Home » » PAROKO WA RC IFUNDA APOTEZA MAISHA KATIKA AJALI AKITOKA MSIBANI NJOMBE

PAROKO WA RC IFUNDA APOTEZA MAISHA KATIKA AJALI AKITOKA MSIBANI NJOMBE

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Saturday, April 27, 2013 | 12:30 PM                Hili ndilo gari ambalo  limesababisha  kifo cha paroko ( picha na Gogers Stivin Mselu wa FG Blogu Mafinga)
             ............
PAROKO  wa kanisa la RC parokia ya Ifunda Alphonce Mhamilawa amefariki  dunia katika ajali mbaya ya gari  iliyotokea katika eneo la Saba  saba Mafinga wilaya ya Mufindi mkoani Iringa.

Mashuhuda  wa  ajali  hiyo wameueleza mtandao  huu  wa  www.francisgodwin.blogspot.com  kuwa ajali  hiyo ilitokea  majira ya saa 2 usiku  wa  kuamkia  leo wakati paroko  huyu akitoka mkoani Njombe katika  shughuli  ya Mazishi

Mmoja kati ya mashuhuda  hao Bw  Saugo Ndemo  alisema  kuwa paroko  huyo alikuwa akiendesha gari dogo Paina ya Toyota  Hilux (Pick Up) yenye  namba  za usajili  T434 APP mali ya Kanisa la Roman Katoliki Parokia ya Ifunda.

Ndemo  alisema  kuwa chanzo  cha ajali  hiyo ni Paroko  kuligonga gari aina ya Lori  kwa  nyuma na kuwa lori  hilo halikuweza  kusimama .

Alisema  kuwa  paroko  huyo alifia eneo la tukio baada ya  ajali  hiyo  iliyopelekea  kichwa  chake  kupasuka .

Mmoja kati ya askari  wa usalama barabarani ambae hakutaka  kutaja jina lake kwa  kuwa si msemaji  mkuu  wa  jeshi la  polisi alisema  kuwa  chanzo cha ajali  hiyo ni mwendo kasi.

Pia alisema   kuwa lori ambalo  paroko  huyo aliligonga  linasadikika  kuwa lilibeba mbao huku  likivutana na  lori  jingine na baada ya ajali  hiyo halikuweza  kusimama .
....................................

Picha  za ajali  hii mbaya  zitakujia hivi punde hapa
HABARI  HII KWA  UDHAMINI MKUBWA  WA  KITUO CHA MAFUTA CHA HOPE SERVICE STATION HAPA HUDUMA NI MASAA 24


Wengi hukimbilia kununua mafuta hapa HOPE SERVICE STATION eneo la CRDB barabara ya Iringa -Dodoma katikati ya mji wa Iringa kituo kinachouza mafuta masaa 24 ,wewe wasumbuka na nini jiunge na kituo cha wengi sasa .

KITUO CHA MAFUTA CHA HOPE SERVIRCE NI MABINGWA WA UUZAJI WA MAFUTA MKOANI IRINGAKARIBU UJAZE MAFUTA KWENYE GARI YAKO HAPA HOPE SERVICE STATION TUPO JIRANI NA BENKI YA CRDB MIYOMBONI BARABARA YA IRINGA DODOMA
Share this article :

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA