Home » » BREAKINGNEWzzzzzz WALIMU NA WANAFUNZI WAPANDWA NA MASHETANI WAANGUKA

BREAKINGNEWzzzzzz WALIMU NA WANAFUNZI WAPANDWA NA MASHETANI WAANGUKA

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Monday, August 9, 2010 | 9:55 AM


WANAFUNZI 33 na walimu wawili wa shule ya sekondari Lyandembela iliyopo kijiji cha Ifunda wilaya ya Iringa vijijini mkoani hapa leo walisitiza vipindi vya masomo kwa siku nzima baada a kukumbwa na ugonjwa wa ajabu wa kuweweseka na kuanguka .

Hata hivyo polisi walilazimika kufika shuleni hapo na kufanya kazi ya zaada ya kuwatawanya wanafunzi hao ambao walikuwa akitaka kuteketeza shule hiyo kwa moto pamoja na mkuu wa shule hiyo kwa madai kuwa ndie chanzo cha wao kupawa na ugonjwa huo.

Pamoja na ugonjwa huo kuwakumba wanafunzi hao na walimu bado wanafunzi zaidi ya 200 shuleni hapo waligoma kurudi nyumbani na badala yake kufanya fojo ikiwa ni pamoja na kufunga barabara za shule hiyo wakishinikia mmoja kati ya walimu shuleni hapo atolewe nje ili waweze kumwadhibu kwa kipigo wakidai kuwa ndio chanzo cha wao kuanguka.

Tukio hilo la wanafunzi kuanguka lilitokea majira ya saa mbili asubuhi mara baada ya wanafunzi hao kumaliza kuimba wimbo wa Taifa na wakiwa mbioni kuingia madarasani ghafla wanafunzi 10 kwa mpigo waliweza kuanguka huku wengine wakiangua vilio kabla na wao kuanza kuanguka .

Alisema mmoja kati ya walimu wa shule hiyo ambaye hata hivyo hakupenda jina lake kuandikwa gazetini kwa kuwa si msemaji wa shule hiyo,kuwa ndani ya dakika 20 jumla ya wanafunzi 33 na walimu wawili wa kike walikuwa wameanguka .

"Kweli kila mwanafunzi anapoanguka akiamka anaanza kuweweseka na kudai kuwa alikuwa nyumbani kwa mkuu wetu wa shule anafanya usafi mara alikuwa kwa mwalimu mwenzetu ambaye kwa sasa ni marehemu .....sasa wamekuwa wakitamka kila mmoja lake ila wengi wanamtaja mkuu wetu wa shule kuwa ndie anayewafanyia hivyo"

Wanafunzi waliokumbwa na ugonjwa huo wa kuanguka shuleni hapo ni pamoja na Christine Utenga,Dafroza Mtove, Benadetha Mduda, Candida Mfugale, Veronica Lulangasi,Elda Mwepela, Fotuatha Lyandala, Jovitha Nyalusi , Robetha Ngwaulanga, Gresy Samwel, Tea Mazi, Tiba Nyaluke, Mary Samwel, Agnes Kanyika, Jelda Mgumba, Helema Seudwa, Esta Komba, Goletha Dominick ,Huruma Kivovele, Lela Joas na Coretha Kibuga.


Wengine ni Devotha Mfugale, Asia Mazengo, Jane Lunyungu, Jovita Logo, Jane Daudi, Grace Kidugo,Tulakela Ngulo, Ephesi Mpinge, Silivia Kisinini,Winfrida sanga, Mwaija Kisinda , kaka mkuu wa shule hiyo Nickson Bange huku walimu ni Faraja Ngakonda na Araph Kalembo.


Hata hivyo kutakana na wanafunzi na walimu wa shule hiyo kukumbwa na tatizo hilo la kuanguka uongozi wa elimu mkoa wa Iringa ukiongowa na afisa elimu takwimu mkoa wa Iringa Leonard Msigwa pamoja na vyombo vya ulinzi na usalama umefika shuleni hapo na kufanya kikao na walimu wa shule hiyo na viongozi wa serikali ya kijiji na kuamua kumsimamisha mmoja kati ya walimu na nafasi yake kupewa kwa muda aliyekuwa mkuu wa shule na nafasi yake kukaimishwa Cyprian Mwasallah ambaye alikuwa ni makamu mkuu wa shule hiyo.

Pamoja na kumsimamisha mkuu huyo wa shule hiyo bado viongozi wa dini waliofika shuleni hapo walidai kuwa pamoja na kuwa mkuu huyo wa shule kutajwa kuwa ni chanzo cha wanafunzi na walimu kuanguka ila bado inaonyesha viongozi wa dini wamechangia tatizo hilo baada ya kuwafanyia maombezi na kuwatoa mapepo wanafunzi hao huku wao wenyewe wakiwa hawana upako wa kufanya hivyo.

Alisema mchungaji wa kanisa la EAGT Ifunda mchungaji Eziekiel Mbwela kuwa hivi sasa kila kiongozi wa dini amekuwa akiigiza kufanya kazi ya kutoa watu mapepo na badala yake hukuza tatizo kwa wale anaowatoa kutokana na yeye mwenyewe kutokuwa na uwezo wa kuombea zaidi ya kkuombewa hivyo alitaka serikali kuchunguza utendaji kazi wa makanisa hayo.

"Ujue toka wanafunzi hao walipoanza kwenda katika kanisa moja kijijini hapa jina hatulitaji kwa sasa wameanza kuanguka na kutamka maneno ya ajabu wakati awali hali hii haikuwepo kabisa"

Share this article :

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA