Home » » GODWIN SIBONIKE MALILA HAYUPO TENA NASI...

GODWIN SIBONIKE MALILA HAYUPO TENA NASI...

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Saturday, April 10, 2010 | 1:39 AM


Mwanahabari Francis Godwin wa gazeti la Tanzania Daima na Msemakweli kwa niaba ya familia ya mzee Godwin Sibonike Malila wa Soweto Mbeya anasikitika kutangaza kifo cha baba yake mdogo mzee Godwin Sibonike Malila (Pichani) kilichotokea tarehe 8 mwezi huu wa nne katika jijini Mbeya.
Habari ziwafikie kaka wa marehemu Bw Kenani Kazimoto Ngao wa Makete Iringa na Ally Kikombe wa Sumbawanga Rukwa Mdogo wa marehemu Luvoneko Siwonike wa Sumbawanga Rukwa na Enock Malila wa Chunya Mbeya.Shemeji wa marehemu Mh.Wiliam Lukuvi mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam na mbunge wa jimbo la Ismani Iringa ,Wadau wenzangu wote katika tasnia hii ya habari pamoja na ndugu jamaa na marafiki popote pale walipo.
Mazishi yanataraji kufanyika leo tarehe 10.4.2010 majira ya saa saba mchana katika makaburi ya sabasaba jijini Mbeya.
Kwa pamoja tunaamini kabisa Mungu ni muweza wa mambo yate pamoja na sisi kumpenda zaidi baba yetu mpendwa Mungu yeye kampenda zaidi yetu hivyo hatuna budi kusema jina la Bwana na libariiwe daima.AMINA.
NB. Mpendwa mdau wa mtandao huu kutokana msiba huu napenda kukuomba uvumilivu wako kwa muda wa siku mbili kuanzia leo mtandao huu na ule wa http://www.matukiodaima.blogspot.com/ hakuta kuwa na tukio lolote jipya kwani nitakuwepo katika maombolezo .nashukuru kwa ushirikiano wako.Bofya hapa
Share this article :

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA