Home » » ALEXIA WILIAM AWA MISS VODA COM DAR CITY CENTER

ALEXIA WILIAM AWA MISS VODA COM DAR CITY CENTER

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Sunday, May 15, 2011 | 2:01 AM

Mshindi wa kwanza wa taji la Vodacom Miss Dar City Center Alexia William akiwa kwenye picha ya pamoja na mshindi wa pili Salha Israel (Kushoto) na mshindi wa tatu Jenifer Kalokola mara baada ya kutangazwa washindi. Shindano hilo lilifanyika mwishoni mwa wiki jijini Dares salaam.
Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Slaa akimkabidhi mshindi wa kwanza wa taji la Vodacom Miss Dar City Center Alexia William zawadi ya shilingi Milioni 1/- zilizotolewa na waandaaji wa shindano hilo. Anayeshuhudia ni mke wa Meya Slaa, shindano hilo lilifanyika mwishoni mwa wiki jijini Dares salaam.
Vodacom Miss Dar City Center Alexia William akipunga mkono mara baada ya kutawazwa kuwa mlimbwende wa kanda hiyo. Wengine kutoka kulia kwake ni mshindi wa pili Salha Israel, wa pili kutoka kulia ni mshindi wa tatu Jenifer Kalokola, wa kwanza kutoka kushoto ni mshindi wa nne Maryvine Kenzia na kulia mshindi wa tano Lilian Paulo, shindano hilo lilifanyika mwishoni mwa wiki jijini Dares salaam.
Mkuu wa itifaki wa kamati ya Vodacom Miss Tanzania Albert Makoye, Mtaalam wa Masuala ya Habari wa Vodacom Tanzania Matina Nkurlu na Afisa Udhamini wa kampuni hiyo Ibrahim Kaude wakisoma ujumbe wenye jina la mshindi wa Miss University (UDSM) Chiaru Masonobo ili walitangaze kwenye shindano la Vodacom Miss Dar City Center lililofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Saalam.(picha na Michuzi Blogu)
Share this article :

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA