Home » » BREAKINGNEWZzzzzzzzzzzz ,SIMU YA MCHINA YALIPUKO NA KUTEKETEZA NYUMBA IRINGA

BREAKINGNEWZzzzzzzzzzzz ,SIMU YA MCHINA YALIPUKO NA KUTEKETEZA NYUMBA IRINGA

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Sunday, April 17, 2011 | 4:05 AM

Simu aina ya Nokia ya Kichina iliyolipuka
mali zilizoteketea
MALI mbali mbali mali ya Tito Kilale mkazi wa kihesa katika manispaa ya Iringa zimeteketea kwa mkubwa ambao unasadikika kutokana na hitirafu ya umeme baada ya simu aina ya Nokia ya mchana iliyokuwa ikichajiwa kulipuka .

Wakielezea tukio hilo leo katika mahojiano maalum na mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com wapangaji wa nyumba hiyo walisema kuwa mmiliki wa chumba hicho wakati tukio hilo likitokea majira ya saa 4.45 asubuhi alikuwa safarini nje ya mji wa Iringa.

Walisema kuwa chanzo cha chumba hicho kuteketea kwa moto ni hitirafu ya umeme iliyosababishwa na simu ambayo ilikuwa imewekwa chaji na mmoja wapangaji kwenye sebule ya mpangaji mwenzao huyo .

“Sisi tulikuwa tumekaa nje tukiendelea na shughuli zetu ghafla tulisikia kishindo kikubwa cha mlipuko kama baruti vile ila hatukuweza kuchukulia manani sana tulijua ni panya wameangusha kitu ndani ila baada ya kama dakika 10 hivi toka kishindo hicho kitokee ndipo tuliona moshi mzito unatoka ndani…kutokana na mlango wa chumba kuwa umefungwa na mpangaji mwezetu aliyekuwa na funguo ambaye alikuwa amechaji simu hiyo kuwa mbali tulilazimika kuvunja mlango na madirisha ili kujaribu kuokoa mali”

Hata hivyo wakazi hao wa Kihesa walisema kuwa tukio hilo ni somo kwa watumiaji wa simu ambao wamekuwa na kawaida ya kuzilaza katika chaji kuwa ni vizuri sasa kujifunza kwa tukio hilo na kuepuka kuacha simu zao katika chaji ili kuepuka madhara kama hayo.

Mtoto wa mmiliki wa chumba hicho Kashiru alisema kuwa mmiliki wa chumba hicho ni babake mdogo na kuwa wakati tukio hilo likitokea alikuwa kijijini na chumba chake alikuwa amefunga na kukabidhi ufunguo kwa mmoja kwa majirani zake.

Alisema kuwa mali zilizookolewa ni zile zilizokuwa chumbani pekee ambazo ni pamoja na Laptop na kitanda pamoja na masanduku ya nguo huku mali mbali mbali ambazo ni nyigi zaidi zilizokuwa sebuleni zote ziliteketea kwa moto.

Hata hivyo alisema kuwa pamoja na wakati moto huo ukitokea nje ya chumba hicho kulikuwa na watoto wakicheza ambao waliokolewa pamoja na magari madogo aina ya land Rover mawili ambayo yalikuwa yameegeshwa nje ya nyumba hicho ambayo pia yalinusurika kuteketea kwa moto.

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Iringa Evarist Mangalla na mmiliki wa chumba hicho hawakuweza kupatikana ili kuelezea hasara iliyosababishwa na moto huo.

Share this article :

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA