Home » » KINANA AWAHIMIZA WAKAZI WA GAIRO KUWA NA MOYO WA KUFANYA KAZI KWA KUJITEGEMEA

KINANA AWAHIMIZA WAKAZI WA GAIRO KUWA NA MOYO WA KUFANYA KAZI KWA KUJITEGEMEA

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Thursday, April 18, 2013 | 3:55 PM

Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdurhaman Kinana akizungumza na wakazi wa kata ya Chakwale,wilaya ya Gairo mapema leo mchana,alipokuwa akizindua shina jipya la wakereketwa wa chama hicho.katika uzinduzi huo Kinana aliwaasa  na kuwahimiza wakazi wa eneo hilo kuwa na moyo wa kufanya kazi kwa kijitegemea badala ya kusubiri serikali iwafanyie kila kitu ikiwemo na suala la kuwapa ajira.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdurhaman Kinana akiwapa kifuta jasho baadhi ya wazee-waasisi wa chama cha CCM,kabla ya kufanyika kwa uzinduzi wa shina jipya la kata yao ya Chakwale,Wilaya ya Gairo mapema leo mchana.Ndugu Kinana na Ujumbe wake wa CCM wako ndani ya Wilaya ya Gairo katika ziara ya kuimarisha chama cha CCM mkoani Morogoro sambamba na kuangalia shughuli mbalimbali za maendeleo.
Katibu wa NEC-Itikadi na Uenezi-CCM,Nape Nnauye akizungumza jambo mbele ya wakazi wa Chakwale mara baada ya shina la kata hiyo kuzinduliwa mapema leo mchana,ndani ya wilaya ya Gairo.Baadhi ya Wazee waasisi ndani ya CCM-Kata ya Chakwale wakionesha kadi zao za chama cha CCM walizonazo tangu kuanzishwa kwa chama hicho,kwenye shughuli fupi ya kuzindua shina la kata hiyo.
Kijana aliyekuwa Mwanachama wa CHADEMA akiwa ameinyanyua kadi ya chama chake cha awali,na kukabidhiwa kadi ya chama cha CCM,akiwa kama mwanachama mpya wa chama hicho cha CCM.
Share this article :

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA