Home » » BREAKINGNEWZzzzzz MWAKALEBELA AACHA PENGO TFF ANG'ATUKA RASMI LEO ,RAIS AMWOMBEA USHINDI JIMBO LA IRINGA MJINI

BREAKINGNEWZzzzzz MWAKALEBELA AACHA PENGO TFF ANG'ATUKA RASMI LEO ,RAIS AMWOMBEA USHINDI JIMBO LA IRINGA MJINI

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Thursday, July 15, 2010 | 6:27 AMMlimani TV hawapo nyuma katika kuhabarisha umma ,hapa wakimchukua Rais wa TFF Tenga wakati akieleza sifa za Mwakalebela kushoto ambaye anakwenda kugombea ubunge jimbo la Iringa mjini
Wengi washindwa kuamini kuondoka kwa Mwakalebela japo wamwombea ushindi katika kinyang'anyiro cha ubunge jimbo la Iringa mjini

Wanahabari wakiwa wamepigwa na butwaa kuondoka kwa Mwakalebela TFF wasema kibarua kumpata atakayefanana na yeyeMwakalebela (kulia) akiwaaga wanahabari
Wanahabari wakiwa hawaamini


Wapiga picha za habari wakichukua kumbukumbu zao za mwisho ya picha za MwakalebelaRAIS wa Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) Leodegar Tenga leo amemuaga aliyekuwa katibu mkuu wa TFF Frederick Wilfred Lameck Mwakalebela ambaye anakwenda kugombea ubunge jimbo la Iringa mjini kupitia chama cha mapinduzi (CCM) na kuwa wao kama TFF wamempoteza kiongozi mchapa kazi na kuwa wakazi wa jimbo la Iringa mjini wakimchagua Mwakalebela watakuwa wame mpata mbunge mchapa kazi.

Rais Tenga amemumwagia sifa hizo Mwakalebela leo katika ukumbi wa TFF mbele ya wanahabari wakati wa hafla fupi ya kumuaga katibu huyo ambaye amepelekea Taifa kupata heshima kubwa katika soka kutokana na utendaji kazi wake mzuri.

Alisema kuwa kuwa kuondoka kwa Mwakalebela TFF ni jambo la kupongweza ndani ya TFF kuwapata wanamichezo wabunge ambao watakwenda kutetea michezo bungeni ila bado Mwakalebela alikuwa ni kichwa chenye uwezo wa kubuni na kuchapa kazi ilivyo ndani ya TFF.

"Kweli mimi kama Rais wa TFF kwa niaba ya kamati ya utendaji na wanamichezo wote Tanzania na Afrika tunampongeza sana Mwakalebela kwa kwenda kugombea ubunge jimbo la Iringa mjini ila pia tunamuombea dua ili ashinde nafasi hiyo ....mimi namfahamu vyema Mwakalebela ni mpole na mchapa kazi asiyependa majivuno"alisema Tenga huku akionyesha dalili za kutokwa na machozi ya huzuni kwa kuondoka katibu huyo TFF.

"Nasema tutaendelea kumtumia Mwakalebela kama mdau wetu mkubwa wa TFF hata pale atakapokuwa mbunge katika jimbo la Iringa mjini ...ila zaidi tutamtumia hata bungeni pia kama atashinda ubunge jimbo hilo"

Kuhusu hatua ya Mwakalebela kugombea ubunge na kuacha kiti hicho alisema kuwa wao kama TFF wanampongeza na hawaoni kama ni kosa kwa Mwanataalum kugombea ubunge kwani kazi anayokwenda kuifanya ni uwakilishi wa wananchi kama ilivyo kuwa TFF japo katika ubunge atafanya mengi zaidi kwa Taifa na wananchi wake.

Hivyo Tenga aliwaomba wanahabari na wakazi wa jimbo la Iringa mjini kumuunga mkono katibu huyo ili aweze kushinda kwa kishindo nafasi hiyo ambayo anagombea .

"Nasema kuwa Mwakalebela sisi tunamgombea na tunaomba wana Iringa pia waweze kutuunga mkono kwa kumpokea kwa mikono miwili ili aweze kuwa mbunge katika jimbo hilo"

Kwa upande wake Mwakalebela akiwashukuru wanahabari na TFF kwa kumpa baraka za kugombea ubunge jimbo hilo alisema kuwa jumatatu anataraji kuchukua fomu ya kugombea ubunge jimbo hilo.

Hivyo alipongeza ushirikiano mkubwa kwa wanahabari ambao wamepata kuonyesha kwake na kuwa akiwa mbunge wa jimbo hilo kubwa analotegemea kufanya ni kupigania maendeleo ya wana Iringa na kurejesha heshima ya kasi ya uzalishaji wa mazao katika mkoa wa Iringa.

Huku akiwataka wana Iringa kuunganisha umoja wao ila kuungana na wakazi wa Iringa wanaoishi nje ya jimbo hilo katika kujiletea maendeleo na kumuunga mkono katika kugombea ubunge jimbo hilo ambalo linaongozwa na Monica Mbega ambaye ni mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro anayemaliza muda wake wa ubunge wiki hii.BOFYAHAPA
Share this article :

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA