Home » , , » NIPO TAYARI KUKUFUATA DAUDI MWANGOSI ......

NIPO TAYARI KUKUFUATA DAUDI MWANGOSI ......

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Wednesday, January 30, 2013 | 10:03 AM

Marehemu Daudi Mwangosi akiwa na kamera ambayo alikuwa nayo kabla ya kulipuliwa kwa bomu ,hapa akiwa katika hifadhi ya Taifa ya Ruaha Iringa kuhamasisha utalii wa ndani kwa wanahabari na watanzania
Daudi Mwangosi kulia akiwa na Mahija Zayumba kutoka Nuru Fm na katibu msaidizi wa klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Iringa (IPC) Francis Godwin ambaye pia ni shemeji yake ,hapa ni ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Ruaha wakati wa wanahabari Iringa walipotembelea hifadhi hiyo April 26 mwaka huu Kwa hisani ya Francis Godwin Blog
Daudi Mwangosi akiwa katika hifadhi ya Taifa ya Ruaha hapa akitoka kuamka tayari kwa kwenda kutazama Tembo aliyekufa na kuwasaka Simba ,kiatu ,suruali na Laptop hiyo ndivyo alivyokuwa navyo hata siku ya kifo chake Nyololo
Daudi Mwangosi akiwa katika picha ya pamoja na Sima Bingileki siku aliposhinda uenyekiti wa IPC ,Sima alikuwa mpinzani wake katika nafasi hiyo
Daudi Mwangosi akiwa na Sima Bingileki na Oliver Motto siku wanachama wa IPC walivyofanya ziara Pemba
Daudi Mwangosi akiomba kura kwa wanachama wa IPC ili kuwa mwenyekiti wao
Daudi Mwangosi (kulia) akiwa na Rais wa umoja wa vilabu vya waandishi wa habari nchini Keneth Simbaya (katikati) na katibu mtendaji wa IPC Frank Leonard siku alipokwenda kushiriki sherehe ya mwanahabari Conrady Mpila wa kitulo FM kuoa ,harusi ambayo bado kufanyika na alipania kwenda kushiriki huko Makete Njombe
Hapa Daudi Mwangosi akitaniwa na mmoja kati ya wanahabari kutoka Kitulo Fm kunywa pombe aina ya Mbege ambayo aligoma kunywa kutokana na kutokuwa na kawaida ya kunywa pombe ya aina yoyote ile
Daudi Mwangosi (katikati) akiwa na mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa Mhe.Ritta Kabati na mkuu wa chuo cha Tumaini Iringa Profesa Nicholaus Bangu siku ya mkutano wa wadau wa habari uliofanyika ukumbi wa Manispaa ya Iringa
Daudi Mwangosi (wa pili kulia) akiongoza wanahabari Iringa kuvuka daraja la kamba lililopo hifadhi ya Taifa ya Ruaha wakati wa ziara yao ya kuhamasisha utalii wa ndani iliyofanyika mwaka huu
Wahabari walioungana na Daudi Mwangosi kutembelea hifadhi ya Taifa ya Ruaha kutoka kulia ni Oliver Motto , Francis Godwin, Paulina Kuye ,Sophia Mpunga na Happynes Matanzi


IWAPO mwenyekiti wangu katika klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Iringa (IPC) Daudi Mwangosi angelijua ya mbeleni kamwe asingekubali kukifukizia kifo siku ya jumapili tarehe 2/9/2012 kule Nyololo wilayani Mufindi mkoani Iringa.

Mwangosi ambaye kwangu mimi Francis Godwin mbali ya kuwa ni mwenyekiti wangu ambaye tulipata kushirikiana vema kuendesha IPC yeye akiwa mwenyekiti mimi nikiwa katibu msaidizi pia ni shemeji yangu na mshauri wangu katika mambo mbali mbali yakiwemo ya kimaisha .

Daudi Mwangosi katika uhai wake alikuwa ni mfano kwa wengi kutokana na kuwa na msimamo usioteteleka katika utoaji wake wa maamuzi na katika kutetea maslahi kwa wanahabari pia alikuwa hapendi kuona mwanahabari akinyanyasika na ndio maana hata siku nilipokamatwa na jeshi la polisi pale sekondari ya Tosamaganga kwa madai ya kutoa taarifa ya polisi kutumia nguvu zaidi kwa kuwatawanya wanafunzi walioandamana kupinga manyanyaso katika shule hiyo alikuwa kunitoa mahabusu pale kituo cha polisi Iringa mjini wakati huo kamanda wa polisi akiwa Evarist Mangalla .

Nakumbuka akiwa pale polisi mbali ya askari aliyehusika kunikamata na kunipa vitisho vingi ambavyo nisingependa kuvitoa hapa afande Mrisho bado Mwagosi alionekana kumwomba Mrisho kuwa ni vema busara zaidi ingetumika badala ya polisi kutanguliza jazba na visasi kwa kila jambo .

Nasema kuwa maneno ya hekima ya Daudi Mwangosi ambayo alikuwa akiyatoa huku akinipa pole kwa yaliyonikuta na ikiwa ni pamoja na askari hao kunisulutisha kwa kunipakia katika gari ya FFU huku wakipiga king'ora kama wanaongoza msafara wa kiongozi wa kitaifa ama kama kuna jambo la hatari zaidi kweli hekima hiyo ilizaa matunda kwa mimi kutoka mahabusu majira ya saa 1 usiku tena huku nikitakiwa kujidhamini mwenyewe kesi ambayo hadi leo bado sijaijua na wala kupelekwa mahakamani .

Mbali ya Daudi Mwangosi kushughulikia sakata la kukamatwa kwangu na polisi bado aliweza kuongoza maandamano ya wanahabari mkoa wa Iringa kupinga hatua ya uongozi wa serikali ya mkoa wa Iringa chini ya uongozi wa Dkt Christine Ishengoma kunyanyasa wanahabari zoezi ambalo Mwangosi aliweza kulishughulikia hadi sasa wanahabari na ofisi ya mkuu wa mkoa kuwa na mahusiano mazuri zaidi.

MAANDALIZI YA KIFO CHAKE.

Daudi Mwangosi siku tatu kabla ya kifo chake aliandaa CV yake katika ukumbi wa Maktaba ya mkoa wa Iringa ambako kulikuwa na mafunzo ya uandishi wa makala kwa wanachama wa IPC na CV hiyo alikuwa akiitoa na mwanahabari Getrude Madebwe ndie alikuwa akiiandika.

Tarehe 31/9/2012 majira ya saa 3 usiku tukiwa katika sherehe ya kumuaga aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Iringa Mohamed Abdulaziz na kumkaribisha Dkr Christine Ishengoma wakuu meza kuu ambayo ilipambwa na mkuu wa wilaya ya Iringa Leticia Warioba na Dkt Ishegoma na Abdulazi na katibu tawala wa mkoa wa Iringa Getrude Mpaka ilipata kuniita mbele baada ya umeme kukatika katika ukumbi huo wa St.Dominic na moja kati ya swali walilopata kuniuliza ni juu ya kukosekana kwa Daudi Mwangosi katika sherehe hiyo siku wa jibu ila nilitoka nje ya kumpigia simu Mwangosi ili kujua kama atafika ama lah!

Baada ya kumpigia simu simu iliita sana na baada ya muda ilipokelewa na Mwangosi aliongea kwa sauti ya unyonge kuwa unasemaje bwana mdogo Godwin ,nilimwambia kuwa viongozi akiwemo Ras mama Mpaka wanakuuliza katika sherehe ndipo alipojibu kuwa najisikia kuumwa mdogo wangu niwakilishe nitachukua picha kwako kesho ili nitume Chanel Ten.

Asubuhi ya tarehe 1/9/2012 IPC tulikuwa na mkutano mkuu wa IPC pale ukumbi wa Maktaba japo ilitupasa kufika majira ya saa 2 asubuhi yeye kama mwenyekiti hakuweza kufika muda huo alifika kwa kuchelewa na hivyo kupelekea mkutano kuanza kwa kuchelewa zaidi.

Wakati wanachama wakijiandaa kuingia ukumbini ghafla nilimwona Daudi Mwangosi akiwa jirani na ofisi yake jengo la Motto Familia akiwa na begi la Laptop yake begani akivuka barabara upande wa pili kuja ukumbini alipaza sauti shemeji yangu Godwin upo kweli jana nilikuwa nikiumwa sana.

Baada ya hapo aliingia ukumbini na siku hiyo alionekana kuwa tofauti na siku nyingine kwani alitumia maneno mafupi zaidi kufungua mkutano huo tofauti na siku nyingine ambazo huwa akichukua muda zaidi .

Baada ya kufungua mkutano huo alipata kuuendesha vema kwa kushirikiana na katibu mtendaji huku kwa upande wangu kama katibu msaidizi siku hiyo sikuweza kutulia zaidi katika kiti changu mbele kwani homa ilinianza ghafla na hivyo kulazimika kumtumia ujumbe mfupi kwa simu kuwa shemeji leo sipo poa naumwa kweli kwa kuwa nilikuwa nimekaa kando na meza kuu na wanachama wenzangu alinitazama na kuonyesha tabasam huku akituma meseji kuwa pole mdogo wangu .

Kabla ya mkutano huo kufika ukingoni Daudi Mwangosi aliingia katika zoezi zito la kuwataka wanachama kutoa uamuzi juu ya mmoja kati ya wanahabari wanachama ambaye alionekana kutaka kuvuruga zoezi la sensa na kukiuka maadili ya katiba ya IPC na jambo ambalo aliwaomba kutoa uamuzi na kulazimika kuwaomba kila mmoja kupiga kura za siri .

Baada ya kura kupigwa kwa wanachama hao Daudi Mwangosi alipata kutoa uamuzi mzito wa kutangaza kumfuta uanachama mwanachama huyo jina kapuni kwa sasa ,huku akiomba sauti yake ambayo nilipata kumrekodi kuhusu kumfuta uanachama mwanachama huyo kurushwa radioni kuanzia siku ya jumatatu jioni katika radio za Iringa na Radio Ushindi FM ya Mbeya kurushwa siku ya pili .
Share this article :

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA