Home » » USHINDI WA DR.SHEIN MASHAKANI KUIGAWA CCM VISIWANI ......

USHINDI WA DR.SHEIN MASHAKANI KUIGAWA CCM VISIWANI ......

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Saturday, July 10, 2010 | 11:28 PM


USHINDI wa kura 117 alioupata mgombea urais wa CCM kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Zanzibar Dr.Alli Mohamed Shein juzi usiku dhidi ya wapinzani wake watatu unaweza kusababisha mpasuko mkubwa ndani ya chama hicho baada ya wajumbe kutoka Unguja kuamua kuchana fulana zao za chama wakipinga Dr.Shein kuwa mgombea wa CCM na wale kutoka Pemba wakionyesha kupendezwa na ushindi wa Dr.Shein.

Pamoja na uchaguzi huu kwa wa chama kimoja ulioshirikisha wajumbe kutoka bara na visiwani bado yalizuka makundi ya uunguja ,upemba na ubara mara baada ya matokeo hayo kutangazwa mjini hapa majira ya saa 3 usiku.

Wakizungumza kwa jazba nje ya makao makuu ya CCM mjini Dodoma wajumbe kutoka ugunja walisema kuwa kuchaguliwa kwa Dr.Shein kuwa mgombea nafasi ya urais ni mwanzo wa kuisambaratisha CCM katika visiwa hivyo na kuwa wana kama wana CCM wapo tayari kumchagua mgombea urais wa upinzani na sio Dr.Shein wa CCM.

Walisema kuwa hatua ya uchujaji wa majina hayo ya wagombea kufanyika bara mjini Dodoma badala ya Zanzibar ni jambo ambalo kwao kama wana CCM wamelifananisha na njama za viongozi wa juu wa CCM ambao wametumia nguvu zaidi ya kuhakikisha mtu wao Dr .Shein anapita na kuwa wao wanatambua kuwa chaguo lao ni Dk Gharib Alli Bilali kutoka unguja na sio Dr.Shein kutoka Pemba.

Kwani walisema kuwa Dr.Bilal ni kijana wao na kiongozi aliyetukuka kwa uongozi na muda wote amekuwa Zanzibar na kujiandikisha huko na sio Dr.Shein ambaye hata kujiandikisha hajajiandikisha Zanzibar na wakati sheria za uchaguzi na mgombea zinamtaka mzanzibar mkazi na sio Mzanzibari wa kuja .

"Tena tunasema hata hotuba ya mwenyekiti wa CCM Taifa na mgombea urais wa CCM bara Rais Jakaya Kikwete inaonyesha wazi kumbeba Dr.Shein na bila hotuba yake wajumbe wangeweza kumpigia kura Dr .Bilal ambaye ni chaguo letu....ila hotuba yake na wajumbe wa bara ndio wamemchagua Dr.Shein na sio wazinzibar " walisema wajumbe hao huku baadhi yao wakichana fulana za kikwete Chaguo letu na chagua CCM ambazo walikuwa wamevaa.

Huku wajumbe wa mkutano mkuu kutoka Pemba wakieleza furaha zao kwa kuchaguliwa Dr.Shein kuwa atasaidia kukisambaratisha chama cha wananchi (CUF) Pemba kutokana na mgombea huyo kuwa tishio huko Pemba.

Hata hivyo alisema kuwa hatua ya wajumbe hao kutoka unguja kuchana fulana zao za CCM ni kutokana na makundi yaliyokuwepo na wagombea hao na kuwa Dr.Shein atafanikisha kuvunja makundi ya upenda na uunguja na sio mwanachama mwingine.

Mwasisi wa Tanu na CCM mzee Tasili Mdoga akizungumzia mchakato huo wa kumpata mgombea urais Zanzibar kupitia CCM Dr.Shein alisema kuwa makundi hayo yanatokana na jazba za muda za watu wao kushindwa ila ukweli kuchaguliwa kwa Dr.Shein kati ya wana CCM 11 ni hatua nzuri na kuwa kiongozi huyo ni msafi kuliko na hajapata kuwa na tuhuma yeyote mbaya ambayo imepata kumgusa wala kukigusa chama na serikali kupitia kwake.

Mzee Mgoda alisema kuwa kabla ya kushika ukamaku wa Rais na baada ya kuwepo katika nafasi hiyo wao kama wazee wamekuwa wakimchunguza mwenendo wake ambao umejionyesha sasa mjini hapa.

Hivyo alisema kuwa kwa kampeni za uchaguzi mkuu mwaka huu kampeni kwa CCM hazitakuwa ngumu kutokana na wapemba kwa mara ya kwanza kumtoa mgombea urais na kumaliza kilio chao cha siku nyingi cha kukosa mgombea wa nafasi hiyo na kuwa ni vyema makundi kuvunjwa na kuwa kundi moja na watu wamoja wazanzibar na sio wapemba na unguja.

Wakati huo huo wagombea ubunge wa nafasi mbali mbali ambao walitaka kuvamia mkutano mkuu huo wa CCM bila kuwa na vitambalusho jana wameumbuka baada ya kuzuiliwa kupita getini bila kuwa na vitambulisho huku mgombea ubunge wa CCM jimbo la Mufindi kusini Michael Mlonganile akilazimika kwenda makao makuu ya CCM kuomba kitambulisho hicho na wengine wakilazimika kukaa nje ya geti hilo kwa kukosa kitambulisho.

Katika mchakato huo Dr.Shein aliwabwaga wapinzani wake kwa kupata kura 117 huku Dr.Bilal akiambulia kura 54 na Shams Vuai Nahodha akipata kura 33 kati ya kura 204 zilizopigwa.
Bofyahapa
Share this article :

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA