Home » , , , , , » RIPOTI KAMILI YA SOKO LA MAGAZETI IRINGA

RIPOTI KAMILI YA SOKO LA MAGAZETI IRINGA

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Friday, August 17, 2012 | 3:16 AM

Wananchi wa Manispaa ya Iringa wakisoma bure ama wakinukuu vichwa vya magazeti katika eneo la Posta mjini Iringa leo
Mwakilishi msaidizi wa gazeti la Mwananchi Iringa Diana Kangusi (kulia) akiwa na mwandishi wa gazeti la The Citizen Iringa Clement Sanga wakionyesha kwa wanahabari za uchunguzi nakala ya magazeti hayo leo baada ya kufika katika ofisi za Mwananchi kwa ajili ya uchunguzi wa soko la magazeti Iringa.
Wakala wa magazeti mbali mbali mjini Iringa Salum Zingilwa akiwa amebeba mzigo wa mabaki ya magazeti yaliyorudishwa na wauzaji
Hapa ni kusoma bure na kuondoka hakuna mnunuzi hapa

Iimeelezwa kuwa tatizo la kushuka kwa soko la magazeti mkoani Iringa limechangiwa na baadhi ya wauza magazeti kukodisha magazeti hayo pamoja na vituo vya radio na Runginga kuendesha vipindi vyake kwa kutegemea magazeti hayo .

Uchunguzi uliofanywa na wanahabari mjini Iringa umebaini hayo baada ya kuzungumza na makundi mbali mbali likiwemo kundi la wauza magazeti na wadau mbali mbali kuhusiana na hali halisi ya soko la magazeti kwa sasa.

Mwenyekiti wa wauza magazeti mjini Iringa Mashaka Kayoka amesema mbali ya kuwa baadhi ya magazeti yamekuwa yakiongoza kwa mauza na kuonekana kumalizika mapema katika vibanda vya magazeti ila asubuhi wakati wa kurudisha mabaki vijana hao wanaofanya kazi ya kutembeza magazeti wamekuwa wakirudisha mabaki ambayo kimsingi ni mabaki yanayotoka kwa wateja wao ambao hukodi kwa kiasi cha shilingi 100-200 kwa kila gazeti.

Kayoka alisema kuwa hadi sasa wauza magazeti hao wameonekana kuyumba kiuchumi zaidi kutokana na kufungiwa kwa gazeti la Mwanahalisi ambalo lilikuwa ni gazeti maarufu ambalo kila wiki linapotoka huchukua nakala nyingi kati ya 100 hadi 200 na kumaliza mapema na hivyo kujipatia faida zaidi tofauti na magazeti mengine ya wiki.

Alisema kuwa sasa baada ya mwanahalisi kufungiwa gazeti la wiki linaloongoza ni Raia mwema na kufuatiwa na Rai ,wakati magazeti ya kila siku yanaongoza kwa kuuzwa zaidi ni Mwananchi, Tanzania daima na Nipashe huku magazeti ya dini ,Jibu la Maisha, Nyakati ,Msemakweli huku gazeti la Kiongozi AN-Nuur na Kisiwa yakichuana katika soko.

Mbali ya magazeti hayo alisema magazeti ya udaku (magazeti Pendwa ) kama Uwazi, Ijumaa na kiu kwa upande wa mauzo yamekuwa yakiungoza kwa kuuzwa nakala nyingi kuliko gazeti lolote nchini.

Huku wadau mbali mbali akiwemo Salim Mbata alisema kuwa bei kubwa ya magazeti imechangia kwa upande wao kushindwa kununua magazeti na kuwa kwa sasa amekuwa akilazimika kusikiliza radio na kutazama Runginga na kama kuna gazeti ambalo amevutiwa ama halijasomwa katika vyombo hivyo vya habari ndilo hununua.

Meneja wa vipindi katika kituo cha Radio Nuru Fm Paulina Kuye alisema kuwa kuendesha vipindi kwa njia ya magazeti kunawezesha radio kusikilizwa zaidi ikiwa ni pamoja na kupata wazo la habari kwa siku husika.

Huku akidai kuwa kwa upande wao magazeti hayo ambayo huyatumia kuendesha vipindi wamekuwa wakinunua kwa pesa za ofisi kama walivyowateja wengine.


Wakala wa magazeti ya Majira, Nipashe , Jamboleo , Habari leo mkoani Iringa Salm Zingilwa amesema kuwa soko la magazeti limekuwa likiyumba kutokana na habari zinazoandikwa kwa siku husika .

Akitolea mfano Habari ya Kushambuliwa kwa mwenyekiti wa chama cha madaktari nchini Stivin Ulimboka na habari za bungeni na matukio makubwa katika Taifa pamoja na habari zinazohusu mkoa wa Iringa zimekuwa na wasomaji wengi zaidi .

Alisema kwa upande wake kwa gazeti la Nipashe amekuwa akipokea nakala 140 na mabaki ni kati ya 30 na 35 wakati Majira hupokea nakala 100 mabaki huwa nakala 40 ,Jamboleo nakala 60 mabaki ni kati ya 20 au 25 huku Habari leo hupokea nakala 30 hubaki 5 na gazeti la kiu nakala 400 hubaki 50 Daily News huletwa nakala 50 mabaki ni nakala 10

Mwakilishi msaidizi wa mkoa wa Iringa kwa gazeti la Mwananchi Diana Kangusi alisema kuwa kati ya nakala 900 hadi 1000 mbazo huletwa mkoani Iringa mabaki huwa nakala 150 hadi 100 wakati gazeti la Citizen kati ya nakala 70 mabaki huwa ni 29 au 30

Wakati kwa gazeti la Kwanza jamii Iringa kwa mjibu wa mhariri gazeti hilo Greyson Mgoi amedai kuwa kati ya nakala 5000 mabaki ni nakala 1000 pekee.

Uchunguzi huu umefanywa na Francis Godwin, Conrad Mpila, Getrude Madembwe , Janeth Matondo , Vicky Macha na Said Ng'amilo.


Share this article :

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA