Home » » BREAKINGNEWzzzzzz ABIRIA MIKOA YA KUSINI WAKWAMA WAFUNGA BARABARA

BREAKINGNEWzzzzzz ABIRIA MIKOA YA KUSINI WAKWAMA WAFUNGA BARABARA

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Thursday, February 18, 2010 | 10:31 AM


ABIRIA wanaosafiri kuelekea mikoa ya kusini na nchi za kusini mwa Tanzania jana wamefanya vurugu kubwa katika eneo la ukaguzi wa magari (Check Pint ) Igumbilo mjini Iringa ikiwa ni pamoja na kuifunga kwa muda barabara kuu ya Tanzania ,Zambia na Msumbiji (TANZAM ) na kuwapiga madereva wakorofi kama njia ya kupinga hatua ya askari wa kikosi cha usalama barabarani mkoani hapa kuwakamata madereva sita wa mabasi waliyokuwa wamepanda.


Tukio lilo ambalo lilidumu kwa zaidi ya masaa manne na kupelekea jeshi la polisi kuingilia kati kumaliza utata huo kwa kuwapa dhamana madereva hao ,lilitokea majira ya saa 8 mchana baada ya madereva wa mabasi hayo kuendesha bila kinyume na sheria ya sumatra.


Wakizungumza kwa niaba ya abiria wenzao kuhusiana na tukio hilo abiria Chriss Kashillila , Cleva Mlungu na Salima Mwakasyela walisema kuwa wanashangazwa na hatua ya jeshi la polisi mkoa wa Iringa kuwakamata madereva wa mabasi hayo zaidi ya sita kwa madai ya kufika mapema zaidi eneo hilo pamoja na kuendeshwa na dereva mmoja wakati toka walikotoka jijini Dar es Salaam na kupita mikoa zaidi ya miwili askari wa usalama barabara wamewaacha wapite bila kuzuiwa.


Alisema Mlungu kuwa wanaingiwa na hofu juu ya utekelezaji wa sheria za usalama barabarani ambazo zinawataka wamiliki wa vyombo vya usafiri nchini hasa mabasi yanayofanya masafa marefu kuweka madereva wawili .


Kwani alisema sheria hiyo imekuwa ikitekelezwa katika mkoa wa Iringa pekee hali ambayo imekuwa ikizidi kulipaka matope jeshi la polisi nchini hasa katika mkoa wa Iringa ambako madereva wamekuwa wakiendesha kwa kufuata sheria ila wanapopita Iringa sheria imekuwa ikiachwa bila kufanya kazi.


Hata hivyo alisema wao kama abiria hawapingani na utendaji kazi wa jeshi la polisi mkoa wa Iringa ila wanaomba sheria hiyo iwe kwa mikoa yote .


Wakielezea kuhusiana na hatua yao ya kufunga barabara hiyo walisema wamelazimika kufunga barabara na kugoma kuendelea na safari baada ya madereva waliopewa jukumu la kuwaendesha kutokuwa na sifa za udereva baada ya wao wenyewe kugoma kuendesha mabasi hayo kwa madai kuwa hawana uzoefu.


“Hapa tulipo tuna watoto wadogo ambao hawajala chochote sasa hatua ya abiria kukalishwa hapa kwa zaidi ya masaa 3 ni unyanyasaji mkubwa na sisi kama abiria hatupo tayari kuendelea na safari kwa kuendeshwa na dereva mmoja tena asiye na sifa ya udereva”


Pia walisema kama sheria inataka basi liendeshwe na madereva wawili iwaje jeshi la polisi limchukue dereva mmoja na kutaka basi liendeshwe na dereva mmoja.


Hata hivyo mbali ya kufunga barabara hiyo abiria hao zaidi ya 200 walionyesha kuwapiga makofi madereva wa daladala katika Manispaa ya Iringa na wale wa magari ya serikali ambao walikuwa wakitaka kulazimisha kupita eneo hilo kwa nguvu .


Walisema watakuwa tayari kufungua barabara hiyo iwapo mkuu wa Iringa Mohamed Abdulaziz ili kutoa malalamiko yao kwake na si vinginevyo.


Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Iringa (RTO) Kedmund Mnubi akizungumza na abiria hao alisema kuwa kukamatwa kwa madereva hao kumetokana na ukiukwaji wa maazimio 18 ya baraza la Taifa la usalama barabara lililoketi mjini Dodoma chini ya mwenyekiti wake waziri mkuu Mizengo Pinda ambapo moja kati ya maazimio hayo ni pamoja na kuagiza mabasi ya masafa marefu kuwa na madereva wawili.


Pia alisema madereva hao wanadaiwa kuendesha magari yao kwa mwendo kasi na ndio sababu ya kufika kufika mapema mkoani Iringa kinyume na utaratibu wa Sumatra ..


Kamanda wa polisi wa mkoa wa Iringa (ACP) Evalist Mangalla alimweleza mwandishi wa habari hizi kwa njia ya siku kuwa hatua ya abiria hao kufunga barabara ni kosa na kuwa hawakupaswa kufunga barabara kama njia ya wao kupinga hatua hiyo.


Madereva waliokamawa na watafikishwa mahakamani kesho Ijumaa ni pamoja na dereva wa basi la Sumry lenye namba za usajili T 658 ACT Bw . Kasim Siulanga, dereva wa basi la New Force lenye namba T 777 DCR Bw Habibu Suleiman ,dereva wa basi la Abood lenye namba T 277 ATH Bw. Kasim Mangalla wengine ni dereva wa basi la Hood lenye namba za usajili T 447 AAZ Bw. Omary Mohamed na mwenzake Omary Ally aliyekuwa akiendesha basi lenye namba za usajili T 242 ARU ,Ibrahim Omary wa basi la Happy National lenye namba za usajili T 181 AQP huku dereva wa basi la Sumry Bw Efrehem Mwakapala akisakwa na polisi baada ya kuwakimbia mara baada ya kukamatwa.Kwa mujibu wa sheri ya Sumarta ya mwaka 2007 kifungo cha 18 A,C kinatoa adhabu ya mahakama kumfunga jela mwaka mmoja ama kumtoza faini kati ya shilingi 200,000 hadi 500,000 dereva anayeendesha basi la abiria kwa mwendo kasi .


Hivyo kwa mujibu wa sheria hiyo kuna uwezekano wa madereva hao leo kutozwa faini ama kufungwa jela kwa ukiukaji wa sheria hiyo.

Mabasi hayo yanadaiwa kufika mkoani Iringa majira ya saa 7.30 mchana badala ya saa 7.45 kama ambavyo ratiba yao inavyoonyesha.


Share this article :

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA