Home » » KIKOSI CHA TAIFA STARS KUINGIA KAMBINI KESHO

KIKOSI CHA TAIFA STARS KUINGIA KAMBINI KESHO

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Wednesday, November 2, 2011 | 4:47 AM


Timu ya Taifa (Taifa Stars) inaingia kambini kesho (Novemba 3) kujiandaa kwa mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia dhidi ya Chad itakayochezwa Novemba 11 jijini N'Djamena. Wachezaji wote wanatakiwa kuripoti kambini kesho, isipokuwa wale wanaocheza mpira wa kulipwa nje ya nchi ambao wataanza kuingia nchini Novemba 4 mwaka huu.

Kambi ya Taifa Stars itakuwa hoteli ya New Africa na mazoezi yatafanyika Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Dar es Salaam kulingana na programu za Kocha Mkuu wa timu hiyo Jan Poulsen. Timu inatarajiwa kuondoka nchini Novemba 8 usiku kwenda N'Djamena.

Waamuzi wa mechi ambao wote wanatoka Nigeria ni Bunmi Ogunkolade, Tunde Abidoye, Baba Abel na Abubakar Ago. Mtathimini wa waamuzi atakuwa Idrissa Sarr kutoka Mauritania wakati Kamishna wa mchezo huo ni Hamid Haddadj (Algeria).

PRESS NOTICE
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kesho (Novemba 3, 2011) litakuwa na mikutano miwili na waandishi wa habari.
Mkutano wa kwanza;
Muda: saa 4.00 asubuhi
Mahali: TFF

Mkutano wa pili;
Muda: saa 6.00 mchana
Mahali: TFF

Regards,
Boniface WamburaMedia OfficerTanzania Football Federation (TFF)
Share this article :

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA