Home » » SHIRIKISHO LA GRANDMALT LAWACHEFUA WANACHUO KIKUU MKWAWA, WAPANGA KUJITOA

SHIRIKISHO LA GRANDMALT LAWACHEFUA WANACHUO KIKUU MKWAWA, WAPANGA KUJITOA

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Friday, April 19, 2013 | 2:14 AM

===============================================
Na Gustav Chahe
 
WANAFUNZI wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Mkwawa wamepanga kujitoa katika mchezo wa shirikisho la mpira wa miguu ulioandaliwa na kudhaminiwa na kampuni ya vinywaji Grandmalt.
Akizungumza na mtandao huu kwa njia ya simu leo, Waziri wa michezo katika serikali ya wanafunzi wa chuo hicho Mlipano Henry alisema wila wamepanga kujitoa katika shirikisho hilo endapo madai yao hayatasikilizwa na kutimizwa.
Amesema katika michuano iliyofanyika mwaka jana walishiriki kwa mateso na kuahidiwa kutimiziwa kila kitu mwishgoni kwa michuano jambo waliloachwa njiapanda na kampuni hiyo pasipo maelezo ya kueleweka.
“Kwanza nasikitika sana kuona tunatumiwa kama watoto na kampuni inayofanya biashara. Sisi ni watu wazima ambao tunajua kuwa tunadanganywa. Mwaka jana kamapuni hii ilikuja kutuomba kushirikia katika michuano hiyo bila kutupatia vifaa vya michezo na kutuomba tutumie nguvu zeti ili mwishoni tupate kila kitu pamoja na kurudisha gharama tulizotumia lakini baada ya michuano kuisha wakaona walichokuwa wanatafuta wamekipata wakatuacha njiapanda wakisema hawana kitu” amesema Waziri Mlipano.
Amesema waliahidiwa na kampuni hiyo kuwa kila timu inayoshiriki itapewa jezi na mipira mitano mitano pamoja na gharama zingine zilizotumika jambo ambalo hailikufanyika hadi leo.
“Nashangaa tena mwaka huu wamekuja kwa njia ile ile wakitutaka tushiriki bila kutimiza ahadi za nyuma hata kukumbishia tu. Pia waliahidi kuwa watakuja kupanda miti katika chuo chetu kama sehemu ya utunzaji mazingira lakini hilo lilisahaulika siku ile ile walipokuwa wakiahidi” amesema.
Hata hivyo amesema baada ya kufanya nao mawasiliano na kuona hakuna kinachoendelea, waliomba kupewa katoni 28 za vinywaji ili waweze kuuza na kununua vifaa walivyoahidiwa lakini baada ya kuzungusha kwa muda mrefu waliambulia kupewa katoni 5 tu ambazo haziwezi hata kukunua mpira.
“Sisi tunaamini kuwa ile ni kampuni inayofanya biashara lakini kinachoonekana hapa wanataka kututumia sisi kufanya biashara zao na mwishowe kutuacha kama wajinga fulani. Sisi tunasema kuwa, kama ahadi za nyuma na madai yetu hatujatimiziwa hatuwezi kuingia mkenge kama walivyotutumia mwaka jana. Haya siyo maamuzi yangu bali ni ya wachezaji wenyewe” amesema.
Kwamba “hata kwa wale wasiolielewa hili tunataka wajue ili wasije wakaingia mkenge kama sisi tulivyo fanya mwaka jana” amesema.
Alipotafutwa kwa njia ya simu kutolea maelezo juu ya jambo hilo, meneja wa kampuni ya Grandmalt na mwandaaji wa mashindano hayo katika Mkoa wa Iringa Protas Singu amesema yeye hakujua kama kuliwa na ahadi hizo ambazo wanachuo wanadai na kuahidi kukaa nao mezani ili kumaliza tatizo.
“Nimepata malalamiko hayo lakini kiukweli mimi binafsi sijui na kama yasengekuwa mashindano haya, nisingejua kitu. Hivyo, nakuahidi kukupa mrejesho mara baada ya kukaa mezani na kuyamaliza” amesema Singu.
Alipotakiwa kutolea maelezo juu ya wanafunzi hao kutangaza kujitoa na huku ikiwa imebaki siku moja tu ili mashindano yaanze, Singu alisema kila jambo linazungumzika na kufikia mwafaka.
“Nisingependa tufikie hapo. Tunaingia mezani ili tulijadili kwa pamoja na kushughulikia madai yote. Nina imani kuwa tutafikia makubliano na hatimaye watashiriki” amesema.
Shirikisho hilo linatarajiwa kuanza kutimua vumbi katika viwanja vya chuo kikuu cha Mkwawa jumapili ya Aprili 20 mwaka huu iwapo mwaka jana ilifanyika katika viwanja vya Chuo Kikuu Kishiriki cha Tumaini.
Share this article :

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA