Home » » MAKWETA AMALIZWA JIMBONI

MAKWETA AMALIZWA JIMBONI

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Saturday, February 27, 2010 | 7:05 AM

SAKATA la kufungwa kwa kiwanda cha chai Lupembe wilaya ( Lupembe Tea Factory ) wilayani Njombe mkoani Iringa limezidi kuonekana mwiba kwa mbunge wa jimbo la Njombe Kaskazin mzee Jackson Mwaketa baada ya mwekezaji wa kiwanda hicho Nawab Mulla ambaye ni mwenyekiti wa chama cha mapinduzi (CCM) mkoa wa Mbeya kuvunja ukimya na kuamua kumlipua mbele ya wapiga kura wake kwa kumtaja kuwa ni mmoja kati ya watu waliohusika kuwatapeli wananchi fedha zao.

Kutokana na zogo kuibuka ndani ya kikao hicho cha kutafuta suluhu ya kiwanda hizo mkuu wa mkoa wa Iringa Mohamed Abdulaziz alilazimika kumwomba mwekezaji huyo kukaa chini asiendelee kumwanika mbunge huyo ambaye alikuwa akizomewa na wananchi ambao ni wakulima wa chai huku mbunge akijichanganya kwa kutomjua Mulla zaidi ya kumsikia na badae kudai ni rafiki yake.

Mulla alitoa kauli hiyo baada ya Mbunge huyo kutamka mbele wa wajumbe wa mkutano wa viongozi wa mkoa na wakulima kuwa hamjui mwekezaji huyo na ndo kwanza anamuona kwa mara ya kwanza jana jambo ambalo si kweli.

Akisoma kumbukumbu zake za vikoa ambavyo mbunge huyo alihusika na wajumbe pamoja na picha zao Mulla alisema anamshangaa mbunge kutamka kuwa hamjui wakati kwenye moja ya michakato hiyo mbunge alishiriki na picha zake zipo.

“ Kama mnasema nilipata kiwanda hiki kwa ujanja ujanja basi walioni uzia ni pamoja na Makweta…na viongozi wa vyama vyote vya wakulima….” Alisema Mulla huku akiwataja mmoja baada ya mwingine hatua iliyowafanya wakulima kumshangilia huku wangine wakitokwa na machozi.

Baada ya kuona kuwa mbunge anaumbuka mkuu wa mkoa wa Iringa Mohamed Abdulaziz alilazimika kuingilia kati na kumkatisha Mzee Mulla maelezo yake na kumruhusu mbunge Makweta kujitetea.

Akijitetea Makweta alimtaka mwekezaji huyo kuacha kutaja jina lake kwani yeye hafahamiani naye na ndio mara yake ya kwanza kumuona siku hiyo.

“Kwanza hapa tatizo sio Mulla, na nimekuwa nikimtetea sana Mulla popote nilipoenda, hapa tatizo ni makundi ndani ya umoja wa wakulima ambayo kila moja lina maslahi binafsi” alisema Makweta huku akikubali hoja ya mkuu wa mkoa iliyotaka kiwanda kifunguliwe4 kesi ziendelee.

Malumbano hayo yalifuatia baadhi ya wakulima kudai kuwa mwekezaji alipata kiwanda hicho kwa njia ya wizi na kwamba hakufuata taratibu hivyo kuiomba serikali iwarudishie kiwanda ili waendeshe wao.

Katika kikao hicho kilichoitwishwa na mkuu wa mkoa wa Iringa kwa lengo la kuwataka wakulima na mwekezaji wakubaliane ili kiwanda kianze kazi, wakulima wengi walikubali mwekezaji huyo hana matatizo hivyo aendelee hata kama kuna kesi mahakamani.

Kikao hicho kilichofanyika katika ukumbi wa Tarafa ya Lupembe iliamriwa na mkuu wa mkoa kuwa wahusika baada ya kukubali kuwa kiwanda kifunguliwe kwa njia ya maridhiano, basi kuundwe kamati ya watu 6 ambapo watatu watatoka kwenye vyama vya msingi vya wakulima na watatu watatoka chama cha ushirika cha MUVYULU chenye ubia wa asilimia 30 wa kiwanda hicho.

Kwa mujibu wa mkuu wa mkoa kamati hiyo itakutana na mwekezaji nay eye mkuu wa mkoa Machi 20 mwaka huu ili kupanga namna ya kukifungua kiwanda.
MWISHO
Share this article :

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA