Home » » CCM MKOA WA IRINGA KUWAFUTA WAGOMBEA UBUNGE WAONGO

CCM MKOA WA IRINGA KUWAFUTA WAGOMBEA UBUNGE WAONGO

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Sunday, July 18, 2010 | 8:07 AM
CHAMA cha mapinduzi (CCM) mkoa wa Iringa kimepiga marufuku wagombea wa nafasi za ubunge katika majimbo mbali mbali ya mkoa huo kuendesha kampeni za kuchafuana pamoja na kudanganya wanachama kuwa wametumwa na Rais Jakaya Kikwete kuja kugombea nafasi za ubunge jambo ambalo si la kweli na yeyote atakayebainika kukiuka kanuni za chama ataenguliwa katika kinyang’anyiro hicho hata kama atashinda katika kura za maoni.

“ Wapo baadhi yenu wanapita mitaani na kusema kuwa wametumwa na Mheshimiwa Rais Jakaya Mrisho kikwete kuja kugombea nafasi na kuwachafua wengine kuwa hawafai …kwa taarifa yenu hakuna hata mgombea mmoja ambaye ametumwa na Rais Kikwete kwenda kugombea jimbo lelote la Tanzania na Rais hawezi kumtuma mwanachama kuja kugombea”

Katibu wa CCM mkoa wa Iringa Mary Tesha na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa Deo Sanga walitoa kauli hiyo leo mjini Mafinga katika ukumbi wa BP Kangesa wakati wa semina ya pamoja ya wagombea wote wa nafasi za ubunge viti maalum na majimbo 11 ya uchaguzi mkoani hapa.

Viongozi hao walisema ni marufuku kwa mgombea yeyote wa CCM kutumia vibaya jina la Rais Kikwete katika kampeni zake ikiwa ni pamoja na kutumia jina hilo kudanganya wanachama kuwa wanagombea baada ya kutumwa na kiongozi huyo na mwenyekiti wa CCM Taifa.

Walisema kuwa kulitumia jina la Rais Kikwete vibaya na kufanya kampeni za kupakana matope ni mwanzo wa kukichafua chama hicho na kuwa yoyote atakayebainika kukiuka hatafumbiwa macho atafuntwa katika orodha ya wagombea ubunge .

Hata hivyo Katibu huyo wa CCM mkoa wa Iringa alisema kuwa chama kimeruhusu wanachama wake kutumia vipeperushi katika kampeni ila hakiruhusu vipeperishi vya kuchafuana kutumika katika kampeni hizo.

Pia alisema kuwa kwa upande wa wabunge na mawaziri pamoja na kuwa zoezi la uchukuaji fomu linaanza leo nchi nzima ila bado wataendelea kuheshimiwa kama wabunge na mawaziri hadi bunge litakapovunjwa rasimi na hadi Rais mpya atakapoapishwa .

Aidha alisema kuwa utaratibu wa kampeni kwa wagombea wote watatumia gari moja na kuwa kwa mgombea ambaye atakuwa na gari lake ataruhusiwa kuingia nalo katika msafara japo wagombea wote hawataruhusiwa kuruidi nyuma baada ya kumaliza kujieleza na wapambe wao hawaruhusiwi wala mbwembwe wakati wa kuchukua na kurejesha fomu hazitaruhusiwa .

Kuhusu CV za wagombea katibu huyo alisema wagombea hawana sababu ya kudanganya sifa zao na badala yake kueleza ukweli na kuwa sifa ya mgombea udiwani na ubunge wa CCM ni yule anayejua kusoma na kuandika na kuwa japo nakala halisi ya vyeti vya wagombea zinahitajika kuwasilisha ofisi za chama wilaya wakati wa kurejesha fomu.

Mwenyekiti wa CCM mkoa Sanga alisema kuwa ni vyema wagombea wote kujenga utamaduni wa kupendana bila kuchafuana ili kukijenga chama badala ya kuendesha kampeni za kuchukiana na kupakana matope na kuwa mgombea mwenye tabia hiyo hana sifa ya kuwa mbunge wa CCM.

Kwa upande wao wagombea hao zaidi ya 50 waliojitokeza kugombea majimbo 11 ya uchaguzi na nafasi za ubunge viti maalum katika mkoa wa Iringa na Njombe walieleza kufurahishwa kwao na hatua ya CCM mkoa kutoa semina kabla ya kuchua fomu hizo.

Japo kwa upande wake mbunge wa Njombe kaskazin Jackson Makweta alisema kuwa kwa upande wake anapingana na hatua ya chama kutaka wagombea kupeleka vyeti halisi na kuwa wengi wao walisoma shule za zamani na kama wanataka kujua ukweli wa elimu yao ni vyema kufuatilia katika shule walizo soma.

Huku kwa uoande wake mgombe ubunge wa jimbo la Iringa mjini Frederick Mwakalebela ,mgombea ubunge jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe na mgombea ubunge jimbo la Njombe Magharibi Thomas Nyimbo walimepongeza hatua hiyo na kuwa itawawezesha wagombea wote kupata haki sawa na japo hatua ya wagombe kuendelea kuitwa waheshimiwa hadi Augost 2 ni moja ya hatua ya kuwabeba wabunge hao.
Share this article :

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA