Home » » DKT BILAL ATAKA JITIHADA ZAIDI KUPUNGUZA UMASIKINI NCHINI

DKT BILAL ATAKA JITIHADA ZAIDI KUPUNGUZA UMASIKINI NCHINI

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Tuesday, May 8, 2012 | 6:29 AMMakamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake wakati akizindua rasmi Jukwaa la Uchumi wa Kijani, litakaloendelea kwa siku tatu Mkoani Iringa. Uzinduzi huo umefanyika leo Mei 8, 2012, katika Ukumbi wa Shule ya Msingi Mtakatifu Dominic Savio, mkoani Iringa. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
MAKAMU wa rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Mohamed Gharib Bilal jitihada zaidi kufanyika ili kupunguza kasi ya umasikini katika jamii nchini.

Alisema kuwa ili kuharakisha maendeleo nchini jitihada za makusudi za kupunguza umaskini na kuleta maendeleo lazima zifanywe kwa kuzingatia uhalisia wa mambo ikiwa ni pamoja na kulenga wakazi na uchumi kwa wananchi wa vijijini.
Makamu wa Rais aliyasema hayo mjini Iringa leo wakati akizindua jukwaa la Uchumi wa Kijani jana katika ukumbi wa St.Dominic Savio .

Dkt Bilal alisema kuwa upo uhusiano mkubwa kati ya watu maskini hasa wa vijijini na mazingira kutokana na watu wa vijijini huishi karibu na mazingira ya asili na hutegemea rasilimali za ardhi, maji na misitu kwa maisha yao.

"Mara nyingi matumizi hayo yamezisababishia hasara jamii ikiwa ni pamoja na upotevu wa maisha na kipato"
Alisema kuwa pamoja na kuzungumzia uharibifu wa mazingira unaofanywa vijijini bado ni tatizo na hakuna budi jamii kuendelea kuelimishwa zaidi .

Bilal alisema kuwa, masuala ya mazingira mijini pia ni muhimu kuzingatiwa kutokana na maeneo mengi ya miji hukabiliwa na changamoto za ubadilishaji wa matumizi ya ardhi kunakoendana na ukataji wa miti, uchimbaji mawe na pia ukaushaji wa ardhioevu kwani mambo hayo huchangia kwa kiasi kikubwa katika mabadiliko ya tabia ya nchi.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya UONGOZI Profesa Joseph Semboja alisema kuwa amepata faraja kuona idadi kubwa ya watunga sera, watoa maamuzi na viongozi mbalimbali wamedhibitisha kushiriki katika uzinduzi wa jukwaa la uchumi wa kijani.Alieleza kuwa ukuaji wa uchumi endelevu ndio njia pekee ya kufikia ustawi wa kudumu kwani jukwaa hilo linalengo la kutoa njia madhubuti kwa viongozi wa serikali, sekta binafsi na asasi za kiraia pamoja na wote watakaochagua kufuata mkondo huo.


Aidha Naibu waziri wa kilimo, chakula na ushirika Adam Malima ameahidi kutoa ushirikiano kwa tasisi hiyo ili kukabiliana na tatizo la uharibifu wa mazingira ambao unapelekea mabadiliko ya tabia ya nchi.

kupata habari za sasa Bofya hapa
Share this article :

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA