Home » » CHADEMA IRINGA YAELEZA KUSIKITISHWA NA MATOKEO

CHADEMA IRINGA YAELEZA KUSIKITISHWA NA MATOKEO

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Thursday, February 11, 2010 | 11:47 PM


PRESS RELEASE

CHADEMA (M) IRINGA – kimepokea matokeo ya kidato cha 4 kwa masikitiko makubwa . Hii ni kutokana na utengo wa wazi unaoonekana kati ya matabaka makubwa 2 ya Watoto wa wenye nacho na Watoto wa Watanzania masikini wakawaida .

Haiingii akilini kuona idadi kubwa ya Vijana wetu wamepewa daraja 0 na daraja la 4 .ambao walikuwa wakisoma Shule za Serikali ,huko Shule zinazo itwa BORA ambazo si za Serikali zinazoongoza kutoa vijana waliopewa daraja la I .

Shule hizo zinatoza ada/karo kubwa ambazo watanzania walio wengi hawawezi kumudu kuwapeleka Watoto wao huko ,na hivyo kutoa nafasi kwa Watoto wa Vigogo.

Hivyo kutimiza ule usemi wa Serikali ya CCM kuwa –killimo kwanza kwa vijana wa walala hoi ,na Elimu kwanza kwa Vijana wa Vigogo.

CHADEMA TUNAAMINI kwamba Elimu ndio urithi wa thamani kupita vitu vyote ambavyo vijana wetu wamepaswa kupewa ,lakini kwa mtindo huu hakika wasio nacho watazidi kuwa masikini wa mambo yote na wenye nacho watazidi kuwa juuya mambo yote ya Taifa letu ,Hii ni hatari na haikubaliki na inatakiwa ilaaniwe na wazalendo wote wa Nchi hii .

Angalia Shule bora za wakubwa na Shule za mwisho za walala hoi.

SHULE ZA PESA BORA SHULE ZA KATA( KILIMO KWANZA )

1 MARIAN GIRLS 1 KIZARA

2 ST JAMES 2 MINGUMBI

3 DON BOSCO 3 SONGOLO

4 ST FRANCIS 4 MARAMBO

5 ST MARY’S 5 DOLE

6 URU SEMI 6 NAHUKAHUKA

7 FEZA BOYS 7 RUPONDA

8 ANWARITE 8 MPUNYULE

9 MAUA SEM 9 RURUMA

10 ST MARY GORET 10 VIZIWI NJOMBE.

JAMBO LA PILI: Ni vipi shule za Serikali ziwe nyuma kimaendeleo kuliko hizo nyingine ,Tatizo haliko kwa wanafunzi tatizo liko kwa Wizara ya Elimu – Nadhani wanaagenda ya siri dhidi ya vijana wetu. Mbona taasisi nyingi za Serikarili ziko juu kuliko nyinginezo ,sasa inashindwa nini upande wa Elimu?Mlaji akishindwa kula chakula wakulaumiwa ni mpishi, katika hili wizara ya Elimu wanapaswa wawajibishwe . Wanawajali na kuwaenzi vipi Waalimu wetu ?Mwalimu ndiyo nguzo ya Elimu popote pale Duniani ,Serikali ya CCM inalitambua hilo ?

WITO : Walimu na Vijana msikate tamaa wala kujaribu kujidhuru kama baadhi walivyo fanya na kupoteza maisha –Ni wakati sasa wa kuwa chachu ya mabadiliko katika familia zenu na taifa kwa ujumla. Uchaguzi unakuja na ndio wakati muafaka wa kuondoa uongozi unaodumisha matabaka haya .

Simameni Walimu na vijana tushirikiane tulete mabadiliko ya kweli vinginevyo tutabaki kulalamika tu, na wenye nacho watazidi kudumu kutukandamiza katika Nyanja zote za maisha yetu

Wamemwaga mboga yetu, sisi tumwage ugali wao wakati wa uchaguzi.

Ni wakati sasa wa kuonyesha nguvu ya umma, wenzetu ambao ni wachache wanajivunia pesa ,Sisi tuliowengi ni lazima tuunganishe nguvu zetu na sauti zetu .hakika hakuna pesa wala silaha iwezayo kushinda nguvu ya UMMA.

Imetolewa na mwenyekiti wa Chadema mkoa wa Iringa Bw.Beny Mwigongo Kapwani .

CHADEMA - NGUVU YA UMMA
IRINGA.

Share this article :

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA