Home » » KIJANA ANUSURIKA KUUWAWA KWA KICHAPO BAADA YA KUKUTWA AKIBAKA MTOTO WA MIAKA 10 ENEO LA MWANGATA

KIJANA ANUSURIKA KUUWAWA KWA KICHAPO BAADA YA KUKUTWA AKIBAKA MTOTO WA MIAKA 10 ENEO LA MWANGATA

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Tuesday, June 4, 2013 | 6:07 AMWananchi  wakitembeza  kichapo kwa mbakaji  huyo mjini Iringa leo 
Mbakaji  akivuja  damu baada ya kupasuliwa na mawe kichwani 
Mtuhumiwa wa ubakaji akipelekwa  polisi  leo 
Huyu  ndie mtoto  aliyebakwa na jemba hilo 

mwananchi  mwenye hasira  kali akimwadhibu kwa ngumi mtuhumiwa wa ubakaji wa mtoto mjini Iringa mchana  huu.
......................................................................................................................................................

WAKATI  mkoa  wa Iringa ukiwa ni mkoa  wa pili kwa maambukizi ya virusi vya UKIMWI ukiwa nyuma ya mkoa wa Njombe ambao  ndio unaongoza huku  vitendo vya ubakaji na mapenzi yasiyo salama vikitajwa ni  sababu ,Jemba mmoja  mkazi  wa Mwangata katika Manispaa ya  Iringa amenusurika  kuuwawa na  wananchi  wenye hasira kali baada ya  kubambwa akibaka  kitoto  cha miaka 10 mchana kweupe.

Mashuhuda  wa tukio  hilo  wameueleza mtandao huu  wa www.matukiodaima.com na  www.francisgodwin.blogspot.com kuwa  tukio hilo  limetokea  mida ya saa8 mchana baada ya  mama mazazi wa binti  huyo kusikia  mtoto  wake akilia kwa uchungu kuomba msaada  zaidi kwa wananchi baada ya kukamatwa kwa nguvu na kijana  huyo mbakaji

Mama mzazi wa mtoto  huyo ambae Jina lake na la  mtoto  wake kwa  sasa yamehifadhiwa na mtandao huu  kutokana na  sababu  za kimaadili ,alisema  kuwa  wakati  tukio  hilo  likitokea  yeye alikuwa akiendelea na shughuli  zake nyumbani na kusikia sauti ya mtoto  wake akilia kwa uchungu kulalamika  kubakwa .

Hata  hivyo  alisema baada ya  kutoka nje na  kuelekea  eneo hilo ambalo  sauti ilisikika alishuhudia kijana  huyo akiendelea  kumbaka mtoto  wake  jambo  lilopelekea  kupiga  kelele  kuomba msaada kwa wananchi ili  kusaidia  kumkamata mtuhumiwa huyo  wa ubakaji.

Mwanamke huyo  alisema  kuwa jitihada za  wananchi  wa  eneo hilo la Mwangata  kumkamata  mtuhumiwa ziliweza kufanikiwa pamoja na mtuhumiwa huyo kutaka kujaribu kukimbia eneo hilo.

Mmoja kati ya  wananchi  walioshiriki kumkamata  kijana  huyo mbakaji  aliyejitambulisha kwa jina la Samweli kalinga alisema  kuwa  kijana  huyo  amekuwa na tabia ya kuwabaka  watoto  katika eneo hilo la Mwangata na mara  nyingi  watoto  wamekuwa  wakibakwa  ila  walikuwa hawajui ni nani anayeendesha  vitendo hivyo vya ubakaji .

Hivyo  alisema kukamatwa  kwa mtuhumiwa huyo wa ubakaji  kulepelekea wananchi  wenye hasira kali  kuanza kumwadhibu kwa kichapo na hata  kutaka  kumchoma moto kabla ya baadhi ya  wananchi kutumia busura na kutaka  afikishwe kituo cha  polisi.


Mtuhumiwa  huyo amefikishwa katika kituo  kikuu cha polisi mjini Iringa huku akiwa hoi kwa kichapo na kupelekea  kuvuja damu kupita  kiasi kichwani  kutokana na kichapo alichokipata  kutoka kwa wananchi.
Share this article :

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA