Home » » IRINGA SI SHWARI MVUTANO KATI YA MACHINGA NA POLISI WATISHIA USALAMA

IRINGA SI SHWARI MVUTANO KATI YA MACHINGA NA POLISI WATISHIA USALAMA

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Sunday, April 28, 2013 | 1:27 AM


Machinga wakiendelea na shughuli zao kama kawaida eneo la mashine Tatu asubuhi hii kutokana na kauli ya mbunge Msigwa kuwaruhusu kurejea ,chini polisi wakiwa eneo hilo

Hali si shwari katika Manispaa ya Iringa baada ya kauli mbunge wa jimbo hilo Mchungaji Peter Msigwa (Chadema) kuwataka wafanyabiashara wadogop wadogo (machinga) kurejea kufanya kazi katika eneo la barabara ya Mashine tatu kutekelezwa na machinga hao.
Msigwa ambae aliitoa kauli hiyo April 23 mwaka huu katika mkutano wa wabunge wa chadema waliosimamishwa bungeni ,mkutano uliofanyika katika uwanja wa Mwembetogwa mjini hapa,kwa kuwataka Machinga kurejea eneo hilo na iwapo mtu atafika kuwanyanyasa basi wana----!!!?
Machinga hao leo wameitikia kauli hiyo kwa kurejea eneo hilo na kupelekea askari wa kutuliza ghasia (FFU) kutanda eneo hilo na kushindwa kutumia nguvu zaidi ya kuwataka wafanyaiashara hao kuendelea na shughuli zao eneo hilo .

Share this article :

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA