Home » » SAKATA LA MAZINGIRA TATA YA RUSHWA KWA TAFFIC 11 KIZUNGUMKUTI............

SAKATA LA MAZINGIRA TATA YA RUSHWA KWA TAFFIC 11 KIZUNGUMKUTI............

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Wednesday, January 20, 2010 | 3:04 AM


Pichani ,Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Iringa (RTO) Kedmund Mnubi akionyesha picha ya mabasi ya kampuni ya Hekima ambayo bosi wake amehukumiwa kwenda jela miezi nane kwa kushindwa kuajiri madereva wawili hivi karibuni .

UTATAwaibuka kati ya madereva ,wananchi na wadau wa usafiri mkoani Iringa kuhusiana na kuchunguzwa kwa askari wa usalama barabarani 11 walioonekana katika kituo kimojawapo cha Runinga hapa nchini wakiwa katika mazingira yenye utata wakituhumiwa kupokea rushwa .


Wakizungumza kwa nyakati tofauti na mtandao huu madereva wa malori na wale wa mabasi makubwa walisema kuwa si kweli rushwa ambayo polisi wamekuwa wakipokea ni zaidi ya shilingi 2000.Madereva hao akiwemo mzee Samweli Juma (70) na Kefa Kalinga (45) walisema kuwa pamoja na kuwa baadhi ya mazingira yamekuwa yakiashiria rushwa ila hakuna dereva ambaye anaweza kutoa rushwa ya shilingi 50,000 ama 100,000 kwa askari wa usalama barabarani wakati ukitaka kufuata sheria faini ya shilingi 20,000.


Hivyo walisema iweje dereva akubali kutoa rushwa ya shilingi 50,000 ama 100,000 ambazo ni fedha nyingi asitoe fedha halali shilingi 20,000.


“ Kweli hatukatai rushwa ipo tena sio Iringa peke yake ila ….tuwe wakweli katika kulizungumzia suala hili ..hawa askari wanapokea fedha za maji na matunda na sio fedha kukwa kiasi hicho …..lakini kwanini iwe kwa askari pekee hapa kwetu Tanzania rushwa kila kona wewe nenda leo ofisi ya serikali utaona kama ofisi za umma na askari wa usalama barabarani nani zaidi”Walisema ni vyema mkuu wa polisi nchini kuwa makini na tuhuma hizo kwa askari hao vinginevyo ari ya askari kutimiza wajibu wao inaweza kupungua iwapo wananchi wataendelea kujenga chuki na askari hao .“ Ujue kama askari watafanya kazi zao kikamilifu kero itakuwa kwetu wenyewe madereva kwani hata haya magari tunayoendesha sio mazima asilimia 100 ila wanatuvumilia tu …..hivyo tunapotoa fedha kama zawadi kwa kazi yao tusigeuke kuwaita wala rushwa wakubwa “Huku wananchi mjini Iringa wakionyesha kupinga hatua kukamatwa na kuwa jeshi la polisi linapaswa kuunda kamati ya kuchunguza badala ya kutoa hukumu kutokana na picha hizo za Runinga ambazo hata moja haikuonyesha fedha .Walisema Amina Juma (50) mkazi wa Kihesa na Samweli Mpalanzi (45) mkazi wa Mlandege kuwa iwapo jeshi la polisi litawafukuza kazi askari hao kuna uwezekano mkubwa kukongeza wimbi la ujambazi wa kutumia silaha hapa nchini na kuwa suala la rushwa halipo kwa askari peke yake bali lipo zaidi ngazi za juu serikalini .Kwa upande wake mwenyekiti wa kamati ya usalama barabarani mkoani Iringa Salim Abri Asas alisema kuwa kimsingi utendaji mzuri wa askari wa kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Iringa ndio ambao umepekelea mkoa kuendelea kuwa na matukio kidogo ya ajali za barabarani ukilinganisha na mikoa mingine hapa nchini.Hivyo alisema kwa upande wao kama kamati wanaendelea kuwapongeza askari wa kikosi hicho chini ya mkuu wa usalama bararani mkoa wa Iringa (RTO) Kedmund Mnubi kwa kazi nzuri ya kupunguza ajali za barabani mkoani hapa na kutaka jitihada zaidi ziendelee kuonyeshwa bila askari kuvunjwa moyo ya watu wasiopendezwa na utendaji wao.Mwenyekiti wa Sumatra mkoa wa Iringa Abed Kiponza alisema kuwa bado ripoti ya rushwa iliyotolewa na kituo hicho cha Runinga haikuweza kuwahoji madereva husika waliopigwa picha wakitoa chochote kwa askari hao 11 kama walitoa rushwa hiyo kwa malengo gani.“Nimetazama vizuri sana kile kipindi ila sikuona mwandishi akiwahoji wahusika wa utoaji rushwa ili kujua walitoa kwa ajili ya makosa gani ili kujua kama askari hao walipokea rushwa kwa ajili ipi”

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Iringa (ACP) Evarist Mangalla ameuthibitishia mtandao huu kuwa jumla ya askari 11 ndio ambao wanahojiwa na jeshi la polisi na kutakiwa kuandika barua kuhusiana na tukio la kunaswa na camera ya kituo hicho cha Runinga.

Kamanda huyo alisema kuwa kwa sasa hawezi kutaja majina ya askari hao kwani haijathibitika kuwa walikuwa wamepokea rushwa na kuongeza kuwa suala la rushwa lina pande mbili mtoaji na mpokeaji .

Hata hivyo alisema kuwa hatua za kinidham zitachukuliwa kwa askari watakaobainika kuhusika kwa namna moja ama nyingine na tukio hilo la kupokea rushwa.


.............ITAENDELEA ....................

Share this article :

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA