Home » » MFANYAKAZI WA KAMPUNI YA MAFUTA ATUPWA JELA MWAKA MMOJ

MFANYAKAZI WA KAMPUNI YA MAFUTA ATUPWA JELA MWAKA MMOJ

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Wednesday, September 7, 2011 | 12:10 AM

Na Esther Macha, Mbeya


MAHAKAMA ya hakimu Mkazi Mkoa wa Mbeya,imemuhukumu kifungo cha miaka 24,Haji Abdalah,ambaye ni mfanyakazi wa kampuni ya Panoni inashughulika na uuzaji wa mafuta katika Mji wa Tunduma,baada ya kupatikana na hatia ya kuitia hasara kampuni hiyo kiasi cha shilingi Milioni36.

Hukumu hiyo ilitolewa na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa mahakama ya Mbeya, Zaward Laizer,baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo na upande wa mashtaka uliowasilishwa na mwendesha mashtaka wakili wa serikali Basilius Namkambe.

Awali, akisoma hukumu hiyo hakimu Laizer mbele ya mwendesha mashitaka,Namkambe alidai kuwa mshitakiwa alitenda kosa hilo machi 16 mwaka jana kwa kuiba kiasi cha Lita 8000.

Pia alieleza kuwa machi 16 mwaka jana mshitakiwa huyo alijaribu kuiba kwa kutorosha kiasi cha sjhilingi milioni moja,ambapo alimtumia mfanyakazi mwenzake baada ya mawasiliano yao kubainika kupitia ujumbe mfupi wa maandishi ya simu mkononi.

Kabla ya kutolewa kwa hukumu hiyo mwendesha mashitaka wakili wa serikali Namkambe, alimuomba hakimu kuwa atoe adhabu kali kwa mshitakiwa ili iwe fundisho kwa watu wengine wenye tabia kama hiyo.

Mshitakiwa alipopewa nafasi ya kujitetea alimuomba hakimu huyo ampunguzie adhabu kwa kuwa anakabiliwa na matatizo ya macho, pia anafamilia ambayo ni mke na watoto ambao wanamtegemea kwa asilimia 100.

Mwisho.
Share this article :

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA