Home » » MISS ILULA -KILOLO 2010 YAFANYIKA KILOKOLE HAKUNA MAVAZI YA AIBU

MISS ILULA -KILOLO 2010 YAFANYIKA KILOKOLE HAKUNA MAVAZI YA AIBU

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Sunday, May 9, 2010 | 6:16 AM


Mshindi wa taji la Miss Ilula wilaya ya Kilolo mwaka 2010 Diana Beny (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na mshindi wa pili Ziada Mbega na mshindi wa tatu Catherin Kisinda mara baada ya kutangazwa juzi jumamosi usiku na Chifu jaji mwanahabari Edo Bashir ambaye ni mratibu wa Miss Iringa kwa miaka 8 mfululizo
MSHIRIKI Diana Beny amefanikiwa kutwaa taji la Miss Ilula katika shindano lililofanyika jumamosi usiku ambalo ni shindano la pili kufanyika toka wilaya hiyo ilipoanzishwa miaka kwa zaidi ya miaka 6 sasa.

Shindano hilo la aina yake lilipambwa na burudani kali kutoka kwa msanii wa muziki wa kizazi kipya hapa nchini kutoka jijini Dar es Salaam Joseline wasanii wa chipukizi kutoka Ilula huku msanii maarufu wa comedy nchini kutoka kundi la Enye Athuman Mussa a.k.a Mwalubadu akipagawisha mashabiki kwa upande wa U MC.

Katika shindano hilo ambalo jumla ya washiriki 6 walipata kushiriki akiwemo mshiriki ,Diana Beny na Ziada Mbega ,Catheline Kisinde,Mary Mgimwa ,Suma Mushi na Pili Abdulaaman wakionyesha kuchuana vikali katika upande wa ubunifu wa mavazi tofauti na ilivyotegemewa na wengi kuwa yawezekana washiriki hao wangechumka katika shindano hilo.

Chifu jaji Bashir katika shindano hilo alipata kuwauliza swali moja pekee washiriki watano waliopata kuingia tano bora baada ya mshiriki Pili Abdulaaman kuchemka mapema .

katika swali lake hilo Bashir alitaka kujua iwapo washiriki hao watashinda taji la Miss Ilula kitu gani ambacho watabadilisha katika mji huo ,swali ambalo washiriki walionyesha kujikanyaka kupitia kiasi kuweza kulijibu ukiacha mshindi Diana Beny ambaye ambaye alisema cha kwanza na kutoa elimu kwa vijana juu ya janga la UKIMWI ,elimu na uzazi wa mpango na kupigania wodi ya akina mama wajawazito katika eneo hilo pamoja na kutafuta ufumbuzi kero ya maji katika mji huo.

Akitangaza matokeo hayo Bashir alimtaja Diana Beny kuwa mshindi wa kwanza akifuatiwa na Ziada Mbega pamoja na Catheline Kisinde aliyepata nafasi ya tatu .

Huku nafasi ya nne ikichukuliwa na Mary Mgimwa nafasi ya tano Suma Mushi .

Awali ofisa utamaduni wilaya ya Kilolo Stephan Sanga akimkaribisha mratibu wa onyesho hilo Philimon Elias alisema kuwa wilaya hiyo imepiga hatua kubwa kwa kuendesha shindano hilo ambalo ni la pili kufanyika ambapo shindano la kwanza lilifanyika mwaka 2002.

Kwa upande wa mratibu wa onyesho hilo Elias alisema kuwa shida kubwa katika onyesho hilo ilikuwa ni kuwapata washiriki ambapo wazazi walikuwa wakiwazuia watoto wao kushiriki kwa madai kuwa shindano hilo ni uhuni jambo ambalo halina ukweli wowote.

Huku mgeni rasmi katika shindano hilo ofisa maendeleo ya jamii wilaya ya Kilolo Eriko Kawanga akiwapongeza waandaaji wa onyesho hilo pamoja na zawadi ya DVD na shilingi 10,000 kwa mshindi wa kwanza na pasi la umeme na shingili 10,000 kwa msindi wa tatu pamoja na saa na mkononi na shilingi 10,000 kwa mshindi wa tatu huku washiriki wote wakiambulia kifuta jasho cha shilingi 10,000 kila mmoja.
Share this article :

+ comments + 1 comments

May 20, 2010 at 3:14 AM

Big - Up na miji midogo mingine iige. Ili kila mdau ajue kuwa U-miss siyo uhuni na si lazima kuwepo na mavazi ya aibu!

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA