Home » » MWENGE WA UHURU WAHAMASISHA MAENDELEO MUFINDI

MWENGE WA UHURU WAHAMASISHA MAENDELEO MUFINDI

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Tuesday, August 3, 2010 | 1:55 PM


Halmashauri ya wilaya ya Mufindi mkoani Iringa imeendelea kuunga mkono jitihada za serikali iliyopo madarakani chini ya Rais Jakaya Kikwete katika ukuzaji ajira ambapo halmashauri hiyo imeanzisha vikundi 56 vya uzalisai mali kwa vijana pamoja na kutenga fedha zaidi ya shilingi milioni 10 kwa lengo la kuvwezesha vikundi hivyo.

Haya yamo katika risala ya utii ya wananchi wa wilaya ya Mufindi kwa Rais Jakaya Kikwete iliyotolewa na mkuu wa wilaya hiyo Bi.Evarista Kalalu jana katika uwanja wa Mashujaa kwa kiongozi wa mbio za mwenge kitafa Dr Nassoro Ally Matuzya.


Mkuu huyo wa wilaya amesema kuwa wilaya hiyo imekuwa mbee katika kuywawezesha vijana ili kuboresha maisha yao na kuwa hadi sasa pamoja na vikundi hivyo pia kuna vikundi 180 vya wavulana na vikundi 100 vya wasichana

Bi Kalalu amesema kuwa hadi sasa mgawanyo wa mapato kwa vikundi hivyo umefikia kima cha chini cha mshahara wa serikali huku kasi ya vijana kuondoka katika vijiwe na kujiunga katika vikundi vya kiuchumi ikizidi kuongezeka zaidi.

Aidha amesema kuwa kumekuwepo mkakati wa kuviimarisha vikundi vilivyo anzishwa vikiwemo vile vya wanawake na watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI .

Kuhusu janga la UKIMWI amesema kuwa bado janga hilo kwa wilaya ya Mufindi ni changamoto kubwa na kuwa hadi sasa kasi ya maambukizi ni asilimia 16 huku wilaya ikiendelea na jitihada`za kupunguza kasi hiyo.

Mkuu wa wilaya amesema kuwa wananchi wa Mufindi kwa mwaka huu wameweza kuchangia uanzishaji wa miradi 14 ya mwenge yenye thamani ya shilingi kiasi cha zaidi ya shilingi Bilioni 1 huku wananchi wakichangia shilingi 297,626,000 na Halmashauri ya wilaya ikichangia na wahisani wakichangia shilingi 133,074,000 na serikali kuu imechangia shilingi 612,669,674.

Ameitaja miradi hiyo iliyoanzishwa kuwa ni pamoja na elimu,afya ,maji ,Kilimo na miundo mbinu na miradi mingine mingi ya kiuchumi.
Share this article :

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA