Home » » RPC AMTAKA NICKSON KULISAIDIA JESHI LA POLISI KUKUTANA NA MISUKULE 10

RPC AMTAKA NICKSON KULISAIDIA JESHI LA POLISI KUKUTANA NA MISUKULE 10

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Sunday, February 14, 2010 | 2:38 AM


KUIBUKA kwa kijana Nickson Bonifasi Kabonge (23) kushoto mkazi wa Mafinga wilaya ya Mufindi ambaye anadaiwa kufariki dunia na kuzikwa mwezi wa 10 mwaka jana na kuibuka tena mwezi Januari mwaka huu kumezidi kuzua utata baada ya kamanda wa polisi mkoa wa Iringa (ACP) Evalist Mangalla (pichani) kuonyesha kumtamani kijana huyo na kutaka alisaidie jeshi la Polisi ili kujua ilipo misukule 10 inayodaiwa kucha kijana huyo porini .

Utata wa suala hili umeonyeshwa kuzidi kuchukua sura mpya ndani ya mkoa wa Iringa huku jeshi la polisi likizidi kupinga kwa nguvu zote kuibuka kwa msukule huo hali ambayo inaweza kupelekea kaburi la linalosakikika kuzikwa kijana huyo kufukuliwa ili kujua kilicozikwa ndani ya kaburi hilo.

Wakizungumza katika kikao cha pamoja na waandishi wa habari mkoa wa Iringa ambao walitaka kujua uchunguzi wa jeshi la polisi kuhusiana na msukule huo na utata uliojitokeza ndani ya mkoa wa Iringa na baadhi ya maeneo hapa nchini, waandishi wa habari waliliomba jeshi la polisi kufanya uchunguzi wa kina juu ya suala hili badala ya kuendelea kupinga bila kufanya uchunguzi wowote.

Wanahabari hao zaidi ya 10 walioshiriki kikao hicho walionyesha kutoliamini jeshi la polisi mkoa wa Iringa kutokana na hatua yake ya kupinga taarifa za mashuhuda wa tukio hilo ambalo walishiriki mazishi ya kijana huyo na hata baadhi yao kuchangia michango yao ili kufanikisha mazishi hao.

Kwani walisema taarifa za kifo cha kijana huyo kwa sasa zimeenea kote nchini ila hakuna mtanzania ambaye ameibuka na kutoa taarifa za kupotelewa kwa ndugu yake mwenye jina hilo ila bado jeshi la polisi Iringa limeendelea kukanusha suala hilo bila kuwa na uhakika wa kutosha.

Hivyo wana habari hao waliliomba jeshi la polisi Iringa kushirikiana na vyombo vya habari ili kupata ukweli wa kijana huyo badala ya kuendelea kukanusha bila kuwa na uhakika wa jambo hilo.

Aidha walihoji kwa kipindi cha miezi mitatu ambayo kijana huyo alizikwa katika mji wa Mafinga kuna taarifa ya mtu kupotelewa na ndugu yake na kama hakuna na jeshi la polisi linapinga taarifa za kijana huyo kwanini kaburi hilo lisifukuliwe ili kuchukuliwa vipimo vya DNA ili kuwa na uhakika zaidi .

Pia wanahabari hao walilitaka jeshi la polisi mkoani Iringa kumbana mwajiri wa kijana huyo ili kuweza ili kujua uhalali wa kifo chake pamoja na kulisaidia jeshi la polisi kujua mtu aliyezikwa katika kaburi hilo.

Kwa upande wake Kamanda Mangalla alisema alisema kuna haja ya kijana huyo ambaye amekuwa akidai kuwa katika eneo ambalo alikuwepo amewekwa msukule amewaacha wenzake 10 kwa upande wake atamtaka kijana huyo kwenda kumwonyesha walipo wenzake hao ili kufanya nao mazungumzo zaidi.

Akizungumza kwa jazba kamanda huyo alisema kuwa vyombo vya habari hazikupaswa kuripoti habari hiyo ambayo inaonyesha ni habari za kishirikina na kuwa katika ushuhuda wake Nickson iwapo atamtaja mtu na mtu huyo kuguswa anaweza kuchukua hatua za kisheria japo kwa sasa hawezi kumchukulia hatua yeyote kijana huyo kwa ushuhuda wake anaoendelea kutoa katika makanissa mbali mbali.

Kwa upande wake mzazi wa kijana huyo mzee Bonifasi kabonge alilihakikishia jeshi la polisi mkoa wa Iringa kuwa kijana huyo kweli alikuwa amezikwa na kuwa kama polisi wanaendelea kubisha ataomba kaburi lake lifukuliwe ili kujiridhisha zaidi kwani mazishi ya kijana wake yalihudhuriwa na umati mkubwa wa wakazi wa mji huo na wote walishiriki kuaga mwili huo.

Hata hivyo alikanusha madai ya jeshi la polisi kuwa yawezekana mwili uliozikwa katika kaburi hilo ni wa mtu mwingine kutokana na hofu ya wazazi .

Kwani alisema iwapo polisi hawakupaswa kufanya kazi kwa kufikiri badala yake walitakiwa kutoa taarifa sahihi kwa umma ikiwa ni pamoja na kujiridhisha badala ya kuonyesha kufanya kazi kwa kukisia jambo ambalo linaweza kuondoa imani ya wananchi .

Kwa undani zaidi wa sakata hili soma gazeti la msemakweli la leo ama tafuta gazeti la Mwananchi la Alhamisi wiki iliyopita

Share this article :

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA