Home » » UAMUZI MDOGO WA KESI YA MWAKALEBELA KESHO

UAMUZI MDOGO WA KESI YA MWAKALEBELA KESHO

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Thursday, February 24, 2011 | 12:09 PM

Mwakalebela katikati akitoka mahakamani leo na ndugu zake
MAHAKAMA ya hakimu mkazi mkoani Iringa jana imeshindwa kuendelea na usikilizaji wa kesi ya Frederick Mwakalebela kutokana na kifo cha aliyekuwa jaji mfawidhi wa mahakama kuu kanda ya Iringa jaji Laurence Uzia .


Wakili wa Mwakalebela Basil Mkwata aliwaeleza waandishi wa habari mara baada ya kesi hiyo kusogezwa mbele hadi kesho itakapoendelea tena Mahakamani hapo kuwa kimsingi leo ilipaswa kutolewa kwa maamuzi madogo ya kesi hiyo kama iendelee kusikilizwa ama lah.


Hata hivyo alisema kuwa kusogezwa mbele kwa kesi hiyo kumetokana na maelezo ya hakimu anayesikiliza kesi hiyo maelezo ambayo yamekubaliwa pande zote mbili kuwa kesi hiyo itaendelea keshoHakimu wa wilaya ya Iringa Festo Lwila alisema kuwa kusogezwa mbele kwa kesi hiyo ni kutokana na kujitokeza matatizo hayo na kuwa kulikuwa na uwezekano wa maamuzi ya kesi hiyo kuandikwa na kutolewa jana ila bado ana omba afanye kazi hiyo kwa uhuru zaidi hadi kesho ndipo kesi hiyo itaendelea.Mwakalebela ambaye ni kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) anaokabiliwa na tuhuma ya rushwa katika mchakato wa kura za maoni za kumpata mgombea ubunge wa Jimbo la Iringa Mjini, shitaka la kesi ya jinai namba 4 ya mwaka 2010, inayohusiana na kutoa hongo kinyume cha sheria namba 15 (1) (b) ya Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ambayo ilisomwa pamoja na kifungu cha cha 21 (1) ((a) na 24 (8) ya Sheria ya Gharama za Uchaguzi ya mwaka 2010 ambapo kwa upande wa Takukuru inawakilishwa na wanasheria wake Imani Nitume, na Prisca Mpeka,

Mwakalebela anadaiwa kutoa hongo ya Sh.100,000 kwa Mwenyekiti wa kijiji hicho, Hamisi Luhanga, ili azigawe kwa wapiga kura 30 wa CCM ili wampigie kura za maoni za kumchagua mtuhumiwa wa kwanza (Mwakalebela), Agosti Mosi, 2010.

Hata hivyo tayari Mwakalebela na mkewe walipata kukana kosa hilo na kupewa dhamana na mahakama hiyo yenye masharti ya kuwa na wadhamana wawili mmoja wao mtumishi wa serikali na kila mmoja kuweka dhamana ya Sh. 5,000,000.
Bofya hapa
Share this article :

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA