Home » » MTOKEO DARASA LA SABA SOUTHERN HIGHALD YATESA

MTOKEO DARASA LA SABA SOUTHERN HIGHALD YATESA

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Friday, December 3, 2010 | 3:30 AM


SHULE ya kimataifa ya Soutthern Highland Mufindi na Brokebond zafanya vizuri mtihani wa taifa wa darasa la saba mwaka 2010 katika mkoa wa Iringa na kuzipita kwa mbali shule za msingi zinazosimamiwa na serikali huku mapacha walioungana kiwili wili wa Makete wakifanya maajabu makubwa ya ufaulu.


Akitangaza matokeo ya mtihani wa darasa la saba leo mjini Njombe mwenyekiti wa kikao hicho cha kuchuja majina ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwakani 2011 katibu tawala wa mkoa wa Iringa Getrude Mpaka mbali ya kuzipongeza shule hiyo kwa kuuwezesha mkoa wa Iringa kuendelea kushika nafasi ya tatu ya ufaulu kitiafa bado alisema changamoto kubwa ni utoro wa wanafunzi zaidi ya 560 ambao hawakuweza kufanya mtihani huo .


Mpaka alisema kuwa takwimu za watahiniwa wa elimu ya msingi mwaka 2010 ni watahiniwa 44,275 kati yao wavulana ni 20,991 na wasichana ni 23,284 japo idadi ya watahiniwa waliofanya mtihani ni wavulana 13,709 na wasichana 14,190 ambapo ufaulu wao ni asilimia 63.01 wa watahiniwa wote.


Alisema kuwa mkoa wa Iringa umeongeza kiwango cha ufaulu kutoka asilimia 59.65 mwaka 2009 hadi kufikia asilimia 63.01 mwaka 2010 kutokana na kazi nzuri na ushirikiano uliofanywa na viongozi wa elimu kata ,wilaya na mkoa katika kuongeza jitihada za kupambana na changamoto mbali mbali ndani ya sekta ya elimu.

Pia alisema mkoa wa Iringa umeendelea kuwa na changamoto kubwa ya wanafunzi kutofanya mtihani kutokana na utoro kwa asilimia 75.19 ambapo wanafunzi wapatao 566 wameshindwa kufanya mtihani huo ukilinganisha na mwaka 2009 ambao wanafunzi 816 pia hawakufanya mtihani huo .

Aidha aliipongeza wilaya ya Kilolo kwa kuongeza juhudi zaidi ya ufaulu kwa kutoka asilimia 39.71 mwaka 2009 hadi kufikia asilimia 42.56 mwaka 2010 huku wilaya ya Iringa ikipanda kutoka asilimia 42.56 mwaka 2009 hadi asilimia 53,08 mwaka 2010 .

Mpaka alizitaja shule zilizofanya vizuri na kuwepo katika orodha ya shule tano bora kati ya shule 853 ndani ya mkoa wa Iringa kuwa shule ya kwanza ni Southern Highland (Mufindi ), ikifuatiwa na Broke Bond(Mufindi),Lingstone (Njombe mji) Star(Iringa mjini) na St.Dominic Savio (Iringa mjini).

Kwa upande wakeafisa elimu mkoa wa Iringa Salum Maduhu alisema kuwa kuwa kwa ujumla kiwango cha ufaulu ndani ya mkoa wa Iringa kwa mwaka huu kimezidi kuongezeka japo changamoto kubwa ni idadi ya wanafunzi wanaoanza darasa la kwanza kushindwa kufika mwisho.

Maduhu alizitaja shule 10 bora katika mkoa wa Iringa kuwa ni St. Benedict( Njombe mji),Southern Highland (Mufindi) Lingstone (Njombe mji) Ukombozi (Halmashauri ya Manispaa ya Iringa) LUpalama ‘A’) (Halmashauri ya wilaya ya Iringa), Lihogosa (njombe mji), Star (iringa mjini) LUgarawa (Ludewa) na shule ya 10 ni St.Dominic Savio (iringa mjini).

Huku shule 10 za mwisho kimkoa ni Mbalwe (Mufindi) Kipingu( Ludewa) Idunda ( Kilolo),Mholo (ludewa),Mfalasi (ludewa), MBongo(Ludewa), Luvungo(Ludewa),Ikulimambo (Njombe),Makangalawe( Makete) na shule ya mwisho ni Itonya iliyopo wilaya ya Kilolo.
Kwa upande wa Halamshauri iliyoongoza katika matokeo hayo ni Manispaa ya Iringa, Mufindi,Njobe mji, Halmashauri ya wilaya ya Njombe,Makete,Ludewa ,Halmashauri ya wilaya ya Iringa na Kilolo ikishika nafasi ya mwisho kimkoa japo imepanda katika ufaulishaji kwa mwaka huu uki linganisha na mwaka jana.


Wakati huo huo wanafunzi wawili wakazi wa wilaya ya makete ambao waliungana kiwili wili wamekuwa ni miongoni mwa wanafunzi waliofaulu vizuri mtihani huo wa taifa wa darasa la saba mwaka 2010,wanafunzi hao ni Consolatha Mwakikuti na Maria Mwakikuti ambao wote wamepata alama 151 huku wakitofautiana katika somo la Maharifa ya jamii kwa Consolatha kupata alama 29 na maria kupata alama 25 ,Sayansi Maria amemzidi Consolatha kwa kupata alama 31 kwa 29 kama ilivyo katika soko la kingereza ambalo Maria pia amemzidi Consolatha kwa kupata alama 36 kwa 34.


bofya

Share this article :

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA