Home » » MWANDISHI ESTHER MACHA AICHAMBUA KAULI YA WAZIRI PINDA KUHUSU POLISI KUPIGA RAIA

MWANDISHI ESTHER MACHA AICHAMBUA KAULI YA WAZIRI PINDA KUHUSU POLISI KUPIGA RAIA

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Wednesday, June 26, 2013 | 10:44 AM


Na Esther Macha
KAULI ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda imeonekana kuwa mwiba kwa wananchi kwani ni kitu ambacho hakikutegemewa kutamkwa na kiongozi mkubwa kama huyo badala yake walitegemea kupata ushauri ambao utarejesha amani zaidi.

Lakini pia kauli hii inaweza kuwa silaha kwa polisi kuamua kupiga wananchi watakavyo ili mradi tu kutimiza kauli hii ambayo si nzuri kwa matamshi .

Binafsi suala hili linanipa shida na kubaki kujiuliza iweje vyombo vya dola vipewe meno kiasi hiki na kiongozi huyu  na je hakuna njia nyingine ya kutumia zaidi ya  kupiga.

Siku zote polisi wamekuwa wakifanya uonevu kwa wananchi na sasa wamepewa lungu na Pinda kuwa wapige tu kwa madai wamechoka,kwa kauli hii hali inaweza kuwa mbaya kwa siku za usoni.

Kinachoangaliwa hapa ni amani kwa watanzania kama viongozi wa Taifa hili wakae na kuangalia nini  kifanyike ili kurejesha hali ya usalama iliyokuwepo zamani lakini si kutumia mabavu .

Hali iliyopo hivi sasa hakuna anayeipenda wala kuifurahia kwani imefanya wananchi waishi kama wakimbizi katika maeneo yao kutokana na vurugu za watui wachache zilizopo katika maeneo mbali mbali nchini.

Nadhani kama Waziri Mkuu atafute njia mbadala ambayo itaweza  kuleta suluhu ya matatizo haya yaliyopo kuliko kutumia kauli hii ,ambayo imekuwa kama nyoka kwa wananchi.

Nionavyo  katika hili  ni Pinda  kuona kuwa akitumia  kauli hiyo ya kuwataka polisi kupiga tu labda ingekuwa jibu  zuri kwake  kumbe imeleta picha tofauti machoni mwa watanzania wanaomtegemea kama kiongozi wao.

 Pia ifike wakati kwa viongozi wakubwa wanapotaka kutoa maamuzi makubwa kama  haya kukaa na kutulia  na kutafakari kwa kina wakati wa kutaka kulitoa hadharani  jambo hilo, kwani hali inakuja kujitokeza kutokana na kutumia hasira zaidi.

Kauli hii ni  hatari sana kwa musatakabalai wa nchi yetu, hasa Waziri Mkuu wa nchi anapotangaza bungeni na kuhamasisha uvunjifu wa sheria na amani inanikumbusha wakati ule aliposema washukiwa wa mauaji ya albino nao wapigwe risasi na kuuliwa papohapo.

Ninachoamini ni kwamba mtu yeyote anapofanya kosa ni vema afikishwe mahakamani  kwanza lakini si kuwaua wananchi   bila kufikishwa mahakamani ,hili kama waziri mkuu lazima alione  na kulifikiri kwa kina zaidi.
Ninachotaka kusema hapa ni kuwa kauli hii ya kiongozi wetu inaweza kuwa mwiba bila yeye kujua matokea mabaya yatakayokuwepo kwa siku za usoni.

Akizungumza katika Kipindi cha Maswali ya Papo kwa Hapo kwa Waziri Mkuu, bungeni Dodoma jana, Pinda alisema watu wanapokaidi wanajitakia matatizo na vyombo vya dola.

Pinda alitoa kauli hiyo juzi wakati alipokuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Kilwa Kaskazini (CCM), Murtaza Mangungu aliyeuliza: “Serikali ipo tayari kiasi gani kubainisha na kuchukua hatua stahiki, badala ya kusakama makundi fulani, tujue chanzo halisi cha vurugu hizi na matatizo haya na jinsi gani vyombo vya dola vinavyoshughulikia kwa sababu yapo malalamiko katika baadhi ya maeneo kama Mtwara kwamba wananchi wanapigwa na vyombo vya dola?”

Nionavyo  kuhusu kauli hii binafsi sikubaliani nayo kwani endapo wananchi nao wakiamua amani  kulipiza kisasi nchi hii itakalika na kutawalika  inapaswa kutumia busara katika jambo hili kusiwepo na machafuko.

Hapa ninachokiona ni kuwa Pinda  amesemea jambo hili kwa hasira bila kufikiria  madhara yake yatakuwa vipi kwani wananchi nao wakiamua kuzipigana  na polisi itakuwaje?hapo kuna  umuhimu wa kukaa  na kujiuliza athari za badae kuliko kutekeleza kauli hii.

Si  kwamba napingana na kiongozi huyu lakini ninachotaka kusema ni kuwa kama kweli alihitaji kutoa kauli hii asingetamka hadharani  badala yake angewanong'oneza askari kuliko kuliweka hadharani na TBC inamrusha live.

Ninachojiuliza je raia wakijikusanya kwa pamoja   nguvu yao inazidi hata kwa risasi hivyo hapa itumike busara tu katika kuleta amani kwa watanzania.

Ushauri wangu kwa kiongozi wetu ni afute tu kauli kwani hapo ikitokea vurugu kwa wananchi na polisi itakuwa vita kubwa kutokana na polisai kupewa men ohayo makali na wao kutekeleza lile waliloambiwa   la kupiga tu.

 Lakini pia kwa hadhi  panda hakupaswa kutoa kauli ya kuchoma kiasi hicho kama kiongozi mkubwa wan chi  bali ili ilipaswa kuchuja jambo hilo madhara yake na jamii itapokea vipi kauli hiyo.

Nianavyo katika hili  hii inaonesha ni jinsi gani tunaserikali dhaifu ambayo watu wanaweza kusema chochote na wao kusubiri mpaka yatokee waanze kufanya maamuzi Wataalamu wa Saikolojia na rasilimali watu wanashauri usifanye maamuzi ukiwa umekasirika au una furaha hiyo ndiyo matokeo yake.

Kilichotakiwa kufanyika hapo ni kukaa  na  viongozi wa vyama vyote kuhakikisha nchi inaendeshwa kwa amani. Lakini si kwa kauli hii ambayo imetolewa hadharani bila kujua atahari yake.

Jambo hili lilotamkwa na Kiongozi si zuri bali linapaswa kufanyiwa kazi kwa pamoja wakiwashirikisha viongozi  wote wa vyama vya siasa kujua kina cha tatizo na kufikia mwafaka mzuri ambao utarejesha amani ya  nchi ambayo  imeanza kupotea.

Kwa namna nyingine viongozi wengine wanaweza kufikiri ni jambo la mzaha lakini ni kitu ambacho ni kikubwa  kinachotakiwa kufanyiwa kazi haraka ili madhara yasiweze kutokea.

Namshauri Pinda ambaye anapingana na Sera nzuri za Said Mwema za Utii bila shuruti ambazo zilianza kuibadili nchi  Vitisho, vipigo, matusi haviwezi kuwajenga watu zaidi sana vinawapa usugu, mwisho wa siku wanaweza kuzoea kupigwa na kuwa tayari kufa hata kama watakufa ili mradi tu wapate haki yao. mfano mzuri ni kule Brazil na nchi nyingine.
Mwisho.
Share this article :

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA