Home » » NYUMZA ZAIDI KU BOMOKA KWA MAFURIKO IDODI...............

NYUMZA ZAIDI KU BOMOKA KWA MAFURIKO IDODI...............

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Tuesday, January 26, 2010 | 12:32 PM

IDADI ya nyumba zilizobomoka kwa mafuriko yaliyotokea juzi katika kijiji cha Idodi tarafani wilaya ya Iringa vijijini ambako ni nyumbani kwa mbunge wa jimbo la Ismani Wiliam Lukuvi imeongezeka na kufikia nyumba 17 huku nyumba nyingine 39 zikiwa mbioni kubomoka.
Hata hivyo kutokana na tukio hilo mbunge wa jimbo la Ismani na Lukuvi ambaye ni mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam jana amefika kutoa pole kwa wahanga wa mafuriko hayo pamoja na kutoa msaada wa vyakula wenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 2.
Hata hivyo uchunguzi wa kina uliofanywa na mtandau huu katika kijiji hicho na kuthibitishwa na uongozi wa serikali umebaini kuwepo kwa nyumba zaidi kubomoka tofauti na taarifa za awali ambazo zilionyesha nyumba 15 pekee ndizo zilizobomoka.
Nyumba ambazo zipo katika hali mbaya kutokana na kulowa na maji kupitia kiasi na baadhi zimeendelea kubomoka ni nyumba hizo 39 huku baadhi ya familia zimeanza kuhama katika nyumba hizo na kwenda kutafuta hifadhi kwa majirani na katika ofisi za CCM ,kata na nyumba za madarasa katika shule ya msingi ya kijiji hicho .
Wahanga wa mafuriko hayo Edina Myinga ,Ibrahimu Kideo na Peter Gembe walisema kuwa kwa sasa hivi sasa zaidi ya nguo ambazo walivaa wakati wakitoka kujiokoa katika tukio hilo hawana nguo wala chakula na kuwa wamekuwa wakiishi katika ofisi za taka na CCM na vyumba vya madarasa.
"kama unavyo tuona hapa ndivyo tulivyo hatuna chakula ,nguo wala pesa ...kila kitu kilisombwa na mafuriko tunachoshukuru Mungu afya zetu ni salama"
Mwenyekiti wa serikali ya kijiji hicho Mussa Kigelero alisema kuwa familia zaidi ya 57 ndizo ambazo zimeathirika vibaya kwa mafuliko hayo huku familia 17 nyumba zao zikiwa zimebomoka kabisa na nyumba zilizobaki zipo mbioni kuanguka wakati wowote kuanzia sasa.
Pamoja na kaya hizo zaidi ya 50 kukumbwa na mafuriko na kupoteza mali mbali mbali pamoja na vyakula bado alisema katika kijiji hicho wananchi wengine wanahitaji msaada wa chakula kama gunia 250 na kuwa mahitaji ya chakula cha msaada katika kijiji ni asilimia 55.
Aidha alisema sehemu kubwa ya miundo mbinu kama barabara kuu ya kuelekea hifadhi ya Taifa ya Ruaha karibu kilometa zaidi ya mbili zimeharibika vibaya na kama jitihada za kutengeneza hazitafanywa upo uwezekano wa watalii kukwama kwenda katika hifadhi hiyo.
Mratibu wa elimu kata ya Idodi Ngola Mwangosi alisema kuwa wakati wa tukio hilo likitokea wanafunzi karibu nusu ya shule walikwama kwenda shule kutokana na kuhofia mafuriko ambayo yalisababisha barabara na maeneo mbali mbali kujaa maji.
Maratibu elimu huyo alisema kuwa athari kubwa ambazo zimejitokeza upande wa elimu ni kuharibika kwa miundo mbinu ya maji hali iliyopelekea shule ya sekondari Idodi kukosa huduma ya maji kwa siku mbili sasa baada ya mabomba kuharibiwa vibaya na mafuriko.
Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Iringa vijijini Fundi Mihayo alisema kuwa halmashauri inaendelea na tathimini ya mafuliko hayo ikiwa ni pamoja na kutafuta misaada mbali mbali kwa ajili ya wahanga.
Akizungumza na wakazi wa kijiji hicho ambao wamekumbwa na mafuliko mbunge Lukuvi alisema kuwa wakati serikali ikitathimia athari zilizojitokeza kutokana na mafuliko hayo bado wananchi wanapaswa kuendelea kuchukua tahadhari zaidi kwa kuangalia uwezekano wa kupata viwanja katika maeneo yenye miinuko zaidi.
Lukuvi alisema kuwa serikali inaouwezo wa kuwasaidia wahanga wa tukio hilo chakula na mahitaji madogo madogo ila gharama za kujenga nyumba bado ni jukumu la wananchi wenyewe.
"Nitakuwa nawadanganya kama nitawaeleza kuwa serikali itawajengea nyumba wote mliokumbwa na mafuriko ....serikali hana utaratibu wa kuwajengea nyumba wananchi ila ina uwezo wa kuendelea kuwasaidia chakula hivyo nawahakikishieni kuwa suala hili litachukuliwa kwa uzito mkubwa na serikali ili kuhakikisha kuwa hakuna mtu atakayekufa njaa"
Hata hivyo aliwaomba wadau mbali mbali kujitokeza kuwasaidia vyakula na mahitaji mengine wahanga hao wa mafuriko Idodi.
Kwani alisema serikali kupitia kitengo cha maafa itaendele kuwasaidia wahanga hao kwa kuleta mahema na mahitaji mengine kama chakula kwa wahanga wa mafuriko hayo.
"Kama mbunge wenu nimeguswa sana na tukio hili hivyo nimelazimika kujipiga piga haraka kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 2 kwa ajili ya kupata vyakula hivyo ambazo ni unga,mboga ,sukari na mafuta kwa ajili ya familia zilizokumbwa na mafuliko haya"
MWISHO
Share this article :

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA