Home » » MTOTO CATHEEREN FRANKI WA MIAKA 8 KUTOKA IRINGA AANZA KUMCHANGIA MTOTO TUMTUFYE

MTOTO CATHEEREN FRANKI WA MIAKA 8 KUTOKA IRINGA AANZA KUMCHANGIA MTOTO TUMTUFYE

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Monday, January 25, 2010 | 9:50 PM


SIKU mmoja baada ya mzazi wa mtoto Tumtufye Mwakasaka (8) mzee Rashid Mwakasaka kumwomba Rais Jayaka Kikweye pamoja na wsasamaria wema wengine msaada wa fedha zaidi ya shilingi milioni 5 kwa ajili ya kumpeleka nchini India mtoto wake huyo anayesumbuliwa na tatizo la fiho mtoto wa miaka 8 Cathereen Frank amejitokeza kumsaidia mtoto mwenzake huyo kiasi cha shilingi 100,000.


Akizungumza na mtandao huu kwa niaba ya mtoto Cathereen mama wa mzazi wa mtoto huyo Lucy Frank alisema kuwa mtoto wake amelazimika kutoa kiasi hicho cha fedhe kutoka katika mauzo yake albam yake ya nyimbo za injili baada ya kumwonea huruma mtoto mwenzake huyo na kutaka kuokoa maisha yake.
Hata hivyo alisema kuwa watoto wengi wamekuwa wakipoteza maisha yao kutokana na kukosa misaada matibabu kutoka kwa jamii inayowazunguka ambo ambalo mtoto Cathereen ameamua kuonyesha mfano kwa kuwa mtanzania wa kwanza kuguswa na ugonjwa wa mtoto mwenzake huyo kwa kujitolea kiasi hicho kama sehemu ya kuanzisha harambee kwa watanzania kujitokeza kuokoa maisha ya mtoto huyo.

Pia alisema kuwa pamoja na mtoto huyo kujitokeza kuomba msaada wa matibabu ila bado wapo watoto wengi na wazazi wengi ambao watoto wao wanapoteza maisha yao kwa kukosa fedha za matibabu kutoka kwa watanzania wenye mapenzi mema.

Hivyo allisema kuwa kuna uwezekano kubwa maisha ya mtoto Tumtufye yakaokolewa na watanzania wenye mapenzi mema iwapo watajitokeza hata kwa kuchangia kila mmoja kiasi kidogo cha fedha kinaweza kusaidia kumsafirisha mtoto huyo hadi nchini India kwa matitabu.

Aidha alisema kuwa pamoja nna utamaduni ambao watanzania tumejiwekea wa kuchangia sherehe mbali mbali bado utamaduni huo utaonekana mzuri zaidi iwapo jamii itaelekeza nguvu zake katika kuwakumbuka watu wenye shida kama hao badala ya kuendelea kuchangia sherehe mamilioni ya shilingi huku wengine wakipoteza maisha kwa kukosa fedha za matibabu.


Mbali ya kuwaomba wafanyabiashara ndani ya mkoa wa Iringa na maeneo mbali mbali ya Tanzania kujitokeza kumsaidia mtoto huyo pia aliiomba serikali kupitia wizara ya afya kusaidia matibabu ya mtoto huyo kwenda nchini India kama ambavyo serikali ilivyojitolea kwa manajimu wa nyota hapa nchini Shehk Yahaya Hussein kwenda kutibiwa nje ya nchi.

Mtoto Tumtufye anasumbuliwa na ugonjwa wa figo na kupelekea mwili wake kuvimba na kutokwa na malengelenge .

Wasamaria wema ambao wataguswa na mateso anayopata mtoto huyo kusaidia kumwokoa kwa kutuma fedha zao katika account namba 4172502537 NMB kwa jina la Rashid Mwakasaka ama ile ya mama wa mtoto Rachel Mshana ambayo ni 040201120412 NBC.
Share this article :

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA