Home » » MAADHIMISHO YA SIKU YA MAALBINO KUFANYIKA IRINGA KITAIFA

MAADHIMISHO YA SIKU YA MAALBINO KUFANYIKA IRINGA KITAIFA

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Sunday, May 2, 2010 | 5:29 AM


WAKATI waziri mkuu wa Mizengo Pinda mei 4 anataraji kuwa mgeni rasmi kwenye maadhimisho ya siku ya watu wenye ulemavu wa ngozi (maalbino) Tanzania yatakayofanyika mkoani Iringa ,maalbino wameeleza kusikitishwa na unyama unaofanywa dhidi yao na kutishia kutoshiriki kupiga kura katika uchaguzi mkuu iwapo hawatawekewa ulinzi.

Maalbino hao wamelaani vitendo vya wenzao 50 kuuwawa kinyama toka yalipoibika mauwaji ya maalbino mwaka jana hadi sasa na kuwa pamoja na serikali kupitia kwa waziri mkuu Pinda kuonyesha kuweka mikakati mbali mbali ya kuwalinda ila bado vitendo hivyo vimeendelea kujitokeza alisema mmoja kati ya maalbino hao Janeth Anatoli jana wakati akizungumza na mwandishi wa habari hizi.

Alisema kuwa kwa upande wake haoni sababu ya yeye kushiriki katika uchaguzi mkuu kupiga kura kuchagua viongozi akiwemo Rais ,wabunge na madiwani wakati amani kwa upande wao ikiendelea kuota mbawa .

Kwani alisema kuwa pamoja na kuwa Tanzania kutajwa kuwa ni moja kati ya nchi zenye amani na utulivu lakini mambo yanayotendeka kwa sasa ni ukiukwaji wa haki za binadamu na kuwa amani hiyo kwao kama maalbino haipo tena na wamekuwa wakiishi maisha ya wasiwasi kama wanyama.


Soma habari hii katika gazeti la Tanzania Daima kesho
Share this article :

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA