Home » » HUYU NDIE SISTER ' FEKI' RAIA WA KENYA ALIYEKAMATWA KWA UTAPELI IRINGA

HUYU NDIE SISTER ' FEKI' RAIA WA KENYA ALIYEKAMATWA KWA UTAPELI IRINGA

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Thursday, May 16, 2013 | 5:22 AM


 Mwanamke - anayejiita Sister Phylis Wanjiru Kamau, raia wa Kitui nchini Kenya akiwa ofisi za kamanda wa jeshi la Polisi mkoa wa Iringa, baada ya kukamatwa.
Taarifa za kipolisi, za kukamatwa kwa Sister Feki Phylis Wanjiru Kamau.
.....................................................................................

 
MAANDIKO matatatifu ya  kibiblia  yanasema  kuwa siku za mwisho yatatokea mambo mengi ya  kushangaza  dunia ,kamwe kama dalili  za siku  za mwisho basi naweza  kusema ndizo hizi kwani kila kukicha ni mambo mapya ya kushangaza .
 
Wakati Taifa  likiwa katika maswali yasiyo na majibu  juu ya  tukio la bomu kuua Kanisani mkoani Arusha ,mkoani Iringa  mwanamke mmoja anayetambulika kwa Phylis Wanjiru ( 44)raia wa Kitui nchini Kenya amekamatwa akitaka  kuwatapeli Masister wenzake .
 
Mwanamke  huyo akiwa amevalia ya kitawa mfano wa  masister wa kanisa Kathoriki alikamatwa na kufanyiwa upekuzi na kukutwa na baadhi ya vielelezo vilivyothibitisha  utapeli  wake  huo .
 


Wanjiru ambaye ni raia wa nchi ya Kenya amekamatwa na jeshi la polisi baada ya masister wenzie kubaini kama si mmoja wao, kutokana na kushindwa kufanya baadhi ya masuala  ambayo ni msingi wa utawa wao.

Taarifa  kutoka ndani ya jeshi la polisi mkoa wa Iringa zinaeleza  kuwa  mwanamke huyo kabila lake ni Muwembu wa nchini Kenya amekamatwa katika nyumba  za masista zilizopo Ipogolo mjini Iringa.
 
Hata  hivyo  mwanamke huyo ambaye awali aligoma kutoa maelezo ya kina juu ya ujio wake nchini Tanzania, katika upekuzi walimkuta na baadhi ya chip (Line) za makampuni mbalimbali ya simu ya ndani na nje ya nchi.

 Sister huyo feki alikutwa pia akiwa na hati za kusafiria (Passport) mbili, moja ikiwa niya Africa Mashariki yenye namba Ke. 020659 huku hati ya nyingine ikiwa na jumuiya ya Kenya namba A. 1790366.
 
Amesema Sister huyo feki katika hati hizo ilionyesha kuwa alitembelea nchi ya Rwanda, Uganda pamoja na nchini Tanzania ambapo siku za hivi karibuni alikuwa Mkoani Mara Tarime.
Sister huyo amekuwa akitumia mbinu ya kujiangusha kama mtu mwenye ugonjwa wa kifafa pindi anapofanyiwa mahojiano, jambo linalowawia vigumu jeshi hilo kupata maelezo ya kina dhidi ya dhamira yake ya kuingia humu nchini.
Share this article :

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA