Home » » NHIF YASAIDIA HUDUMA YA MADAKTARI BINGWASOKOINE HOSP LINDI TAREHE HADI 13 APR MNAKARIBISHWA

NHIF YASAIDIA HUDUMA YA MADAKTARI BINGWASOKOINE HOSP LINDI TAREHE HADI 13 APR MNAKARIBISHWA

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Thursday, April 11, 2013 | 4:47 AMMkurugenzi mkuu wa Nhif akitoa taarifa fupi
ya mfuko wa Bima ya Afya kwa Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Lindi kuhusiana na
mpango endelevu wa kuleta madaktari Bingwa 


Mikoani 

Kukabidhi.........Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Lindi Abdallah Ulega
akikabidhi msaada uliotolewa na NHIF kwa hospital ya SokoineBaadhi ya madaktari Bingwa wanaotoa tiba katika Hospital ya
Mkoa wa Lindi kwa Ufadhili wa NHIF
.
.Kaimu mkuu wa mkoa wa Lindi akizindua tiba ya Madaktari
Bingwa toka Muhimbili watakaotoa tiba kwa wateja wa Nhif na wasio
wateja hadi tarehe 13 April
.Baadhi ya wadau waliohudhuria uzinduzi huo
,,Baadhi ya viongozi wakiwasili sokoine
hospital kwa ajili ya uzinduzi wa Tiba kwa madaktari Bingwa

Na Abdulaziz Video,Lindi

Wananchi mbalimbali wa Wilaya zote Za Mkoa wa Lindi leo wameanza
kupata tiba na Uchunguzi toka kwa Madaktari Bingwa wa Kizalendo toka
hospital ya Taifa ya Muhimbili kufuatia ufadhili uliotolewa na Mfuko
wa Taifa wa Bima ya Afya ili kurahisha Huduma ya Matbabu kwa Jamii
Huduma hizo zimeanza kutolewa leo hadi tarehe 13 mwezi huu baada ya
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Lindi,Ambae pia ni Mkuu wa wilaya ya
Kilwa,Abdallah Ulega  kuzindua mpango huo unaotolewa na mfuko wa Taifa
wa Bima ya Afya kwa kuanzia Mikoa yenye Upungufu wa Madaktari Bingwa
kwa kuanzia na Mkoa wa Lindi.
Akizindua mpango huo ni ambao utasaidia kuwapunguzia mzigo Wagojwa
kufuata huduma Kwa madaktari Bingwa  na kuchukua muda mrefu na
mafanikio ya kuonana na kupata huduma stahiki.
Aidha katika Hafla hiyo,Ulega alitoa wito kwa jamii kuunga mkono
jitihada hizo kwa kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii(CHF) Huku
akisisita kuwa serikali itaendelea kuchangia asilimia mia kwa Michango
ya Chf itakayochangwa
‘Ndg zangu wa Lindi huu mfuko ni kwa ajili yenu ili kuwapunguzia
gharama za matibabu kwa Kaya,,,Ukichangia elfu 10 na serikali
inachangia elfu 10 na tumejipanga kuhakikisha huduma zinaboreka na
dawa zinapatika Nawaomba Mchangamkie kuliko malipo ya papo kwa hapo
kila ukiumwa lakini CHF ni mwaka mzima wewe na familia’Alifafanua
Ulega

Kwa Upande wake,Mkurugenzi  mkuu wa Mfuko,Emmauel Humba Akizungumzia
ujio wa madaktarihao alisema utaratibu huu  unaofanywa na madaktari
hao kupitia Wizara ya Afya,Sokoine Hospital na Ofisi yake unawapa
fursa  wananchi wa vijijini na Mjini ili kupata  utaalamu wa kupimwa
kuwaondoshea usumbufu wa maradhi yaliyoficha na hatimaye kupatiwa
tiba.

Alitoa wito kwa wananchi wanapopata taarifa za kufikiwa na madaktari
bingwa wa maradhi mbalimbali, wasipuuze kwenda kufanyiwa uchunguzi,
kwani huenda wakawa wanaishi na maradhi ambayo hayajajitokeza

Nhif imeanza huu utaratibu hasa kwa mikoa ambayo ina upungufu wa
madaktari Bingwa na Tumeanzia Lindi na katika kuunga Jitihada za Mama
Kikwete kuleta vifaa hii imetufurahisha sana kwa kuwa Wateja wa Mfuko
wetu sasa watapata huduma bora na Vipimo,,,Naomba wateja wa Bima na
wasio wateja watumie fursa ya kuonana na Madaktari hawa na wale wale
wa mkoani wafike mawilayani na itakuwa zoezi Endelevu..Alimalizia
Emmanuel Humba,Mkurugenzi mkuu NHIF

Sambamba na kuishukuru Serikali kupitia NHIF,Bi Amina Machenza na
Sheikh Mkuu waMkoa wa Lindi,Sheikh Mohamed Mushangani licha ya
kutambua uwepo wa  uhaba wa madaktari unaozikabili hospitali na vituo
vya afya vilivyoko vijijini, Wameomba huduma za kuletwa kwa Madaktari
Bingwa Ziwe Endelevu kwa jamii nyingi ni za kipato cha chini

Sambamba na Madaktari hao Mfuko huo umekabidhi vifaa mbalimbali  kwa
hospital hiyo vyenye thamani ya Tshs Milion 20 huku Wagonjwa
mbalimbali watakaojitokeza  watapatiwa huduma hizo kwa kupimwa na
kutibiwa maradhi ya macho, pua, kifua, masikio magonjwa ya akinamama
na Watoto ikiwemo Upasuaji
Share this article :

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA