Home » » HAKUNA KANISA LILIPULIWA KWA BOMU DAR LEO - KAMANDA KOVA

HAKUNA KANISA LILIPULIWA KWA BOMU DAR LEO - KAMANDA KOVA

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Saturday, May 11, 2013 | 6:09 AMJeshi la polisi kanda maalum ya Dar es Salaam limetolea ufafanuzi juu ya taarifa zilizoripotiwa na mitandao ya kijamii ukiwemo mtandao huu juu ya kuwepo kwa mlipuko katika kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Kunduchi jijini Dar es Salaam .

kamanda wa polisi wa kanda maalum Suleiman Kova ameueleza mtandao huu wa www.matukiodaima.com kuwa hakuna tukio la kanisa kulipuliwa ila kkilichotokea ni polisi kurusha bomu la machozi wakati wakipambana na waharifu katika kichaka kimoja eneo la jirani na kanisa hilo.

Kamanda Kova alisema kuwa polisi walikuwa katika harakati zao za kutafuta genge la waharifu waliokuwa karibu na kanisa hilo na kurusha bomu la machozi hivyo wananchi kuhisi kama kuna mlipuko kanisani
Share this article :

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA