Home » » ASKARI WA FFU IRINGA AJIPIGA RISASI MBILI HADI KUFA AKIWA IKULU

ASKARI WA FFU IRINGA AJIPIGA RISASI MBILI HADI KUFA AKIWA IKULU

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Friday, July 9, 2010 | 6:28 AM


SIKU chache baada ya askari wa kike Tarime mkoani Mara kujiua kwa kujipiga risasi baada ya kuupoteza msafara wa Rais Jakaya Kikwete askari mwingine kutoka Musoma mkoani humo mwenye namba G 13 PC Mashauri (24) wa kikosi cha kutuliza ghasia (FFU) Iringa amejiua kwa kujipiga risasi Ikulu ndogo nyumbani kwa mkuu wa mkoa Iringa kwa kile kinachosadikika kuwa ni wivu wa kimapenzi.

Imedaiwa kuwa askari huyo alikuwa na mpenzi wake wa kike na juzi majira ya usiku alimfumania mpenzi wake huyu ambaye alikuwa ameachana naye kwa zaidi ya miezi miwili akiwa na mwanaume mwingine ambaye ni mfanyakazi wa taasisi ya Bay Port dare s Salaam.

Akithibitisha kutoka kwa tukio hilo kamanda wa polisi wa mkoa wa Iringa (ACP) Evarist Mangalla alimweleza mwandishi wa habari hizi kwa njia ya simu kuwa askari huyo alijiua mwenyewe kwa kujipiga risasi mbili chini ya kidevu chake jana Julai 8 majira ya saa 3 usiku akiwa lindoni eneo la Ngangilonga nyumbani kwa mkuu wa mkoa wa Iringa Mohamed Abdulaziz.

“ Ni kweli kuna tukio la askari huyo mwenye namba G 13 kujiua kwa kujipiga risasi mbili shingoni katika eneo la makazi ya mkuu wa mkoa wa Iringa baada ya kumnyang’anya bunduki askari mwezake aliyekuwa amepangiwa lindo hilo”

Kamanda Mangalla alisema sababu za skari huyo kujiua ni wivu wa kimapenzi dhidi ya mpenzi wake wa zamani WP7137 Zuhura ambae pia ni askari mwenzake.

Alisema kuwa akari huyo kabla ya kujiua alikuwa amepangiwa lindo katika Banki ya CRDB, lakini alicha lindo hilo na kwenda nyumbani kwa mpenzi wake huyo wa zamani anaeishi kihesa mtaa wa mafifi na alipofika huko alimkuta mwanaume aliyetambulika kwa jina la Sanday Tumaini ambaye ni mfanyakazi wa Banki ya bay port Dar e Salaam na kuanza kuwatishia kuwapiga risasi wote wawili kabla ya mwanamke huyu kufanikiwa kumpokonya silaha hiyo.


“Kabla Mashauri hajafyatua risasi mpenzi wake huyo kwa ujasiri alinyang’anya silaha hiyo na kupiga makelele na baada ya kuzidiwa na wananchi kufika eneo hilo PC Mashauri alikimbia alikimbia na kuacha silaha hiyo mikononi mwa mpenzi wake huyo….silaha ambayo alikuwa ameichukua kwa ajili ya kwenda katika lindo benk…”

Hata hivyo alisema baadae askari huyo alikwenda katika makazi ya mkuu wa mkoa ambako askari wenzake walikuwa wamepangiwa lindo na alipofika alianza kuongea nao, ghafla alimrukia askari aliyekuwa na bunduki na kunyang’anya bunduki kisha kufyatua risasi hewani na hatimae na mwezake huyo kutimua mbio kuhofia usalama wake na nyuma Mashauri aliamua kujiua kwa kujipiga risasi mwenyewe.

Mwili wa askari huyo umehifadhiwa katika chumba cha maiti hospitali ya mkoa wa Iringa ukisubiri kusafirishwa kwenda nyumbani kwao Musoma kwaajili ya mazishi na hakuna mtu anayeshikiliwa na jeshi la polisi kwa tukio hilo.

“Amejiua mwenyewe hatuwezi kumshikilia mtu yeyote katika hili ….kwani nyumbani kwa mwanamke ulitokea ugomvi na baada ya kushindwa aliamua kukimbia kwenda kwa mkuu wa mkoa katika lindo ambalo hata hivyo halikuwa lake na kwenda kupokonya silaha na kujiua”
Bofya hapa
Share this article :

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA