Home » » ALIYESHINDA UDIWANI AKATAA KUENDELEA KUGOMBEA TENA

ALIYESHINDA UDIWANI AKATAA KUENDELEA KUGOMBEA TENA

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Tuesday, November 9, 2010 | 3:04 AM


Na Francis Godwin,Iringa
ALIYETANGAZWA mshindi katika uchaguzi mkuu kwa nafasi ya udiwani katika kata ya Mtwivila katika jimbo la Iringa mjini kupitia cha mapinduzi (CCM) Victor Mushi (pichani mwenye cheti ) amekataa kuendelea kugombea nafasi hiyo tena mara baada ya kumaliza kipindi chake kimoja cha miaka mitano.

Mushi alitoa kauli hiyo mbele ya wananchi wake katika ofisi ya afisa mtendaji kata ya Mtwivila leo wakati akiwapongeza wananchi wa kata hiyo walioandamana kwa ajili ya kumpongeza kwa kushinda katika uchaguzi mkuu na kukabidhiwa cheti chake cha kutambulika kama diwani mteule.

Alisema kuwa wapo baadhi ya watu ambao wanageuza nafasi wanavyopewa kama sehemu ya utawala wao wa maisha kwa wananchi na kuwanyima nafasi wanachama wengine ambao wanasifa ya kuongoza nafasi hizo jambo ambalo kwake halitakuwa hivyo na badala yake ataheshimu matakwa ya wananchi wa kata hiyo ambao wamemchagua kwa kipindi kimoja pekee na sio zaidi ya hapo.

"Ndugu zangu wananchi wa kata ya Mtwivila ambao mlinichagua kwa kura za kishindo katika uchaguzi mkuu uliofanyika octoba 31....naomba sana mzingatie kauli yangu hii leo ....kuwa sitagombea tena udiwani katika kata hii na wala sijaingia katika nafasi hii ili kuwa meya wa Manspaa ya Iringa ....mimi nimegombea kwa ajili ya kata hii na nitafanya kazi ndani ya kata yangu sina mpango wa kuwatelekeza japo baada ya miaka mitano kumalizika sitagombea tena udiwani kipindi hiki kimoja kinatosha sana"

Hata hivyo Mushi ambaye pia amepata kuwa mwenyekiti wa CCM wilaya ya Iringa mjini alisema kuwa pamoja na jimbo la Iringa mjini kuwa ni moja kati ya majimbo machungu wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu ila kwa upande wake hakuweza kucheza rafu kwa kutumia lugha chafu wakati wa kampeni zaidi ya kunadi sera za CCM.

Hivyo anaamini kabisa wananchi wa kata hiyo wale waliomchagua na wasio mchagua wataungana na kuwa kituo kimoja katika kuleta maendeleo ndani ya kata hiyo na jimbo la Iringa kwa ujumla.

Alisema kuwa katika uongozi wake atahakikisha anatanguliza mbele maslahi ya wakazi wa kata hiyo na CCM ili kuhakikisha kuwa wananchi wote wanaendelea kufanya kazi kwa uwazi na ushirikiano wa hali ya juu.

Mushi alisema kuwa kwa upande wake aliomba udiwani katika kata hiyo na sio jimbo la Iringa mjini na kuwa pamoja na kuwa anayosifa ya kuwa mstahiki meya wa Manispaa ya Iringa ila bado hayupo tayari kuchukua nafasi hiyo ambayo hajaiomba na kama watamtaka awe meya basi anaweza kufanya hivyo.
Share this article :

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA