Home » » MWAKALEBELA AZUSHIWA JAMBO IRINGA.....................

MWAKALEBELA AZUSHIWA JAMBO IRINGA.....................

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Monday, January 11, 2010 | 3:11 AM


KUNA kila dalili za katibu mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF),Frederick Mwakalebela kufukuzwa ama kufikishwa mahakamani kwa matumizi mabaya ya madaraka yake ikiwa ni pamoja na kutuhumiwa kujitangaza kugombea ubunge jimbo la Iringa mjini kwa kugawa vifaa vya wadhamini wa TFF kwa ajili ya ligi kuu ya Voda com.


Mwakalebela akiwa Mtendaji Mkuu TFF, anatumia kuchukua baadhi ya vifaa vinavyotolewa na wadhamini mbalimbali wa Ligi Kuu ya Vodacom kwa matumizi yake binafsi ikiwa ni pamoja na kuvigawa katika jimbo la Iringa mjini kwa lengo la kumng'oa mbunge wa sasa wa jimbo hilo Monica Mbega (CCM).


Hata hivyo tuhuma hizo zimetolewa huku ikiwa imepita siku moja tu toka Mwakalebela kumalizika mashindano aliyokuwa ameyadhamini ya kuwania kombe la Krimas na mwaka mpya katika Jimbo la Iringa Mjini ambako alikwishatangaza kuwania kiti cha Ubunge kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM),katika uchaguzi Mkuu, baadaye mwaka huu.


Mashindano hayo yanadaiwa kugharimu karibu Sh.milioni 15 gharama ambayo ilijumuisha fedha za uendeshaji, fedha za zawadi, vifaa vya michezo kama mipira na jezi ambapo gharama zote hizo zikitolewa na Mwakalebela.


Vifaa vilivyotolewa kama zawadi kwa timu shiriki na zisizoshiriki, siku ya kufunga mashindano hayo, Januari 10,mwaka huu,zilikuwa na nembo ya Vodacom, TACAIDS na PSI na si kampuni ya Mwakalebela ya Vanedrick Ltd hali iliyozusha hisia kwamba huenda vifaa hivyo vimechukuliwa TFF.


Pia katika hali ya kushangaza iliyoonyesha kuwa Mwakalebela alikuwa amezidiwa na vifaa hivyo vya wadhamini ni pale alipogawa jezi na mipira kwa timu ambazo hata hazikushiriki mashindano hayo kama Lipuli Fc, Polisi Iringa, Magereza, Kihesa ,Afrika wandaras na nyingine nyingi.

Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Iringa,Benny Mwigongo kapwani alisema kuwa CCM wameanza kampeni mapema huku TAKUKURU wakiwatazama na kuonya kuwa watu wanaotaka nyadhifa za siasa wasitumia vyeo vyao vya umma kujitangaza kama ilivyo kwa katibu huyo ambaye tayari amepoteza sifa ya kuwa kiongozi wa TFF.


“Kitu cha kushangaza katika ashindano haya, linapokuwa suala la zawadi imetolewa mipira yenye nembo ya Vodacom na TACAIDS,…tunashangaa na kusikitika sana , tunaomba Takukuru wachunguze michezo hii hadi huko TFF,” alisema Kapwani na kuongeza.


“Mwelekeo wa mashindano haya si ya kimichezo hata kidogo, angalia uwanjani wamejaa makaatibu wa CCM wa mitaa na madiwani wa CCM, hii ni hatari sana mtu asiye na uwezo kuandaa mashindano kama haya ndani ya CCM hawezi kuchaguliwa, hii ni rushwa sijuwi kwa nini Takukuru hawakusimamisha mashindano haya”.


Hata hivyo, Mwakalebela alikanusha vikali madai hayo na kueleza kuwa yeye kugombea ubunge si sababu ya kumzuia kufanya shughuli za kuendeleza michezo Mkoani kwake (Iringa).


Kuhusu vifaa vyenye nembo ya makampuni alikanusha kuchukua vifaa vya TFF vinavyotolewa na wadhamini bali alisema si kosa kuomba kwa marafiki zake na kuleta nyumbani kwao.


“Msipende kuwa negative (mtizamo hasi) kwenye mambo jamani, yaan mimi kuleta vifaa Mkoani kwagu ni kosa?, mpira ukiwa na nembo ya vodacoma au TACAIDS kuna kosa gani, ndiyo maana watu hawapendi kujitolea kwa sababu ya mambo haya ya kuonekana wabaya,” alisema.


Alipoulizwa kama atasemaje kama watu wakisema anachukua vifaa vya TFF na kuvitumia kwa maslahi yake binafsi alisema : “Kwa taarifa yako mimi nina duka la vifaa vya michezo na hata kama watu hawajuwi waje niwazelekeze.


katika mchezo huo wa fainali mbali ya wageni rasimi kuwepo watatu akiwepo mratibu wa kombe la Mungano Mufindi Daud Yasin ambaye alianza kuingia uwanjani bado alikuwepo mwenyekiti wa CCM wilaya Abed Kiponza, na mwisho zawadi kwa mabingwa timu ya Miyomboni Kitanzini alikabidhi RCO Crausy Mwaisyeba


Msikilize mwenyekiti wa Chadema mkoa wa Iringa Beny Kapwani anavyoelezea juu ya Mwakalebela kisha bonyeza hapa
Share this article :

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA