Home » » MZAZI ASEMA CCM IKIMPITISHA MTOTO WAKE ASKOFU KUGOMBEA UBUNGE ATAHAMA JIMBO

MZAZI ASEMA CCM IKIMPITISHA MTOTO WAKE ASKOFU KUGOMBEA UBUNGE ATAHAMA JIMBO

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Saturday, June 12, 2010 | 2:06 AM


WAKATI mwamko kwa wataalam mbali mbali kujitokeza kutangaza kuwania ubunge na udiwani ndani ya chama cha mapinduzi (CCM) na vyama vya upinzani kuzidi kuwa mkubwa katika majimbo mbali mbali hapa nchini baba mzazi wa msaidizi wa askofu katika kanisa la kiinjli la Kilutheri Tanzania (KKKT) Njombe askofu Isaya Mengele mzee Japhet Lumuliko Mengele (pichani) amemtaka mtoto wake huyo kutoa gombea ubunge katika jimbo la Njombe Magharibi na kuwa iwapo atagombea na kushinda kwa upande wake atahama jimbo hilo .

Mzee huyo ambaye ni mwenyekiti mstaafu wa kijiji cha Kanamalenga Njombe ametoa kauli hiyo leo wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na hali ya kisiasa ndani ya CCM katika jimbo hilo na idadi kubwa ya wagombea kujitokeza kutoka kupambana na mbunge wa sasa wa jimbo hilo mbunge Yono Kevella(CCM).

Alisema kuwa haoni sababu ya mtoto wake huyo ambaye ni mtumishi wa Mungu ambaye amekuwa akiheshimika na ikutegemewa na kanisa kama msaidizi wa askofu kuacha kulitumikia kanisa na kukimbilia katika siasa ambayo kimsingi hataiweza .

"Mimi hapa nilipo nina matatizo ya macho na nyumba ambayo ninaishi nikiwaonyesha waandishi mnaweza msiamini kama mimi nina mtoto ambaye ni msaidizi wa askofu ....sasa kama mwanangu ameshindwa kunisaidia mimi baba yake ataweza kuwasaidia wakazi wa jimbo la Njombe Magharibi ....kweli naomba asigombee kabisa ubunge na kama atagombea na kushinda basi mimi nitahamia jimbo la Njombe kusini kwa mbunge wake Anna Makinda "

Alisema kuwa atalazimika kuhama jimbo hilo kutokana na kumwogopa mtoto wake huyo kuwa kiangozi katika jimbo hilo kwa madai kuwa iwapo kwa sasa ambavyo si kiongozi wa serikali amekuwa hamsaidii pale atakapokuwa kiongozi itakuwaje.

Mzee Mengele alisema kuwa lazima wakazi wa jimbo la Njombe magharibi na majimbo mengine ya Tanzania kuwa makini wataalam wakiwemo viongozi wa dini ambao wanakimbia makanisa na kuutaka ubunge ama udiwani .

Kwani alisema ili kujua kama kweli viongozi hao wanaokimbilia kwenye siasa kama wana mapenzi mema na wananchi wao ni vizuri kuwachunguza walichokifanya katika sehemu zao za kazi .

Akielezea kuhusu mtazamo wa wazee katika jimbo hilo la Njombe Magharibi dhidi ya mbunge wa sasa Kevella na wagombea wengine ambao wameendelea kujitokeza kutaka kugombea ubunge katika jimbo hilo alisema kuwa ni haki ya kila wana CCM kujitokeza kuomba kuchaguliwa na kuchagua japo aliwataka wapiga kura wa jimbo hilo la kuwa makini na wagombea hao wanaojitokeza kwa sasa .

Alisema kwa upande wao kama wazee bado wanaimani kubwa na mbunge wao wa sasa mbunge Kevella na kuwa iwapo kuna mapungufu ameyafanya wanaamini wanaweza kumrekebisha .

"Hivi mwaka 2005 tulipokuwa katika uchaguzi CCM walisema tuchague mafiga matatu kwa maana ya diwani ,mbunge na Rais Jakaya Kikwete ....sasa iweje leo tubadilishe mawifa mawili na kuliacha figa moja Rais kwani kama diwani ama mbunge hafai ni wote watatu hawafai ila kama Rais anaongezewa muda basi hata wagunge wa CCM wasipingwe"alisema mzee huyo

Share this article :

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA