Home » » MWAMOTO APANIA KURUDI BUNGENI TENA......................

MWAMOTO APANIA KURUDI BUNGENI TENA......................

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Thursday, January 7, 2010 | 3:27 AM


BAADA ya kimya kirefu hatimaye aliyekuwa mbunge wa jimbo la Kilolo mkoani Iringa na kushindwa kwa kura mbili katika kura za maoni ndani ya CCM Bw Venance Mwamto ameibuka na kueleza kusikitishwa kwake na jumuiya ya wazazi wa CCM katika wilaya ya Kilolo kwa hatua yao ya kutaka kumchukulia fomu mbunge huyo huku ikijua kuwa kila mwanachama ndani ya CCM ana haki ya kugombea na kuungwa mkono na CCM na jumuiya zake zote.

Pamoja na kuilalamikia jumuiya hiyo pia Mwamoto amesema kuwa amejiandaa vya kutosha kwa ajili ya kumpokea nafasi ya ubunge mbunge wa sasa nayemaliza muda wake Profesa Peter Msolla ambaye ni waziri wa mawasiliano ,sayansi na Teknolojia.

Akizungumza na waandishi wa habari jana mjini hapa ,Mwamoto alisema kuwa kipindi cha miaka mitano ambayo amekuwepo nchi ya ubunge baada ya kupokelewa na mwanachama mwenzake Prof. Msolla kimetosha kwake kujifunza na kujua nini ambacho wana Kilolo wanataka kutoka kwa wabunge wao.

Hivyo alisema kuwa yapo mambo mengi ambayo aliyaanzisha akiwa madarakani kabla ya kumwachia mbunge Msolla mwaka 2005 ambayo yameshindwa kuendelezwa na kwa yale yaliyoendelezwa hayajamalizika na hivyo kuamua kurudi kumalizia kama alivyowaahidi wana kilolo .

Mwamoto alisema kuwa pamoja kuwepo baadhi ya mambo yaliyofanywa katika kipindi cha uongozi wa waziri Msolla ila sehemu kubwa ni yale yaliyoanzishwa wakati yeye akiwa mbunge wa jimbo hilo.

" Ukweli ni kwamba maendeleo haya yote yanayoonekana katika majimbo ,kata na nchi ni yale ambayo mipango yake iliwekwa kuanzia kipindi cha awamu ya tatu chini ya uobngozi wa rais Benjamin Mkapa ambapo na mimi nilikuwepo kama mbunge....hivyo naomba wabunge waliopo madarakani wanavyoelezea utekelezaji wa Ilani ya CCM wasitusahau wabunge tuliopita"

Hata hivyo Mwamoto ameelezwa kusikitishwa kwake na hatua ya jumuiya ya wazazi wa CCM wilaya ya kilolo kutamka wazi kumchukulia fomu mbunge Msolla wakati fomu zitatolewa kwa wanachama wote.

Kwani alisema kuanza kutoa matamko kama hayo kwa sasa ni kuminya demokrasia ndani ya CCM na kuwazuia wanachama wengine wenye sifa kushindwa kujitokeza kutimiza haki yao ya kidemokrasia na kikatiba.

" Sipingi watu kujitokeza kumchukulia fomu mgombea ila isiwe jumuiya ya chama kwani jumuiya inapaswa kuungana na chama kuwaunga mkono wagombea wote bila kuwabagua"

Pia alisema kwa upande wake amejiandaa vya kutosha kuhakikisha anampokea ubunge waziri Msolla kama ambavyo waziri huyo alivyofanya kumpokea kwa kura mbili mwaka 2005.

"Uzuri ndani ya CCM nafasi ya Urais, ubunge na udiwani ni kipindi kimoja kimoja cha miaka mitano ....hivyo kwa kuwa Msolla kipindi chake cha miaka mitano imemalizika ni vizuri naye akaanza kujiandaa kwa ajili ya kupokelewa kama alivyo nipokea mimi"

Baadhi ya wapembuzi wa mambo ya siasa mkoani Iringa wanasema kuwa kwa utaratibu wa kura za maoni ndani ya CCM ulivyo sasa kuna uwezekano mkubwa wa Mwamoto kurudi katika nafasi hiyo kutokana na wananchi wengi kuanza kuonyesha imani kwake.
MWISHO
Share this article :

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA