Home » » HII INASIKITISHA SANA.......!!?

HII INASIKITISHA SANA.......!!?

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Wednesday, July 14, 2010 | 2:52 AM


Idadi ya watu waliokufa katika mashambulio mawili ya mabomu yaliyotikisa wakati mashabiki wakiangalia mechi ya fainali ya Kombe la Dunia mjini Kampala huko Uganda, imeongezeka kufikia 74, maafisa wanasema.

Watu wengine 70 walijeruhiwa katika mashambulio hayo yaliyolengwa klabu ya mchezo wa raga ya Kampala na mgahawa mmoja wa vyakula vyenye asili ya Ethiopia.

Ingawa wanamgambo wa Al Shabab wamekiri kuhusika, polisi wanachunguza endapo walifanya mashambulio ya kujitolea muhanga.

Kulinda amani

Wanajeshi wa kulinda amani wa Uganda wanatumikia nchini Somalia, na al-Shabab wametishia kushambulia Kampala katika siku zilizopita.

Takriban askari 5,000 wa kulinda amani wa Umoja wa Afrika kutoka Uganda na Burundi wapo Mogadishu kusaidia serikali ya mpito ambayo si imara.

Jeshi la AU nchini Somalia (Amisom) limekuwa likikabiliwa na mashambulio ya mara kwa mara kutoka kwa wanamgambo wanaodhibiti sehemu kubwa ya kusini na katikati ya Somalia.

Mashambulio yote mawili yalisababisha vifo na majeraha, ingawa watu wengi zaidi walikufa kwenye klabu ya mchezo wa raga, ambako mashabiki walikuwa wakifuatilia mechi hiyo kupitia skirini kubwa,Mpendwa mdau wa mtandao huu nakuomba radhi kwa picha hii ya kusikitisha japo tuzidi kuwaombea wote waliopoteza maisha katika tukio hili

Share this article :

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA