Home » » MZAZI AWAZAWADIA SUTI WALIMU WA SHULE BORA TZ YA SOUTHERN HIGHLANDs MAFINGA BAADA YA MTOTO WAKE KUFAULU.................

MZAZI AWAZAWADIA SUTI WALIMU WA SHULE BORA TZ YA SOUTHERN HIGHLANDs MAFINGA BAADA YA MTOTO WAKE KUFAULU.................

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Sunday, February 14, 2010 | 3:42 AM


Viongozi wa dini wakifungua kwa maombi sherehe ya kuwapongeza walimu katika shule ya kitamaifa ya Southern Highlands Mafinga ,siri ya kufanya vizuri ni maombi
Mkurugenzi mtendaji wa shule hiyo Mwl .Mary Mungai (kushoto ) akisakata dansi la injili na wageni waalikwa


Lazima tufurahi matokeo ya watoto wetu


Hapa hakuna urangi wote tujipongeze pamoja

'Huu Msosi wa leo funga kazi tunapenda kama kila siku tungekuwa tunakula na kunywa kama leo' ni walimu wa shule hiyo

Shule nyingine ziige mfano huu wa kutukutanisha pamoja

Hapa tumeshiba sasa basi

Faida ya kusomesha imeanza kuonekana mapema

SHULE ya kimataifa ya Southern Highlands Mafinga mkoani hapa imefanya sherehe kubwa ya kuwapongeza kwa zawadi walimu wa shule hiyo kwa kuiwezesha kushika nafasi ya kwanza kimkoa na nafasi ya 14 kati ya shule zaidi ya elfu kumi na tatu kitaifa katika matokeo ya mtihani wa Taifa wa darasa la Saba mwaka jana.

Pamoja na uongozi wa shule hiyo kutoa motisha kwa walimu na wanafunzi pia mzazi Awariywa Nnko ametoa zawadi binafsi kwa walimu wote wa shule hiyo kwa kumwezesha mtoto wake Gift Nnko kuchaguliwa kujiunga na shule ya vipaji maalum ya Kihaba mkoani Pwani.

Akizungumza katika sherehe hiyo ya kuwapongeza walimu iliyoandaliwa na mkurugenzi mtendaji wa shule hiyo Bi.Mary Mungai ,mzazi huyo Nnko alisema kuwa pamoja na kuwa katika shule hiyo wanafunzi wote zaidi ya 20 waliweza kufaulu mtihani wa darasa la saba mwaka jana ili kwa upande wake ameamua kuwa pongeza walimu hao kwa kuwanunulia vitambaa vya kushona suti kama njia ya ukumbusho kwao.


Nnko alisema kuwa shule hiyo imekuwa tishio kitaaluma katika mkoa wa Iringa kutokana na uongozi wa shule hiyo kuwa na mshikamano mzuri ikiwa ni pamoja na mkurugenzi wa shule hiyo kuwapongeza walimu wanaofanikisha watoto kufanya vizuri.

Hivyo alisema kuwa utaratibu huo ni mzuri hata kwa shule za msingi za na sekondari zinazoendeshwa na serikali katika kuwafanya walimu kuongeza juhudi katika ufundishaji.

Kwani alisema kuwa shule za serikali zimeendelea kuwa nyuma kitaaluma kutokana na walimu kuendelea kusaulika na kukosa motisha pale wanapofanya vizuri.

Mbali ya serikali kushindwa kutoa motisha kwa walimu pia alisema hata wazazi wa wanafunzi wanaosoma katika shule za serikali na zile za binafsi wamekuwa hawana utamaduni wa kuwashukuru walimu mara baada ya watoto wao kufanya vizuri.

Kwa upande wake walimu wa shule hiyo Jema Mkunela na mkuu wa shule hiyo Njoroge Francis wakishukuru kwa niaba ya walimu wenzao waliopewa zawadi kutoka kwa mzazi huyo na uongozi wa shule hiyo ,walisema kuwa hatua ya mzazi huyo na uongozi wa shule kukumbuka kuwapongeza walimu ni changamoto kubwa kwao na inawapa moyo zaidi wa kujituma katika kazi.

Mkurugenzi wa shule hiyo Mary Mungai alisema kuwa amelazimika kuwapongeza walimu na wanafunzi wa shule hiyo kama njia ya kuwaunganisha walimu pamoja katika utendaji kazi zaidi.

Pia alisema kuwa toka shule hiyo ilipoanzishwa na kuanza kutoa darasa la saba mwaka 2001 imekuwa ikifanya vizuri katika matokeo yake kiasi cha kupelekea wazazi wengi kutoka maeneo mbali mbali ya nchi kusomesha watoto wao katika shule hiyo.

Alisema kuwa kwa mara ya kwanza ilipoanza kutoa matunda ya darasa la saba mwaka 2001 shule hiyo ilishika nafasi ya 5 kitaifa na mwaka jana imeweza kushuka kwa kushika nafasi ya 14 japo bado ni nafasi nzuri ukilinganisha na shule za serikali ambazo zimeendelea kufanya vibaya zaidi.

Hata hivyo anasema kwa sasa shule hiyo imekuwa ikizidi kupata umaarufu mkubwa hasa baada ya kujitangaza katika mtandao huu na Radio Ebony Fm ya Iringa .

Alisema kuwa kuwa kwa sasa nafasi za wanafunzi katika shule hiyo zipo kuanzia darasa la kwanza na kuwa lengo ni kuanzisha shule ya sekondari katika shule hiyo .

Wakati shule hiyo ya Southern ikiendelea kufanya vema uchunguzi uliofanywa na mtandao huu katika shule mbali mbali za sekondari ndani ya mkoa wa Iringa umebaini kuwepo kwa idadi ndogo ya wanafunzi waliofaulu mtihani wa Taifa wa darasa la saba mwaka jana kujiunga na kidato cha kwanza kutokana na baadhi ya walimu wakuu wa shule kuwa kikwazo cha wazazi kutosomesha watoto hao sekondari kutokana na kutoza michango nje ya utaratibu wa wizara ya elimu na mafunzo ya ufundi.

Katika shule ya sekondari ya Kibengu wilaya ya Mufindi wazazi wamekuwa wakilalamikia michango mbali mbali inayotozwa na uongozi wa shule hiyo ikiwemo mchango wa taalum shilingi 10,000,mtihani wa Mock kwa kidato cha nne 15,000,Tuition 1000 kwa kila mwanafunzi na ulinzi shilingi 5000 wakati genereta shilingi 2000 kila mwanafunzi kwa mwezi .

Aidha mwanafunzi wa kidato cha kwanza ili aweze kuanza masomo pamoja na ada ya shilingi 20,000 pia anatakiwa kutoa michango mbali mbali nje ya utaratibu ikiwa ni pamoja na kuwalipa mishahara walimu wapya ambayo inafika zaidi ya 90,000 .

Wanafunzi 30,187 sawa na asilimia 59.65 ndio ambao walifaulu mtihani wa Taifa wa darasa la saba mwaka jana na kuchanguliwa kwa ajili ya kuanza masomo ya sekondari January mwakani 2010 .
kama wataka kujiunga na shule ya Southern Highlands Mafinga bonya hapa

Share this article :

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA