Home » » WATEJA BENKI YA NBC WAPONA KUTEKETEA KWA MOTO

WATEJA BENKI YA NBC WAPONA KUTEKETEA KWA MOTO

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Friday, April 23, 2010 | 6:48 AM

WATEJA wa Benki ya NBC tawi la Iringa leo walilazimika kutimua mbio kutoka ndani ya benki hiyo baada ya moto mkubwa ambao chanzo chake bado hakikuweza kufahamika mara moja kushika jingo hilo.Kutokana na tukio hilo la moto wateja na wafanyakazi wa benki hiyo walilazimika kutimua mbio na kutoa nje ya jengo hilo huku askari wa kikosi cha kutuliza ghasia (FFU) pamoja na askari kanzu ,askari wa usalama barabarani wakiongozwa (RCO) mkoa wa Iringa Crausy Mwasyeba wakiwa wameimarisha ulinzi katika eneo hilo la benki.

Benki hiyo iliyopo eneo la Mshindo mjini hapa ilianza kushika moto majira ya saa 5.45 asubuhi moto ulioanzia katika moja kati ya vyumba za watumishi wa jego hilo ambao wamekuwa wakiishi katika ghorofa ya mwisho ya jego la benki hiyo.Baadhi ya wateja wa benki hiyo ambao walikuwa nje wakisubiri kuhudumiwa katika mashine ya kutolea fedha ya ATM walimweleza mwandishi wa habari hizo kuwa moto huo ulianza juu ya jengo hilo ambapo kwa upande wao wakiwa chini ya jengo hilo walianza kuona mosho na cheche za moto zikianguka kutoka juu ya jengo hilo hali tukio lililowafanya kuwajulisha wahusika wa benki hiyo.

Alisema John Sanga kuwa baada ya taarifa hiyo askari polisi waliokuwepo katika lindo hapo waliweza kutoa taarifa katika kituo cha polisi na mara moja idadi kubwaya askari walifika eneo hilo kabla ya askari wa kikosi cha zimamoto Manispaa ya Iringa hawajafika.Hata hivyo alisema jitihada kubwa zilizofanywa na askari wa kikosi cha zimamoto na wale askari polisi katika kuzima moto huo zimepelekea kulinusuru jengo hilo kuteketea kwa moto.Mkuu wa kikosi cha Zimamoto mjini Iringa Mohamed Japhar alisema kuwa baada ya kupokea taarifa waliweza kufika eneo hilo haraka na kufanikiwa kuukabili moto huo ambao tayari ulianza kuchukua kasi kubwa.Pamoja na kufanikiwa kuzima moto huo bado alisema chanzo cha moto huo hakijaweza kufahamika na kuwa idara yake na shirika la umeme Tanzania (TANESCO) na jeshi la polisi wanaendelea na uchunguzi zaidi juu ya tukio hilo.

Meneja wa benki hiyo mkoani Iringa hakuweza kupatikana kuelezea undani wa tukio hilo huku kwa upande wake kaimu meneja ambaye ni mwasibu katika benki hiyo Henry Mwakasendo akiwagomea wanahabari waliofika ofisini kwake kuzungumza chochote juu ya tukio hilo japo alikiri kuwepo wakati wa tukio hilo la moto .“Naomba ndungu wana habari mnielewe vizuri mimi si msemaji mkuu wa tukio hilo … kama mnataka msubiri meneja ambaye kwa sasa hapa hayupo “


Kamanda wa polisi wa mkoa wa Iringa Evarist Mangalla amethibitisha kutokea kwa tukio hilo japo alisema kuwa bado uchunguzi zaidi unaendelea ikiwa ni pamoja na kujua hasara zilizopatikana katika tukio hilo.

MWISHO
Share this article :

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA