Home » » HUYU NDIE MREMBO MWANACHUO MDOKOZI WA VIATU KTK DUKANI MJINI IRINGA APOKEA KICHAPO

HUYU NDIE MREMBO MWANACHUO MDOKOZI WA VIATU KTK DUKANI MJINI IRINGA APOKEA KICHAPO

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Thursday, April 18, 2013 | 3:54 PM

 Mrembo  huyu  aliyejitambulisha  kwa  ni mwanafunzi  wa chuo  kikuu  kimojawapo mjini Iringa akilia baada ya kupokea  kichapo kutoka kwa mwanamke mfanyabiashara  eneo la Miyomboni mjini Iringa baada ya  kuiba viatu  vya mtumba na kuficha kwapani
Hapa  akimpigia  simu mpenzi  wake  ili aweze kumkomboa baada ya  kutakiwa  kulipa Tsh 50,000 kwa viatu pea mbili alizoiba .

Si  kila anayekwenda  dukani  kuuliza bidhaa ni mteja  wengine ni matapeli na  wezi na si kila mrembo na tabia yake ya  kirembo lah! hasha  wengine sivyo .

Hii ni kauli ya  mwanamke mfanyabiashara  wa eneo la  Miyomboni jengo la  Santon aliyefahamika kwa jina la mama Masawe ambae  amekumbwa na tukio la  kuibiwa  viatu na mrembo huyu  pichani aliyejitambulisha kuwa ni mwanafunzi  wa  chuo  kikuu  kimoja wapo maarufu mkoani Iringa na mkazi  wa Kihesa  Kilolo mjini hapa.

Tukio la mrembo  huyo  kupokea  kichapo na kuvuliwa  nguo na  kupokonywa  simu yake na mikoba zaidi ya mitano  pamoja na kiasi cha TSh 15,000 ambazo alikuwa amezihifadhi limetokea  jumapili  wiki hii katika  eneo la Miyomboni mjini Iringa.

Akielezea juu ya mkasa  huo  wa aina yake  leo mfanyabiashara   huyo  mama Masawe  alisema kuwa eneo  hilo amekuwa na kawaida ya  kuibiwa  viatu katika  duka  lake la viatu  vya mtumba na  kuwa  mbali ya  kukamatwa kwa mrembo  huyo  bado amepata  kukamata  vijana  zaidi ya  wawili watanashati ambao  wamekuwa wakifika na kujifanya wakichagua viatu na  kuishia  kuiba na kutoweka .

Hivyo  alisema aliyesema kuwa za mwizi arobaini  wala hakukosea na kuwa  binti   huyo mrembo  pia  alifika  eneo hilo na  kutumia mbinu na kuchagua  viatu na  kuficha  kwapani japo  yeye kama mhusika  wa  duka  hilo alikuwa amemwekea mtego na  kushuhudia picha nzima  japo  alijitahidi  kunyamaza hadi  mrembo huyo alipoaga na  kutaka  kuondoka ndipo timbwili na  kichapo  lilipoanza kwa mrembo huyo ambae aliomba  kupunguziwa adhabu kutokana na kuwa na ujauzito  wa miezi kama mitatu ama  minne.
Alisema  kuwa  kutokana na maombi ya mrembo huyo  kupunguziwa adhabu  hakuweza kumfikisha  polisi  zaidi ya kumpa kichapo  cha kufa mtu na kumpokonya  mali  zote alizokuwa ametoka  kuiba katika maduka ya  Miyomboni mjini hapa pamoja na  simu  yake ya kiganjani
Share this article :

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA