Home » » BREAKINGNEWSZzzzz MMILIKI WA SHULE ZA SEKONDARI EFATHA NA RETCO IRINGA MATATANI KWA RUSHWA YA TSH.30,000

BREAKINGNEWSZzzzz MMILIKI WA SHULE ZA SEKONDARI EFATHA NA RETCO IRINGA MATATANI KWA RUSHWA YA TSH.30,000

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Wednesday, November 2, 2011 | 4:03 AM


Boss wa Takukuru nchini Dkt Edward Hosea
MMILIKI wa shule ya Sekondari Efatha na Retco Education Center mwalimu Paul Tabani (48) amefikishwa mahakamani kwa tuhuma ya kuomba na kupokea rushwa ya shilingi 30,000 kutoka kwa mwanafunzi wake wa kike.

Mmiliki huyo amefikishwa katika mahakama ya hakimu mkazi wa mkoa wa Iringa leo na taasisi ya ya kuzuia na kupambana na rushwa nchini (TAKUKURU)

Tabani alipandishwa kizimbani majira ya saa 5 asubuhi mbele ya hakimu Mathar Mpaze wa mahakama ya hakimu mkazi wilaya ya Iringa na kusomewa mashtaka mawili katika kesi namba 15(1)(a) ya kuomba na kupokea rushwa kinyume na sheria ya Takukuru ya mwaka 2007.

Akisoma mashtaka hayo mbele ya hakimu Mpaze mwendesha mashtaka wa TAKUKURU mkoa wa Iringa Restituta Kessy aliieleza mahakama hiyo kuwa mshtakiwa Tabani ambaye kitaaluma na mwalimu na mkazi wa Kleruu katika Manispaa ya Iringa alitenda makosa hayo Octoba 25 mwaka huu akiwa katika eneo la Retco Education Center mjini Iringa.

Alisema kuwa Tabani aliomba na kupokea rushwa hiyo kutoka kwa mwanafunzi Christina Wandilage ambaye amehitimu kidato cha nne mwaka huu 2011.

Mwendesha mashtaka huyo alisema kuwa Tabani ambaye alikuwa ameishikilia simu ya mwanafunzi huyo baada ya simu hiyo kukamatwa na mwalimu wake wa RETCO mwalimu Ady Sanga ,kuwa alimtaka mwanafunzi huyo kuweza kumpa kiasi hicho cha fedha ili aweze kabidhiwa simu yake.

Hivyo alisema kuwa mtuhumiwa huyo kosa la kwanza ni kuomba rushwa na kosa la pili ni kupokea rushwa ambapo ni kinyume na sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa kifungu namba 15(1)(a) ya mwaka 2007.

"Uchunguzi wa shitaka hilo umekamilika japo hatuna pingamizi yeyote na dhamana kwa mshtakiwa ...mheshimuwa hakimu"alisema mwendesha mashtaka wa Takukuru Iringa.

Hata hivyo mshtakiwa huyo mbali ya kukana makosa yote mawili na mahakama hiyo kutoa masharti ya dhamana kuwa ni kuwa na mdhamini mmoja atakaye saini dhamana ya maandishi ya shilingi 100,000 ,bado Tabani alinusurika kutupwa mahabusu baada ya barua za dhamana zilizofikishwa mahakamani hapo zote mbili kuwa na makosa ikiwemo moja ya awali iliyokuwa haijatolewa nakala ya pili wala picha kugongwa mhuri wa afisa mtendaji huku barua ya pili mdhamini wake ambaye ni mwalimu wake kujiandikia barua mwenyewe ya dhamana hali ambayo mahakamani hiyo ilipinga barua zote kabla ya kufanyiwa masahahisho ile ya kwanza.Kesi hiyo itafika tena mahakamani hapo Novemba 16 mwaka huu kwa ajili ya kutajwa .
Share this article :

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA