Home » »

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Thursday, May 16, 2013 | 5:23 AM

MAHAKAMA IRINGA YAMGEUKA RPC KAMUHANDA .....................

  kaimu msajili  wa  mahakama kuu Tanzania kanda ya Iringa Godfrey Isaya  akizungunza na  wanahabari leo
 Baadhi ya mahakimu  na  watumishi  wa mahakama  wakimsikiliza kaimu msajili  huyo
 
 Wanahabari  wakimsikiliza kaimu msajili wa mahakama kuu  Tanzania kanda ya Iringa
  kaimu msajili  wa  mahakama kuu Tanzania kanda ya Iringa Godfrey Isaya  akionyesha chumba cha vielelezo ambacho kipo  salama  kabisa
 Hapa  ndipo bangi  hiyo  ilipoteketezwa 
 
 
 
 Dirisha la chumba  hicho  cha  vielelezo mahakamani  likiwa  salama kabisa
..................................................................................................
 
 
 
MAHAKAMA kuu ya Tanzania kanda ya Iringa  imepinga  vikali taarifa  ya  jeshi la polisi mkoa  wa Iringa (RPC) Michael Kamuhanda  aliyoitoa jana kwa vyombo vya habari  kuwa inamshikilia mtumishi  wa mahakama hiyo kwa kuiba bangi iliyofikishwa mahakamani hapo kama kielelezo.
 
"Taarifa  ya kamanda  wa  polisi kuwa bangi  imeibiwa mahakamani si  ya kweli na imelenga  kuichafua mahakama  hiyo na kuwa  wao kama mahakama   hawajapata  kuibiwa na kuwa taarifa  hizo si za kweli kabisa".
 
Akizungumza na  wanahabari  leo ofisini kwake kaimu msajili  wa  mahakama kuu Tanzania kanda ya Iringa Godfrey Isaya alisema  kuwa  wao kama mahakama  wanasikitishwa taarifa  hiyo ya  kuibiwa kwa  vielelezo  iliyotolewa na jeshi la polisi  kuwa haina ukweli  wowote .
 
Isaya  alisema  kuwa jeshi la polisi limepotosha umma kwa kutoa taarifa  ya uogo bila kufanya uchunguzi na  kuwa kama ni kuibiwa  vielelezo ilipaswa  kuwepo kwa mlalamikaji ambaye ni Mahakama kwenda kufungua kesi polisi na si vinginevyo.
 
" Tunakanusha  vikali kuwepo kwa  upotevu  wa kielelezo cha bangi katika mahakama  hii Exhitibit Room haijavunjwa iko intact .....tulikuwa na kielelezo P.3 katika shauri  hilo la jinai namba 24/2012 ambayo ni bangi  viroba 8 amri ya mahakama ya kuteketeza ilitolewa tarehe 13/2/2013 na bangi  hiyo iliteketezwa chini ya uangalizi  wa afisa wa  jeshi la polisi na kesi hiyo  ilikwisha tarehe 13 /2/2013 na mshtakiwa alihukumiwa kifungo cha miaka miwili  jela"
 
Alisema kama ilivyokuwa katika kesi nyingine za jinai tunatoa wito kwa  jeshi la polisi  Iringa kufanya uchunguzi wa kina kuona bangi hiyo imepatikana  wapi kwani  sisi kama mahakama hatujapata kuibiwa bangi katika mazingira  yoyote na kama tukio hili lingekuwepo basi taarifa   polisi zingeripotiwa .
Pia  alisema kama kweli mahakama kuna vielelezo  vilivyoibwa basi polisi  wangefika kufanya upelelezi hata  kuwahoji kama njia ya kuchunguzi .
 
" Tunalishauri jeshi la polisi kufanya utafiti  wa  kina kuhusu  suala hili kabla ya kutoa taarifa katika vyombo vya habari "
 
hatua ya mahakama hiyo kupinga taarifa ya jeshi la polisi mkoa  wa Iringa imekuja siku  moja baada ya  jeshi  hilo kutoa taarifa kwa vyombo vya habari  kuwa  linamshikiria mtumishi wa Mahakama ya Wilaya ya Iringa kwa tuhuma za kuiba vielelezo vya madawa ya kulevya aina ya bangi.

Kwa mujibu  wa kamanda  wa  polisi mkoa  wa Iringa Bw Kamuhanda alisema tukio hilo limefanyika tarehe 14  ambapo mtuhumiwa huyo wa mahakama  Lwitiko Lusekelo Minga ambaye ni mlinzi wa Mahakama ya Wilaya ya Iringa, aliiba bangi yenye uzito wa kg 371.2
“Tukio la kupatikana kwa bangi, eneo la Flerimo mtuhumiwa Juma Nzowa alikamatwa na bangi na baada ya kuhojiwa mtuhumiwa alimtaja Lwitiko Lusekelo Minga Mlinzi wa Mahakama kuwa ndiye aliyemuuzia kielelezo hicho cha mahakama,” Alisema Kamuhanda.
Pia amesema kielelezo hicho awali kilikamatwa Wilaya ya Kilolo na kufikishwa mahakamani kama ushahidi na ndipo ilipoibiwa tena.
Amesema kutokana na uwepo wa watumishi wasio waaminifu kumekuwa na tabia hiyo hasa kwa madawa hayo ya kulevya, vielelezo vyake na kurudi tena mitaani huku wao wakiendelea na zoezi la kukamata.
Hata hivyo kumekuwa na malalamiko mbalimbali juu ya vielelezo hivyo kuibiwa pindi vifikapo Mahakamani, hasa kwa vidhibiti hivyo vya madawa ya kulevya na  vipodozi mbalimbali ambapo huuzwa katika maduka na wananchi kuendelea kutumia.
Aidha vielelezo kama vyombo vya thamani navyo vimesemekana mara nyingi hupotelea Mahakamani na hata katika vituo vya Polisi.
Share this article :

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA