Home » » MAANDALIZI YA MWISHO KAMBI YA MISS IRINGA

MAANDALIZI YA MWISHO KAMBI YA MISS IRINGA

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Thursday, May 20, 2010 | 7:54 AMMsanii wanne star akiwanoa warembo hao


WASHIRIKI wa taji la Voda com Miss Iringa walivyojiandaa kupanda jukwaani kesho ili kuanza safari ya kuelekea katika shindano la kumpata mrembo wa Voda Com Miss Tanzania mwaka 2010 ambapo Iringa imejihakikishia kutwaa taji hilo.

Mkoa wa Iringa ambao kihistoria haujapata kutwaa taji la Taifa la urembo kutokana na washiriki wake kushindwa kujiandaa vya kutosha na wengi wao kushindwa kupata wadhamini wa kuwasaidia gharama za mavazi ,mwaka huu washiriki hao wameonyesha kuja kivingine zaidi baada ya kujiandaa vya kutosha tofauti na miaka ya nyuma.

Maaandalizi makubwa yamefanyika na warembo hao pamoja na waandaaji wa shindano hilo kwa miaka nane mfululizo sasa Radio Ebony FM ambapo wameendelea kuboresha kambi za washiriki hao na kuzifanya kuwa kambi zenye hadhi ya urembo kinyume na miaka mingine ambapo washiriki wamekuwa wakitokea makwao ama kukaa kambini mjini.

Shindano hilo la kumsaka Voda Com Miss Iringa ambalo kwa miaka zaidi ya miwili sasa linadhaminiwa na kampuni ya simu za mkononi Voda Com bado idadi ya wadhamini kwa mwaka huu ndani ya mkoa ni kubwa zaidi anasema mratibu wa shindano hilo Edo Bashir .

Anasema kuwa hadi sasa wadhamini ni pamoja na Hoteli ya Star Com KItonga, kampuni ya Kinywaji baridi cha Pepsi,TBL kupitia kinywaji cha Redes,Nems Collection na Net Saloon .

Bashir anasema kuwa washiriki wa mwaka huu ambao wanataraji kupanda jukwaani leo ni washiriki wenye uzoefu wa kutosha katika masuala ya urembo tofauti na miaka mingine ambapo kambi ya mafunzo huwa ngumu zaidi kutokana na uelewa mdogo wa washiriki .

Amesema kuwa mkakati wa mkoa ni kutwaa taji la Voda Com Miss Tanzania na kuwa mkakati huo umeenda sambamba na kuwaandaa washiriki wenye elimu ya kutosha ambao wanaweza kumudu ushindani katika kinyang’anyiro cha kumsaka mrembo wa Taji la kanda na lile la Taifa.

Hivyo alisema idadi kubwa ya washiriki ni wale waliohitimu elimu ya sekondari na vyuo na kuwataja washiriki hao kuwa ni pamoja na Mary Kigali(20) Mary Mgimwa(20),Grace Simon(19),Madia Rabihi(19),Dayana Beny(18),Rahma Gege(20)Catheline Kisinde(20),Ziada Mbega(20),Prisca Mlekwa (22) na Faraja Kivenule(18)

Maratibu huyo anasema kuwa washiriki hao ni wale wenye uwezo mkubwa wa kujieleza na wanauelewa mpana wa masuala ya urembo na kuwa kutokana na uelewa wao huo wanauwezo mkubwa wa kuutoa mkoa katika aibu ya kuendelea kuwa wasindikizaji katika jati hilo.

Bashir anasema kuwa mkuu wa mkoa wa Iringa Mohamed Abdulaziz ambaye amealikwa kumtazawa mrembo wa mkoa atamzawadi mshindi wa kwanza shilingi 600,000,mshindi wa pili atapata shilingi 400,000 na mshindi wa tatu shilingi 300,000 wakati washiriki wote wataondoka na kifuta jasho cha shilingi 50,000 kila mmoja.

Hata hivyo anasema kuwa warembo hao watasindikizwa na burudani kutoka kwa mshindi wa Tuzo za Kilimanjaro mwaka 2010 Diamond Belle 9 na msanii wa nyimbo za asili kutoka mkoani Mbeya Awilo wa Mbeya na kuwa washiriki hao wamenolewa na mwalimu Wanne Star pamoja na aliyekuwa miss Iringa mwaka 2009 .

Pamoja na mratibu huyo kueleza matumaini zaidi ya mkoa wa Iringa kujiweka pazuri katika kutwaa taji la urembo Taifa baada ya safari ya leo kumpata mrembo wa mkoa kukamilika katika ukumbi wa St.Dominic mjini hapa ,bado washiriki hao wameonyesha kutambiana zaidi na kila mmoja akieleza kujipanga kuchukua taji hilo.

Wakati kwa upande wao wadhamini wakuu voda Com pamoja na wadhamini wengine wa onyesho hilo wameeleza kufurahishwa na maandalizi makubwa ya kambi hiyo na kuwa upo uwezekano mkubwa mkoa wa Iringa kutimiza ndoto yake kama washiriki walivyopaniaani kutwaa taji hilo.

Share this article :

+ comments + 1 comments

June 12, 2010 at 1:01 AM

Karibu kwenye kibaraza chetu upate ufahamu mzuri zaidi. Ninakupongeza kwa kusoma kitabu changu "JANGA LINALOTAKA KUIKUMBA TANZANIA, OIC NA MAHAKAMA YA KADHI"sasa fuatilia kwenye blog hii www.findtruefaith.blogspot.com utapata mengi sana

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA