ibara hii pamoja na masharti yake ya kazi havitabadilishwa,

baada ya mtumishi huyo kuteuliwa, kwa jinsi ambayo itapunguza maslahi

ya mtumishi huyo, lakini maelezo haya hayahusiki na posho anayolipwa

mtumishi huyo.

(4) Iwapo mtumishi wa Serikali anayehusika na masharti ya Ibara

hii ana hiari ya kuchagua kima cha mshahara au aina ya masharti ya kazi,


86

basi kwa madhumuni ya ufafanuzi wa masharti ya Ibara ndogo ya (3),

mshahara wa kima hicho atakaochagua na aina hiyo ya masharti ya kazi

atakayochagua vitahesabiwa kuwa vina maslahi zaidi kwake kuliko kima

cha mshahara kingine chochote ambacho anaweza kuchagua au aina ya

masharti ya kazi nyingine yoyote ambayo angeweza kuchagua.

(5) Masharti ya Ibara hii yatatumika kwa Jaji Mkuu, Naibu Jaji

Mkuu, Jaji wa Mahakama ya Juu, Mwenyekiti wa Mahakama ya Rufani,

Naibu Mwenyekiti wa Mahakama ya Rufani
, Jaji wa Mahakama ya

Rufani, Mwenyekiti na Mjumbe wa Tume ya Haki za Binadamu na

watumishi wengine watakaotajwa na sheria itakayotungwa na Bunge.

(b) Deni la Taifa na Mikopo ya Serikali ya Jamhuri ya MuunganoDeni la Taifa

212.-(1) Deni la Taifa litadhaminiwa na Mfuko Mkuu wa Hazina

ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano.

(2) Kwa madhumuni ya ufafanuzi wa Ibara hii, deni la Taifa maana

yake ni deni lenyewe na pia riba inayolipwa juu ya deni hilo, fedha

zinazowekwa akiba kwa ajili ya kulipa deni kwa awamu na gharama zote

zinazoambatana na usimamizi wa deni hilo.

Mamlaka ya

kukopa ya

Serikali ya

Jamhuri ya

Muungano.


213.-

(1) Serikali ya Jamhuri ya Muungano itakuwa na mamlaka ya

kukopa fedha ndani na nje ya Jamhuri ya Muungano kwa ajili ya

kugharamia shughuli zilizo chini ya mamlaka yake.

(2) Bunge linaweza kutunga sheria ambayo:

(a) itaweka masharti ya kuzingatiwa na Serikali wakati wa kukopa;

na

(b) itaweka utaratibu wa Serikali kutoa taarifa Bungeni kuhusu

mikopo.

(3) Kwa kuzingatia masharti ya Ibara ndogo ya (2)(b), taarifa

itakayowasilishwa Bungeni pamoja na mambo mengine itaeleza:

(a) kiasi cha deni lililopo na riba yake;

(b) matumizi yaliyofanywa au yatakayofanywa kutokana na fedha

za mkopo husika;

(c) utaratibu uliowekwa wa kulipa deni husika; na

(d) hatua iliyofikiwa katika kulipa deni husika.

Mamlaka ya

kukopa

fedha ya

Serikali za

Washirika

wa

Muungano.


214.-

(1) Serikali ya Mshirika wa Muungano itakuwa na mamlaka

ya kukopa fedha ndani na nje ya Jamhuri ya Muungano kwa ajili ya

kugharamia shughuli zilizo chini ya mamlaka yake.

(2) Endapo mkopo utahitaji dhamana, Serikali ya Jamhuri ya

Muungano, baada ya kushauriana na kukubaliana na Serikali ya Mshirika,

inaweza kutoa dhamana kwa mkopo unaoombwa.

(3) Bunge litatunga sheria itakayoweka utaratibu wa Serikali ya

Jamhuri ya Muungano kudhamini mikopo ya Serikali za Washirika wa

Muungano.

(4) Katika kipindi cha miezi mitatu tangu kumalizika kwa mwaka

wa fedha, Serikali itachapisha ripoti katika Gazeti la Serikali itakayoelezea

mikopo iliyodhaminiwa na Serikali katika mwaka wa fedha uliopita.


87

(c) Vyanzo vya Mapato ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano na

Manunuzi ya UmmaVyanzo vya

mapato vya

Serikali ya

Jamhuri ya

Muungano


215.

Vyanzo vya mapato ya Serikali ya Jamhuri ya

Muunganovitakuwa:

(a) ushuru wa bidhaa;

(b) maduhuli yatokanayo na taasisi za Muungano;

(c) mchango kutoka kwa Washirika wa Muungano; na

(d) mikopo kutoka ndani na nje ya Jamhuri ya Muungano.

Manunuzi

ya Umma


216.-

(1) Katika kufanya manunuzi ya umma, Serikali na taasisi

zote za umma zitatakiwa kutumia au kuweka mfumo utakaozingatiahaki,

uwazi, maslahi ya umma, uwajibikaji, ushindani na unaozingatia thamani

halisi ya fedha.

(2) Katika kufanya manunuzi ya umma, Serikali na taasisi zake

zitatakiwa kutumia au kuweka mfumo ambao utazingatia kununua bidhaa

zinazozalishwa au huduma zinazotolewa nchini kwa kuzingatia masharti

yaliyoainishwa katika Ibara hii na sheria itakayotungwa na Bunge.

(3) Bunge litatunga sheria itakayoweka masharti ya usimamizi na

udhibiti wa manunuzi ya umma.

(d)Benki Kuu
Benki Kuu

ya Jamhuri

ya

Muungano.


217.-

(1) Kutakuwa na Benki Kuu ya Jamhuri ya Muungano wa

Tanzania itakayojulikana kuwa “Benki Kuu” ambayo itakuwa na

majukumu yafuatayo:

(a) kutoa sarafu, kudhibiti na kusimamia mzunguko wa sarafu;

(b) kuandaa na kusimamia Sera na Mipango inayohusiana na

sarafu;

(c) kudhibiti na kusimamia masuala ya fedha za kigeni; na

(d) kusimamia Benki za Washirika wa Muungano.

(2) Katika utekelezaji wa majukumu yake, Benki Kuu itakuwa huru

na haitaingiliwa ama kwa kupewa maelekezo au kudhibitiwa na mtu au

mamlaka yoyote.

(3) Bunge litatunga sheria itakayoweka masharti kuhusu muundo wa

Benki Kuu itakayozingatia uwakilishi wa pande zote mbili za Muungano,

mamlaka, shughuli na utendaji wa Benki Kuu.

Benki za

Serikali za

Washirika


218.

Serikali za Washirika zitakuwa na Benki zitakazokuwa

najukumu la kutunza akaunti ya fedha za Serikali husika, kusimamia Sera

za Kifedha na benki za biashara katika mamlaka zao.

SURA YA KUMI NA TANO

U
LINZI NA USALAMA KATIKA JAMHURI YA MUUNGANO

(a) Ulinzi na Usalama wa TaifaUsalama

wa Taifa


219.-

(1) Jukumu la ulinzi na Usalama wa Jamhuri ya Muungano ni

la kila raia.


88

(2) Usalama wa Jamhuri ya Muungano unahusu ulinzi wa mipaka

yote ya eneo la Jamhuri ya Muungano ikiwa ni pamoja na anga na bahari

kuu, watu wake, mali zao,haki, uhuru na maslahi mengine ya kitaifa dhidi

ya vitisho vya ndani na nje.

(3) Ulinzi na Usalama wa Jamhuri ya Muungano utaimarishwa na

kuhakikishwa kulingana na kanuni zifuatazo-

(a) usalama wa taifa unaongozwa na mamlaka ya Katiba hii na

Bunge;

(b) usalama wa taifa utatekelezwa kwa kuzingatia sheria, ikiwemo

sheria za kimataifa, na kwa kuheshimu kikamilifu utawala wa

kisheria na haki za binadamu; na

(c) taasisi za usalama wa Taifa zitaheshimu utamaduni wa aina

mbalimbali wa jamii katika kutekeleza majukumu yake.

Taasisi za

Ulinzi na

Usalama

wa Taifa.


220.-

(1) Taasisi za ulinzi na usalama wa Taifa ni-

(a) Jeshi la Wananchi wa Tanzania;

(b) Jeshi la Polisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; na

(c) Idara ya Usalama wa Taifa.

(2) Lengo la kimsingi la taasisi za ulinzi na usalama wa Taifa na

mfumo wa usalama ni kulinda maslahi ya raia na watu wengine na mali zao

na haki na uhuru, na mamlaka, amani, umoja wa kitaifa na mipaka ya

Jamhuri ya Muungano.

(3) Katika utekelezaji wa majukumu yao, taasisi za ulinzi na

usalama wa taifa na kila mtumishi wa taasisi hizo hataruhusiwa-

(a) kuwa na upendeleo kwa njia yoyote;

(b) kuendeleza maslahi ya chama chochote cha kisiasa au sera zake;

(c) kuhujumu maslahi ya kisiasa au mpango wa kisiasa ambao ni

halali chini ya Katiba hii;

(d) kutishia, kudhulumu au kuwatendea raia ukatili; na

(e) kutii amri yoyote isiyokuwa halali.

(4) Mtu hataruhusiwa kuanzisha taasisi, kampuni, jumuiya au

shirika linalohusiana na ulinzi na usalama wa taifa au ushirika wa kijeshi,

isipokuwa kama inavyoruhusiwa na Katiba hii au sheria ya Bunge.

(5) Taasisi za ulinzi na usalama wa Taifa zitakuwa chini ya

mamlaka yaRais.

(6) Rais anaweza kuunda chombo cha ulinzi na usalama kwa

kushauriana na Baraza la Ulinzi na Usalama la Taifa.

(7) Bunge litatunga sheria kuweka masharti kuhusu utekelezaji wa

majukumu, utaratibu na usimamizi wa taasisi za ulinzi na usalama wa Taifa.

Kuanzishwa

kwa Baraza

la Ulinzi na

Usalama

wa Taifa.


221.-

(1) Kutakuwa na Baraza la Ulinzi na Usalama wa Taifa

litakalokuwa na wajumbe wafuatao-

(a) Rais wa Jamhuri ya Muungano;

(b) Makamu wa Rais;

(c) Rais wa Tanzania Bara;

(d) Rais wa Zanzibar;

(e) Waziri mwenye dhamana na ulinzi;


89

(f) Waziri mwenye dhamana ya mambo ya ndani ya nchi;

(g) Waziri mwenye dhamana na mambo ya nje;

(h) Waziri mwenye dhamana na usalama wa taifa;

(i) Waziri mwenye dhamana ya fedha;

(j) Mwanasheria Mkuu wa Serikali;

(k) Mkuu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania;

(l) Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa; na

(m)Mkuu wa Jeshi la Polisi la Jamhuri ya Muungano wa

Tanzania.

(2) Mwenyekiti anaweza kumwalika mtu yeyote anayeshika nafasi

ya madaraka katika taasisi za Serikali, Bunge au Mahakama kushiriki katika

kikao cha Baraza la Usalama wa Taifa.

(3
) Kutakuwa na Sekretarieti ya Baraza la Ulinzi na Usalama la

Taifa itakayoongozwa na Katibu Mkuu Kiogozi.

(4) Vikao vya Baraza la Ulinzi na Usalama la Taifa vitaongozwa na

Rais, endapo kama Rais hayupo vitaongozwa na Makamu wa Rais.

(5) Baraza la Ulinzi na Usalama la Taifa litaweka utaratibu wa

mwenendo wa vikao vyake.

(6) Bunge litatunga sheria itakayoweka masharti kuhusu utekelezaji

wa majukumu ya Baraza la Ulinzi na Usalama la Taifa.

Majukumu

ya Baraza

la Ulinzi na

Usalama

la Taifa.


222.-

(1) Baraza la Ulinzi na Usalama wa Taifa litakuwa na jukumu

la-

(a) kuunganisha sera za ndani, sera za kigeni na za kijeshi

kuhusiana na usalama wa Taifa ili kuwezesha taasisi za ulinzi

na usalama wa Taifa kushirikiana kikamilifu;

(b) kutathmini na kuchunguza malengo, kujitoleana hatari kwa

Taifa kuhusiana na usalama wa nchi; na

(c) kuanzisha sera kuhusu masuala ya maslahi ya pamoja ya

kiusalama ya taasisi za kiusalama na kudhibiti taasisi hizo.

(2) Rais atatoa taarifa kwa Bunge kila mwaka kuhusiana na hali ya

usalama katika Jamhuri ya Muungano.

(b)Jeshi la Wananchi wa TanzaniaKuanzishwa

kwa Jeshi

la

Wananchi

wa

Tanzania.


223.-

(1) Kutakuwa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania litakalokuwa

na mamlaka ya kusimamia ulinzi na usalama wa wananchi na mipaka ya

Jamhuri ya Muungano.

(2) Rais anaweza kuanzisha vikosi vingine vya Jeshi la Wananchi

wa Tanzania kama atakavyoona inafaa.

Uteuzi wa

Mkuu wa

Majeshi


224

. Kutakuwa na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ambaye atateuliwa

na Rais baada ya kushauriana na Baraza la Ulinzi na Usalama la Taifa.

Madaraka

ya Amiri

Jeshi Mkuu


225.-

(1) Bila ya kuathiri masharti yatakayowekwa na sheria yoyote

iliyotungwa na Bunge, miongoni mwa madaraka ya Rais akiwa Amiri Jeshi

Mkuu ni kuyaamuru majeshi ya nchi yatende mambo yanayohusika na vita

vya ulinzi wa Jamhuri ya Muungano, mambo ya kuokoa maisha na mali ya


90

watu katika hali ya hatari na mambo mengineyo ambayo Amiri Jeshi Mkuu

ataona inahitajika, na kwa ajili hiyo Amiri Jeshi Mkuu anaweza kuyaamuru

majeshi hayo yatekeleze mambo hayo ama ndani au nje ya Tanzania.

(2) Bila ya kuathiri masharti yatakayowekwa na sheria iliyotungwa

na Bunge, madaraka juu ya mambo yafuatayo yatakuwa mikononi mwa

Amiri Jeshi Mkuu-

(a) madaraka ya kuwateua viongozi katika majeshi ya ulinzi ya

Jamhuri ya Muungano;

(b) madaraka ya kuwateua wanajeshi watakaoongoza vikosi mbali

mbali vya majeshi ya ulinzi; na

(c) madaraka ya kumwamuru mwanajeshi yeyote asitumie

madaraka yoyote aliyokabidhiwa na ambayo yanaambatana na

kuwa kwake mwanajeshi.

(3) Jambo lolote atakalotenda mwanajeshi yoyote kinyume cha amri

iliyotolewa na Amiri Jeshi Mkuu kwa mujibu wa masharti ya ibara ndogo

ya (1) na (2) ya ibara hii litakuwa batili.

Tume ya

utumishi ya

Jeshi la

Wananchi

wa

Tanzania


226

.-(1) Kutakuwa na Tume ya Utumishi ya Jeshi la Wananchi wa

Tanzania itakayokuwa na jukumu la kusimamia masuala yote ya utumishi

wa wanajeshi wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania na vikosi vyake.

(2) Bunge litatunga sheria itakayoweka masharti kuhusu muundo,

majukumu na mambo mengine yanayohusu Tume ya Utumishi ya Jeshi la

Wananchi wa Tanzania.

(c) Jeshi la Polisi la Jamhuri ya MuunganoJeshi la

Polisi la

Tanzania


227.-

(1) Kutakuwa na Jeshi la Polisi la Jamhuri ya Muungano

litakalokuwa na jukumu la ulinzi wa watu na mali zao chini ya masharti ya

Katiba hii.

(2) Bunge litatunga sheria kuweka masharti ya utekelezaji wa kazi

na majukumu ya Jeshi la Polisi la Jamhuri ya Muungano kwa kuzingatia

haki za raia na sheria za kimataifa.

Misingi ya

utendaji wa

Jeshi la

Polisi


228.

Katika utekelezaji wa majukumu yake, Jeshi la Polisi la

Jamhuri ya Muungano litazingatia-

(a) viwango vya juu vya kitaaluma na nidhamu miongoni mwa

wafanyakazi wake;

(b) ulinzi na ukuzaji wa haki za binadamu;

(c) kanuni za uwazi na uwajibikaji;

(d) kuzuia rushwa na ufisadi; na

(e) kukuza mahusiano na jamii.

Uteuzi wa

Mkuu wa

Jeshi la

Polisi


229

. Kutakuwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi la Jamhuri ya Muungano

ambaye atateuliwa na Rais baada ya kushauriana na Baraza la Ulinzi na

Usalama wa Taifa.

Tume ya

Utumishi

ya Jeshi la

Polisi


231.-

(1) Kutakuwa na Tume ya Utumishi ya Jeshi la Polisi

itakayokuwa na jukumu la kusimamia masuala yote ya utumishi wa Jeshi la

Polisi na idara zake.

(2) Katika suala la uajiri wa maofisa na watumishi wengine wa Jeshi


91

la Polisi, Tume ya Utumishi waJeshi la Polisi itazingatia Kanuni na Misingi

ya Utumishi iliyoainishwa katika Katiba hii.

(3) Bunge litatunga sheria kuweka masharti ya muundo na

utekelezaji wa kazi na majukumu ya Tume ya Utumishi waJeshi la Polisi.

Polisi wa

Washirika

wa

Muungano.


232

.-(1) Bila ya kuathiri masharti ya Katiba hii, nchi washirika wa

Muungano wanaweza kuanzisha vikosi vya ulinzi vitakavyosimamia

masuala ya usalama wa watu na mali katika maeneo yao.

(2) Vikosi vya ulinzi vya Washirika wa Muungano, vitatekeleza

majukumu yao kwa ushirikiano na Jeshi la Polisi la Jamhuri ya Muungano

ili kuepusha mgongano wa mamlaka katika utekelezaji wa majukumu

katika maeneo hayo.

(d) Idara ya Usalama wa Taifa ya Jamhuri ya MuunganoKuanzishwa

kwa Idara ya

Usalama ya

Taifa.


233.-

(1) Kutakuwa na Idara ya Usalama wa Taifa ya Jamhuri ya

Muungano.

(2) Idara ya Usalama ya Jamhuri ya Muungano itahusika na

shughuli za kuimarisha usalama wa Jamhuri ya Muungano na kulinda

Katiba hii, maslahi ya Taifa na ya watu na itatekeleza majukumu mengine

kama yatakavyoainishwa na Sheria itakayotungwa na Bunge.

Uteuzi wa

Mkurugenzi

wa Idara ya

Usalama wa

Taifa.


234

.- Rais, baada ya kushauriana na Baraza la Ulinzi na Usalama la

Taifa, atamteua Mkurugenzi wa Idara ya Usalama wa Taifa.

Usalama

wa

Washirika

wa

Muungano


235.

Bila ya kuathiri masharti ya Katiba hii, Washirika wa

Muungano wanaweza kuanzisha Idara au Taasisi zitakazoshughulika na

mambo ya kiusalama katika mamlaka zao ambazo zitafanya na kutekeleza

majukumu yao kwa kushirikiana na Idara ya Usalama ya Jamhuri ya

Muungano.

SURA YA KUMI NA SITA

M
ENGINEYO

Masharti

kuhusu

utaratibu

wa

kukabidhi

madaraka


236

.-(1) Mtu yeyote mwenye dhamana ya kazi yoyote iliyoanzishwa

na Katiba hii pamoja na kazi ya Waziri, Naibu Waziri au Mbungeanaweza

kujiuzulu kwa kutoa taarifa iliyoandikwa na kutiwa saini kwa mkono wake,

kwa kufuata masharti yafuatayo:

(a) iwapo mtu huyo aliteuliwa au kuchaguliwa na mtu mmoja,

basi taarifa hiyo ya kujiuzulu atawasilisha kwa mtu huyo

aliyemteua au aliyemchagua, au iwapo aliteuliwa au

kuchaguliwa na kikao cha watu, basi taarifa hiyo ya kujiuzulu

ataiwasilisha kwenye kikao hicho;

(b) iwapo mtu huyo ni Rais, basi taarifa hiyo ya kujiuzulu

ataiwasilisha kwa Spika;

(c) iwapo mtu huyo ni Spika au Naibu Spika wa Bunge, basi


92

taarifa hiyo ya kujiuzulu ataiwasilisha kwenye Bunge; na

(d) iwapo mtu huyo ni Mbunge, basi taarifa hiyo ya kujiuzulu

ataiwasilisha kwa Spika.

(2) Mtu aliyetoa taarifa ya kujiuzulu kwa mujibu wa masharti ya

Ibara ndogo ya (1), atahesabiwa kuwa amejiuzulu tangu siku ile ambayo

taarifa yake ya kujiuzulu itakapopokelewa na mtu anayehusika au kikao

kinachohusika na itakapopokelewa na mtu yeyote aliyeruhusiwa kuipokea

taarifa hiyo na mtu anayehusika au kikao kinachohusika, lakini kama taarifa

hiyo ya kujiuzulu imeeleza kwamba mtu huyo atajiuzulu tangu siku

nyingine baada ya taarifa hiyo kupokelewa na mtu anayehusika au kikao

kinachohusika, basi mtu huyo atahesabiwa kuwa amejiuzulu tangu siku

hiyo nyingine ya baadaye.

(3) Endapo mtu yeyote mwenye dhamana ya kazi yoyote

iliyoanzishwa na Katiba hii, pamoja na kazi ya Waziri, Naibu Waziri au

Mbunge, amejiuzulu, basi ikiwa anazo sifa zote zinazohitajika na kwa kila

hali anastahili, anaweza kuteuliwa au kuchaguliwa tena kushika madaraka

ya kazi hiyo kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii.

(4) Masharti yaliyomo katika Ibara ndogo ya (3) hayatamzuia mtu

ambaye ni Rais kuchaguliwa tena kuwa Rais wakati bado ameshika

madaraka ya kazi ya Rais.

Masharti

kuhusu

madaraka

ya kazi


237

.-(1) Kwa madhumuni ya ufafanuzi wa masharti ya Katiba hii

kuhusu utaratibu wa kukabidhi madaraka ya kazi katika utumishi wa

Serikali ya Jamhuri ya Muungano, ifahamike kuwa mtu yeyote mwenye

mamlaka, kwa mujibu wa Katiba hii, ya kumteua mtu mwingine kushika

madaraka ya kazi pia atakuwa na uwezo wa kumteua kaimu au mtu ambaye

atashika kwa muda na kutekeleza madaraka ya kazi hiyo:

Isipokuwa kwamba maelezo hayo hayatatumika kwa madaraka ya

kazi ya Waziri, Naibu Waziri, Jaji wa Mahakama ya Juu, Jaji wa

Mahakama ya Rufani, Mjumbe wa Tume yaMaadili ya Uongozi na

Uwajibikaji au Mjumbe wa Tume Huru ya Uchaguzi.

(2) Kanuni zifuatazo zitatumika pia kwa madhumuni ya ufafanuzi

wa masharti ya Katiba hii kuhusu utaratibu wa kukabidhiana madaraka ya

kazi katika utumishi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano, yaani:

(a) iwapo kuna mtu mwenye madaraka ya kazi aliyokabidhiwa kwa

mujibu wa masharti ya Katiba hii na mtu huyo yupo likizo na

wakati huo huo anangojea kuacha kazi hiyo, basi anaweza

kuteuliwa mtu mwingine na kukabidhiwa madaraka ya kazi

hiyo, bila ya kujali kuwapo kwa yule mtu anayengojea kuacha

kazi hiyo;

(b) iwapo kuna watu wawili au zaidi ambao kwa wakati mmoja

wote wanashika madaraka ya kazi fulani kutokana na uteuzi

wao uliofanywa kwa mujibu wa Kanuni iliyoelezwa katika aya

ya (a) ya Ibara hii ndogo, basi katika hali hiyo kukitokea haja ya

kutekeleza shughuli yoyote inayohusika na madaraka ya kazi

hiyo yule mtu wa mwisho kuteuliwa ndiye atakayehesabiwa

kuwa mtu pekee mwenye dhamana ya kazi hiyo; na

(c) iwapo mtu ameteuliwa, kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii,

kuwa kaimu au kushikilia madaraka ya kazi fulani wakati mtu


93

maalum aliyeteuliwa kushika madaraka ya kazi hiyo

anashindwa kutekeleza shughuli zinazohusika na kazi hiyo, basi

haitaruhusiwa kufanya uchunguzi wowote au kutoa hoja yoyote

juu ya uteuzi wa huyo kaimu kwa sababu mtu huyo maalum

aliyeteuliwa kushika madaraka ya kazi hiyo ameshindwa

kutelekeza shughuli zinazohusika na kazi hiyo.

Ufafanuzi

238.-(1) Katika Katiba hii, isipokuwa kama itaelezwa vinginevyo:

“amri ya Jeshi” maana yake ni sheria au amri iliyotolewa kwa mujibu wa

sheria, ya kusimamia nidhamu katika jeshi;

“askari” likitumika kuhusiana na jeshi lolote, maana yake ni pamoja na

askari yeyote ambaye kwa mujibu wa amri ya jeshi hilo ni mtu

anayewajibika kinidhamu;

“Bunge” maana yake ni Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

lililoanzishwa katika Ibara ya 105;

“Chama cha Siasa” maana yake ni chama cha Siasa kilichoandikishwa kwa

mujibu wa sheria za nchi;

“Jamhuri ya Muungano” maana yake ni Jamhuri ya Muungano wa

Tanzania;

“Jaji Mkuu” maana yake ni Jaji Mkuu wa Mahakama ya Jamhuri ya

Muungano wa Tanzania aliyeteuliwa katika Ibara ndogo ya 151

ambaye inajumuisha Kaimu Jaji Mkuu;

“Jeshi” maana yake ni lolote kati ya majeshi ya ulinzi na ni pamoja na jeshi

lolote jingine lililoundwa na Katiba hii au kwa mujibu wa sheria na

linalotawaliwa kwa amri ya jeshi;

“Jumuiya ya Madola”maana yake ni jumuiya ambayo wanachama wake ni

Jamhuri ya Muungano na kila nchi ambayo inahusika na masharti ya

Sheria ya Uraia;

“madaraka ya kazi katika utumishi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano"

maana yake itabidi ifahamike kwa mujibu wa maana ya kawaida ya

maneno hayo na ni pamoja na utumishi katika Majeshi ya Ulinzi ya

Jamhuri ya Muungano na katika Jeshi la Polisi au jeshi linginelo

lililoundwa kwa mujibu wa Sheria;

“mahakama” maana yake ni mahakama yoyote yenye mamlaka katika

Jamhuri ya Muungano isipokuwa mahakama iliyoundwa kwa amri ya

jeshi;

“Mwanasheria Mkuu” maaana yake ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya

Jamhuri ya Muungano aliyeteuliwa chini ya masharti ya Ibara ya 97;

“Raia” maana yake Raia wa Jamhuri ya Muungano kwa mujibu wa masharti

ya Katiba hii na sheria za nchi;

“Serikali” maana yake ni Serikali ya Jamhuri ya Muungano na mtu yeyote

anayetekeleza madaraka au mamlaka yoyote kwa niaba ya Serikali;

“Tanzania Bara” maana yake ni eneo lote la Jamhuri ya Muungano ambalo

zamani lilikuwa eneo la Jamhuri ya Tanganyika;

“Zanzibar” maana yake ni eneo lote la Jamhuri ya Muungano ambalo zamani

lilikuwa eneo la Jamhuri ya Watu wa Zanzibar;

“Uchaguzi Mkuu” maana yake ni uchaguzi wa Rais na uchaguzi wa

Wabunge wanaowakilisha majimbo ya uchaguzi unaofanywa baada

ya Bunge kumaliza muda wake;


94

“Waziri” maana yake ni mtu aliyekabidhiwa madaraka ya kazi ya Waziri,

isipokuwa Naibu Waziri;

(2) Kanuni zifuatazo zitatumika kwa madhumuni ya ufafanuzi wa

masharti ya Katiba, yaani -

(a)kila yanapotajwa madaraka ya Rais, ifahamike kuwa madaraka

yanayohusika ni pamoja na mamlaka ya kutekeleza shughuli za kazi

mbalimbali na vile vile wajibu wa kutekeleza shughuli na kazi mbali

mbali kama Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano, na pia

mamlaka mengine kama hayo au wajibu mwingine kama huo ikiwa

imeelezwa katika Katiba hii au katika sheria nyingine yoyote

kwamba mamlaka hayo mengine ni ya Rais au kwamba wajibu huo

mwingine ni wa Rais;

(b)kila yanapotajwa madaraka ya kazi katika utumishi wa Serikali,

ifahamike kuwa kazi inayohusika ni kazi katika Utumishi wa

Serikali ya Jamhuri ya Mungano isipokuwa kama imeelezwa

vingine, na kila inapotajwa Idara ya Serikali ifahamike kuwa idara

inayohusika ni idara ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano,

isipokuwa kama imeelezwa vingine;

(c)iwapo kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii kuna jambo lolote

linalotakiwa litekelezwe au lishughulikiwe na chama chochote cha

siasa, basi, jambo hilo litatekelezwa au litashughulikiwa na chama

hicho kwa mujibu wa utaratibu uliowekwa na chama hicho kwa ajili

hiyo, na pia kwa kuzingatia masharti ya Katiba hii au Sheria yoyote

iliyotungwa na Bunge kwa ajili hiyo;

(d)kwa madhumuni ya Katiba hii, mtu hatahesabiwa kuwa ana

madaraka ya kazi katika utumishi wa Serikali ya Jamhuri ya

Muungano kwa sababu tu kwamba anapokea malipo ya uzeeni au

malipo mengine ya aina hiyo kwa ajili ya utumishi wake wa zamani

katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano au katika Jeshi la Ulinzi au

la Polisi la Serikali ya Jamhuri ya Muungano au Serikali ya zamani

ya Zanzibar;

(e)katika Katiba hii, isipokuwa kama maelezo yahitaji vingine, kila

anapotajwa mtu mwenye dhamana ya kazi kwa kutaja madaraka ya

kazi yake, ifahamike kuwa mtu anayehusika ni pamoja na mtu

yeyote ambaye ni Kaimu au aliyeteuliwa kihalali kushikilia

dhamana ya kazi hiyo;

(f) katika Katiba hii, kila yalipotajwa mamlaka ya kumwondoa mtu

katika madaraka ya kazi katika utumishi wa Serikali ya Jamhuri ya

Muungano, ifahamike kuwa mamlaka yanayohusika ni pamoja na

mamlaka yaliyotolewa kwa mujibu wa masharti ya Sheria yoyote

yanayomtaka mtu huyo au yanayomruhusu mtu huyo kustaafu:

Isipokuwa kwamba maelezo ya Kanuni hii yasifahamike kuwa

yanampa mtu yeyote mamlaka ya kumtaka Jaji wa Mahakama au

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu astaafu; na

(g)katika Katiba hii, kila ilipotajwa sheria ambayo inabadilisha au

kufuta sheria nyingine, ifahamike kuwa sheria inayohusika ni

pamoja na sheria ambayo inarekebisha sheria hiyo nyingine au

ambayo inaendeleza kutumika kwa hiyo sheria nyingine, ama bila

mabadiliko au baada ya kubadilishwa au kurekebishwa; au sheria


95

________________

NYONGEZA

[Imetajwa katika Ibara ya 60]

Mambo ya Muungano

________________


1. Katiba na mamlaka ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania;

2. Ulinzi na Usalama wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania;

3. Uraia na Uhamiaji;

4. Sarafu na Benki Kuu;

5. Mambo ya Nje;

6. Usajili wa Vyama vya Siasa; na

7. Ushuru wa bidhaa na mapato yasiyo ya kodi yatokanayo na

mambo ya Muungano.

ambayo inaweka masharti mapya katika sheria nyingine.

Jina la

Katiba na

kuanza

kutumika.


239

.-(1) Jina kamili la Katiba hii ni Katiba ya Jamhuri ya Muungano

wa Tanzania ya mwaka 2013.

(2) Katiba hii itaanza kutumika mara baada ya kuzinduliwa Rasmi

na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kufutwa

kwa Katiba

ya Jamhuri

ya

Muungano

ya mwaka

1977.


240.

Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya mwaka 1977 inafutwa na

itaacha kutumika mara baada ya kuanza kutumika kwa Katiba hii.
Share this article :

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA