Home » » AJALI YAUA IRINGA

AJALI YAUA IRINGA

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Sunday, April 7, 2013 | 9:14 AM 
 Wananchi  wa  Iringa  wakishuhudia ajali(picha ya Maktaba ya Fg Blogu)
...............................................................................

Watu  zaidi ya  wawili  wamefariki dunia  papo hapo na  wengine zaidi ya 10  kujeruhiwa  vibaya  baada ya gari aina ya costa mali ya  Lutengano  yenye namba za usajili T 986 AFU kugongana  uso kwa uso la gari ndogo aina ya Dyana yenye namba za IT  44 20   iliyokuwa  ikisafirishwa kwa  nchi  za kusini mwa Tanzania huku  ikivu gari  jingine aina dogo lenye namba za IT  .

Mashuhuda  wa ajali  hiyo  wameueleza mtandao  huu  wa www.francisgodwin.blogspot.com  kuwa ajali  hiyo imetokea  majira ya  saa 2 asubuhi ya  leo  eneo la Ulete katika barabara  kuu ya Iringa - Mbeya.

Akizungumzan na mtandao  huu  Abel Mkuyu  alisema  kuwa   waliokufa katika ajali  hiyo ni pamoja na dereva  wa costa  hiyo ya Lutengano na abiri mmoja  aliyekuwemo katika gari  hilo aina ya IT 44 20 Dayana lililokuwa  likielekea  barabara  ya Mbeya .

Hata  hivyo  shuhuda  huyo alisema  kuwa  chanzo cha ajali  hiyo ni mwendo kasi  wa gari hilo aina ya Dyna IT ambalo  lilikuwa  likishuka katika mteremko wa Ulete na  hivyo kufeli  breck na  kuligonga daladala   hilo la Lutengano .
Alisema  kuwa  baada ya ajali  hiyo  watu  wawili  waliokuwemo katika gari  hilo ya Dyna  ambalo  lilionyesha  kufeli  break na  kuingia katika costa  hiyo.
 
Hata  hivyo katika ajali  hiyo  watu  wawili ambao  walikuwemo katika gari hilo dogo  walikufa  papo hapo huku  dereva  wa daladala  ya  Lutengano  akikimbizwa katika Hospitali ya  wilaya ya Mufindi akiwa mahututi baada ya  kuvunjika vunjika  miguu  yote  miwili na kuumia vibaya  katika paji lake la uso na habari  zisizothibitishwa  inasemekama amefariki  dunia  akiwa njiani kuelekea Hospital.


MATUKIO HAYA KWA  UDHAMINI MKUBWA WA   HOPE SERVICE STATIONAL WALIOPO IRINGA MJINI ENEO LA CRDB NA GAPCO ENEO LA MSHINDO
 Ni  kituo  bora cha mafuta mkoa mzima  wa Iringa na mikoa ya nyanda za juu  kusini ,karibu Iringa mjini karibu kujaza mafuta katika kituo cha HOPE SERVICE STATIONAL kilichopo eneo la CRDB na kituo pacha cha GAPCO MSHINDO
 
 Tupo kiukombozi  zaidi fika  ukombolewe  hapa kwa mafuta  yenye ubora


 
Share this article :

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA