Home » » BREAKING NEWssssssssMELI I YAZAMA BAHARI YA HINDI MCHANA HUU IKIWA NA ABIRIA ZAIDI YA 200

BREAKING NEWssssssssMELI I YAZAMA BAHARI YA HINDI MCHANA HUU IKIWA NA ABIRIA ZAIDI YA 200

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Wednesday, July 18, 2012 | 8:46 AM

Meli iliyokuwa imewabeba takriban watu miambili imethibitiswha kuzama katika bahari ya hindi eneo la Chumbe kisiwani Zanzibar. Meli hiyo kwa jina SKAGIT ilikuwa inatoka Dar Es Salam kuelekea Zanzibar.
Kulingana na taarifa za vikosi vya wanamaji , meli hilyo ilianza kupata matatizo baada ya kutokea mawimbi makali.
Jeshi la polisi la wanamaji nchini Tanzania limeanza shughuli za kuwaokoa watu zaidi ya mbia mbili wanaohofiwa kuwa kwenye meli ya Skagit inayoripotiwa kuzama huko visiwani Zanzibar.
Kwa mujibu wa taarifa za polisi, ingawa hawajathibitisha idadi kamili ya abiria waliomo kwenye meli hiyo, lakini wamethibitisha kwamba meli hiyo imepigwa na dharuba ya upepo mkali katika eneo la Chumbe pindi ilipokuwa inatoka jijini Dar es Salaam kuelekea visiwani Zanzibar.
Itakumbukwa kwamba, ni takriban mwaka mmoja sasa tokea ajali ya meli iliyokuwa imezidisha mizigo kuzama katika pwani ya kisiwa cha Zanzibar ikiwa na watu takriban 800.

Kwa habari za sasa hivi bofya hapa
Share this article :

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA