Home » » MOHAMED GULAMI DEWJI AHAHIDI NEEMA JIMBO LA SINGIDA

MOHAMED GULAMI DEWJI AHAHIDI NEEMA JIMBO LA SINGIDA

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Saturday, September 25, 2010 | 2:13 AM


MO, akisistiza kuwa Katika kipindi cha miaka saba michezo imeweza kupaa katika mkoa wa singida ambapo Kindai Shoting, timu ya mkoa ilibeba kombe la kilimanjaro Taifa Cup kwa mara ya kwanza katika hiostoria ya mkoa huo.Na Mwandishi wetu.Singida.Mgombea ubunge kwa tiketi ya CCM, Mohamed Gulami Dewji, amesema endapo wananchi watampa ridhaa ya kuendelea kuwawakilisha tena bungeni, atatekeleza Ilani ya CCM kwa kasi zaidi ikiwemo kutafuta ufumbuzi wa namna ya kupunguza upungufu wa ajira kwa vijana.

Dewji alisema katika ilani uchaguzi, CCM imeainisha wazi kwamba inatambua tatizo la ajira na hasa ajira ya vijana wanaomaliza elimu ya msingi, sekondari na vyuo vikuu kila mwaka kuwa, ni kubwa mno.“Vijana hawa wote ni nguvu kazi ya taifa ambayo inaweza kutumika katika kazi na shughuli halali za ujenzi wan nchi yetu na ikapiga hatua kubwa ya kimaendeleo”,alisema Dewji. Mgombea huyo,alisema ili kukabiliana na tatizo hilo,CCM ina mpango wa kupanua mafunzo ya VETA yaweze kuchaukua vijana wengi zaid, ili waandaliwa kujiajiri wenyewe.Aidha, alisema vijana watahamasishwa kuanzisha miradi ya kiuchumi na kujiunga katika vikundi vya ushirika vya kuweka na kukopa (SACCOS) ili waweze kupata mikopo kwa masharti nafuu.“Katika miaka mitano iliyopita, nimewatafutia kazi vijana kutoka jimboni kwetu kwenye kiwanda changu cha nguo cha Afritex kilichopo mkoani Tanga., Kuajiri vijana hao, nimefanikiwa kwa kiasi fulani kupunguza idadi ya vijana wetu wanaomaliza elimu ya sekondari, kukaa vijiweni”,alisisitiza huku akishangiliwa na mamia ya wananchiDewji aliyasema hayo jana katika mkutano wa Kampeni zake, uliofanyika kwenye viwanja vya shule ya msingi Unyambwa.

Wakati huo huo,Dewji alitumia fursa hiyo kumwombea kura mgombea urais Jakaya Kikwete kwa madai kwamba ameonyesha uwezo mkubwa wa kusimamia utekelezaji wa ilani za uchaguzi.

Aidha, alimnadi mgombea wa udiwani wa kata hiyo, ya Unyambwa Salum Satu na kuomba apewe kura za kutosha kumwezesha kushika nafasi hiyo.
Share this article :

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA