Home » » WAUZA MAGAZETI IRINGA WAJA NA MBINU YA KUWAUMBUA WASOMAJI BURE MAGAZETI MEZANI..

WAUZA MAGAZETI IRINGA WAJA NA MBINU YA KUWAUMBUA WASOMAJI BURE MAGAZETI MEZANI..

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Thursday, February 18, 2010 | 10:21 AM


UMOJA wa vijana wauza magazeti katika Manispaa ya Iringa umeanzisha mkakati wa kuwabana kwa kuwatoza malipo ya shilingi 2000 wale wote wenye tabia ya kusoma bure magazeti yakiwa mezani .

Mkakati huo ambao umefikiwa hivi karibuni katika kikao chao cha pamoja ambacho mwenyekiti wake alikuwa mwandishi wa habari hizi ,utekelezaji wake umeanza jana kwa wauza magazeti hao kusambaza matangazo katika meza zote ikiwa ni pamoja na kuwatoza faini ya shilingi 2000 wale waliofika kusoma bure.

Akizungumza na mtandao huu mwenyekiti wa muda wa umoja huu Mashaka Kayoka alisema kuwa mauzo ya magazeti limeendelea kushushwa na tabia za wateja wenye kawaida ya kufika mezani na kusoma bure kisha kuondoka bila kununua gazeti.

Hivyo alisema pamoja na kuwa tabia hiyo inachangia kushusha mauzo na kuwafanya vijana wauza magazeti kuichukia kazi hiyo kutokana na kushindwa kuuza magazeti kwa wingi.

"...kazi hii ni kazi kama zilivyokazi nyingine kwani mwanzoni kabla ya wateja kuanzisha tabia hiyo ya kusoma bure mezani .....wauza magazeti walikuwa na maisha mazuri lakini kwa sasa wengi wao wanaishia kulipa madeni katika makampuni pekee"

Kayoka alisema matangazo yaliyobandikwa ni yale ambayo yanapiga marufuku tabia ya watu kusoma bure magazeti mezani na kuhamasisha utamaduni wa kufika na kununua magazeti na kuondoka bila kuweka msongamano katika meza.

Alisema kuwa mbinu hiyo ambayo ilianza mapema jana imeanza kuonyesha mafanikio makubwa baada ya watu wanaoongoza kwa kusoma bure magazeti mezani kufika na kununua baada ya kusoma tangazo hilo .

Kayoka alisema kuwa baadhi ya wateja wamekuwa wakifika na kununua gazeti moja na kusoma matatu lakini kwa sasa haitaruhusiwa ni vyema kila mtaja kufika na kununua na kuondoka badala ya kununua gazeti la kampuni moja na kusoma bure magazeti ya makampuni mengine zaidi ya kumi.

Kwani alisema ni vyema mteja kujiwekea malengo toka akitoka nyumbani kuwa anakwenda kununua gazeti lipi na kujua bei yake badala ya kufika na kuanza kupekua magazeti yote na kuishia kununua gazeti moja ama kutonunua kabisa.

Hata hivyo bado amewaomba waandishi wa habari ambao wanapiga picha za magazetini pamoja na wale wa Runinga kutembelea katika meza za magazeti kwa lengo la kuwapiga picha watu wanaosoma bure mezani .

Kwani alisema wauza magazeti wamekuwa wakifanya kazi ya kupanga magazeti baada ya kupanguliwa na watu hao wanaofika kusoma bure mezani bila kununua.

katika hatua nyingine Kayoka amewataka waendeshaji wa vipindi vya kutoka magazetini katika runinga na radio hapa nchini kusoma vichwa vya habari pekee badala ya kusoma habari yote kama ilivyo.

Kwani alisema usomaji wa habari zote katika Tv na radio umekuwa ukichangia kushuka kwa mauzo ya magazeti kwa kuwafanya wateja kutofika kununua kabisa magazeti.

Mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com umejipanga vya kutosha na kuweka wapiga picha zaidi ya 10 ambao watafanya kazi ya kupiga picha wale wote watakaokutwa wakisoma magazeti bure mezani na kila picha itanunuliwa shilingi 3000 kwa ajili ya kuwekwa katika mtandao huu na magazeti ya uwazi,Tanzania Daima,Taifa Tanzania,Msemakweli na Mwanasoka kila wiki wasomaji bure watawekwa magazetini na katika mtandao huu.
Share this article :

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA